Moyo wa kujitolea wa madaktari wa China wathaminiwa na wagonjwa waliotibiwa na kupona wa Tanzania

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
2024011781bdfd7e082149ada83a673e3729dbe2_2024011789a0aadb452e4e9f978051b0a9d26470.png


Hivi karibuni serikali ya Tanzania iliishukuru serikali ya China kwa kutuma timu za madaktari wa kwenda kusaidia kutoa huduma za afya kwa watu wa nchi hiyo. Imekuwa ni desturi ya serikali ya China kutuma timu za madaktari katika nchi za Afrika kila baada ya miaka miwili. Kupitia ushirikiano huu katika sekta ya afya, madaktari wa Tanzania wamekuwa wakinufaika sana na utaalamu wanaoupata kutoka kwa wenzao wa China.

Mkurugenzi wa huduma za tiba katika Wizara ya Afya ya Tanzania Paschal Ruggajo, amesema zaidi ya wataalamu 1,500 wa timu za madaktari za China wametumwa Tanzania katika miaka sitini iliyopita, ambapo wameweza kuokoa maisha ya Watanzania zaidi ya milioni 20 waliokuwa na magonjwa hatari, na pia kusaidia kushughulikia mapungufu mbalimbali ya kiteknolojia katika hospitali za nchi hiyo.

Kawaida madaktari wa China wanapokuwa katika nchi za Afrika, mbali na kutibu magonjwa makubwa kwa madogo, pia wanahamisha ujuzi wao kwa kutoa mafunzo kwa madaktari wenyeji. Wahenga wanasema “ni bora kumfundisha mtu kuvua kuliko kumpa samaki”. Kupitia kutoa mafunzo madaktari wengi sasa wameongeza kiwango cha ujuzi wao wa kutibu wagonjwa.

Kwa upande wa pili shukurani za wagonjwa wanaotibiwa na kupona zimekuwa zikimiminika kwa wingi wakiwashukuru madaktari wa China kwa kuwatibu na kupona kabisa. Wakati mwaka mpya wa jadi wa China ulipoanza, timu ya 27 ya madaktari wa China nchini Tanzania ilipokea barua ya shukurani kutoka kwa familia za wagonjwa wa huko.

Barua hiyo ilisema, "Asante timu ya madaktari wa China kwa matibabu na kuchangia gharama za matibabu yetu. Asanteni kwa yote mliyofanya.” Mgonjwa aliyetajwa kwenye barua hii ya kusisimua ni mwanafunzi wa shule ya msingi Ruweiss Ali Kato ambaye ana umri wa miaka minane.

Timu ya madaktari ya China inayosaidia Tanzania iligundua kwamba Kato aliugua ngiri ya kitovu ya kuzaliwa nayo wakati alipokwenda kliniki ya bure. Kwa sababu ya umaskini, hakuwa na uwezo wa matibabu, hivyo baadaye ngiri yake ikawa kubwa na kubadilika kuwa ngiri kubwa ya ukuta wa tumbo.

Chini ya msaada wa timu ya madaktari ya China, Kato alikwenda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na kutibiwa. Hivyo baada ya uchunguzi wa kina, alipangiwa mpango wa upasuaji na madaktari wa China. Kwa kuwa familia ya Kato haikuweza kumudu gharama za matibabu, madaktari wa timu ya 27 pamoja na kampuni ya ujenzi wa reli ya China iliyopo Afrika Mashariki “China Railway Construction Engineering Group East Africa” waligharamia matibabu ya mtoto Kato na hatimaye upasuaji ukaenda vizuri.

Licha ya kwamba timu hizi za madaktari zinakwenda katika nchi za Afrika kutekeleza jukumu walilotumwa na nchi yao la kutoa huduma za matibabu, lakini pia wanabeba moyo wa imani na huruma kwa watoto na wagonjwa wengine ambao hawana uwezo wa kujitibu. Imani na huruma hii kwa wagonjwa wao, inawafanya hadi wenyeji wawatake madaktari wa China kuwaita majina ya Kichina watoto wao, ili kuenzi juhudi za madaktari hawa.

Misaada ya huduma za matibabu kwa nchi za nje, siku zote imekuwa sehemu muhimu ya misaada ya nje ya China. Ikumbukwe kuwa mwaka huu sio tu kwamba China na Tanzania zinaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi, bali pia ni maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano wa matibabu kati ya China na Tanzania. Tangu Agosti 1964, timu za madaktari wa China zimeanza kutoa msaada wa kimatibabu nchini Tanzania. Mpango huu ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na China.

Kwa kuwa madaktari wa China wamepiga hatua kubwa katika matibabu ya magonjwa mbalimbali, bilashaka madaktari wa Tanzania na nchi nyingine za Afrika nao pia wataweza kuchota maarifa na ujuzi na hatimaye kuweza kuboresha zaidi uwezo wao wa kitabibu.
 
Kuna mada hapa kuhusu wachina sio watu kuchanganya mambo.ingekuwa kaja mwarabu au mzungu basi kaleta na mambo yake kama sio kulazimisha tabia zake basi imani yake
 
Back
Top Bottom