China yapendekeza ukarabati wa reli ya TAZARA wenye thamani ya dola za Marekani bilioni moja

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG11447661393.jpg


Katika hali ya kufurahisha na kufufua matumaini, hivi karibuni balozi wa China nchini Zambia Bw. Du Xiaohui alimwambia waziri wa uchukuzi wa Zambia Bw. Frank Tayali, kuwa serikali ya China inapanga kutumia dola bilioni 1 za kimarekani kuifanyia ukarabati reli ya TAZARA, inayounganisha eneo la ukanda wa shaba la Zambia, na bandari ya Dar es salaam. Dokezo hilo la Balozi Du, limevutia ufuatiliaji mkubwa kwa wadau wa maendeleo na wale wa siasa za kimataifa.

Kwa wale wanaofuatilia mambo yanayohusu siasa za kijiografia na mivutano kati ya nchi kubwa, wanaweza kukumbuka kuwa reli ya TAZARA ni moja kati ya reli ambazo zimekuwa zikitupiwa jicho na nchi za magharibi, kwanza kabisa ilikuwa ni katika kipindi cha mapambano ya kujipatia uhuru ya nchi za kusini mwa Afrika, na pili ni baada ya reli hiyo kuonesha umuhimu mkubwa katika kipindi baada ya ukombozi, kwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza uchumi wa nchi zinazotumia reli hiyo. Lakini hivi karibuni reli hiyo imekuwa ikifuatiliwa zaidi kutokana na umuhimu wake kimkakati na kwenye siasa za kijiografia za nchi kubwa.

Kwa Tanzania na Zambia ambazo zimekuwa na uhusiano mzuri na China, ni wazi kabisa kuwa China ikiwa ni mjenzi wa reli hiyo na rafiki wa muda mrefu, si ajabu kusikia utayari wa kuihuisha reli hiyo na kuendana na mahitaji ya sasa ya kiteknoloijia na kiuchumi. Lakini pia ni muhimu kwa China kujihusisha kwa karibu kwa kuwa, tayari baadhi ya nchi za magharibi zimeonesha utayari wake wa kujipenyeza kwenye reli hiyo kwa maslahi yao yenye hila.

Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikitaja wazi kuhusu mvutano kati ya nchi kubwa duniani kutaka kudhibiti njia muhimu za biashara ya madini barani Afrika, na kutumia udhibiti huo kuongeza ushawishi wake kiuchumi na kisiasa. Nchi za magharibi ambazo kwa muda mrefu zimeziweka pembeni nchi za Afrika zimeanza kuona haya, kwa kuwa zimeachwa nyuma sana na China kwenye kuhimiza ujenzi wa miundombinu barani Afrika, na hata kujaribu kujipenyeza kwenye reli iliyojengwa na China.

Bahati mbaya iliyofanya reli ya TAZARA kudorora, ni kwamba Tanzania na Zambia ziliendelea kuichukulia reli hiyo kama reli ya uhuru, yaani kusaidia mapambano ya ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, na hazikubadilisha reli hiyo kikamilifu na kuendana na mazingira mapya ya kisiasa na kiuchumi. Kwa sasa Tanzania na Zambia zimedhamiria kuifanya reli hiyo kuwa reli ya kisasa na iendane na mazingira mapya ya kiuchumi.

Mwezi Desemba mwaka jana kikundi cha wataalam wa China kilikamilisha ukaguzi wa kibiashara na kiufundi wa reli ya TAZARA na kutoa ripoti ya tathmini, na kwamba Tanzania na Zambia ziko tayari kushirikiana na Zambia kuhuisha reli hiyo. Tayari serikali ya China imeliteua Shirika la Ujenzi wa Reli la China, kufanya mazungumzo ya makubaliano na upande wa Tanzania na Zambia kuhusu kuendesha reli hiyo kibiashara.

Pamoja na kuwa ni mapema sana kuanza kufurahia habari hii, ni vizuri tukitaja kuwa China inaendelea kufanya vizuri katika kuhimiza maendeleo ya miundombinu muhimu katika bara la Afrika. Reli mpya ya TAZARA itakuwa ni mwendelezo tu wa hatua za ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika kwenye ujenzi wa miundombinu kama ilivyofanya kwenye reli ya Abuja, Addis Ababa-Djibouti na reli ya SGR ya Kenya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom