Poverty Elimination in Tanzania is a 'Result Oriented Business'

Mkandara, ogah, Azimio Jipya:

Nitajadili hii hoja ya maadili. Lakini nitajaribu kuachana na kuingiza maazimio ya kisiasa hili tusije tukazua midahalo ya awamu za viongozi. Na nitatumia mifano tu lakini sitakuwa na nia ya kusema azimio la Arusha au lile la Zanzibar.

Kwanza watanzania wengi wakiwemo viongozi wa juu wanaendesha shughuli za serikali au kijamii kwa kutumia hisia zao na sio kufuata sheria au kanuni.

Kwa mfano Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani aliwahi kuhamua mwanamke aliyeachwa na mumewe apewe nyumba wakati kazi ya maamuzi ni ya mahakama.

Wakati wa Sokoine. Watu walikamatwa kama wahujumu uchumi kwa kukutwa na kamera au TV. Hii peke yake inaonyesha kuwa hata pale nchi ilipokuwa na maadili mazuri vitabuni bado viongozi walitumia hisia na sio kufuata sheria za nchi.

Kwa maoni yangu binafsi, umefika wakati katiba ya nchi iwe THE SUPREME LAW OF THE LAND. Hili wananchi waweze kuwakaba viongozi na sio viongozi kutoa maamuzi yao na yakufanya kuwa ni kanuni za uongozi au za nchi.

Kiongozi yoyote anayetaka kubadilisha tabia za watanzania na kuwafanya wafuate maadili ni lazima awe "Result Oriented". Ni lazima achukue hatua na maamuzi mazito pale viongozi wanaposhindwa kutimiza majukumu yao.

Kwa mfano: Jiji la New York lilikuwa na matatizo makubwa katika miaka ya mwanzo wa 90 na kurudi nyuma. Na ilisemeka kulikuwa hakuna uwezekano wa kubadilisha mwenendo wa Jiji hilo. Lakini walipopatikana viongozi walioweka zero tolerance policy na mambo mengi waliweza kubadili fortunes za Jiji hilo.
 
Mkuu wangu umenipa shibe.. yaani nimeshiba na darsa hili vizuri sana kiasi kwamba nakubaliana na wewe 100%..lakini umesahau kitu kimoja tu ambacho kipo juu ya yote haya - DIRA

Unajua binafsi yangu naamini sababu ya umaskini wetu ni kukosa DIRA..na ndilo lililosukuma sisi kupoteza hata Principals, ethic na moral values kwa sababu hatujui tunakwenda wapi.. Nothing bound us together to begin with, hata tufikie kuweka maazimio. Tatizo la umaskini wetu sii tu sisi wananchi kwa ujumla wetu ama leadership bali vyote hivi vimefikwa na mapungufu kwa sababu hatuna DIRA ya Taifa gani tunalotaka kulijenga isipokuwa taifa la kufikirika kama hadithi za vitabuni zinazosubiri kutengenezwa sinema. Tusijidanganye ya kwamba tunataka kujenga Taifa la Ujamaa na Demokrasi hii ni hadithi maana haiwezekani na wala hakuna chumi yoyote duniani unaolenga Demokrasia na Ujamaa kama malengo ya Utaifa ktk kutafuta maendeleo. HAKUNA kitu kama hicho ktk mwongozo wa Kitaifa maana huu ni UTU ambao maskini na hata tajiri wote kwa ujumla wao wanzipenda zifa hizi.

Hivyo hata maendeleo yetu yanayopatikana ni sinema tu hayana ukweli ndani yake maana hayalengi kutafuta yaliyo juu ya Umaskini, Ujinga na Maradhi maana haya ni Maazimio yetu tu ambayo kama tutafanikiwa kuyapata tutatafuta maazimio mengineyo wakati dira yetu haibadiliki. Lakini kama Taifa tunataka tuwe nini?. Sasa baada ya hapo ndipo vitu kama ethic na moral values zinapokuja in play ili tupate objective resultrs..
Kwa mfano, kwa kijana anayetaka kuwa daktari, huyu anakuwa na malengo yake toka shule na ndiyo yatamsukuma ktk dira ya kufikia kuwa Daktari japokuwa nyumbani ni maskini lakini umaskini ule hauwezi kuwa sababu yakle kuutaka Udaktari ama ili apate kufuta umaskini ni lazima awe Daktari..Hivyo atakwenda shule ku pursue Udaktari na sii umaskini na ndio itakuwa dira yake. Na maadam focus yake kubwa itakuwa kuwa daktari, basi umaskini utamwondokea siku atakapo kuwa daktari kwa sababu lengo lake halikuwa kufuta umaskini wa familia yake bali awe daktari na mengine yatajijaza yenyewe. Kama Azimio lake ni kuondokana na umaskini basi hata shule hatamaliza atajikuta anauza Nyanya au Umachinga barabarani kwa sababu hakuwa na Dira ya who he wonna be isipokuwa azimio la kuondokana na umaskini..

Hivyo basi sisi wananchi wote kwa sababu tunaweka sana matumaini ktk kuondoa Umaskini, tunafikiria Umachinga kama ndio njia rahisi na nyepesi kutokana na shida kubwa tulizonazo, tunauza madini yetu kwa bei na karanga, hatujali tunaibiwa kiasi gani ili mradi tunapeleka chakula mezani kila kukicha lakini hatufahamu 20 years from now who we wonna be..wala hatuna malengo zaidi ya kutazama umachinga huu utachukua muda gani kutuondoa ktk umaskini tofatui kabisa na nchi za Asia wao walilenga kuwa taifa la ushindani na wakawekeza ktk kujiwezesha kufikia hapa walipo na bado hawajafika wakutakako.

Mkandara,

Mimi ni mgumu wa ku-endorse DIRA. Hii ni kwa sababu viongozi wanakuwa fanatics wa mawazo yao na kuwabana watu wanapokosoa DIRA hizo.

