Prof. Baregu: Zitto ni mzigo

Prof. Baregu: Zitto ni mzigo

Aliposema ana majina ya walioficha uswiss na atawataja na hakuuwataja hadi leo ndio nikasema hakuna mnafiki kama zito kabwe
 
Baregu naye ni miongoni mwa wazee mizigo kabisa akili zake zimenyonyoka kama nywele zake.
..........sina hakika kama ulichokisema hapa umemaanisha, na kama hivyo ndivyo, jukwaa hili sio saizi yako; pia epuka kutoa hoja kwa ushabiki, ni ushauri tu, hutaki unaacha.
 
wahaya bwana shida tu yaan mpaka akukubal labda umshinde kesi mahakamani! Hivi baregu kaifanyia nchi hii nini cha kuepuka kua mzigo hata yeye
 
Baada ya Zitto kuaga rasmi Bungeni na kutangaza kujiunga na chama kipya cha ACT-Tanzania, mwachama wa CHADEMA, Mzee Mweisigwa Baregu ameibuka na kumponda Mwanasiasa huyo kijana na machachari kuwa ni hovyo huku akikiri kuwa pamoja na Mama yake ZITTO marehemu Shida Salum(R.I.P) yeye(BAREGU) ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kumlea Zitto kisiasa.

blogger-image-1719127225-1-620x309.jpeg

Said Kubenea anaandika alichokisema Baregu:

PROFESA Mwesiga Baregu, mmoja wa watu wanaoheshimika nchini amesema, aliyepata kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, anaponzwa na kibuli cha kujiona hakuna zaidi ya yeye. Anandika Saed Kubenea … (endelea).

Amesema, Zitto ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara na naibu kiongozi wa upinzani bungeni, anafanya kazi asiyoifahamu na ambayo haina mavuno.

"Ninamfahamu vizuri. Wakati tuhuma hizi za usaliti zilipoanza kuibuka, Kamati Kuu ilinikabidhi jukumu la kumsaidia mama yake mzazi kumlea kijana huyu."

Kauli ya Baregu ilitolewa siku moja baada ya Zitto kujiondoa bungeni na baadaye kujiunga na Chama cha ACT – Tanzania.

Prof. Baregu aliwahi kuwa "mlezi wa Zitto" ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Alikabidhiwa jukumu hilo na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto (marehemu), baada ya mama huyo kuiomba Kamati Kuu (CC) ya chama hicho "kusaidia k

Ikumbukwe kuwa siku chache baada ya Mwanasheria wa CHADEMA, TUNDU ANTIPAS LISSU kutangaza kuwa Zitto siyo mwanachama wa CHADEMA kufuatia hukumu ya Mahakama, Ni MWEISIGWA BAREGU huyuhuyu alisikika kupitia shirika la habari la Ujerumani akisema kuna haja ZTTO na CHAMA chake cha CHADEMA kufikia muafaka kwa vile kuondoka kwake kutakuwa na athari kubwa kwa chama kwa vile ana watu wengi nyuma yake.

Hoja ya msingi hapa ni kuwa huenda U-HOVYO wa ZITTO unatokana na MALEZI ya HOVYO aliyoyapqta kutoka kwa MLEZI WA HOVYO.
BEREGU anapaswa kujitathmini kama anapaswa kupewa nafasi tena siku nyingine kumlea kijana kisiasa.

Source: Tanzania CLASSIC.blogspot.com
 
Hiyo deutchwelle ulisikia mwenyewe au? lakini wewe ni ccm mambo ya chadema yanakuhusu nini wewe bwabwa???
 
huku tunapoelekea na siasa zetu ni kazi.

ndio maana warioba alipendekeza sana maadili. lazima tukubali kujenga maadili na kuanzisha misingi ya kuendesha siasa za kistaarabu
 
Aliposema ana majina ya walioficha uswiss na atawataja na hakuuwataja hadi leo ndio nikasema hakuna mnafiki kama zito kabwe

List aliitoa, sema tu haikupata popularity na watu walii-criticize. Lakini nikukumbushe kitu uone jinsi Chadema ilivyo na double standards; Mbowe si alishawahi kusema ana mkanda wa bomu la Arusha unoonyesha kuwa wahusika ni police? Mbona yeye hajawahi kuutoa?
 
