Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,252
Wabunge na viongozi wa serikali huitana waheshimiwa, hivyo kutulazimu kuwaita hivyo. Ni waheshimiwa kwa lipi? Kuna tofauti gani kati ya raia huyo aliyekuwa anagombea ubunge mwaka jana na mwaka huu yupo mjengoni (kariakoo)? Ana kipya kipi cha kumzidi yule ambaye aligombea nae ama yule raia aliyempigia kura? Au ni hizo posho na hiyo mikopo na mishahara minono? Hakuna tofauti. Ifike muda sasa wabunge na viongozi serikalini, pawe na sera ya kuitana NDUGU