Posho na Mishahara ya wabunge...

Posho na Mishahara ya wabunge...

Mi nadhani muda wa kuwa waoga inabidi uishe!! coz bajeti ya upinzani ndio bajeti ambayo itakomboa mtanzania masikini!!!hivi kwanini tunashindwa kufanya maandamano ya kudai bajeti ya upinzani ipitishwe kama bajeti kuu kwa mwaka huu wa fedha????

Tukiacha shughuli zetu na kwenda Mnazi Mmoja kudai bajeti ya ya upinzani tutapewa!!! wananunua magari ya kifahari, wanataka posho. wanataka pesa ya jimbo, pesa ya mafuta ya gari bado mshahara!!!!

Mi nadhani sisi watanzania tusipojipanga na kulishikia kidete hili suala tutakuwa wajinga kuliko hata huyo Mijengo Iliyopinda!!!

Sante Wazee
 
watanzania wa kawaida jmn tuamke,wanasiasa wanapeana pesa nyingi sn
 
Hawajajiuzulu kina ngeleja, mwinyi, mwamunyange, kikwete ndo ajiuzulu pinda?
 
Zitto Kabwe: Nasikitika kuwa W-Mkuu amerejesha suala la posho za vikao
kwenye mjadala ilhali lilimalizwa baada
ya Bunge kupitisha Mpango wa
m...aendeleo wa miaka 5.Kitendo cha
W-Mkuu kulilia posho kinaonyesha jinsi
asivyo tayari kusimamia na kutetea sera za serikali
anayoongozwa.Anapaswa kuchukua
hatua 2,ama afukuzwe kazi kwa
kwenda kinyume na maamuzi ya kisera
ya serikali yaliyopitishwa na baraza la
mawaziri na Bunge,au ajiuzul.
COMMENTS:
Juma Kh Ali W/Mkuu anadai katiba inamruhusu kutetea posho.
Hata hvyo katiba inaundwa na watu na
watu hawako tyr kuona watu 300 pale
mjengoni wanakula bl 900 kiulaini
ilhali maticha, madokta wanahaha
kusubiri vilaki vichache mwisho wa mwezi.
So km kuna sheria kandamizi si
iwekwe kapuni tuundwe
isiyokandamizi?
Km TZ inajiweza nasisi walala hoi
watupe sitting allowances
Sos Peter Anasema yeye mtoto wa mkulima sasa mbona hamtetei mkulima
mwenyewe nadhani ni waziri mkuu
kivuri maana hana maamuzi
kabisa....yupo pale kwa maslahi yake
na magamba wenzie...big up ZITTO
tupo nyuma yako kaka.
Sania Sezzy: hiyo ndo Tanzania bana, nchi inayoendeshwa kwa haki na
usawa. ngoja tuone.
Van Albert: Maskini Tanzania!!!! Kelvin Paul: pinda kapinda na atapindwishwa zaidi na sera na
mikakati mibovu ya chama chake
hawezi kuongea kitu kikanyooka
bwana aaah
Jabir Ally: Jamanniiii....watu walimuamini pinda eti MTOTO WA
MKULIMA......PINDA HAJUI HATA KAMA
KUNA MAWAZIRI WANAOISH HOTELINI
WAKATI WAANDISHI
WANAJUA.....ASHAONJA PEPO HIYO YA
UTAWALA....SO NI VIGUMU SANA KUZIKATAA POSHO....MBONA MPANGO
WA MASHANGINGI UMEMSHINDA??????
Jabir Ally: Suala la kujiuzuru lirudishe mjengoni@z.kabwe Kin Provy Ze Mhaya ila shock abzoba amefulia au kwa vle alud tena kwenye
siasa
Daniel Mwakay: Dat z politics. Mkulima hajui hata jembe ni nn cku hz. Hacmamii
alichokiamin awali bali matakwa ya
wa2 fulan. God gv us sighting eyes.
 
Nani wa kumfuta kazi Waziri Mkuu? Sio rahisi hoja ya Zitto ambayo kwanza inatoka kwa wapinzani ambao, idadi yao ni ndogo mno.Laiti ingetoka CCM,ambao nao wanamuunga mkono.Hata hivyo mwajiri wake ni Raisi,naye sidhani kama ana mpango huo.Tupende tusipende ubavu wa kumuondoa Mheshimiwa Pinda haupo kwa mazingira ya Bunge la sasa lenye Spika Makinda.
 
