Posho na Mishahara ya wabunge...

Posho na Mishahara ya wabunge...

ccm haimpi mtu cheo kupitia JF kwa kutetea upuuzi ila endelea na jitihada za kutetea yawezekana nape akakuona ukamsaidia kutetea ulaji wa kundi flani
Mbona hiyo posho ya katibu mkuu unaitetea sana?? Au unaona ni sahihi yeye kuipata?
 
POSHO na KUJIVUA GAMBA........ ni vitu ambavyo kwa msamiati wa siasa za sasa HAUPO...!
CHADEMA WANASHINDWA KUACHA POSHO......CCM WAMESHINDWA KUJIVUA GAMBA
Ni mijadala mibovu ambayo haitaji kwa vitendo namna ya kuimarisha uchumi wa nchi na kumkomboa mwananchi HASA WA CHINI....!
WATANZANIA TUWE KITU KIMOJA ...... TUIMARIKE..... KELELE ZETU ULAJI WAO.....! AMKA,NIAMKE,TUAMKE KAMA TAIFA LENYE MWELEKEO
 
Ati waziri mkuu mzima anatetea posho za wabunge kwa kusema zinawasaidia wabunge kuzigawa kwa wapiga kura wao wanaowafuata kwa kuomba nauli mara watokapo nje ya ukumbi wa bunge. Hivi utetezi huu rahisi unafanana na mtoto wa mkulima kweli.aache kutuhadaa watanzania. yeye na watetezi wenzake wote hawana hoja za msingi zaidi ya 'ulafi' tu.
 
Wazt ni wadanganyika anajua sisi ni watu wa kulalamika tu kwa hiyo anaweza kuropoka chochote tukalalamika na asiathilike kwa chochote/lolote...............siamini km kweli alistahilio kuwa w/mkuu, nadhani ilitakiwa nafasi hiyo iwe wazi tu kwani toka akalie kiti hicho bado sijaona kilichofanyika zaidi ya kubabaisha tu na kuhadaa watz................
 
kwani nyoka anazaa mjusi?? huyu nae ni walewale, babake alishawahi kusema eti dawa ya babu wa loliondo ilikuwa kwenye ilani yao, mmmh!! simshangai zuzu mtoto.

Kaka hoja yako inaweza kuwa na mshiko lakini lugha ya kejeri na matusi inaitoa thamani. Kwani hoja haiwezi kujengwa bila kumwita kijana wa watu "zuzu"? Kwa kesi ya baba yake au udhaifu wa baba yake unamhusu nini kijana. Nayeye au wafuasi wake wakiamua kujibu kwa lugha kama yako au zaidi patakalika hapa Jamii Forum. Wanajamii tujifunze kutofautiana kwa lugha ya kistaarabu
 
Ndugu raia Fulani, sisi wananchi tuliowachagua Wabunge (Waheshimiwa) ndio Wadharauliwa, hujabaini hili ndugu. Kama kweli hawatudharau wanafanya nini cha maana ili kutusaidia sisi???? Toka Bunge la kwanza hadi leo hakuna juhudi za waziwazi kumsaidia Mdharauliwa. Kama hawatudharau unafikiri kungekua na kauli kama "Hata mkila nyasi, Ndege ya Rais itanunuliwa."

Leo umeleta hoja ya kulifuta jina la Mh. ambalo kimsingi lina wakweza bila sababu ya Msingi na kutufanya tulivae jila la Wadharauliwa. Ila mimi pia na leta hoja ya Kulifuta jina La Bunge TUKUFU. Lile Bunge letu lina UTUKUFU gani au labada mimi mafikirio yangu ni duni (ntakubali hili) kama kuna Mtu humu ndani na nje ya Jukwaa, atakapo kuja na kujaribu kuniaminisha UTUKUFU wa bunge letu.

Sina uhakika, japo kuwa nilisha acha na kufuta imani yangu kwa dini za Kigeni, ila kama neno UTUKUFU, litaacha kama lilivyo then, ntaingiwa na mashaka makubwa sana na watu wanaohusishwa na neno hilo.
 
Wazt ni wadanganyika anajua sisi ni watu wa kulalamika tu kwa hiyo anaweza kuropoka chochote tukalalamika na asiathilike kwa chochote/lolote...............siamini km kweli alistahilio kuwa w/mkuu, nadhani ilitakiwa nafasi hiyo iwe wazi tu kwani toka akalie kiti hicho bado sijaona kilichofanyika zaidi ya kubabaisha tu na kuhadaa watz................

Uko sahihi kabisa. Kama angelijua kuwa akiropoka ovyo kuna mamlaka itamshukia asingelropoka hivyo. sasa anajua kuwa yuko juu ya kila kitu hapa Tanganyika ndio maana anasema bila kutafakari. Kumbe alivyolia siku ile alikuwa anadanganya bunge lisimshukie!!!!!!!!!!!!!I cant imagine mtu aliyelia kwa kuwaonea watanzania uchungu leo anahalalisha kuwaibia watanganyika, SHAME UP On HIM!!!!!!!
 
ikishindikana kabisa kuondoa posho, CDM wachukue posho lakini zisinufaishe familia zao waanzishe clubs shule za msingi,sekondari na vyuoni kushughulikia matatizo yanayokabili makundi haya na ipendekeze cku ya jumapili au jumamosi kama siku ya kukutana na kupeana changamoto za kielimu kwa kuwashindanisha kwa mitihani na kuwafundisha haki za binnadamu,mwanafunzi;kisiasa kwa kuwajengea uwezo wa kujenga hoja na kutetea,michezo kwa kurefresh
ni wazo zuri...sisi kama CDM tutalifikiria , mie ndo ntakalo liwasilisha kwa katibu mkuu...worry not
 
Huyu nilishamukuwa crap long time anatafuta mafao yake akafie mbele hana jipya msanii
 
Ndugu raia Fulani, sisi wananchi tuliowachagua Wabunge (Waheshimiwa) ndio Wadharauliwa, hujabaini hili ndugu. Kama kweli hawatudharau wanafanya nini cha maana ili kutusaidia sisi???? Toka Bunge la kwanza hadi leo hakuna juhudi za waziwazi kumsaidia Mdharauliwa. Kama hawatudharau unafikiri kungekua na kauli kama "Hata mkila nyasi, Ndege ya Rais itanunuliwa." Leo umeleta hoja ya kulifuta jina la Mh. ambalo kimsingi lina wakweza bila sababu ya Msingi na kutufanya tulivae jila la Wadharauliwa. Ila mimi pia na leta hoja ya Kulifuta jina La Bunge TUKUFU. Lile Bunge letu lina UTUKUFU gani au labada mimi mafikirio yangu ni duni (ntakubali hili) kama kuna Mtu humu ndani na nje ya Jukwaa, atakapo kuja na kujaribu kuniaminisha UTUKUFU wa bunge letu. Sina uhakika, japo kuwa nilisha acha na kufuta imani yangu kwa dini za Kigeni, ila kama neno UTUKUFU, litaacha kama lilivyo then, ntaingiwa na mashaka makubwa sana na watu wanaohusishwa na neno hilo.
kweli mkuu. Kimsingi kinachotokea hapa ni kujikweza kulikopitiliza. Na hili la utukufu ni kashfa nyingine kwa mwananchi. Maneno yanatumika bila kumaanisha uhalisia. 'Mheshimiwa mbunge ndani ya Bunge tukufu...' kiukweli yanahitajika mabadiliko.
 
kwa mantiki hiyo basi hata salamu yetu ya kiswahili yaani SHIKAMOO!! na MARAHABA!! nayo inakuza matabaka kwani ilikuwa ni salamu ya mtumwa kwa bwana wake kwa hiyo tuwe tunasalimiana habari za asubuhu, mchana na jioni tuache yale mambo ya primary school shikamoo mwalimu!!
 
kwa mantiki hiyo basi hata salamu yetu ya kiswahili yaani SHIKAMOO!! na MARAHABA!! nayo inakuza matabaka kwani ilikuwa ni salamu ya mtumwa kwa bwana wake kwa hiyo tuwe tunasalimiana habari za asubuhu, mchana na jioni tuache yale mambo ya primary school shikamoo mwalimu!!
tutabadili mengi sana, hadi jina la nchi hii maana nasikia ni kuna jina la mtu na imani yake kwenye tanzanIA
 
Wabunge na viongozi wa serikali huitana waheshimiwa, hivyo kutulazimu kuwaita hivyo. Ni waheshimiwa kwa lipi? Kuna tofauti gani kati ya raia huyo aliyekuwa anagombea ubunge mwaka jana na mwaka huu yupo mjengoni (kariakoo)? Ana kipya kipi cha kumzidi yule ambaye aligombea nae ama yule raia aliyempigia kura? Au ni hizo posho na hiyo mikopo na mishahara minono? Hakuna tofauti. Ifike muda sasa wabunge na viongozi serikalini, pawe na sera ya kuitana NDUGU

Hakika umeniwahi nilitaka kuanzisha mada ya neno hili . Nakerwa mno na kuitwa waheshimiwa .Ugumu wa kuwaita waheshimiwa hao jamaa ndiyo ule ule ninao upata wa kumwita mtu mwenye PhD mara Prof au DR. Yaani majina yanakufa wanakuwa ni watu wa pekee huku hawana faida kwa mendeleo ya wanaishia kwenye ma title tu . Inakera sana . Mbona hao wazungu na PhD zao bado wanataka waitwe kwa majina yao kwa nini ni big deal kiasi hicho ?
 
Waswahili husema chema chajiuza... Pangekuwa na tija katika majukumu yao hakuna ambaye angehangaika kuwachokonoa hawa. Ila kwa matendo na kauli zao, huo uheshimiwa wanauonea
 
Hapana, wakati wa Nyerere kulikuwa hakuna uheshimiwa wala utukufu. Wote tuliitana NDUGU; k.m. Ndugu Mwenyekiti, ndugu rais, ndugu katibu, ndugu waziri, ndugu mbubge, e.t.c. Utukufu na uheshimiwa vilianza wakati wa mwinyi
UNACHOKIZUNGUMZA KINA UKWELI, NAKUMBUKA WAKATI WA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA KWANZA NA AWAMU YA PILI MARAIS WALIKUWA WANAITWA 'WATUKUFU':bange: LAKINI ALIPOKUJA KAKA BENI AKAKATAA KUITWA MTUKUFU NDIPO LIKAANZA 'MHESHIMIWA' :israel:KWA UPANDE WA RAIS.HIVYO HATA KWA WABUNGE INAWEZEKANA TU, MBONA KWA RAIS IMEWEZAKANA?NA IWE HIVYO
 
Kwanza nasikitika kuwa Waziri Mkuu
amerejesha suala la posho za vikao
kwenye mjadala ilhali lilimalizwa baada ya
Bungekupitisha Mpango wa maendeleo wa
miaka 5. Kitendo cha Waziri Mkuu kulilia
posho kinaonyesha jinsi asivyo tayari
kusimamia na kutetea sera za serikali
anayoongozwa. Anapaswa kuchukua
hatua mbili, ama afukuzwe kazi kwa
kwenda kinyume na maamuzi ya kisera ya
serikali yaliyopitishwa na baraza la
mawaziri na Bunge, au ajiuzulu. Hatuwezi
kuvumilia viongozi wanaokwenda
kinyume na sera za serikali.
Waziri Mkuu: Mizengo Pinda
Categories: MIZENGO PINDA, Posho
za Vikao, Tanzania, WAZIRI MKUU,
Zitto Kabwe
 
Haya wana JF,
maelezo hayo nimeiba kwenye twitter from HONS. Zitto Kabwe....
Mimi, namuunga mikono yangu miwili!
 
Back
Top Bottom