Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
- Thread starter
- #101
Mkandara, ogah, Azimio Jipya:
Nitajadili hii hoja ya maadili. Lakini nitajaribu kuachana na kuingiza maazimio ya kisiasa hili tusije tukazua midahalo ya awamu za viongozi. Na nitatumia mifano tu lakini sitakuwa na nia ya kusema azimio la Arusha au lile la Zanzibar.
Kwanza watanzania wengi wakiwemo viongozi wa juu wanaendesha shughuli za serikali au kijamii kwa kutumia hisia zao na sio kufuata sheria au kanuni.
Kwa mfano Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani aliwahi kuhamua mwanamke aliyeachwa na mumewe apewe nyumba wakati kazi ya maamuzi ni ya mahakama.
Wakati wa Sokoine. Watu walikamatwa kama wahujumu uchumi kwa kukutwa na kamera au TV. Hii peke yake inaonyesha kuwa hata pale nchi ilipokuwa na maadili mazuri vitabuni bado viongozi walitumia hisia na sio kufuata sheria za nchi.
Kwa maoni yangu binafsi, umefika wakati katiba ya nchi iwe THE SUPREME LAW OF THE LAND. Hili wananchi waweze kuwakaba viongozi na sio viongozi kutoa maamuzi yao na yakufanya kuwa ni kanuni za uongozi au za nchi.
Kiongozi yoyote anayetaka kubadilisha tabia za watanzania na kuwafanya wafuate maadili ni lazima awe "Result Oriented". Ni lazima achukue hatua na maamuzi mazito pale viongozi wanaposhindwa kutimiza majukumu yao.
Kwa mfano: Jiji la New York lilikuwa na matatizo makubwa katika miaka ya mwanzo wa 90 na kurudi nyuma. Na ilisemeka kulikuwa hakuna uwezekano wa kubadilisha mwenendo wa Jiji hilo. Lakini walipopatikana viongozi walioweka zero tolerance policy na mambo mengi waliweza kubadili fortunes za Jiji hilo.