Bado tuu mnamimba ya Zitto? Kha!! unajua tunawashangaaa! simfanye yenu ya kuchukua dola 2015 Ingawa mnaota mchana kweupeeee "foward ever backward never"
 
List aliitoa, sema tu haikupata popularity na watu walii-criticize. Lakini nikukumbushe kitu uone jinsi Chadema ilivyo na double standards; Mbowe si alishawahi kusema ana mkanda wa bomu la Arusha unoonyesha kuwa wahusika ni police? Mbona yeye hajawahi kuutoa?

Tukumbushe pia, Mbowe aliahidi kuutoa sehemu gani kweli huo mkanda!?
 
Unaongelea ule waraka ulioandikwa na Makamba kwa jina la Wangwe?hujiulizi kwa nini muda mfupi baada ya ajali laptop ya Wangwe ilikutwa kwa Makamba?kesi ya Deus Malya ilishaje?tafuta mtu mwenye akili akusaidie kufikiri haya maana ntakuonea bure kwani una ubongo mdogo kama mbegu ya ulezi!

Mkuu achana na hii mitoto ya mafisadi, haijielewi na haijui itaishije baada ya nchi kukombolewa na utawala wa RAIA kutamalaki
 
PROFESA Mwesiga Baregu, mmoja wa watu wanaoheshimika nchini amesema, aliyepata kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, anaponzwa na kibuli cha kujiona hakuna zaidi ya yeye.

Amesema, Zitto ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara na naibu kiongozi wa upinzani bungeni, anafanya kazi asiyoifahamu na ambayo haina mavuno.

“Ninamfahamu vizuri. Wakati tuhuma hizi za usaliti zilipoanza kuibuka, Kamati Kuu ilinikabidhi jukumu la kumsaidia mama yake mzazi kumlea kijana huyu.”

Kauli ya Baregu ilitolewa siku moja baada ya Zitto kujiondoa bungeni na baadaye kujiunga na Chama cha ACT – Tanzania.

Prof. Baregu aliwahi kuwa “mlezi wa Zitto” ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Alikabidhiwa jukumu hilo na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto (marehemu), baada ya mama huyo kuiomba Kamati Kuu (CC) ya chama hicho “kusaidia kumlea.”

Prof. Baregu ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema anasema, “Zitto hamnazo. Amekuwa anajiona yeye ni zaidi ya chama. Hashauriki.”

Anasema wakati ule alipopewa kazi ya kumlea Zitto “katikakati ya migogoro, tulikuwa tunazungumza naye mara kwa mara. Ninamfahamu. Kazi hii ya kumlea tulikabidhiwa mimi na mama yake mzazi, Bi. Shida Salum,” anaeleza Baregu.

Mama mzazi wa Zitto, alifariki dunia Juni mwaka jana, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kauli ya Prof. Baregu ilifuatia gazeti hili kutaka maoni yake juu ya mustakabali wa kisiasa wa Zitto baada ya kuwahi kujiondoa ndani ya Chadema.

Acha ujinga ww mtowa post na aliesema maneno hayo
Mtumzima utamalea vp ww sumbuwa ubongo wako nawe
 
Last edited by a moderator:
List aliitoa, sema tu haikupata popularity na watu walii-criticize. Lakini nikukumbushe kitu uone jinsi Chadema ilivyo na double standards; Mbowe si alishawahi kusema ana mkanda wa bomu la Arusha unoonyesha kuwa wahusika ni police? Mbona yeye hajawahi kuutoa?

Hivi unaweza kuwapa mkanda watuhumiwa wa mauaji? kinachomwogopesha Mr dhaifu kuunda tume ya kijaji ni nini kama ccm na policcm hawahusiki? tumia kichwa kufikiri
 
Naona baregu kapagawa na kubenea kapinda
Magazeti ya udaku kama kubenea huwasisumbuku nayo hata siku 1
 
Back
Top Bottom