Umetoa mfano wa Tanzania kutaka kujenga nchi ya kijamaa na kidemokrasia. Hakuna watanzania waliokuwa wanajua wanakwenda wapi na njia yenyewe ilikuwa haifahamiki.

Kutokana na idadi ya wananchi wetu, kutokana na ukubwa wake, kutokana utamaduni mbalimbali, Tanzania inatakiwa kuwa na sera zinazolenga watu na maendeleo katika maeneo yao.

Nchi inaondoka na umasikini kwa kuwa na sera. Kwani sera zina muda maalumu na zinaweza kubadilishwa kulingana na wakati. Dira ni kama dini na mara nyingi ni vague.
 
Zakumi mimi belief yangu ni kua walau kuna hope for the future kuliko huko nyuma... Nimependa huo mtazamo wako wa "Missing Link" Na nikijaribu kufikiria hapa kweli kabisa jawabu sina ila ninazo assumptions nyingi sana; which does not solve the matter. Na hii inayofanya kue na quest ya kutaka kujua quest ya what/where/why we are stagnant na kurudi nyuma Ki mantik badala ya kusongas inasukumwa na the fact kua zile nchi (hasa Asian) ambazo tulikua nazo sambamba sio wenzetu tena na sasa wanadevelop kwa kasi ya ajabu!

BTW Tunarudi kule kule.... wapi naweza pata hicho kitabu kwa uraisi?

Yeap, Tanzania's best years are ahead of us, but we still have some ground work to finish. We need to instill right mentality and stop mambo jumbo.

Kuhusu kitabu, ninaweza kukutumia sehemu yoyote ilipo. Nitaangalia kama kuna ebook.
 
What i gathered from Zakumi ni kwamba...........Result Oriented Business must follow sera husika za kipindi hicho na must be guide by the supreme law of the land............

Taifa letu pamoja na maandishi mengi mazuri yaliyomo vitabuni.....sheria/taratibu/kanuni..........tunakosa pia effectiveness ya checks and balances.........kwa sababu ya muingiliano katiika vyombo vikuu vya kiutawala......utakuta some guys in the system are so powerful such that......utendaji wa idara zingine unakuwa mikononi mwa these guys......DAMN!

tunapoelekea kwenye mchakato wa kupata katiba mpya.....hili jambo checks and balances ni la kuzingatiwa sana..........Mfano.....juzi juzi tu kuna Mwanamke mmoja kule Kenya Mkubwa sana kwenye Idara ya sheria.......alipatishwa adabu yake baada ya ku-miss behave akifikir yuko enzi zile za utawala wa akina "Jogoo".........hapa nyumbani bado.....huyu Waziri wetu wa madini Ngeleja.....alifanya vurugu akamtukana mlinzi ambaye alikuwa akifanya kazi yake....kilichotokea ni kwa mlinzi yule kuchukuliwa hatua.........

Kwanini nasema hivyo......nasema hivyo kwa sababu...ifike pahala viongozi wajue kuwa wanawajibika kwa wananchi.....meaning kuwa the ultimate responsibility ya viongozi iwe kwa wananchi na si vinginevyo..........Viongozi wetu wakiwa na uhuru wa utendaji governed by sera na law......we will get there............
Nimefanya kazi na serikali kadhaa kuanzia Africa, Europe, South & Central America na sasa North America........nimeshuhudia na kushauri mengi kuanzia dira/policies, sera, sheria, kanuni, maadili, strategies za maendeleo, mikataba nk nk nk......Tanzania na hasa viongozi hatuna ile moyo per se wa kuwajibika kwa wananchi.......
 
Ogah,

Nimekusoma vema sana!

Hapa ... "Tanzania na hasa viongozi hatuna ile moyo per se wa kuwajibika kwa wananchi ..." Inapofikia mahali pa ku adress misikumo toka kwenye mioyo ya watu mimi nakuwa makini sana. Kwani naamini kuwa kuna a huge Driving force lying dormant there (Human factor) ... na ndio ianakosekana kwenye kutoa mchango ili kujenga maendeleo ya sehemu husika. Sasa hapa ndio ningetaka uzoefu wako ... Tunaivuna vipi hiyo nguvu au huo msukomo kwa kiasi cha kutosha na kuiingiza kwenye jamii yetu ya Kitanzania? Yaani tunawafikia au kuwapata vipi hao viongozi au tuseme huu utamaduni tutaudumishaje kwa Watanzania?

Pili nini kinafanya utamaduni kama huo wa Viongozi kuwajibikia Wananchi uwepo na kudumu kwenye jamii?
 
