Prof. Kabudi afunika bungeni

Prof. Kabudi afunika bungeni

Yeyote aliye ndani ya ccm ni adui wa maendeleo ya kweli kwa watanzania. Vimaendeleo wanavyofanya ni vya hadaa ya kuombea kura tu kipindi cha uchaguzi. Tunasubiri mtakavyotetea ununuzi wa ndege kwa maendeleo ya Taifa kipindi cha kampeni
Tatizo lenu hamna original thinking; you can't make it with reactionary strategy of doing politics. You need to be original. Hivi kuna Mtanzania mwenye akili timamu anaweza kubeza uamuzi wa Serikali kuhakikisha nchi inakuwa na shirika imara ndege (national flag bearer). Nyie sijui mmelogwa na nani. Ndege zimenunuliwa kiwandani kwa mtengenezaji ili kuepuka madalali vishoka wapigaji kama ilivyokuwa wakati wa ununuzi wa radar na ndege ya Rais (2003). Kuweni original thinkers ili watu wenye intellect waweze kuwaunga mkono vinginevyo mtaishia kunawa tu, basi.
 
Alivyo Maliza kwa kusema kuwa kashibana na Waitara na ni Ma Swahiba kuna Mabunge ya Magamba kidogo yatapike kwa Kinyongo na Roho Mbaya na Mengine huenda yakapendekeza Proff ahojiwe kwa usaliti wa Chama
 
Majibu gani unaona kabisa huyu mtu sio mwanasiasa. Agenda za administration laws zinatoka serikarini sio kwa wabunge, unaweza kuanzisha hoja binafsi lakini serikari ailazimishwi kupokea wao ndio wanaamua mipango ya ufanisi sio bunge.

Isitoshe ata mwanafunzi wa A level anaweza kukwambia laws evolve with changing social morality so what is special about that tuwe na tabia za kujisomea sio kutukuza elimu za watu kwa hoja nyepesi mno.
 
Hakika taifa na bunge la JMT linahitaji watu aina ya huyu profesa!

Mosi, ana uwezo wa hali ya juu wa kujibu hoja bila kuudhi.

Pili, ni ubobezi katika eneo husika la sheria anateleza tu na vifungu mpaka raha.

Tatu, matumizi ya lugha ya kiswahili mwanana anapiga misamiati mpaka baadhi ya wabunge kama sugu wanatoa macho.

Mwisho kabisa, anaonekana ni msikivu na mnyenyekevu kwa wabunge wote hata upinzani. Watanzania tunahitaji wabunge na mawaziri wa namna hii kwa kweli.

Mungu amsimamie afike mbali.

Tazama video ya majibu aliyoyatoa leo bungeni,lazima umkubali.

Mvinyo ni ule ule, tofauti chupa tu...
 
Hivi Maprofesa na Madokta aliowateua Magufuli wamebadilisha nini katika taifa hadi sasa? Si ndo kwanza serikali inashindwa kutekeleza bajeti yake? Si ndo kwanza nchi inakwenda kama Lori bovu la mkaa, na dereva anakiri hivyo? Si ndo kwanza hali ya usalama wa nchi inazidi kuzorota? Hivi jitu kama li Mwakyembe nalo bado mnaamini ni msomi wa hadhi ya Udaktari wa Falsafa? Na Magu mwenyewe je, Mzee wa Fonti Feti, haha!
 
Nakutakia mafanikio mema profesa. Mwanzo mwema. Najua hatuwezi kukupima wezo wako wa kazi kwa kujibu maswali kwenye kikao kimoja cha bunge. Una safari ndefu. Kuna mambo ya ofisini kwako na vzur kao na mawaziri wenzio na wakubwa wenzio na kuna mikataba na mambo chungu mzima siwezi kuhesabu
 
Kuna watu wanampima kiongozi Kwa jinsi anavyotoa hotuba. Wakisikia hotuba moja basi kwishnei. Wengine wanampima kiongozi Kwa uwezo wa kutabasamu. Akitabasamu na kujichekea chekea basi, hiyo ni MTU wa watu na anaweza uongozi. Wengine wanampima Kwa ukali. Akiwa mkali wanasema ,yes, hapa tumepata kiongozi

Kiongozi hapimwi kirahisi hivyo
 
Prof. Palamagamba Kabudi baada ya muda atakuwa kama alivyoanza waziri Charles Mwijage (mtu wa sound) mwisho wa siku kwa vile yupo CCM naye atabadilika, maana upinzani tuna maswali magumu ya kutetea wananchi, hata aje mtu mahiri kama Prof. Kabudi maadamu yupo CCM baada ya muda atakuwa ''CCM Halisi'' maana CCM ni ile ile labda akubali kufukuzwa kama Nape Nnauye

Tanzania ya Viwanda-Charles Mwijage Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji

 
Muwe mnasoma soma kidogo historia ya dunia,itawapa ufahamu wa siasa na mapambano ya mwanadamu katika kutawala. CCM siyo adui yako wala cdm siyo rafiki yako,adui yako ni wewe mwenyewe.
 
Hakika taifa na bunge la JMT linahitaji watu aina ya huyu profesa!

Mosi, ana uwezo wa hali ya juu wa kujibu hoja bila kuudhi.

Pili, ni ubobezi katika eneo husika la sheria anateleza tu na vifungu mpaka raha.

Tatu, matumizi ya lugha ya kiswahili mwanana anapiga misamiati mpaka baadhi ya wabunge kama sugu wanatoa macho.

Mwisho kabisa, anaonekana ni msikivu na mnyenyekevu kwa wabunge wote hata upinzani. Watanzania tunahitaji wabunge na mawaziri wa namna hii kwa kweli.

Mungu amsimamie afike mbali.

Tazama video ya majibu aliyoyatoa leo bungeni,lazima umkubali.


Watu wa aina ya kabudi wapo wengi tatizo ni CCM. Yuko wapi Dr Sengondo Mvungi??? Yuko wapi Prof. Chachage????
 
Wewe ni mwongo......Tanzania anafeli kwa sababu ya mfumo wa hovyo wa CCM. Huwezi kuendekeza wawekezaji kwa kila kitu hata visivyo hitaji wawekezaji halafu utegemee maendeleo.
 
Back
Top Bottom