Prof. Janabi na Upepo wa Kisiasa

Prof. Janabi na Upepo wa Kisiasa

Janaba...ni janaba tu!
Hata ufanyeje!... Litatoa harufu! Litanuka tu!

Ndio jina lake! Mwache aongee anachojiskia!... Na yeye ana waumini wake wanaomtii
 
Nimeomba CV yake jamaa kakimbia , shida humu tunachat na wengi non medical ndio maana hatuelewani

Alete CV ya janabi, iliyoandikwa kwenye website ya MNH haijitoshelezi

He is cardiologist by fellowship ?

Atuambie MMED yake aliipigia wapi

Napenda kuona CV yake

Form
6 alimaliza wapi

First degree akapiga wapi
Au ndio Zile master za Urusi degree na master unaunganisha humu humo

Second degree yake was it master of medicine in Cardio au alipiga master of Science akaingia
Kwenye fellowship hili liwekwe wazi

PHD yake alikimbizana nayo wapi

Mimi
I don’t count huo u prof , ukishakuwa na PHD Uprof ni papers published na kama upo kwenye teaching , unaupata

Paper nyingi zinafanywa na wanafunzi , wao wanaboresha nakujipublishia as their work

CV ya Janabi kwenye website ya MNH haipo formal

MNH kuna vichwa na
Vijua na vingine vilishasepa kwenye masilahi

ambao walikuwa na elimu iliyonyooka km wembe na ni MaMEd konki hatua kwa hatua

Ambao hao kama nafasi ya U DG MNH ingekuwa inatangazwa na madokta kushindanishwa, Janabi asingetoboa hata first round ki uwezo na ki CV

huyo alipata popularity baada ya kuinuliwa na JK , na sio kwa uwezo wake

Hoja ya msingi ni matamshi yake ni intimidating na sio scintifically. Kama anatoa warning kwenye jamii kuna namna ya kupresent na sio kusema ukila muhogo kwa siku inatosha, ukikojoa povu figo just because he met cases kama hizo kwa watu 3

Science haipo hivo and it does not entertain hizo symptomatic issues ndio maana mmewekewa maabaara to prove your hypothesis kama unachowaza kupitia pathological history taken ni sahihi
Janabi Kamaliza MD Mwaka 1989 kutoka chuo cha kharkov Medical Institute..

Kafanya Internship mwaka 1990, Muhimbili Medical Center..

Liverpool School of Tropical Medicine Fazakeley Hospital UK Junior House Officer mwaka 1992 akachukua Post Graduate Diploma Ina Tropical Medicine..

Akasoma MMED, University of Queensland in Australia (MMED ya Internal medicine ) Mwaka 1995..

Fellowship Kafanya kutoka Fellow American College of Cardiology (FACC) mwaka 1995 mpaka 2000 na Akapata PhD ya Cardiology...

Post Doctorate Alizofanya ni..

Internal Medicine and Molecular Science, Graduated in School of Medicine Osaka University Hospital Osaka, Japan 2004 (Post Doctorate)

Bergen University Norway Cardiology Department
and Medical University of South Carolina-USA Clinical attachment ya mwaka 2005
 
Proffesor Janabi kafanya Research Nyingi sana and he Is very Respected Man kwa Upande wa Research and Medical Health Studies..

Andiko lako Limejaa Theoretical Arguments Nyingj sijaona Epidemiological Argument au biostatistics Arguments za kupingana ma Proffesor Janabi..

kuhusu Signs Za magonjwa Are you even a Medical Practitioner Even a Junior One??

Kwasababu inashangaza huwezi kujua hata Signs na symptoms za Kdney disease ambazo Janabi anazisema Kila mara na Unataka achunguze sasa achunguze nini tena?

Kama Hutojali Ningependa Kujua UnEthical Arguments au UnEthical Statements Ambazo Janabi amezisema..

Unataka Data Support kwenye dalili za Wagongwa ambazo ni Pathological Findings?
Hizo ni alter Physiological Xtics kama Umesoma Unaweza kujua Kwanini mtu anakojoa Povu..
Na wala usinge kuja Kuandika Uzi kujiabisha kumjudge Proffesor..