Poverty Elimination in Tanzania is a "Result Oriented Business"......Where are we?Wakuu, mengi yenye weledi mmeyaandika.....ninachoona kwenye huu "mnakasha" ni kuwa wachangiaji wanajaribu kuainisha how efficient and/or effective hizo results zaweza kuwa katika jamii yetu hata tukafika pahala tunapopahitaji.............. Pamoja na kuwa kuna risks associated na modern technologies.......hatuhitaji ku-invent another wheel wakati technologies are readily available........due diligence inahitajika kwa vijana wetu wasomi kujua ni technologies zipi ni effective kwa mazingira yetu na ikibidi ziwe adjusted ku-suit (Chinese Government and other South East Asia Countries did a lot on these technologies).............but again/ofcourse not the detriment kwa rasilimali zetu........Community participation kwenye miradi ya maendeleo ni jambo la msingi sana, mjumbe mmoja ameandika hilo katika post zilizopita....however, community bila elimu ya kuweza ku-marry the local/indigenous knowledge and modern knowledge.....itakuwa ni tatizo........Zakumi anasema..........tunaweza tukawa na viongozi walio na maadili kama yalivyoainishwa ndani ya Azimio la Arusha na bado tusiweze kupata kile tunachotarajia...........Maendeleo yeyote yana misingi yake, Uongozi wowote una misingi yake (hata wezi wana misingi yao...joke!), Professionals wana misingi yao.....kwa hiyo suala la maadili viongozi pekee haliwezi kuleta maendeleo kama halitakuwa complemented na nyanja nyingine za maendeleo..............kuhusu Azimio la Arusha....kama sikosei......Ni Azimio Jipya/Rev Kishoka alianzisha mjadala wa kulichambua......ulikuwa mjadala mzuri.......i.e. kuboresha pale tutapoona inafaa......my point here ni kwamba.....kujadili maazimio yaliyoletwa na vyama mbali mbali si dhambi...........hata kama sisi si wanasiasa au wanachama wa vyama husika..........i mean we must start somewhere!......atleast kulikuwepo na watu waliofikiri something.......au hata kuiga....ili mradi isiwe "copy and paste"......we must do our homework right........Once again Wakuu.........heshima mbele kwa mjadala maridhawa........
OgahUmenikumbusha zamani kidogo, Nakumbuka sana ule mjadala, alianzisha Rev Kishoka mimi nilichangia sana ... na wewe? nadhani pia Mkadara nk!!Haya maazimio niliyafuatia sana kwani Mimi niliona yalikuwa na dhana ya Ethics na human value katika utendaji ... details nyingine za maazimio sio constant kulingana na wakati. ILA Kanuni ya Human ethic and Human value naamini haiwezi kupitwa na wakati na haikwepeki. Leo hii ukiingia kwenye maofisi na taasisi nyingi Tanzania ...Swala la uzembe wa Kimadili umekithiri sana na sioni namna ya kuukabili .... !!
 
Mkandara, ogah, Azimio Jipya:... Kiongozi yoyote anayetaka kubadilisha tabia za watanzania na kuwafanya wafuate maadili ni lazima awe "Result Oriented". Ni lazima achukue hatua na maamuzi mazito pale viongozi wanaposhindwa kutimiza majukumu yao.
Za Kumi!Nafikiri huu ndio msingi wa mabadiliko yanayohitajika... Naafikiana kabisa na mtizamo huu! Niongezee tu kuwa iwe ni lazima Kila kiongozi alione jambo la kubadili kitabia na kimaadili ya jamii yetu kuwa ni la msingi ikiwa na maana kuwa yeye mwenyewe awe ni mfano wa hicho anachotaka kukifanya kuonekana kwa anaowaoongoza ... Mtizamo huu niliuta kama ni nguvu ya mkono wa KULIA na "Result Oriented" Kuwa ni nguvu ya Mkono wa KUSHOTO!
 
Mkandara,

Mimi ni mgumu wa ku-endorse DIRA. Hii ni kwa sababu viongozi wanakuwa fanatics wa mawazo yao na kuwabana watu wanapokosoa DIRA hizo.

Umetoa mfano wa Tanzania kutaka kujenga nchi ya kijamaa na kidemokrasia. Hakuna watanzania waliokuwa wanajua wanakwenda wapi na njia yenyewe ilikuwa haifahamiki.

Kutokana na idadi ya wananchi wetu, kutokana na ukubwa wake, kutokana utamaduni mbalimbali, Tanzania inatakiwa kuwa na sera zinazolenga watu na maendeleo katika maeneo yao.

Nchi inaondoka na umasikini kwa kuwa na sera. Kwani sera zina muda maalumu na zinaweza kubadilishwa kulingana na wakati. Dira ni kama dini na mara nyingi ni vague.
Hapa kidogo hujanielewa. DIRA ni ya Kitaifa kama mtoto anyesema mimi nikikua nataka kuwa daktari..Halafu sera ni swala la vyama yaani kila chama kinatupa njia watakazo tumia wao ili mtoto huyo apate kuwa daktari na sisi wananchi tunachagua chama ambacho kwa kufikiria kwetu kitatufikisha kuwa njia sahihi kwa wakati huo kufikia Udaktari. Hivyo DIRA ni lazima iwepo (kama vile darasa la kwanza hadi saba, sekondary, O na A level, chuo kikuu na kadhalika hii ndio dira za elimu nchini, na na sera ni za chama ambacho kitapanga mikakati yake kutimiza sera hizo kwa wakati huo waliochaguliwa kama vile tofauti ya shule ktk mafundisho yake ama carriculum spanning mtoto kufikia Udaktari.

Through that, sisi tunakuwa na kitu kama achievement charts ambayo ina provide guidelines for assessing kila chama at work. Hivyo wakifanikisha (kufaulu kwa watoto) wanaweza chaguliwa tena wakiboronga watu wanatazama (shule) chama na sera nyinginezo japokuwa lengo bado ni kufika palepale kwenye Udaktari. Sijui kama nimejieleza vizuri maana wakati mwngine vigumu nakwama mawazo ninayo kiichwani lakini kuyaweka sawa ieleweke inanipa taabu..

Halafu ile ya Sokoine mkuu wangu umechapia kidogo kwa sababu enzi zile tulikuwa na Camera na binafsi niliinunua pale Jamhuri Street chini ya Holiday Hotel kulikuwa na duka linaitwa Corolama. Na mshikaji wangu akiitwa Spearman sasa ni Alahj Suleiman akipiga picha kabla hata Michuzi hajaingia ktk ulingo huo.. Ila TV kweli zilikuwa zikikamatwa kwa sababu ilikuwa marufuku na kisheria, kwa hiyo ukiwa nayo umevunja sheria..Kumbuka tulikuwa Wakomunist kiaina mkuu wangu ndio DIRA zenyewe hizo.
 
Ni kweli Tanzania tumefikia hapa kwa sababu ya uongozi mbovu.

Swala la kuondoa umasikini Tanzania ni kitu Raisi iwapo haya yatazingatiwa.

