Pongezi za Miaka 60 ya Muungano: Twende Kwenye Muungano Kamili wa Ukweli wa Nchi Moja, Serikali Moja na Rais Mmoja? Kero Zote za Muungano Zitayeyuka!

The best way ni kuiexpose Tanganyika kutoka kwenye koti la muungano, yaan tuunde federation.

Swala la kuunda Union kwa sasa ni ngumu. Huwezi kuunda Union wakati majority ya wazanzibar wanasema wanataka Zanzibar yenye mamlaka kamili, yaani hii kitu ya Zanzibar kuwa mamlaka kamili ni very sensitive Sana, kuna wazanzibar hata ndani ya ccm wanaamini kwenye Zanzibar yenye mamlaka Ila wanaogopa tu kusema hadharani, unless kama tunataka kuwaburuza watu ili iundwe hiyo Union, mwisho wa siku watu wataishi kwa chuki kwenye mioyo kwa kuwalazimisha kitu ambacho hawakitaki.

Muungano unatakiwa uwe na Win Win situation , watu waridhiane na siyo kulazimisha Mambo.
 
Wanabodi,

Loe nchi yetu tumeadhimisha miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuwa nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muungano wetu ni muungano adimu na muungano adhimu, kwasababu hapa duniani hakuna muungano mwingine wowote kama huu muungano wetu. Ni muungano wa nchi mbili kuungana na kuunda nchi moja ya JMT, yenye nchi mbili ndani yake, Tanzania na Zanzibar, wenye marais wawili, rais wa JMT na Rais wa Zanzibar, wenye Katiba mbili, katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, wenye mabunge mawili, Bunge la JMT na Baraza la Wawakilishi, lenye mahakama mbili, mahakama kuu ya Tanzania na Mahakama kuu ya Zanzibar. Kwa maoni yangu, muungano wa aina hii kudumu kwa miaka 60, itoshe, sasa twende kwenye muungano kamili wa nchi moja, serikali moja na rais mmoja!.

Kuungana kwa TANU na ASP
Vyama vya TANU na ASP vilipoungana ile 1977, sii wengi humu walikuwa wamezaliwa!, wengi humu wamezaliwa, wameikuta CCM, hawakuikuta TANU na ASP, hivyo hawajui kwanini TANU na ASP viliungana, na viliungana ili iweje?.

Mimi ni mtu wa 60s, hivyo ile 1977, TANU na ASP zilipoungana nilikuwa darasa la tatu, kijijini Itonjanda, nikikaa kwa bibi mzaa Baba, Bibi Wakawombwe, (RIP) baada ya Baba Mzee Mayalla(RIP) kuhusika na yale mambo fulani ya Mwanza ya 1976!.

Sababu ya TANU na ASP kuungana, ni kuelekea kwenye serikali moja!. Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alisema huu muungano wa vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa chama kipya, Chama cha Mapinduzi, CCM, ni mwanzo wa safari ya kuondoka kwenye serikali mbili, kuelekea kwenye serikali moja!. Jee ndoto hii ya Mwalimu Nyerere, kwa Tanzania kuwa nchi moja ya JMT yenye serikali moja na rais mmoja, itakuja kutimia?.

Watanzania wanahitaji sana kuelimishwa kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu, tena ni Rais Samia, ndie kiongozi wa kwanza wa juu aliyetoa ruhusa watu waachwe huru kujadili muungano. Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.

Elimu ya Uraia Kuhusu Muungano wetu adimu na adhimu!.
Duniani kuna miungano ya aina mbili Kuu,

1. Miungano ya union, nchi mbili au zaidi zinaungana kuunda nchi moja. Zile nchi zote zinakufa na inazaliwa nchi moja mpya.

2. Miungano ya federation, ni nchi mbili au zaidi zinaungana na kuunda nchi moja, ila zile nchi zote zinakuwa na serikali ya muungano, Federal Government na State Government, kila nchi ina utawala wake wa ndani.

Muungano wetu ni very unique, ndio maana unaitwa muungano adimu na adhimu, kwasababu ni muungano pekee duniani ambao upande mmoja ni muungano wa union kwa nchi mbili kuungana kuunda nchi moja ya JMT, na upande wa pili ni muungano wa federation wenye serikali mbili, marais wawili, mabunge mawili na mahakama mbili.