Kuhusu Alcoholism na Magonjwa ya figo..
kuna Research zaidi ya 1000 zimefanyika na Zimeprove hivyo ukitaka Nitakuchambulia..
Ulitaka Research personel au Serikali wapite nyumba kwa nyumba kufundisha Findings za Research hizo???

Ni kukosa Adabu kuandika Vitu ambavyo Huna Elimu navyo na Unahisi Una Elimu navyo wakati hakuna unalojua Kuhusu Hivyo vitu...
Na hii kitu sio sawa ..

Unamu attack Kiongozi mkuu wa Hospitali ya Taifa kwa Misingi Ipi??
Unahisi Unajua Kuhusu Yeye??
Research ngapi umefanya??
Vipi Umefanya Fellowship ipi??
Tujifunze kuwa Na mipaka kwenye kila Kitu sio kila kitu tujifanye tunajua
Walevi wengi hawapendi kuambiwa ukweli kuhusu hatari za pombe kwenye mafigo yao. Wanahisi kuingiliwa undani wa maisha yao.

Unaweza kuponda namna profesa Janabi anavyofikisha ujumbe wake kwa jamii lakini huwezi kuuponda ujumbe wenyewe.
 
Janabi anapotosha sana. Vyakula vya wanga (sukari) ni vingi na vinapaswa kuliwa kwa wingi kwasabb miili inahitaji sukari kwa wingi sana ili kupata nishati (ATP) ya kuuwezesha kufanya kazi mbalimbali za kifiziolojia.

Kuhusu nyama. Wamasai wanakula nyama na maziwa throughout the year lkn hawapati shida yoyote. Janabi anadanganya umma.

Mm nashawishika kuamini kuwa matatizo ya moyo na figo yanasababishwa na pombe, matumizi mabaya ya dawa (neno kutwa linapotpsha wengi sana. Kutwa mara 3. Mtu anameza mara 3 kwa masaa 12 badala ya masaa 24), dawa feki, dawa hazihifadhiwi vizuri kwenye maduka ya madawa,
Wamasai unajuaje kama hawafi, kumbuka hawa hawaishi maisha yasiyo na anwani zinazojulikana. Nyama pia ni mbaya kwa afya.

Prof Janabi anachukiwa kwa sababu anaiambia jamii maneno ya ukweli kuhusu afya zao wenyewe.
 
Prof Janabi anachukiwa kwa sababu anaiambia jamii maneno ya ukweli kuhusu afya zao wenyewe.
Hana takwimu zinazoungwa mkono na sayansi, hivyo anaendeshwa kwa mihemko tu. Ndiyo maana ktk kila hoja yake kuna maswali mengi sana.

Kama nyama ni hatari mbona ktk jamii za wala nyama Kuna wazee?

Kama kunywa pombe ni hatari mbona kule Rombo kunakosifika kwa ulevi kuna wazee?

Yeye mwenyewe janabi mbona ana afya mbovu sana ukilinganisha na watu wengine wa umri wake?

Mfano: Kikwete ni mkubwa kwa Janabi lkn Janabi amevhoka kuliko Kikwete
 
Protein Inahitajika Kuliwa Sana Tena usiache kabisa..
Maana Protein ndo hujenga mwili na Protein pia ndo hutengeneza Enzymes na Hormones kwenye Miili yetu hata Taarifa za Mifumo ya Mwili ni Protein..DNA ni protein na RnA hivyo hivyo..

Sasa protein Kuwa kwenye Mkojo humaanisha nini??

Kwenye Figo Kuna machujio Zaidi ya milions ambayo huitwa nephrons na hizo nephrons zina sehemu mbili ambazo huitwa glomerulus na tubule. Hizo nephrons hufanya kazi mbili kwa kutumia glomerulus inachuja damu yote Kupitia Mishipa ya damu ambayo hupelekwa hapo na kazi ya tubule ni kurudisha baadhi ya Substances ambazo zinahitajika na mwili kwenye damu na Kutoa uchafu tu kupitia Ureter then kibofu then urethra then unakojoa..

