Mchuja Nafaka G
JF-Expert Member
- Oct 1, 2014
- 763
- 253
Mwenye Enzi Mungu atujalie afya njema na pumzi tuweze kuishi na kushuhudia safari ya Zitto Kabwe huko ACT-Wazalendo ili hatimaye atuthibitishie alikotoka walikuwa wanamchelewesha.
Mti wenye matunda ndio unatupiwa mawe.
PROFESA Mwesiga Baregu, mmoja wa watu wanaoheshimika nchini amesema, aliyepata kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, anaponzwa na kibuli cha kujiona hakuna zaidi ya yeye.
Amesema, Zitto ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara na naibu kiongozi wa upinzani bungeni, anafanya kazi asiyoifahamu na ambayo haina mavuno.
"Ninamfahamu vizuri. Wakati tuhuma hizi za usaliti zilipoanza kuibuka, Kamati Kuu ilinikabidhi jukumu la kumsaidia mama yake mzazi kumlea kijana huyu."Kauli ya Baregu ilitolewa siku moja baada ya Zitto kujiondoa bungeni na baadaye kujiunga na Chama cha ACT – Tanzania.
Prof. Baregu aliwahi kuwa "mlezi wa Zitto" ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Alikabidhiwa jukumu hilo na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto (marehemu), baada ya mama huyo kuiomba Kamati Kuu (CC) ya chama hicho "kusaidia kumlea."
Prof. Baregu ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema anasema, "Zitto hamnazo. Amekuwa anajiona yeye ni zaidi ya chama. Hashauriki."
Anasema wakati ule alipopewa kazi ya kumlea Zitto "katikakati ya migogoro, tulikuwa tunazungumza naye mara kwa mara. Ninamfahamu. Kazi hii ya kumlea tulikabidhiwa mimi na mama yake mzazi, Bi. Shida Salum," anaeleza Baregu.
Mama mzazi wa Zitto, alifariki dunia Juni mwaka jana, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kauli ya Prof. Baregu ilifuatia gazeti hili kutaka maoni yake juu ya mustakabali wa kisiasa wa Zitto baada ya kuwahi kujiondoa ndani ya Chadema.
zitto anajiamini hawezi kukubali kila kitu hasa kinachotoka kwa mjingazitto ni mzito sanaa elimu yake inamsaidia kwendea choon. Hana family hana mama nan amshauri? Mzito sana huyu kinyongaaa
Korokodio.
Kama mnasiaga kichaa hamjamuona mmoja ni huyu hapa.CHAMA cha Alliance for Change and Transparance (ACT-Tanzania) kimefanikiwa kuishawishi kwa hoja mahakama kuu ya Tanzania na kushinda katika maombi ya zuio la muda yaliyoombwa na wanachama wake Kadawi Limbu na wenzake ya kutaka mahakama Kuu itoe amri ya zuio la muda kwamba Samson Mwigamba, Peter Mwambuja na Mohamed Masaga wasijihusishe na shughuli yoyote ya Chama mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwaKutokana na kutupwa kwa zuio hilo la muda kesi ya msingi namba 21/2015 imepangwa kusikilizwa April 15 mwaka huu, huku Limbu na wenzake wakitakiwa kulipa theluthi moja ya gharama za kesi hiyoKabla ya Limbu na wenzake kuomba zuio la muda la kutaka Mwigamba na wenzake wasijishughulishe na kazi za Chama kwa nafasi ya Katibu Mkuu,Naibu katibu Mkuu na mhasibu,walifungua kesi ya msingi iliyokuwa na maombi manne1 Mahakama kuu ya Tanzania Itamke kuwa Chama cha ACT-Tanzania haina kamati kuu na Halmashauri kuu2 Mahakama kuu ya Tanzania itamke kuwa kikao halali cha viongozi wa ACT-Tanzania ni kile cha kamati kuu iliyokutana Disemba 31 mwaka jana3 Mahakama kuu itamke kuwa washitakiwa watatu Mwigamba,Masaga na Mwambuja siyo wanachama halali wa ACT-Tanzania4 Mahakama kuu iwatake washitakiwa kulipa gharama zote za kesiKwa upande wake wake Mwigamba na wenzake waliweka pingamizi la kusikilizwa kwa maombi ya zuio la muda ya Limbu na wenzake kwa hoja zifuatazo1 Walalamikaji Limbu na wenzke hawakuonyesha ni kanuni gani ya kisheria waliyotumia kuiomba mahakama itoe zuio la awali2 Kwenye hati ya mlalamikaji katika kesi ya msingi mlalamikaji namba moja ni Kadawi Lucas Limbu,lakini Kwenye hati ya kiapo ya maomb ya zuio la muda mla kiapo namba moja amejitambulisha kuwa ni ACT-Tz3 Maombi hayo yangeweza kuombwa katika mahakama ya chini badala ya mahakama kuuKufuatia hoja hizo tatu za mawakili wanaowawakilisha kina Mwigamba, wakili wa Limbu na wenzake alikiri upungufu katika hati yao ya maombi hivyo mahakama kuu chini ya Jaji J.Mwandambo ikatupilia mbali maombi ya zuio la muda na kumtaka Mlalamikaji Kulipa gharama za kesi.
CHAMA cha Alliance for Change and Transparance (ACT-Tanzania) kimefanikiwa kuishawishi kwa hoja mahakama kuu ya Tanzania na kushinda katika maombi ya zuio la muda yaliyoombwa na wanachama wake Kadawi Limbu na wenzake ya kutaka mahakama Kuu itoe amri ya zuio la muda kwamba Samson Mwigamba, Peter Mwambuja na Mohamed Masaga wasijihusishe na shughuli yoyote ya Chama mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa
Kutokana na kutupwa kwa zuio hilo la muda kesi ya msingi namba 21/2015 imepangwa kusikilizwa April 15 mwaka huu, huku Limbu na wenzake wakitakiwa kulipa theluthi moja ya gharama za kesi hiyo
Kabla ya Limbu na wenzake kuomba zuio la muda la kutaka Mwigamba na wenzake wasijishughulishe na kazi za Chama kwa nafasi ya Katibu Mkuu,Naibu katibu Mkuu na mhasibu,walifungua kesi ya msingi iliyokuwa na maombi manne
1 Mahakama kuu ya Tanzania Itamke kuwa Chama cha ACT-Tanzania haina kamati kuu na Halmashauri kuu
2 Mahakama kuu ya Tanzania itamke kuwa kikao halali cha viongozi wa ACT-Tanzania ni kile cha kamati kuu iliyokutana Disemba 31 mwaka jana
3 Mahakama kuu itamke kuwa washitakiwa watatu Mwigamba,Masaga na Mwambuja siyo wanachama halali wa ACT-Tanzania
4 Mahakama kuu iwatake washitakiwa kulipa gharama zote za kesi
Kwa upande wake wake Mwigamba na wenzake waliweka pingamizi la kusikilizwa kwa maombi ya zuio la muda ya Limbu na wenzake kwa hoja zifuatazo
1 Walalamikaji Limbu na wenzke hawakuonyesha ni kanuni gani ya kisheria waliyotumia kuiomba mahakama itoe zuio la awali
2 Kwenye hati ya mlalamikaji katika kesi ya msingi mlalamikaji namba moja ni Kadawi Lucas Limbu,lakini Kwenye hati ya kiapo ya maomb ya zuio la muda mla kiapo namba moja amejitambulisha kuwa ni ACT-Tz
3 Maombi hayo yangeweza kuombwa katika mahakama ya chini badala ya mahakama kuu
Kufuatia hoja hizo tatu za mawakili wanaowawakilisha kina Mwigamba, wakili wa Limbu na wenzake alikiri upungufu katika hati yao ya maombi hivyo mahakama kuu chini ya Jaji J.Mwandambo ikatupilia mbali maombi ya zuio la muda na kumtaka Mlalamikaji Kulipa gharama za kesi.
Baregu nae ni mzigo, hana kazi yoyote anayofanya ya maana ni profesa lakini kichwani hakuna kitu zero brain
Hapa tunazungumzia u hamnazo wa Zitto.
Kadawi Limbu ni mtu Makini Kabisa na Mwenyekiti Halali wa ACT- Wazalendo
Baregu amechukuliwa mateka na Mbowe