Prof. Baregu: Zitto ni mzigo

Prof. Baregu: Zitto ni mzigo

Baregu naye ni miongoni mwa wazee mizigo kabisa akili zake zimenyonyoka kama nywele zake.
Hivi M2 ni nani?

Mbona Prof. Baregu naye hana historia nzuri ya kulea viongozi, nakumbuka alikuwa mlezi wa Mrema kule NCCR na mambo yakawa mambo kama yalivyokuwa ndani ya NCCR. Na sasa amejinasibu kwamba alikuwa mlezi wa Zitto.

Pia amewahi kuwa mlezi wa Comrade Mugabe hadi walivyoshindanwa.
 
Kiongozi acha kumshambulia Baregu. Kwan una uhakika gani kama kayaongea yeye au maneno ya uchonganishi? Kazi ya vijana wa ufipa ya uzushi umeisahau?

Chanzo cha habari hamna. Na video kaweka ya zito kujiuzulu. Hayo maneno Baregu kayaongelea wapi?

Kazi ya kuhakikisha ukweli wa habari ni ya Moderators mkuu na kama hujui habari nyingi wamezitoa jioni hii ikiwa pamoja ni ile ya"January amjibu tena Lowasa"

Lakini hii habari ipo jamvini toka saa tisa mchana inaelea bila source na wameiacha tu so what do you expect?

Halafu unategemea hao maprofesa waliokubali kulamba viatu vya form 6 failure wanaweza kutoa maoni tofauti na ya kwenye bandiko la jamaa?

Acha tuwaambie ukweli.
 
Kazi ya kuhakikisha ukweli wa habari ni ya Moderators mkuu na kama hujui habari nyingi wamezitoa jioni hii ikiwa pamoja ni ile ya"January amjibu tena Lowasa"

Lakini hii habari ipo jamvini toka saa tisa mchana inaelea bila source na wameiacha tu so what do you expect?

Halafu unategemea hao maprofesa waliokubali kulamba viatu vya form 6 failure wanaweza kutoa maoni tofauti na ya kwenye bandiko la jamaa?

Acha tuwaambie ukweli.

ni habari kamili niliweka na source ila mods waliihariri
 
Zitto ni mzito sanaa elimu yake inamsaidia kwendea choon. Hana family Hana mama nan amshauri? Mzito sana huyu kinyongaaa

hilo la mama ondoa pamoja na madhambi yake kifo cha mama ni kazi ya mola
 
teh teh, hongereni, labda jinias wa usaliti. Kautia aibu mkoa mzima wa kigoma.

Mkuu ukombozi na usaliti ni chanda na pete, kila aliyejaribu kuleta mabadiliko huanza na safari ya kuitwa msaliti, mhaini nk

Chadema wameshajua ni kwa kiasi gani pengo la ZZK ni kubwa, na akiachwa bila kuchafuliwa atang'aa so wanajaribu kumchafua ile mbaya huku wakiungana na vyama vingine vya upinzani kuziba pengo la Zitto.

Hizi ndo siasa zetu.
 
Jinga wewe,hujui kuwa aliyepewa kazi ya kudivice formular ya kuteuwa wabunge wa viti maalum ni Prof Kitila Mkumbo?

Huyu binadamu ni wa kuhurumiwa tu,wakati mwingine post zao zinatusaidia kujua uwezo wao wa kufikiri hivyo tunapata kibali cha kuwapuuza!

We pimbi ndo wakusikitikia,hivi hujui kuwa Mbowe aliyakata majina yalipendekezwa na kuwapachika dada zake na Lissu na vilaza wa aina yake.

Tafuta waraka wa Wangwe ndo ulete tena pua yako hapa.

Halafu uache kuonea huruma wanaume.
 
Huyu mzee atakuwa Profesa wa mizizi na sio kufikiria, ukiwa Counselor wa mtu hutakiwi kutoa siri zake, kidogo tu kaanza kuropoka, zero kabisa naanza kumdharau. Ukiwa mleI haimaanishi kumchunguza mtu ili ukaseme magazetini. Zero kabisa na ndio maana anaongozwa na form four failure bila kujijua
haa haa safari hii wafuasi wa zitto mtakoma! Maana huyo bwana wenu habebeki hata huko act , asipoangalia atatimuliwa na limbu fasta.
 