Sasa kukiwa na Hitilafu kwenye Figo inaamaa nephrone hazitafanya kazi vizuri na Glomerulus hazitachuja damu vizuri na hivyo kusababisha kupitisha baadhi ya substanse ikiwemo Protein na zingine kwenye kwenye Tubule na mwisho wa siku zitapita kwenye ureter.....na utazikojoa..

Kwahyo zikipita Moja kwa moja huko figo and Hence lazma utazikojoa..

Sijui kama umenielewa au nielezee vizuri zaidi..
Kwanini tunapenda Kuitumia Protein kama Kipimo kwa sababu ndyo Particle kubwa kuliko zingine..
So kama Imeweza Kupita Hiyo zingine pia zimeweza kupita
Umetisha mkuu, nimejifunza something new leo...
 
Hapo ndio manapofeli kusema sufficient factor ; shida ya elimu ya TZ ni lots of books than practical

How do you say Alcohol ni sufficient factor ? Mjomba duh

Nikikuletea watu 100 ambao ni drunkes , na tukawafanyia vipimo over follow up na tusiwakute na figo
Would you comment Alcohol kuwa ni sufficient factor ?

Bado kuna shida kubwa kwenye mfumo wa elimu TZ hasa kwenye medical

Na ndio maana mgonjwa anaenda muhimbili anakuwa recommended for surgery , akienda India au Germany , wanamwambia ungeruhusu wakufanyie upasuaji… usingedumu , mgonjwa anafanyiwa treatement ya kawaida na kurudi salama

Bado tunashida kwenye mfumo wa elimu , medical field haipaswi kuwa paper centered ;
Hiki ulichosema ni exactly kilichompata jamaa yangu, alitakiwa afanyiwe upasuaji but kwenda India akapona bila opereseheni...
 
Kwenye Science kila kitu kinakuwa supported na data au statistical significance, kinyume na hapo hiyo inakuwa ni IMANI au personal faith.

Maneno kama ukikojoa mkojo wa povu, wewe una FIGO, kiuno kikizidi 40, una heart disease, ulaji wa sukari unaua figo , ulaji wa wali unaua mwili, unywaji wa Juice ni hatari kwa moyo , na aina nyingine ya maneno yake.

Huu sio ushauri wa kisayansi bali ni intimidation to the public and it is high time now The Ministry of Health should stop him immediately na Wizara ibebe jukumu lake la kuelimisha jamii kupitia taasisi za Chakula na Lishe ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri Rasmi jinsi ya kuepuka non communicable disease.

Janabi yupo ki political fame na hayupo kitabibu, na kwenye Sayansi ni UNETHICAL kuja na conclusions kama za Janabi.

The Flaminggham Heart Study began in 1948 in USA, Massachusetts ambapo ilienda kuangalia factors zinazochangia magonjwa ya moyo ( Cardiovascular disease), it was a cohort study ambayo ilichukua miaka zaidi ya 15 kuja na conclusion kuwa kuna uwezekano wa kupata heart disease kama unavuta snaa sigara, unene, kutofanya mazoezi etc. Na hii haikuwa ni confirmation, it was just a risk factor and not CAUSAL RELATIONSHIP!

Kuna watu wamekuwa wakinywa, wakivuta na wakila nyama nyingi kwenye maisha yao yote hadi wanazeeka hawajui presha ni nini, figo ni nini or anything like that .

Ever wondered why kuanzia miaka ya 2000 ndio matatizo ya figo na moyo yameongeza sana?

kuna watu waliokuwa walevi na wavutaji kama wazee wetu? And all of them died due to old age peacefully, no pressure , no figo no blah blah na walikuwa wakila sna wali , Sukar, nyama etc etc

Matatizo mengi ya figo TZ yanasababishwa na matumizi ya dawa kiholela, na dawa nyingi TZ ni counterfeit, matumizi ya mitishamba bila ya kuwa na standard maalumu, ulaji wa vyakula vya kusindika etc etc na clearly hii ni risk factor sio CAUSAL RELATIONSHIP.

Unawaambia watanzania wale kipande kimoja cha muogo kwa siku, that is very unethical and intimidation. The body needs sugar ya kutosha, fats za kutosha, proteins za kutosha , vitamins and mineral to function healthy and properly.

Why miaka ya sasa tatizo la figo na heart limekuwa ni kubwa? Hapa we need answers and causal relationship na sio intimidation!

