Profesa Janabi: Tuwarithishe watoto mali sio unene

Error 404

JF-Expert Member
Jun 21, 2022
781
799
Habari JF , Hii ni kutoka kwa prof pendwa Janabi .

Iende kwa wote ambao huwa wanajisifa kwetu ni wanene mara nimerithi unene etc...

Binafsi nimeipenda sana hii

---
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Mohamed Janabi amesema unene kupita kiasi si mzuri kwa afya ya mwanadamu na kusisitiza wazazi kuwapa watoto vyakula vyenye afya na kutaka watoto warithishwe mali na sio unene.

Profesa Janabi amasema hayo wakati akiwasilisha mada katika mkutano wa Mafunzo wa 108 wa watayarishaji wa vipindi vya Elimu kwa Umma ulioandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) unaofanyika mkoani Mwanza.

Washiriki wa mkutano huo ni watumishi kutoka taasisi mbalimbali za serikali.

IMG-20240221-WA0041.jpg
 
With my respect kwa professor, anaongelea watanzania wa level ipi?,high class bila shaka,huku lingusenguse hata mlo mmoja uliokamilika ni shida, professor bila shaka yeye anakula protein kama main meal huku wanga, veg vikiwa ni supplements, huku lingusenguse ni tofauti kabisa, ugali(wanga)ndio main meal huku kakibakuli kakiwa na maharage, au mboga mboga, tunaishi kwenye Tanzania moja yenye one of the highest unequal society
 
Naungana na Prof.

Enzi za nyuma, Mkurugenzi wa Hospital ya Taifa alikuwa hajulikani kwa umma isipokuwa kwa Wachache ila sasa Prof anajinadi na kutambulika kila pande ya nchi kupitia maushauri yake haya ya kiafya.

Wale tunaolea watoto hasa wenye kipato cha kati na juu, tuwalee kwa kufuata ushauri wa Prof na sio kuwalea na kuwa na miili kama ya baadhi ya Chipukizi.

Naongezea kwenye ushauri wa Prof, urithi wa mali uendane na urithi wa ujuzi(elimu) ili waje waendelee urthi wa mali
 
Back
Top Bottom