TAMKO JUU YA KAULI ZA WAZIRI MKUU PINDA KUHUSU POSHO

TAMKO LA KATIBU WA WABUNGE WA CHADEMA JUU YA KAULI ZA WAZIRI MKUU PINDA KUHUSU POSHO

Katibu wa Wabunge wa CHADEMA nimeshangazwa na kauli za Waziri Mkuu Mizengo Pinda alizozitoa bungeni tarehe 16 Juni 2011 wakati akijibu maswali ya papo kwa papo.
Waziri Mkuu Pinda ametoa kauli ya kuhalalisha posho za wabunge kwa hoja kwamba zinahitajika kwa ajili ya kuwapa watu wanaowaomba fedha nje ya ukumbi wa Bunge.
Waziri Mkuu Pinda anapaswa kuifuta kauli yake, kwani inapotosha majukumu ya Bunge na Wabunge wake yaliyotajwa kwenye ibara ya 63 (2) na (3) ya kuisimamia serikali, kuwakilisha wananchi, kupitisha mipango na kutunga sheria. Kauli ya Waziri Mkuu Pinda inahamasisha siasa za fadhila (patronage) katika taifa, ambazo ndizo zimetumika na CCM kupandikiza mbegu ya rushwa katika uchaguzi kwa kisingizio cha takrima.

Kadhalika kauli ya Waziri Mkuu Pinda inadhihirisha hana dhamira ya dhati ya kutekeleza kwa ukamilifu na kwa haraka maagizo ya Rais Kikwete kinyume na Katiba Ibara ya 52 (3), ambayo inamtaka atekeleze au asababishe utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.

Aidha, Waziri Mkuu Pinda ametoa kauli bungeni kuwa wabunge wengi wa CHADEMA wanazimezea mate posho hizo na kujaribu kuonyesha kwa umma kwamba hoja ya kutaka mabadiliko katika mfumo wa posho nchini ni ya wabunge wachache ndani ya CHADEMA.
Katibu wa Wabunge wa CHADEMA namtaka Waziri Mkuu Pinda aelewe kwamba suala la kutaka mabadiliko ya mfumo wa posho katika nchi yetu ni la pamoja kwa CHADEMA na natoa mwito aisome ilani ya CHADEMA kupata msingi wa msimamo huo.

Kama sehemu ya kuimarisha uchumi kwa kuondoa ubadhirifu Ilani ya CHADEMA ya Agosti 2010 kifungu cha 5.5.1 kipengele cha 5 imeeleza bayana kwa mifano kwamba serikali ya CCM imekuwa ikitenga kiwango kikubwa cha fedha kwa ajili ya posho. Mfano katika mwaka 2008/2009 Serikali ya CCM ilitenga zaidi ya shilingi bilioni 509 (Zaidi ya nusu trilioni kwa ajili ya posho mbalimbali) ambayo ilikuwa sawa na malipo ya mishahara ya mwaka mzima ya walimu 109,000. Aidha ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010 ilieleza bayana kwamba Ofisi ya Rais Jakaya Kikwete ndiyo iliyoongoza kwa kujigawia posho ya zaidi ya Bilioni 148 kwa mwaka 2009/2010 huku Bunge likijagiwia Bilioni 36 katika kipindi hicho hicho.

Kipengele cha 6 kwenye Ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010 kimeeleza bayana kwamba Serikali ya CHADEMA itaweka utaratibu ili semina, warsha, mafunzo na vikao katika taasisi mbalimbali za umma zifanyike kama sehemu ya kazi bila uwepo wa posho maalum za vikao kwa siku (Sitting Allowances).

Ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010 imefafanua kuwa lengo ni kupunguza posho hizi kwa zaidi ya asilimia 80 zikiendana na nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma kuendana na ujuzi, nafasi, wajibu ili wafanyakazi walipwe kwa haki kwa kile wanachofanya kwa haki. Uamuzi huu ungewezesha pia kuelekeza fedha zinazobaki katika miradi ya maendeleo.

Huo ndio msimamo ambao viongozi wa CHADEMA kwa umoja wetu ikiwemo wagombea wa nafasi mbalimbali tuliunadi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na kwa wabunge walioshinda wa majimbo na viti maalum ndio msimamo watakaoendelea kuusimamia ndani ya Bunge huku Chama kikihamasisha miongoni mwa jamii kwa kuunganisha nguvu ya umma. Suala hilo pia limejadiliwa katika vikao vya kamati ya wabunge ya chama na kuzingatiwa katika Bajeti Mbadala (Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/2012) ambayo imeeleza bayana namna ambavyo kiwango cha posho kimepanda kwenye bajeti ya serikali kwa ari, nguvu na kasi zaidi na kufikia takrikabani trilioni moja.