  1. Tutakapopata Viongozi wabunufu.( Rasilimali tulizonazo ni nyingi sana lakini mpaka leohazijayumika ipasavyo.)
  2. Tutakapopata viongozi ambao watawagusa wananchi kwa namna moja ama nyingine ili kutimiza ndoto za viongozi husika.
  3. Lazima tuwe na viongozi wenye Intergrity ,kitu ambacho leo hatunacho.
  4. Viongozi wenye Humility.
  5. Viongozi wanao weza kubuild teams. Hivi leo kuna makundi katika kila nyanja,kuanzia ngazi zote.Maeneo mengi Viongozi wamepoteza sifa ya kuleta watu pamoja.Hilinitatizo sana.
  6. Kuna tatizo la selfknowledge.Tazama mfumo wa viongozi tulionao uwezo wao wamaarifa ni wa kiwango cha chini sana.Sizungumzii elimu ya darasani bali elimu mbadala.

Lakini pamoja na yote maendeleo yoyoteuletwa na kuthubutu.(taking risk) Hatuna Viongozi ambao wakotayari kuthubutu katika kufanya maamuzi.Na kwasababu viongozi wetu hawathubutu,taifa linaishia kuwa masikini wa kutupwa.

Kwa maana hiyo Uongozi umekuwa ni sababu kubwa sana ya kutufikisha hapa tulipo.
 
Mkandara

Ilibidi nisubiri urespond kwanza ili niwe clear na alicho hoji Zakumi.

Kwani binafsi sikuwa natambua kikamilifu tofauti ya sera na dira. Mimi niliona sio tatizo sana kwani nilichukulia kuwa vyote ni "Results oriented". Lakini sasa baada ya kufafanua hapa ... nafikiri itamkidhi Zakumi ingawa mimi ninaona zote ni result oriented na vyote vikisimamiwa vema kwa Nidhamu na Uadilifu stahili vyaweza kutupa tunachotarajia.

Hapa kidogo hujanielewa. DIRA ni ya Kitaifa kama mtoto anyesema mimi nikikua nataka kuwa daktari..Halafu sera ni swala la vyama yaani kila chama kinatupa njia watakazo tumia wao ili mtoto huyo apate kuwa daktari na sisi wananchi tunachagua chama ambacho kwa kufikiria kwetu kitatufikisha kuwa njia sahihi kwa wakati huo kufikia Udaktari. Hivyo DIRA ni lazima iwepo (kama vile darasa la kwanza hadi saba, sekondary, O na A level, chuo kikuu na kadhalika hii ndio dira za elimu nchini, na na sera ni za chama ambacho kitapanga mikakati yake kutimiza sera hizo kwa wakati huo waliochaguliwa kama vile tofauti ya shule ktk mafundisho yake ama carriculum spanning mtoto kufikia Udaktari.

Through that, sisi tunakuwa na kitu kama achievement charts ambayo ina provide guidelines for assessing kila chama at work. Hivyo wakifanikisha (kufaulu kwa watoto) wanaweza chaguliwa tena wakiboronga watu wanatazama (shule) chama na sera nyinginezo japokuwa lengo bado ni kufika palepale kwenye Udaktari. Sijui kama nimejieleza vizuri maana wakati mwngine vigumu nakwama mawazo ninayo kiichwani lakini kuyaweka sawa ieleweke inanipa taabu..

Halafu ile ya Sokoine mkuu wangu umechapia kidogo kwa sababu enzi zile tulikuwa na Camera na binafsi niliinunua pale Jamhuri Street chini ya Holiday Hotel kulikuwa na duka linaitwa Corolama. Na mshikaji wangu akiitwa Spearman sasa ni Alahj Suleiman akipiga picha kabla hata Michuzi hajaingia ktk ulingo huo.. Ila TV kweli zilikuwa zikikamatwa kwa sababu ilikuwa marufuku na kisheria, kwa hiyo ukiwa nayo umevunja sheria..Kumbuka tulikuwa Wakomunist kiaina mkuu wangu ndio DIRA zenyewe hizo.

Mkandara, Zakumi!

"Dira lazima iwepo" ... haha hah! Ninahamu sana kumsikia Zakumi anasemaje!!!

Binafsi sioni tatizo ... dira ya kitaifa sio muhimu kweli?
 
Elimination? mnaongelea elimination au alleviation?

Wahindi wali project kwamba by 2012 wangeweza ku electrify India nzima, hapo wamechagua sekta moja tu. Imewabidi wajipe muda zaidi.

Lazima tuongelee specific sectors, halafu kabla hatujarukia quixotic quadratics za "poverty elimination" tuanze kutambaa na "poverty alleviation" kwanza.
 
Azimio Jipya,
Haaa haaa haa! Zakumi leo hajui msemo wasemao waswahili kwamba USIPOJUA UNAPOTOKA HUTAJUA UENDAKO una maana gani?..We don't wonna be lost in the jungle mkuu wangu... dira muhimu sana na tumeipoteza. Hata ukiwa na sera nzuri kiasi gani, nguvu kiasi gani, uadilifu kiasi gani kama unasafiri tu bila dira hujui unataka kwenda wapi basi hiyo safari itakuchukua milele na hutafika. Na ndio maana watu wanashindwa kuelewa kama leo hii tumeboreka zaidi au wakati wa Nyerere na ukiwaonmyesha takwimu wanashangaa wasiamini maana tumerudi kule tulikotoka lakini ktk mazinigra tofauti...Dira ndio vision yenyewe na ndio tatizo kubwa la Tanzania tunatazama sana sera na ilani za chama building a bridge to nowhere..

Tumeujenga mji mpya wa Dodoma viongozi hawataki kuhamia na leo Dar imejaa kiasi kwamba watu wanafanya kazi masaa sita hadi matato kwa siku, lakini baa zinafunguliwa 24 hours. Hatuna vision ya kitaifa mkuu wangu hizi sera za sijui Kilimo kwanza na viwanda pasipo kujua wananchi watalima nini ili kilimo kitukomboe, au viwanda gani tunavihitaji tutagawa mashamba kama viwanja vya watu tu kusubiri bei zipande waviuze..