Kama mwanasayansi unapotuambia ukikojoa mkojo wa povu hilo ni figo, unatakiwa kuja na findings ambazo zimekuwa checked scientifically and generalized, any statement unayotoa ni lazima iwe supported na data and proven scientifically .

Huwezi kutumia reference za watu wachache wanaokuja Hosp ambao tayari wanashida zao then ukaanza ku generalize kwa watu wengine publicly bila ya kuwa na sufficient , consistency , coherent and experimental data, you can’t generalize kwa patients wanaokuja who are already sick ….,. That is not science and impractical.

It is unethical for such a prof kuanza kutoa statement kama hizo ambazo hazina data support, ina raise query na questions uhalali wa huo u Prof ! . Hatuwezi kuwa madaktari wa social media na mitandao kwa mitaji ya KISIASA.Ni misleading na intimidation kwenye jamii unnecessarily.

Kama kweli unywaji wa pombe unapanua moyo …… demonstrate it , shows us ….data zipo wapi …..and what about the people who drink day and night… na hawana anything like that …. Tuna conclude vipi?

Ndio maana tunasema science has to be respected ili kuzuia personal experience kutawala.

Badala ya GOVT kufund research za kimkakati ambazo zinaweza kutuletea majibu na causal relationship as to why tatizo la figo na moyo limekuwa kubwa kuanzia miaka ya 2000, tunaenda kuspend billions of money kununua V8 za wakuu wa wilaya. Shame!
Daktar mwenyewe ukimuangalia tu unagundua afya yake haiko vzr. Sasa hivi mpaka suti zinampwaya.
 
Nimeomba CV yake jamaa kakimbia , shida humu tunachat na wengi non medical ndio maana hatuelewani

Alete CV ya janabi, iliyoandikwa kwenye website ya MNH haijitoshelezi

He is cardiologist by fellowship ?

Atuambie MMED yake aliipigia wapi

Napenda kuona CV yake

Form
6 alimaliza wapi

First degree akapiga wapi
Au ndio Zile master za Urusi degree na master unaunganisha humu humo

Second degree yake was it master of medicine in Cardio au alipiga master of Science akaingia
Kwenye fellowship hili liwekwe wazi

PHD yake alikimbizana nayo wapi

Mimi
I don’t count huo u prof , ukishakuwa na PHD Uprof ni papers published na kama upo kwenye teaching , unaupata

Paper nyingi zinafanywa na wanafunzi , wao wanaboresha nakujipublishia as their work

CV ya Janabi kwenye website ya MNH haipo formal

MNH kuna vichwa na
Vijua na vingine vilishasepa kwenye masilahi

ambao walikuwa na elimu iliyonyooka km wembe na ni MaMEd konki hatua kwa hatua

Ambao hao kama nafasi ya U DG MNH ingekuwa inatangazwa na madokta kushindanishwa, Janabi asingetoboa hata first round ki uwezo na ki CV

huyo alipata popularity baada ya kuinuliwa na JK , na sio kwa uwezo wake

Hoja ya msingi ni matamshi yake ni intimidating na sio scintifically. Kama anatoa warning kwenye jamii kuna namna ya kupresent na sio kusema ukila muhogo kwa siku inatosha, ukikojoa povu figo just because he met cases kama hizo kwa watu 3