Nilitarajia kwamba baada ya Serikali ya CCM kuchukua msimamo huo na kuuingiza kwenye Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano 2011/2012-2015/2016 uliosainiwa na Rais Jakaya Kikwete tarehe 7 Juni 2011 ambao kwenye ukarasa wa 17 unatamka bayana kwamba posho za vikao na nyinginezo zinapaswa kufutwa au kuwianishwa; Waziri Mkuu angeipongeza CHADEMA na wabunge wake kwa msimamo wao badala ya kubeza na kupotosha.

Kinyume chake na siku chache baada ya kauli ya Waziri Mkuu; Serikali ambayo yeye ndiye kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 52 (2) imefanya mkakati wa kupenyeza habari ya kuupotosha umma kwa kutumia orodha na saini za wabunge za mahudhurio ya vikao sanjari na habari ya kupindisha kutaka kuupotosha umma kwamba wabunge wa CHADEMA hawana dhamira ya dhati ya kutaka posho za vikao (Sitting Allowance) ziondolewe.
Ni vizuri Waziri Mkuu Pinda na watu wanaotumika ndani ya Serikali kutaka kuichafua CHADEMA na wabunge wake waelewe kwamba ambacho wabunge wa CHADEMA tunataka kwa umoja wetu ni kurekebishwa kwa mfumo mzima wa posho kama ambavyo tumeelezea katika Ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010 na Hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Hali ya Uchumi na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/2012.

Katika kushinikiza msimamo huo kutekelezwa wabunge kwa nafsi na nafasi zao wanauhuru wa kutumia njia mbalimbali kufikia lengo hili la pamoja. Wapo walioandika barua kutaka posho zao zielekezwe katika taasisi za kimaendeleo na wapo ambao wakizielekeza fedha hizo kuchangia shughuli za maendeleo katika majimbo yao kuanzia Novemba mwaka 2010. Hata hivyo, katika kuendeleza msimamo wa pamoja ikiwa Waziri Mkuu hatafuta kauli yake ama Ofisi ya Bunge kutoa ufafanuzi ikiwemo hatua mahususi kuelezwa bungeni kuhusu serikali itakavyoanza kufanya mabadiliko katika mfumo wa posho katika utumishi wa umma wakati wa kuhitimisha mjadala wa bajeti; tutakaa kikao cha Kamati ya Wabunge wa chama (Party Caucus) kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge kifungu 109 na 110 kama sehemu ya kuweka msimamo wa pamoja kuhusu bajeti na kueleza hatua za ziada ambazo tutachukua kuhusu posho hizo za vikao (Sitting Allowance) na ubadhirifu mwingine katika serikali.

Aidha nachukua fursa hii kumtaarifu Waziri Mkuu Pinda kwamba posho ya kikao (Sitting Allowance) haijatajwa kwenye katiba wala kwenye sheria hivyo ni suala la kiutendaji ambalo yeye kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni anapaswa kuwasiliana na Spika kuharakisha taratibu za kuziondoa bila kuleta visingizio vya kikakatiba na kisheria.

Napenda umma wa watanzania ufahamu kwamba Katiba Ibara ya 73 imetamka tu kuwa wabunge watalipwa mishahara, posho na malipo mengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na bunge lakini kifungu hicho hakitaji aina ya posho wala viwango.
Aidha Sheria ya Utawala wa Bunge (National Assembly Administration Act) ya mwaka 2008 kifungu cha 19 kinataja aina ya posho ambazo zinaweza kutolewa kwa wabunge kama ambavyo Rais ataeleza kwa maandishi. Katika kipenge (d) sheria imetaja orodha (i) mpaka (iii) ya posho ambazo wabunge wanastahili kulipwa za usafiri, kujikimu na wasaidizi; katika orodha hiyo hakuna Posho ya Kikao (Sitting Allowance) ambayo inalipwa hivi sasa kwa kuwekwa kwenye akaunti za wabunge moja kwa moja na CHADEMA imetoa tamko la kutaka ifutwe mara moja kama sehemu ya mchakato wa kubadili mfumo mzima wa malipo ya posho kwa watumishi wa umma.

Kifungu 19 (d) (iv) kimempa mamlaka Rais ya kutoa posho zingine kwa wabunge kwa kadiri atakavyoelekeza; kifungu ambacho kimefanya utolewe waraka wa Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Rais wa tarehe 25 Oktoba 2010 wenye kumbukumbu na. CAB111/338/01/83 masharti ya kazi ya mbunge ambao umeeleza viwango vya posho mbalimbali ikiwemo kutoa posho ya vikao (Sitting Allowance).