Nitarudia kusema kwamba tulibinafsisha mashirika ya Umma kwa makosa kwa sababu hatukuwa na dira..Sera ya Ubinafsishaji haikuwa mbaya hata kidogo na ilikuwa results oriented lakini maadam hatukulenga mashirika hayo yanatakiwa yafanye nini tulijikuta tunauza ardhi na spareparts. Mkapa akaweza kulipa madeni na kuongeza akiba ya Taifa watu wote wakamshangilia kama rais mbora zaidi ya wote. Kumbe tulichofaidika ni sawa na Mswahili alouza nyumba yake Kariakoo akenda kupanga Ilala..
 
What i gathered from Zakumi ni kwamba...........Result Oriented Business must follow sera husika za kipindi hicho na must be guide by the supreme law of the land............

Taifa letu pamoja na maandishi mengi mazuri yaliyomo vitabuni.....sheria/taratibu/kanuni..........tunakosa pia effectiveness ya checks and balances.........kwa sababu ya muingiliano katiika vyombo vikuu vya kiutawala......utakuta some guys in the system are so powerful such that......utendaji wa idara zingine unakuwa mikononi mwa these guys......DAMN!

tunapoelekea kwenye mchakato wa kupata katiba mpya.....hili jambo checks and balances ni la kuzingatiwa sana..........Mfano.....juzi juzi tu kuna Mwanamke mmoja kule Kenya Mkubwa sana kwenye Idara ya sheria.......alipatishwa adabu yake baada ya ku-miss behave akifikir yuko enzi zile za utawala wa akina "Jogoo".........hapa nyumbani bado.....huyu Waziri wetu wa madini Ngeleja.....alifanya vurugu akamtukana mlinzi ambaye alikuwa akifanya kazi yake....kilichotokea ni kwa mlinzi yule kuchukuliwa hatua.........

Kwanini nasema hivyo......nasema hivyo kwa sababu...ifike pahala viongozi wajue kuwa wanawajibika kwa wananchi.....meaning kuwa the ultimate responsibility ya viongozi iwe kwa wananchi na si vinginevyo..........Viongozi wetu wakiwa na uhuru wa utendaji governed by sera na law......we will get there............
Nimefanya kazi na serikali kadhaa kuanzia Africa, Europe, South & Central America na sasa North America........nimeshuhudia na kushauri mengi kuanzia dira/policies, sera, sheria, kanuni, maadili, strategies za maendeleo, mikataba nk nk nk......Tanzania na hasa viongozi hatuna ile moyo per se wa kuwajibika kwa wananchi.......

Ogah,

Kwa zile information nilizonazo hakuna nchi iliyojaza makaratasi au blue prints za maendeleo barani Africa inayozidi Tanzania. Hakuna siku toka tumepata uhuru bila kuwepo na mipango ya maendeleo. Lakini kwa sababu hatuna mafanikio, tumeshajenga utamaduni wa kupanga na kutofanyia kazi.

Mfano mzuri ni tume ya rushwa ya ndugu Warioba wakati wa rais Mkapa. Baada ya kupita muda mrefu bila kuyafanyia kazi mapendekezo ya tume hiyo, maswali yaliulizwa na wapenda maendeleo. Jibu walilotoa ni kuwa CCM inayafanyia kazi mapendekezo hayo kisayansi. Majibu hayo yalitolewa na katibu mkuu wa CCM kipindi cha Mkapa.

Kama kulikuwa na sayansi ya kutokomeza rushwa, kwanini sasa tume iliundwa?
 
Ni kweli Tanzania tumefikia hapa kwa sababu ya uongozi mbovu.

Swala la kuondoa umasikini Tanzania ni kitu Raisi iwapo haya yatazingatiwa.

  1. Tutakapopata Viongozi wabunufu.( Rasilimali tulizonazo ni nyingi sana lakini mpaka leohazijayumika ipasavyo.)
  2. Tutakapopata viongozi ambao watawagusa wananchi kwa namna moja ama nyingine ili kutimiza ndoto za viongozi husika.
  3. Lazima tuwe na viongozi wenye Intergrity ,kitu ambacho leo hatunacho.
  4. Viongozi wenye Humility.
  5. Viongozi wanao weza kubuild teams. Hivi leo kuna makundi katika kila nyanja,kuanzia ngazi zote.Maeneo mengi Viongozi wamepoteza sifa ya kuleta watu pamoja.Hilinitatizo sana.
  6. Kuna tatizo la selfknowledge.Tazama mfumo wa viongozi tulionao uwezo wao wamaarifa ni wa kiwango cha chini sana.Sizungumzii elimu ya darasani bali elimu mbadala.

Lakini pamoja na yote maendeleo yoyoteuletwa na kuthubutu.(taking risk) Hatuna Viongozi ambao wakotayari kuthubutu katika kufanya maamuzi.Na kwasababu viongozi wetu hawathubutu,taifa linaishia kuwa masikini wa kutupwa.

Kwa maana hiyo Uongozi umekuwa ni sababu kubwa sana ya kutufikisha hapa tulipo.

Jphine,

Mambo yote uliyozungumza ni mazuri sana. Na katika mjadala huu nilikuwa napenda sana tufanye extension ya hoja zako mbili za mwisho.
 
Elimination? mnaongelea elimination au alleviation?

Wahindi wali project kwamba by 2012 wangeweza ku electrify India nzima, hapo wamechagua sekta moja tu. Imewabidi wajipe muda zaidi.

Lazima tuongelee specific sectors, halafu kabla hatujarukia quixotic quadratics za "poverty elimination" tuanze kutambaa na "poverty alleviation" kwanza.