Muungano wetu kimataifa ni muungano wa union, Tanzania kimataifa ni nchi moja ya JMT, yenye serikali moja ya JMT, chini ya rais mmoja wa JMT, ambaye ni mkuu wan chi, mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu.

Lakini Kitaifa, nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, yenye katiba mbili, katiba ya JMT, na katiba ya Zanzibar, yenye serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya Zanzibar, SMZ, yenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa Zanzibar

Mkanganyiko wa Katiba.

Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.

Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa.

Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, kimuungano ni mabadiko batili, ila, kwa vile mabadiliko hayo ni kwaajili ya Zanzibar tuu, na hayatambuliwi na katiba ya JMT, serikali ya JMT, imeamua kuyapuuza!, lakini kufuatia hizi kelele, tutapuuza mpaka lini?. Si ni bora twende kwenye serikali moja, haya yote yaishe?.

Hitimisho
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, nashauri hili la mkanganyika wa katiba kati ya katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja. Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa tumefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye nchi moja, yenye serikali moja na rais mmoja?

Hongera kwa miaka 60 ya Muungano wetu adimu na adhimu,
Sasa twende kwenye nchi moja, serikali moja na rais mmoja!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea za mwandishi kuhusu muungano na serikali moja.
tuwape tu uhuru wazanzibar wachague, wakitaka kusepa waende tena asubuhi kabisa.
 
Mkuu Yesu Anakuja , umewahi kupendwa usipopenda, ukaamua kumhurumia mpendaji, ukamkubalia kumuoa ili kumsitiri, na baada ya ndoa, ukajikuta na wewe sasa unapenda, ikitokea sasa mpendaji mara anasema hakutaki tena, ungekuwa wewe, talaka utatoa?. Niliwahi kuuliza Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?

Aliyeomba muungano ni Zanzibar,
Ili Tanganyika imsitiri
Tanganyika ikakubali
Tukaungana
Tanganyika ikapenda kufa, ikafa ikaoza, ikajifuta hadi jina la Tanganyika ikalifuta.
Kuna kumwacha tena huyu mwali?!.
Ni kufa na kuzikana!.
Muungano wetu adimu na adhimu, tutaulinda kwa gharama yoyote, milele na milele.
P
 
Ushahidi upi kuwa Zanzibar iliomba Muungano ? Au ni hadithi Za vikao vya mbege hizo ?
 
Tanzania hatuna sheria ya kura ya maoni!, serikali yetu ikitaka kufanya jambo lolote inafanya tuu bila kuwauliza wananchi wenye nchi, lakini Zanzibar, wao wanayosheria ya kura ya maoni, wakitaka kufanya jambo kubwa, wanawauliza Wazanzibari.

Tanzania ndio nchi, halafu Zanzibar ni nchi ndani ya nchi!. Zanzibar wanaweza kupiga kura ya maoni na wakaamua, tatizo ni uamuzi huo huishia Chumbe, Tanzania hatuutambui, Tanzania hatuitambui katiba ya Zanzibar, wala hatuitambui GNU!.
P.

Kama Zanzibar hamuitambui Katiba ya Zanzibar , huyo Lissu na Chadema yake wanalalamika kitu gani kutawaliwa na Mzanzibari ?
 
Sio kama Zanzibar hawaitambui katiba ya Zanzibar, ni katiba ya JMT ndio haitambui katiba ya Zanzibar lakini inawatambua Wazanzibari kama Watanzania wengine wote na wana haki zote sawa sawa ikiwemo kuwa rais wa JMT.
P
 
Kama Zanzibar hamuitambui Katiba ya Zanzibar , huyo Lissu na Chadema yake wanalalamika kitu gani kutawaliwa na Mzanzibari ?
kwa bahati mbaya au nzuri, kile amesema Lisu ndio kipi moyoni mwa Watanganyika wengi, ila wanaogopa tu, ila wangekuwa huru kuongea, ungeshangaa sana. hakuna mtu wa Bara anajua faida tunapata kuungana na zanzibar, given the treatement we receive from zanzibaris na faida wanazozipata wao kwetu wakati sisi kwao hatupati kitu. ni unahudumia mchepuko
 
Kwani Wazanzibari wanapata faida kwa kuuliwa ndugu na jamaa zetu kila uchaguzi kulazimisha kuweka vibaraka vyenu?
 