Hivyo, kwa kuwa Rais Kikwete amesaini tarehe 7 Juni 2011 Mpango wa Miaka Mitano wenye kulenga kuondoa posho hizo Rais Kikwete anapaswa kufuta posho hizo haraka kwa kutoa waraka badala ya kusubiri mabadiliko ya kisheria na kikatiba kama Pinda alivyoeleza bungeni. Aidha, hatua hiyo iende sambamba Rais Kikwete kuonyesha mfano kwa kupunguza gharama za posho mbalimbali za vikao na safari za nje ambazo zinatumiwa na ikulu.

Imetolewa tarehe 19 Juni 2011 na:

John Mnyika
Katibu wa Wabunge wa CHADEMA
Na Kambi Rasmi ya Upinzani
 
Anguko la CCM LIMETIMIA,magamba kwisha habari yao wanatumia makamasi kufikiria,PINDA si kiongozi bali nikiongozi funika kombe mwanaharamu apite.
 
Naona kila mtu CDM anajitahidi kutoa tamko lake haraka haraka.
Matamko yamekuwa mtaji siyo?
 
Mmmmmh......poshooooooo
jaman twiga wanaibiwa hukooooo.....achen stori za poshooooo
 
Naona kila mtu CDM anajitahidi kutoa tamko lake haraka haraka.
Matamko yamekuwa mtaji siyo?
Gamba jipya wewe,nenda kasome shule propaganda mlizokuwa mnazifanya miaka ya nyuma kutudanganya,sasa hivi hatudanganyika,mwishoni umefika nyie CCM,mana kipi ambacho hujakielewa kwenye hiyo ARTICLE au umejivua ufahamu nini,wasalimu masaki na wahi kesho asubuhi ukachukue posho kwa NAPE kwa kazi aliyokutuma.
 
Aidha, Waziri Mkuu Pinda ametoa kauli bungeni kuwa wabunge wengi wa CHADEMA wanazimezea mate posho hizo na kujaribu kuonyesha kwa umma kwamba hoja ya kutaka mabadiliko katika mfumo wa posho nchini ni ya wabunge wachache ndani ya CHADEMA.

Japo Mnyika anajitahidi kuli-spin hili, lakini ni wazi kuwa Wabunge wengi kama sio wote kasoro Zitto wanazimezea hizi posho ndio maana mpaka sasa hawajachukua hatua yoyote ya kuzikataa kwa vitendo.

Hongera Zitto Kabwe kwa kuonyesha mfano, Mnyika na wenzako acheni porojo, kama kweli hamzitamani hizo posho matendo hukidhi haja maridhawea kuliko maneno, Zitto ameonyesha njia...
 
Japo Mnyika anajitahidi kuli-spin hili, lakini ni wazi kuwa Wabunge wengi kama sio wote kasoro Zitto wanazimezea hizi posho ndio maana mpaka sasa hawajachukua hatua yoyote ya kuzikataa kwa vitendo.Hongera Zitto Kabwe kwa kuonyesha mfano, Mnyika na wenzako acheni porojo, kama kweli hamzitamani hizo posho matendo hukidhi haja maridhawea kuliko maneno, Zitto ameonyesha njia...
Kwa taarifa yako hakuna mbunge yeyote wa cdm aliyechukua posho tangu bunge hili linza wiki jana!!
 
CCM wangekubali kuachia posho yaishe. Kuendeleza malumbano kunaonesha mapungufu makuu ya msingi:
1. wabunge wa CCM na viongozi wake walioko serikalini hawazijui sheria na hivyo wamekuwa wanaongoza nchi kwa 'mazoea' pamoja na kwamba waliapa kuongoza kwa mujibu wa sheria za nchi.

2. Hawasomi (hili ni tatizo sugu). Ni majuzi tu Rais kazinduwa mpango wa maendeleo wa miaka 5 na ndani yake posho zinatakiwa kuondelewa. Sasa inakuwaje msimamizi wa shughuli za serikali (waziri mkuu) asilijue hili? Au kipengele cha kuondoa posho kimewekwa kwa makosa? kama kimekwa kwa makosa, tunawezaje kuamini yoooote yaliyomo kwenye huo mpango nayo hayajawekwa kwa makosa? In other words huo mpango ni sahihi?

3. On moral ground: Kama Waziri mkuu anaona kuwa ni halali kwa mbunge kupokea posho kwa kuhudhuria vikao ambavyo kimsingi ni sehemu ya kazi, kwa nini asiruhusu posho kwa madaktari/wauguzi wanaofanya kazi usiku na mchana kuokoa maisha ya watanzania - tena wanafanya kazi chini ya mazingira magumu huku wakiwa wanaokoa roho za binadamu!