Kiranga,

Sababu kubwa ya kuanzisha mjadala huu ni kumbukumbu zangu za Millennium Goals. Nchi wanachama wa UN walipanga kufuta umasikini kufikia mwaka 2015.

Imebakia miaka mitatu na kwa nchi kama Tanzania hakuna chochote cha kuonyesha zaidi ya madarasa ya sekondari za kata.

Na kwa maoni yangu binafsi, tunakwama kwa sababu we aren't result oriented nation. Pamoja na kuwa na matatizo ya uadifu katika uongozi ni lazima tujenge capabilities zingine katika masuala ya uongozi.

Tunaweza kuchagua sector inayowezekana, na yenye kutumia rasimali za nyumbani. Lakini kama tutaendelea na utamaduni wetu kuwa failure is an option hatutafika popote pale.
 
Azimio Jipya,
Haaa haaa haa! Zakumi leo hajui msemo wasemao waswahili kwamba USIPOJUA UNAPOTOKA HUTAJUA UENDAKO una maana gani?..We don't wonna be lost in the jungle mkuu wangu... dira muhimu sana na tumeipoteza. Hata ukiwa na sera nzuri kiasi gani, nguvu kiasi gani, uadilifu kiasi gani kama unasafiri tu bila dira hujui unataka kwenda wapi basi hiyo safari itakuchukua milele na hutafika. Na ndio maana watu wanashindwa kuelewa kama leo hii tumeboreka zaidi au wakati wa Nyerere na ukiwaonmyesha takwimu wanashangaa wasiamini maana tumerudi kule tulikotoka lakini ktk mazinigra tofauti...Dira ndio vision yenyewe na ndio tatizo kubwa la Tanzania tunatazama sana sera na ilani za chama building a bridge to nowhere..

Tumeujenga mji mpya wa Dodoma viongozi hawataki kuhamia na leo Dar imejaa kiasi kwamba watu wanafanya kazi masaa sita hadi matato kwa siku, lakini baa zinafunguliwa 24 hours. Hatuna vision ya kitaifa mkuu wangu hizi sera za sijui Kilimo kwanza na viwanda pasipo kujua wananchi watalima nini ili kilimo kitukomboe, au viwanda gani tunavihitaji tutagawa mashamba kama viwanja vya watu tu kusubiri bei zipande waviuze..

Nitarudia kusema kwamba tulibinafsisha mashirika ya Umma kwa makosa kwa sababu hatukuwa na dira..Sera ya Ubinafsishaji haikuwa mbaya hata kidogo na ilikuwa results oriented lakini maadam hatukulenga mashirika hayo yanatakiwa yafanye nini tulijikuta tunauza ardhi na spareparts. Mkapa akaweza kulipa madeni na kuongeza akiba ya Taifa watu wote wakamshangilia kama rais mbora zaidi ya wote. Kumbe tulichofaidika ni sawa na Mswahili alouza nyumba yake Kariakoo akenda kupanga Ilala..

Mkandara na Ogah,

Inawezekana tunakosana kwenye misamihati ya kiswahili. Dira niliichukulia kama VISION ya kiongozi. Na sera kama policy.

Kwa sasa hivi Dira kama Vision ya viongozi haitufahi kwani maendeleo ya kidunia, ya nchi, ya kijamii yana variables nyingi. Tanzania haiwezi kufuata mwelekeo mmoja wakati mambo yanabadilika kwa haraka sana. Hilo ndilo tatizo nililonalo kuhusu Dira.

Tukirudi kwenye Dira kama alivyoeleza Mkandara, nitakubaliana naye. Lakini nisingeita. Dira ningeita spirit of nation. Mtanzania awe anazaliwa na kukua huku akielewa kuwa anaweza kufanya chochote anachotaka bila kuvunja sheria. Na sheria impe nafasi ya kufanya hivyo.

Sera na utendaji wa serikali zinajenga spirit of nation. Kwa mfano utapeli wa waNigeria unatokana na kuwa serikali za kijeshi. Watanzania kupenda kuzungumza siasa inatoka na siasa zetu za miaka ya nyuma.

Tukitaka kuwa na wataalamu wanaochagua na kupenda shughuli zao au wajasiliamali, kinachotakiwa ni kubadilisha tu sera na katiba za nchi.
 
Ogah,

Kwa zile information nilizonazo hakuna nchi iliyojaza makaratasi au blue prints za maendeleo barani Africa inayozidi Tanzania. Hakuna siku toka tumepata uhuru bila kuwepo na mipango ya maendeleo. Lakini kwa sababu hatuna mafanikio, tumeshajenga utamaduni wa kupanga na kutofanyia kazi.

Mfano mzuri ni tume ya rushwa ya ndugu Warioba wakati wa rais Mkapa. Baada ya kupita muda mrefu bila kuyafanyia kazi mapendekezo ya tume hiyo, maswali yaliulizwa na wapenda maendeleo. Jibu walilotoa ni kuwa CCM inayafanyia kazi mapendekezo hayo kisayansi. Majibu hayo yalitolewa na katibu mkuu wa CCM kipindi cha Mkapa.

Kama kulikuwa na sayansi ya kutokomeza rushwa, kwanini sasa tume iliundwa?

twende mbele turudi nyuma........unajua kile kipindi JK alipoulizwa swali "...then...kwanini Tanzania ni Maskini?...."
.......ukiangalia kwa makini mjadala huu pekee na utata tulionao......pengine ndio hiyo "missing link".......wote hapa tunajikuta tume-fall kwenye jibu lile lile alilotoa Mheshimiwa Rais JK..........why then

Mikakati mizuri yote ya maendeleo tunayo
Tume mbali mbali ziliundwa ili kuwezesha mikakati hiyo na maoni ya tume yapo
Wataalamu wetu wengi wameandika weee mpaka basi.....mwingine juzi (Prof Kironde)...kaanza kusema miundo mbinu wakakti wa ukoloni ilikuwa nibora kuliko miundo mbini 50 years after uhuru
Models mbali mbali za maendeleo tumepewa,....tumepeleka wataalamu wetu wajifunze kutoka South East asia na kwingine.......

What is our problem?..........a missing link? je hi missing link ni sawa na virus wa UKIMWI?......well tuendelee na mjadala

Kiranga,

Sababu kubwa ya kuanzisha mjadala huu ni kumbukumbu zangu za Millennium Goals. Nchi wanachama wa UN walipanga kufuta umasikini kufikia mwaka 2015.

Imebakia miaka mitatu na kwa nchi kama Tanzania hakuna chochote cha kuonyesha zaidi ya madarasa ya sekondari za kata.

Na kwa maoni yangu binafsi, tunakwama kwa sababu we aren't result oriented nation. Pamoja na kuwa na matatizo ya uadifu katika uongozi ni lazima tujenge capabilities zingine katika masuala ya uongozi.

Tunaweza kuchagua sector inayowezekana, na yenye kutumia rasimali za nyumbani. Lakini kama tutaendelea na utamaduni wetu kuwa failure is an option hatutafika popote pale.

Good point!........
Binafsi nimejaribu kuangalia kwa upande wa nchi yangu na compliance ya treaties mbali mbali za UN.....ninakuta paperwise...we are very good........results-wise!....duuh.....tuendelee na mjadala
 
Mkandara na Ogah,

Inawezekana tunakosana kwenye misamihati ya kiswahili. Dira niliichukulia kama VISION ya kiongozi. Na sera kama policy.

Kwa sasa hivi Dira kama Vision ya viongozi haitufahi kwani maendeleo ya kidunia, ya nchi, ya kijamii yana variables nyingi. Tanzania haiwezi kufuata mwelekeo mmoja wakati mambo yanabadilika kwa haraka sana. Hilo ndilo tatizo nililonalo kuhusu Dira.

Tukirudi kwenye Dira kama alivyoeleza Mkandara, nitakubaliana naye. Lakini nisingeita. Dira ningeita spirit of nation. Mtanzania awe anazaliwa na kukua huku akielewa kuwa anaweza kufanya chochote anachotaka bila kuvunja sheria. Na sheria impe nafasi ya kufanya hivyo.

Sera na utendaji wa serikali zinajenga spirit of nation. Kwa mfano utapeli wa waNigeria unatokana na kuwa serikali za kijeshi. Watanzania kupenda kuzungumza siasa inatoka na siasa zetu za miaka ya nyuma.

Tukitaka kuwa na wataalamu wanaochagua na kupenda shughuli zao au wajasiliamali, kinachotakiwa ni kubadilisha tu sera na katiba za nchi.
Mkuu nitasisitiza kwamba bado hujanielewa. Taifa ni lazima liwe na dira yake kabla hujamfikia rais na vision yake kufikia yale yaliyokusudiwa. Mkuu dira ya rais inakuja tu ktk kutekeleza dira kubwa ya Kitaifa. JK leo ni kama CEO ambaye anaendesha shirika lakini mwenye mali ni sisi, hivyo lazima tuwe na vision ya Kitaifa kiasi kwamba kama CEO hakufikia malengo tunayoyataka tutamfukuza kazi na kumweka meneja mwingine. Sisi kama taifa hatuna malengo hayo tunamtegemea JK mwajiriwa wetu na CEO ndiye atueleze atajenga kitu gani.

Kwa mfano wakati wa Nyerere tulikuwa na Malengo ya kuondokana na mambo matatu nayo ni UJINGA, UMASKINI na MARADHI na kufikia mwaka 1990 tulibadilisha ama kwa kuongeza maadui wetu kufikia Nane - 8, kupitia Millenium development.. Hii ndio ilojenga DIRA ya Kitaifa naweza sema lakini ukweli ni kwamba tumefungiwa kanyaboya na IMF au hao wazungu na ndio maana Nyerere hata siku moja hakupenda kupangiwa jinsi gani tutaondokana na maadui hao ama kupata maendeleo yetu.. tulikuwa na dira yetu (compass) sisi wenyewe japokuwa wakati mbaya.

Sasa ukitazama mathlan Umaskini na maradhi, tunachokifanya ni kuukuza zaidi umaskini na maradhi kwa sababu tunapambana na adha zake (umachinga) badala ya kuwekeza ktk vyanzo vitakavyo ondosha umaskini na Maradhi. Na ndio maana nikasema mtoto aliye maskini hawezi kutafuta mbinu za kuondokana na umaskini kwa kuweka malengo ya toka mkononi hadi mdomoni, ila atatakiwa kufikiria atakuwa nani akikua halafu anapanga long term strategy ambayo itamlenga yeye kufanikiwa na sio umaskini kuondoka maana akifanikiwa yeye umaskini unaondoka automatically..Lakini kama ataweka malengo ya kuondokana na umaskini basi hata darasa la kwanza hataweza kulimaliza maana atakuwa akiuza vitu kimachinga barabarani (as short term strategy). Kwa hiyo tunaweza pata results lakini ni za muda mfupi tu.

Makosa yako wapi na kwa nini sisi maskini, labda nimjibu Ogah hapa..Picha kubwa inajionyesha kwamba Malengo yetu ni kufuta Umaskini lakini tunachofanya ni Umachinga, hivyo results tunazozipata ni za muda mfupi not sustainable, umaskini unaendelea kuwepo kama vijana wa kimachinga barabarani ambao wao wanaona wana ajira, wakiacha umachinga watakula wapi? watafanya nini?... lakini ukweli ni kwamba they are being used kuuza mali za mtu mwingine tajiri ambaye hana malengo ya kufuta umaskini maana yeye sii maskini..