Dah, tutasikia mengi kabla ya mwaka huu kuisha. Juzi kati hapa tumeambiwa jaji Werema aka "mwizi" akidai kuwa ZZK hakuwalaumu majaji walipombeba kisheria na kumfanya aendelee na ubunge wake mpaka kukaribia kuvunjwa kwa bunge la 10 walipomgeuka naye kuanza kusingizia misimamo yake juu ya sakata la escrow. Leo watu wanakuja na owongo kuwa prof makini Baregu kasema anayodaiwa kusema kuhusu ZZK; eti prof alipewa jukumu la kumlea ZZK eti hayati Shida (mamake ZZK) ndo kamtwisha prof zigo la kumlea ZZK. Sijui alipewa jukumu hilo toka lini lakini ni dhahiri kazi ilimshinda.

Hata hivyo siamini yote haya yanayosemwa kuhusu Jaji Werema na Pro Baregu. Wawili hawa wote ni binadamu walioumbwa na Mungu lakini pia, kama ilivyo kwa binadamu wengine, "wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Bwana". Wawili hawa ni watu makini ambao siamini kuwa wanaweza kuzungumza yote yanayodaowa kuwa wamezungumza kuhusu ZZK.

Nafikiri baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanatumia vibaya mitandao hii na mwaka huu wa uchaguzi mkuu si ajabu kusikia uongo mwingi kuhusu watu makini simply because watu wanapiga propaganda kwa ajili ya kuendelea kumchafua ZZK ambaye hawezi kuchafuka zaidi na wengi, isipokuwa mimi, wanaamini hawezi kusafishika tena. Historia ndiyo itakayotoa hukumu ya kweli kwa pande zote zinazopingana.

Wadau tutumie mitandao vizuri na tusipoteze muda mwingi kujadili watu (isipokuwa katika muktadha wa issues) na matatizo yao ya kisiasa na au kijamii. Tujadili issues zenye tija na hata tunapojadili watu hebu tudikomee kwenye kujadili uchafu wao ila tujikite katika kujafili namna ya kupata viongozi bora wa sasa na baadaye.
 
PROFESA Mwesiga Baregu, mmoja wa watu wanaoheshimika nchini amesema, aliyepata kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, anaponzwa na kibuli cha kujiona hakuna zaidi ya yeye.

Amesema, Zitto ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara na naibu kiongozi wa upinzani bungeni, anafanya kazi asiyoifahamu na ambayo haina mavuno.

“Ninamfahamu vizuri. Wakati tuhuma hizi za usaliti zilipoanza kuibuka, Kamati Kuu ilinikabidhi jukumu la kumsaidia mama yake mzazi kumlea kijana huyu.”

Kauli ya Baregu ilitolewa siku moja baada ya Zitto kujiondoa bungeni na baadaye kujiunga na Chama cha ACT – Tanzania.

Prof. Baregu aliwahi kuwa “mlezi wa Zitto” ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Alikabidhiwa jukumu hilo na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto (marehemu), baada ya mama huyo kuiomba Kamati Kuu (CC) ya chama hicho “kusaidia kumlea.”

Prof. Baregu ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema anasema, “Zitto hamnazo. Amekuwa anajiona yeye ni zaidi ya chama. Hashauriki.”

Anasema wakati ule alipopewa kazi ya kumlea Zitto “katikakati ya migogoro, tulikuwa tunazungumza naye mara kwa mara. Ninamfahamu. Kazi hii ya kumlea tulikabidhiwa mimi na mama yake mzazi, Bi. Shida Salum,” anaeleza Baregu.

Mama mzazi wa Zitto, alifariki dunia Juni mwaka jana, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kauli ya Prof. Baregu ilifuatia gazeti hili kutaka maoni yake juu ya mustakabali wa kisiasa wa Zitto baada ya kuwahi kujiondoa ndani ya Chadema.


Prof.Baregu, mnafiki sana mbona hakwenda kumzika mama yake Zitto kama kweli mama Zitto alimuachia hayo majukumu.
 
Last edited by a moderator:
maprofesa Wa bongo mizigo aisee. naye ameingia kwenye mipasho. TanZania bado xana . vyeti vyao inabidi vichunguzwe vizuri. ndo maana hatusongi mbele kimaendeleo kwa sababu wasomi kushindwa kufanya kazi znazowahusu
 
Angalizo kwa pro-Chadema msipokuwa makini Zitto atawafanya muwe machizi.
 
Back
Top Bottom