CCM- you cannot win on this ccm - kubalini yaishe!
 
Japo Mnyika anajitahidi kuli-spin hili, lakini ni wazi kuwa Wabunge wengi kama sio wote kasoro Zitto wanazimezea hizi posho ndio maana mpaka sasa hawajachukua hatua yoyote ya kuzikataa kwa vitendo.

Hongera Zitto Kabwe kwa kuonyesha mfano, Mnyika na wenzako acheni porojo, kama kweli hamzitamani hizo posho matendo hukidhi haja maridhawea kuliko maneno, Zitto ameonyesha njia...

Suala la msingi ni Sheria kubadilishwa ili posho ziondolewe kama JK alivyosaini Mpango wa Maendeleo! Tusije tukafanya kama Mtoto wa Mkulima alipokataa VX halafu akija PM mwingine anatumia VX, sasa hapo kimefanyika nini wandugu? Is it not one man's show?
 
Japo Mnyika anajitahidi kuli-spin hili, lakini ni wazi kuwa Wabunge wengi kama sio wote kasoro Zitto wanazimezea hizi posho ndio maana mpaka sasa hawajachukua hatua yoyote ya kuzikataa kwa vitendo.

Hongera Zitto Kabwe kwa kuonyesha mfano, Mnyika na wenzako acheni porojo, kama kweli hamzitamani hizo posho matendo hukidhi haja maridhawea kuliko maneno, Zitto ameonyesha njia...

Utakuwa Nabiii Mku Ha ha ha
 
CCM wangekubali kuachia posho yaishe. Kuendeleza malumbano kunaonesha mapungufu makuu ya msingi:
1. wabunge wa CCM na viongozi wake walioko serikalini hawazijui sheria na hivyo wamekuwa wanaongoza nchi kwa 'mazoea' pamoja na kwamba waliapa kuongoza kwa mujibu wa sheria za nchi.

2. Hawasomi (hili ni tatizo sugu). Ni majuzi tu Rais kazinduwa mpango wa maendeleo wa miaka 5 na ndani yake posho zinatakiwa kuondelewa. Sasa inakuwaje msimamizi wa shughuli za serikali (waziri mkuu) asilijue hili? Au kipengele cha kuondoa posho kimewekwa kwa makosa? kama kimekwa kwa makosa, tunawezaje kuamini yoooote yaliyomo kwenye huo mpango nayo hayajawekwa kwa makosa? In other words huo mpango ni sahihi?

3. On moral ground: Kama Waziri mkuu anaona kuwa ni halali kwa mbunge kupokea posho kwa kuhudhuria vikao ambavyo kimsingi ni sehemu ya kazi, kwa nini asiruhusu posho kwa madaktari/wauguzi wanaofanya kazi usiku na mchana kuokoa maisha ya watanzania - tena wanafanya kazi chini ya mazingira magumu huku wakiwa wanaokoa roho za binadamu!

CCM- you cannot win on this ccm - kubalini yaishe!

Mzee umeongea point tupu!
 
Japo Mnyika anajitahidi kuli-spin hili, lakini ni wazi kuwa Wabunge wengi kama sio wote kasoro Zitto wanazimezea hizi posho ndio maana mpaka sasa hawajachukua hatua yoyote ya kuzikataa kwa vitendo.

Hongera Zitto Kabwe kwa kuonyesha mfano, Mnyika na wenzako acheni porojo, kama kweli hamzitamani hizo posho matendo hukidhi haja maridhawea kuliko maneno, Zitto ameonyesha njia...

Butola,

Nashukuru kwa pongezi zako kwa Zitto na asante kwa maoni yako mengine; tamko hilo linahusu msimamo wa pamoja unaosukuma mabadiliko ya mfumo mzima ambayo ni ya muhimu zaidi kwa taifa.

Hatahivyo; kwa kuwa umenitaka nieleze matendo mahususi ambayo binafsi nimeyafanya kuhusiana na suala la posho na malipo mengine ya wabunge nakuomba rejea majibu yangu hapa: JOHN MNYIKA: Majibu kwa Maswali yenu kuhusu POSHO

Mjadala uendelee mpaka kieleweke

JJ
 
Kujiuzulu kwa Pinda ni sawa lakini kabla hajafanya hivyo, Mkulo, Ngeleja nk wajivue magamba yao!
 
MODs I sijui kwa nini hii thread iko kwenye habari mchanganyiko. Ingefaa kama ingepelekwa kwenye jukwaa la siasa maana inahusu tamko la kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu posho/response ya waziri mkuu. Tafadhali rekebisheni hili.
 
Back
Top Bottom