Precision air hii kitu vipi bhana...?!

Precision air hii kitu vipi bhana...?!

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
951
PRECISION  AIR.jpgPRECISION  AIR.jpg



Februari 24, 2011, shirika binafsi la ndege la Precesion lilizindua unifomu mpya kwa wahudumu wa ndege wa shirika hilo. Unifomu hizo zimebuniwa na kutolewa na Kampuni ya New City ya Bangkok kwa thamani ya Dalali za Kimarekani 170. 000.

Picha hapo juu ni moja ya tangazo la kuonyesha vazi hilo jipya lenye rangi ya unifomu za chama cha "magamba" ambayo unaweza kuipta katika jarida la kampuni hiyo (PAA, complementary copy, April - Jun, 2011, pg. 77). Ubunifu wa staili ya picha una haribiwa na mandhari ya nyuma ya picha hiyo (background) ambayo ni banda la mabati chakavu lenye kutu mbaya (unaweza kuona kufuli ya mlango kwa upande wa kulia) ambayo kwa mtazamo wa haraka haraka unaifanya picha husika kukosa mvuto kabisa .

Hii inaonyesha jinsi gani ambavyo wa watanzania pengine tusivyo makini hata katika mambo yanayohitaji umakini kama kujitangaza kibiashara.

Jaribuni kubadlika bandugu!.
 
Ama kweli hata zile sekata binafsi tulizokuwa tunazitegemea nazo ovyo namna hii...how can they dare kuwa na background mbaya namna hiyo. Are these guys REALLY serious in BNESS?? Utasikia tunalalamika lalamika kwamba hatupatikazi nk nk sasa mimi kweli nitaajiri ama nitamwacha kazini marketing/design whater Manager of this kind. Kama ni kampuni yangu next morning hana kazi. Huu ni ujinga!
 
Jamani,
Nyie vipi?
Hii ni picha tu, nani aliyewaeleza kuwa ni maalum kutangazia biashara?
Usikute Ngoshwe ulipewa kama zawadi na mmojawapo hapo, kisha umeibandika huku!
 
Nashanga! huyo alie ruhusu picha hiyo ibandikwe kwenye shirika kama kivutio cha biashara, hafai kuwachwa kazini hata sekunde moja. Totally irresponsible.
 
mimi nimependa sana hii picha jamaa kaweka ishara ya chadema

View attachment 30161View attachment 30161



februari 24, 2011, shirika binafsi la ndege la precesion lilizindua unifomu mpya kwa wahudumu wa ndege wa shirika hilo. Unifomu hizo zimebuniwa na kutolewa na kampuni ya new city ya bangkok kwa thamani ya dalali za kimarekani 170. 000.

Picha hapo juu ni moja ya tangazo la kuonyesha vazi hilo jipya lenye rangi ya unifomu za chama cha "magamba" ambayo unaweza kuipta katika jarida la kampuni hiyo (paa, complementary copy, april - jun, 2011, pg. 77). Ubunifu wa staili ya picha una haribiwa na manzari ya nyuma ya picha hiyo (background) ambayo ni banda la mabati chakavu lenye kutu mbaya (unaweza kuona kufuli ya mlango kwa upande wa kulia) ambayo kwa mtazamo wa haraka haraka unaifanya picha husika kukosa mvuto kabisa .

Hii inaonyesha jinsi gani ambavyo wa watanzania pengine tusivyo makini hata katika mambo yanayohitaji umakini kama kujitangaza kibiashara.

Jaribuni kubadlika bandugu!.
 
Wameshindwa hata kufanya photoshop..wabongo nuksi aisee kwa incompetence.
 
Hivi kuna binadamu yeyote duniani asiye-mind vitu vidogovidogo kama mbongo? Sijui!
 
Juzi nimesafiri nao Nairobi to Mwanza; nilishindwa kujizuia nikawauliza! Jirani yangu alikuwepo Mzungu kumbe ajua kiswahili alicheka sana!

Air hostess alijitetea sana kuwa uniform has got nothing to do with SiSiMagamba; nikamwambia kuwa sisi tusio itikadi moja na magamba hatutapanda tena! Pia hata mashabiki wa wekundu wa msimbazi watasusa!

Ila kwa ukweli hata haziwapendezi; ile rangi ya mwanzoni ilitulia kishenzi! Pia na huduma zimeshuka cancellation za kuzidi, hadi wanachefua yaani!
 
Precision Air wamechanganywa na ujio wa Fly540 in the same way CCM wanavyo changanywa na CDM.

Ni kampuni ya mtanzania mwenzetu (Mzee Shirima + co) lakini kama huduma mbovu atatuwia radhi, we are shifting to Raila Odinga's.
 
Kwa tangazo hili hawa jamaa walichemka sana.Very poor background.
 
Wewe ndio unajua kama hii ni rangi ya CCM. HIi kampuni ya watu binafsi na imejitahidi sana kupunguza adha ya usafiri wa Anga baada ya Shirika lenu la taifa kuregarega kwa ajili ya mabo ya siasa kama haya mnayotaltaka kuleta. Precission mpaka sasa inafanya vizuri. Big up sana Prec Air. Wewe ulipenda rangi gani ya Uniform wenzako hawako kisiasa wako kwenye biashara na wanafanya market research. Mbona ATC hawana uniform za rangi ya kijani lakini inayumba?
with time atajutia kuvalisha wafanya kazi rangi la ccm
 
Jamani,
Nyie vipi?
Hii ni picha tu, nani aliyewaeleza kuwa ni maalum kutangazia biashara?
Usikute Ngoshwe ulipewa kama zawadi na mmojawapo hapo, kisha umeibandika huku!
PJ hata kama lakini haina mvuto kihivyo?
 
mimi nimependa sana hii picha jamaa kaweka ishara ya chadema
hahahaaaa.... safi sana mkuu,

ila hawa jamaa wameshindwa hata kusoma alama za nyakati... angecheki hata voda wamebadili rangi...

anything kinachofanana na magamba kwa sasa hakivutii
 
Mi nimependa ishara ya CHADEMA hapo kwa selaa... ila hizo rangi za magamba zijazipenda hata kidogo
 
ukisahau kuhusu hilo tangazo, rangi yao ya sasa ni mbaya mno na haipendezi na hakukuwa na sababu ya kubuni rangi ambayo ingetia watu mashaka. Hapa precision wamechemka, uniform walizokuwa wanavaa zamani zilikuwa zimetulia sana sijui nani kawadanganya hiyo mirangi inayoumiza macho ndo mizuri. Poor choice of colours hata kama ingekuwa haimaanishi rangi ya chama au timu yoyote duniani
 
Back
Top Bottom