Science haipo hivo and it does not entertain hizo symptomatic issues ndio maana mmewekewa maabaara to prove your hypothesis kama unachowaza kupitia pathological history taken ni sahihi
Lengo la kuelimika iwe kwa kukaa darasani, chini ya mti au vyovyote vile ni ile hali ya kumpa mtu maarifa ambayo yatamfanya abadilike kutoka hali duni kifikra na kimatendo na kuwa mtu bora, ni hali ya kuondoa au kupunguza mambo hasi ya asili anayozaliwa nayo binadamu na kubaki na yale mambo chanya pia kumuongezea mengine zaidi..Nimesoma maandiko yote aliyoandika mleta mada na kufahamu mambo kadhaa..mtu huyu ana wivu, chuki, mbishi na mjinga, pamoja na kutamka amesoma hakuwahi kufuta ujinga kabisa..bado umo kichwani.
Huhitaji kuuliza sana ili umfahamu Profesa Janabi, mambo kadhaa yako wazi kuyafahamu pale anapoongea ambayo yanamwelezea zaidi juu ya kazi yake ya kuwa Tabibu..ni mtu mjuzi wa eneo alilosomea, mpole, mwenye staha, mnyenyekevu, hana papara na mwerevu pia, hizi ni sifa za msingi kwa mtu yeyote anayetaka kazi ya kuwa Tabibu! siku hizi wapo matatibu kwa kuwa na vyeti lakini hawakupaswa kufanya kazi hii, inayotaka sana matendo na si ujuaji wa mdomoni km wa kuchambua mpira wa simba na yanga.
Mleta mada ameng'ang'ana kusema matamshi ya Profesa Janabi ni ''intimidating" kama kuambia watu ukweli ni kuwa intimidate, basi ni bora zaidi kuwaintimidate kwa aina hiyo kuliko kuwaacha wakafa kwa ujinga! ukisoma kwa kutulia mleta mada anaficha hulka ovu za kabila lake, ulevi ikiwa mojawapo...MNH ilivyo sasa ni tofauti kwa mbali na vile ilikuwa chini ya waliopita kwenye nafasi aliyo nayo Profesa Janabi.
Ni vizuri kujifunza kuangalia mambo kwa upana, kama anachotamka mtu unaona kina kunyanyapaa basi kaa kimya, sababu wapo wengine kinawasaidia sana kuokoa uhai wao, kwa mambo aliyoifanyia Tanzania na binadamu kwa ujumla kupitia fani yake ya Utabibu, utakuwa mpumbavu na punguani kusema matamshi ya Profesa Janabi hayana lengo jema kwa watu!
 
Toka baada ya mzee baba jeshi la mtu mmoja huyu dokta hajui aongee nini!.

Anazidi kupungua mwili na uzito nadhani ana stress vile hawezi kusema!.
 
Janabi yuko sahihi,mfumo wa maisha umebadilika sana hasa mijini. Watu wanakaa sehumu moja muda mrefu bila kujisogeza siku nzima huku wanashindia vitumbua, chapati na chips mayai. Angalia watu wenye viribatumbo na matukunyema walivyojazana, zamani watu karibia wote walikuwa wembamba.

Wamasai wa sasa wana shida nyingi tu za kiafya, zamani ilikuwa nadra sana kumkuta Mmasai bonge ila sasa hivi Wamasai mabonge wamejaa kila mahali.
Tuko Watanzania more than 60 million na majority wako huko vijijini. Je wewe hao unaowazungumzia ni asilimia ngapi?
 
Inaonekana unatetea sana pombe kali kuwa hazina madhara ya figo na kwenye introduction yako, haukugusa kabisa kuhusu pombe. Mm sio daktari, katika specialization hiyo, lakin ni dhahiri na shahiri kuwa pombe kali inauwa, figo. Mfano:Gardiner alikuwa anavimba mwili hizo ni dalili kuwa ana matatizo ya figounatudanganya na alikuwa mnywaji wa pombe kali. Pia nimeshudia rafiki zangu wengi wanywaji wana matatizo ya figo,kwa kuwa wanywaji wa pombe kali. Kwa hiyo ndugu kama ww ni mnywaji, na unatetea pombe kuwa haina madhara kwenye figo, unatudanganya. Jaribu, kupunguza mapenzi kwenye pombe ili uokoe maisha ya watu wengi. Halafu, hilo suala la kuongelea GPA lisikuumize, sana, kwani GPA ni uwezo wa mtu darasani. Kama ulipata GPA ndogo, hiyo ni juu yako.
Hivi JKCI huwa wanatibu magonjwa ya figo au ni Moyo??
 
