Precision air hii kitu vipi bhana...?!

Nyie ndio wale mnaoenda kuomba kupigia picha kwa jirani ili kuficha mazingira duni ya kwenu...... sasa wangeenda kupigia wapi wakati hiyo ndio chemba pekee inayofaa?? sioni tatiozo ka hiyo picha kibongo bongo.
 
Jamani,
Nyie vipi?
Hii ni picha tu, nani aliyewaeleza kuwa ni maalum kutangazia biashara?
Usikute Ngoshwe ulipewa kama zawadi na mmojawapo hapo, kisha umeibandika huku!

Mkuu, PJ, pata Jarida lao la April - Jun kwenye Flight , check ukurasa wa 77 utakutana na hilo tangazo la Kimagagamba limetundikwa na wanajigamba hizo jezi zimegharimu shirika kiasi cha US.Dollars 170, 0000. Sina hakika kama Makamba amepitia huko kwenda kuwaandalia Makao watu wake...najua Mrambaramba ni shareholder may be amewashawishi kuleta hii kitu...
 
Wewe ndio unajua kama hii ni rangi ya CCM. HIi kampuni ya watu binafsi na imejitahidi sana kupunguza adha ya usafiri wa Anga baada ya Shirika lenu la taifa kuregarega kwa ajili ya mabo ya siasa kama haya mnayotaltaka kuleta. Precission mpaka sasa inafanya vizuri. Big up sana Prec Air. Wewe ulipenda rangi gani ya Uniform wenzako hawako kisiasa wako kwenye biashara na wanafanya market research. Mbona ATC hawana uniform za rangi ya kijani lakini inayumba?

Sasa wamefanya market research ipi wakati wanaozikandya hizo rangi na background ndio market yenyewe? Labda walifanyia mwezini
 
View attachment 30161View attachment 30161



Februari 24, 2011, shirika binafsi la ndege la Precesion lilizindua unifomu mpya kwa wahudumu wa ndege wa shirika hilo. Unifomu hizo zimebuniwa na kutolewa na Kampuni ya New City ya Bangkok kwa thamani ya Dalali za Kimarekani 170. 000.

Picha hapo juu ni moja ya tangazo la kuonyesha vazi hilo jipya lenye rangi ya unifomu za chama cha "magamba" ambayo unaweza kuipta katika jarida la kampuni hiyo (PAA, complementary copy, April - Jun, 2011, pg. 77). Ubunifu wa staili ya picha una haribiwa na manzari ya nyuma ya picha hiyo (background) ambayo ni banda la mabati chakavu lenye kutu mbaya (unaweza kuona kufuli ya mlango kwa upande wa kulia) ambayo kwa mtazamo wa haraka haraka unaifanya picha husika kukosa mvuto kabisa .

Hii inaonyesha jinsi gani ambavyo wa watanzania pengine tusivyo makini hata katika mambo yanayohitaji umakini kama kujitangaza kibiashara.

Jaribuni kubadlika bandugu!.

Mmh sina comment maana kiswahili kwenye mtihani wa mwisho O-Level nilijitahidi na kupata G...teh..teeeh....teeeh.
 
Fire designer Magamba Kampuni, wameua shirika letu la Twiga Mnyonge **** magamba wametuzunguka mlango wa nyuma
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom