Prof. Janabi: Nakula mara mbili kwa siku

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,803
4,469
1708448088832.png

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi, amesema katika maisha yake na kile anachoishauri jamii anamaanisha na kukiishi.

Amesema kwa siku anapata mlo mara mbili, na kila mlo unapishana kwa saa kadhaa, akijieupusha kula mara kwa mara.

Prof. Janabi ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam, kwenye mahojiano maalum na vyombo vya habari.
 
Ana nidhamu ya kula. Ishu ya kulakula inategemeana na uwezo wa mtu kupata chakula.

Huwezi kupanga masaa ya kula kama huna uhakika wa kula utakulakula chochote kinacholiwa ukikutana nacho.

Wengine hufakamia vyakula kwa kuwa wamevipata kama bahati na hawana uhakika wa kuvipata tena kwa hiyo wanavibugia.

Unakuta mtu hana utaratibu wa kula kwa kuwa bajeti murua ya chakula hana. Wengine wana uwezo wa kupata chakula aina zote ila nidhamu ya kula hawana
 

MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi, amesema katika maisha yake na kile anachoishauri jamii anamaanisha na kukiishi.

Amesema kwa siku anapata mlo mara mbili, na kila mlo unapishana kwa saa kadhaa, akijieupusha kula mara kwa mara.

Prof. Janabi ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam, kwenye mahojiano maalum na vyombo vya habari.
Hapa namuunga mkono
 
Yupo sahihi

Ila kiukweli katika mambo ambayo wabongo tumeshindwa ni kuacha kula sana usiku..

Usiku mtu anafukia utafikiri anakwenda kupakia mawe..mwishowe ni kuota ndoto mbaya za kukabwa na wachawi..kumbe umevimbiwa

Usiku unatakiwa ule kidogo tena chakula laini au ule tunda ulale..
 
Back
Top Bottom