Yaani mtu na akili zako uache kumsikiliza prof Janabi aliyebobea kwenye hiyo field usikilize hawa clinical officers.....
Mkuu,tunatakiwa kuwa makini sana na hawa tunao waita/tunao waona wasomi na wataalam,hasa utaalam huo unapo husiana na afya zetu.Mtoa mada ameeleza vizuri na kuonyesha mashaka yake kwa mtaalam mbobezi,prof.Janabi kuwa anaingiza siasa kwenye afya za watu,yupo sahihi.Nikukumbushe kidogo, mwaka 2020 kipindi cha janga la ugonjwa wa uviko 19,kulitangazwa kupatikana kwa chanjo ya ugonjwa huo.Wataalam wetu mbalimbali wa afya walielezea mashaka yao juu chanjo hizo, ila kuna huyu Dr.MOLEL-Naibu Waziri wa afya, aliidadavua kisayansi zaidi akidhihirisha ubobevu wake kwenye sayansi na kuonyesha mashaka namna hasara ilivyo kubwa kuliko faida na hata kuishauri serikali ya JP.MAGUFULI isiipokee hiyo chanjo.Lakini Dr.MOLEL huyo huyo [kwenye utawala huu wa SSH]alibadilika na kuisifia chanjo kuwa ni nzuri na haina madhara kama vile hakuwahi kuisemea vibaya,huku akimpongeza raisi kwa kuamua kileta chanjo.Kwaufupi tu,tunapaswa kuwa makini sana nao,tusiwaamini kirahisi tu kwa kigezo utaalam bobevu.
 
Lengo la kuelimika iwe kwa kukaa darasani, chini ya mti au vyovyote vile ni ile hali ya kumpa mtu maarifa ambayo yatamfanya abadilike kutoka hali duni kifikra na kimatendo na kuwa mtu bora, ni hali ya kuondoa au kupunguza mambo hasi ya asili anayozaliwa nayo binadamu na kubaki na yale mambo chanya pia kumuongezea mengine zaidi..Nimesoma maandiko yote aliyoandika mleta mada na kufahamu mambo kadhaa..mtu huyu ana wivu, chuki, mbishi na mjinga, pamoja na kutamka amesoma hakuwahi kufuta ujinga kabisa..bado umo kichwani.
Huhitaji kuuliza sana ili umfahamu Profesa Janabi, mambo kadhaa yako wazi kuyafahamu pale anapoongea ambayo yanamwelezea zaidi juu ya kazi yake ya kuwa Tabibu..ni mtu mjuzi wa eneo alilosomea, mpole, mwenye staha, mnyenyekevu, hana papara na mwerevu pia, hizi ni sifa za msingi kwa mtu yeyote anayetaka kazi ya kuwa Tabibu! siku hizi wapo matatibu kwa kuwa na vyeti lakini hawakupaswa kufanya kazi hii, inayotaka sana matendo na si ujuaji wa mdomoni km wa kuchambua mpira wa simba na yanga.
Mleta mada ameng'ang'ana kusema matamshi ya Profesa Janabi ni ''intimidating" kama kuambia watu ukweli ni kuwa intimidate, basi ni bora zaidi kuwaintimidate kwa aina hiyo kuliko kuwaacha wakafa kwa ujinga! ukisoma kwa kutulia mleta mada anaficha hulka ovu za kabila lake, ulevi ikiwa mojawapo...MNH ilivyo sasa ni tofauti kwa mbali na vile ilikuwa chini ya waliopita kwenye nafasi aliyo nayo Profesa Janabi.
Ni vizuri kujifunza kuangalia mambo kwa upana, kama anachotamka mtu unaona kina kunyanyapaa basi kaa kimya, sababu wapo wengine kinawasaidia sana kuokoa uhai wao, kwa mambo aliyoifanyia Tanzania na binadamu kwa ujumla kupitia fani yake ya Utabibu, utakuwa mpumbavu na punguani kusema matamshi ya Profesa Janabi hayana lengo jema kwa watu!

Kweli ni upi?
Ukweli bila facts ni Imani

Tuseme basi imani ya Janabi
 
Sijui ni kwann watu wanaoonekana wana afya au wanaofanya kazi zinazohusu mambo ya afya mara nyingi utawakuta wanaumwa magonjwa makubwa makubwa.

Tusishangae jamaa akiwa na magonjwa kama kisukari, figo, kifua kikuu n.k
Tatizo kuna elimu isiyo sahihi katika masuala ya afya tena imevishwa ngozi ya sayansi. Kuanzia masuala ya lishe, vyanzo vya maradhi n.k
 
Back
Top Bottom