Result oriented yetu ni ya kimachinga yaani kuweka mkate mezani na ndio maana wanasema mkakati huu wa millenium unalenga asilimia 33 ya maskini nchini wakitupa kazi ya Umachinga na toka 1990 hadi leo ni asimilia chini ya 2 wametoka ktk umaskini kama hawakuongezeka zaidi maana population imeongezeka maradufu. Na pia nikatoa mfano wa mh. Mkapa ktk kuyafilisi mashirika na viwanda vya Umma, mikataba mibovu, Kugawa madini yetu ili mradi tupate asilimia 3 ya ruzuku ambayo inachangia only 1.7% ya mfuko wa Taifa. Ukweli ni kwamba hata leo tukisimamisha uzalishaji wa dhahabu nchini haitakuwa na impact kubwa kwa sababu inachangia only asilimia 2 ya pato la taifa.

Tazama Elimu chini ya Millenium inalenga Achieve universal primary education.. Sasa kweli tumerudi kufikiria kusoma na kuandika kamam msingi wa dira ya Kitaifa wakati tumeshindwa kabisa kuwaandaa vijana wetu wachimbe gas, wachimbe madini, walime ukulima wa kisasa, wafungue viwanda na kadhalika, matokeo yake leo hii tuna vijana wengi waliomaliza darasa la 7, 12, 16 na University hawana kazi. Tena naweza sema walio fail kimasomo ni wengi kuliko waliofaulu na pia kati ya waliofaulu ni wengi hawana kazi kuliko wenye kazi. Hii yote haitokani na uongozi bora kwanza bali kukosa DIRA yetu sisi isipokuwa ya kufungiwa na IMF ambayo inatuweka kama machinga wanaouza vitu barabarani kwa masharti ya Mhindi mwenye duka Kariakoo..

Kama tungejiandaa ama kuwaandaa vijana wetu, rasilimali zetu na kwa kuitazama Tanzania tuitakayo mwaka 2015, toka 1990 leo hii tungekuwa tumefuta baadhi ya malengo yetu, na ukitazama kwa undani zaidi utagundua kwamba matatizo ndio yanazidi kuongezeka.. Haya ukitazama Maradhi, iwe Malaria au HIV yote tunapambana na maradhi yenyewe yanapotokea, kwa kugawa vyandarua na na madawa toka nje wakati hatupambani na vyanzo vya maradhi haya on spot. Maradhi kama Ukoma na utapia mlo yamerudi kwa kasi ya ajabu lakini hatupambani na na viini vyake ila kwa kupitia madawa ya ponya. Hatua zote za Millenium goals hazilengi DIRA nayofikiria mimi au wewe maana haiwezekani kabisa kitaifa ati Hospital hazina dawa wala vifaa vya kufanyia kazi namadaktari hawalipwi mishahara tosha lakini tunaendelea kudai tupo vitani.

Mwisho nachoweza kusema nadhani imefika wakati wadanganyika tusikubali kuendelea na Umachinga. Na binafsi yangu sioni mtu wala kiongozi mwenye guts za kusimama na kwaambia mataifa makubwa kwamba Umachinga basi, sisi tuna malengo haya na tutaweza kuyafikia kwa kufanya kdhaa wa kadhaa.. maana hii ndio dira yetu na compass tutakayotujmia kufika huko tunakotaka kwenda.. Ufisadi ni matokeo ya Umachinga kama wachinga wanavyoibiana ama kugombania wateja kama viongozi wetu na nafasi za ajira.. Kila mmoja wetu anatazama tumbo lake kwanza, tumepoteza UTU..
 
Asante sana Mkuu Bob Mkandara...........Sisi kama Watanzania tuna kila kitu......DIRA na mambo mengine....ila ilifika pahala tumeacha mambo ya DIRA na kufuata UBABAISHAJI/UMACHINGA.........tukiacha ubabaishaji......wa kuruhusu mabwana wakubwa watutumie sisi wenyewe kukwepa kulipa kodi zitakazotusaidia wenyewe......"Umachinga" kwenye biashara zenyewe, kwenye madini nk nk.........

Gari letu leo halina dereva wa kuongoza DIRA yeyote tuitakayo...........hebu ona leo nimemsoma Waziri Mkuu Pinda na mananeno yake kuhusu serikali Vs hali mbaya ya Kifedha...........yaani kauli zake zimeniudhi sana...........wakati leo hii watu wanafikiria jinsi gani ya Kupunguza/kuondoa fuel taxes......eti sisi tunabembeleza wafanyabiashara ambao wametufanya sisi WAMACHINGA.............damn!

.....ndani ya CCM ya leo.......hakuna anayeweza kusema hayo uliyoyaandika Bob........
 
Mkandara, Ogah:

Kwa hiyo Nyerere aliposema kuwa Tanzania inakabiliwa na matatizo matatu: Maradhi, Umasikini na Ujinga, tayari alitangaza DIRA za nchi? Kwa maoni yangu hayo yalikuwa mawazo yake binafsi.

Inawezekana vilevile yasiwe mawazo yake. Inawezekana yalikuwa ni mawazo ya benki ya dunia. Kwani katika sera za benki hiyo za 1968 zilisema kuwa ukiwasaidia watu wa nchi masikini kuondoa maradhi na umasikini basi watu watapata nguvu za kuondoa umasikini.

Na moja ya nchi iliyokuwa beneficiaries wa sera hizo za benki ya dunia ilikuwa Tanzania. Na matokeo yake tunatumia sana rasimali za kutoka nje kufuta ujinga na maradhi hili tuondoe umasikini.

Hivyo sioni ushujaa wowote wa kukataa masharti ya World Bank, na IMF wakati tuliwategemea katika shughuli za mwanzo za huduma za jamii na maendeleo.

Huwezi kuwa na unsustainable model ya maendeleo na baadaye unakuwa m-bishi wakati huna bargaining chip.

Na hili suala la kuwaita watanzania wajinga naona imefika kipindi tuliache. Haya ni matusi ya rejareja. Tuna mapungufu ya skills ambazo hazipatikani kwenye mazingira yetu.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom