Njaa kitu kibaya, hatari mno.
Ameongea utani na mipasho ya kutetea serikali.
Kifupi kaulizwa kwa nini sheria zilizopendekezwa zibadilishwe na Tume ya 1980 zipo mpaka leo?
Jibu lake, kasema, kwa anavyojua yeye kama profesa wa sheria, na muelewa wa mambo ya legal anthlopology, ni kwamba sheria zinazohusu mambo ya kimila, kiitikadi, kidini, kijima, hazibadilishwi kwa kukurupuka.
Akaendelea kusema, ndio maana mpaka leo kwao yeye Waziri wanakeketa vitoto vya kike, na pia kwao mbunge muuliza swali, ambae ni Mkurya, wanawake zao hawapendeki bila kupigwa. Kwa hiyo sheria hizi inshallah zitakuja kubadilishwa. Ndio maneno ya waziri hayo.
Hapo kwenye jibu hilo kuna weledi gani wa kusifiwa?