Siungi mkono hoja maana Mwl Nyerere alikwishalitolea ufafanuzi. Popote pale duniani nchi ndogo kwa ardhi na idadi ya watu inapoungana na nchi kubwa kijiografia na idadi ya watu nchi ndogo huwa na hofu ya kumezwa. Wakati tunaungana Zanzibar ilikuwa na watu 360,000 huku Tanganyika ikiwa na watu 12milioni. Lkn Zanzibar ilikuwa ni nchi kamili. Kutaka Serikali moja na Rais mmoja ni kuidogosha Zanzibar na kuifanya kuwa Mkoa sawa na Mwanza. Tunaweza kuondosha kero za Muungano bila kuidogosha Zanzibar. Kutoka kero 22 Hadi kubakia 4 ni mafanikio makubwa mno.
 
Kwani Wazanzibari wanapata faida kwa kuuliwa ndugu na jamaa zetu kila uchaguzi kulazimisha kuweka vibaraka vyenu?
kwanza mnapata exposure ya alimu,

pili, mnaajiriwa bara ili kulisha watoto wenu.

mnaruhusiwa kumiliki ardhi yeyote mpendayo.

mnateuliwa vyeo serikalini huku bara.

mnakopa ila sisi tunawalipia wakati mna TRA yenu.

vipi,niendeleee?
 
kupata hayo ndiyo mje kuwauwa ndugu na wazee wetu kila ufikapo uchaguzi na kuwaweka vibaraka wenu ??
 
kupata hayo ndiyo mje kuwauwa ndugu nz wazee wetu kila ufikapo uchaguzi na kuwaweka vibaraka wenu ??
ndio tunataka muondoke ili mkaishi peke yenu huko zanji. muondoke kigamboni na DSM na mikoani, mrudi tu kwenu, manake hakuna usawa. kwanza iweje kamkoa kenye watu 2m kajifanye kako sawa na nchi yenye watu 58m. haiji akilini. mmelishwa kila kitu lakini hamridhiki, ajira, ardhi everything hadi ulinzi ila hamridhiki.

GMfDbyWWEAApYhX.jpeg
 
Huu ndio ukweli, tena ukweli mtupu
Wanabodi,

Loe nchi yetu tumeadhimisha miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuwa nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muungano wetu ni muungano adimu na muungano adhimu, kwasababu hapa duniani hakuna muungano mwingine wowote kama huu muungano wetu. Ni muungano wa nchi mbili kuungana na kuunda nchi moja ya JMT, yenye nchi mbili ndani yake, Tanzania na Zanzibar, wenye marais wawili, rais wa JMT na Rais wa Zanzibar, wenye Katiba mbili, katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, wenye mabunge mawili, Bunge la JMT na Baraza la Wawakilishi, lenye mahakama mbili, mahakama kuu ya Tanzania na Mahakama kuu ya Zanzibar. Kwa maoni yangu, muungano wa aina hii kudumu kwa miaka 60, itoshe, sasa twende kwenye muungano kamili wa nchi moja, serikali moja na rais mmoja!.

Kuungana kwa TANU na ASP
Vyama vya TANU na ASP vilipoungana ile 1977, sii wengi humu walikuwa wamezaliwa!, wengi humu wamezaliwa, wameikuta CCM, hawakuikuta TANU na ASP, hivyo hawajui kwanini TANU na ASP viliungana, na viliungana ili iweje?.

Mimi ni mtu wa 60s, hivyo ile 1977, TANU na ASP zilipoungana nilikuwa darasa la tatu, kijijini Itonjanda, nikikaa kwa bibi mzaa Baba, Bibi Wakawombwe, (RIP) baada ya Baba Mzee Mayalla(RIP) kuhusika na yale mambo fulani ya Mwanza ya 1976!.

Sababu ya TANU na ASP kuungana, ni kuelekea kwenye serikali moja!. Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alisema huu muungano wa vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa chama kipya, Chama cha Mapinduzi, CCM, ni mwanzo wa safari ya kuondoka kwenye serikali mbili, kuelekea kwenye serikali moja!. Jee ndoto hii ya Mwalimu Nyerere, kwa Tanzania kuwa nchi moja ya JMT yenye serikali moja na rais mmoja, itakuja kutimia?.

Watanzania wanahitaji sana kuelimishwa kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu, tena ni Rais Samia, ndie kiongozi wa kwanza wa juu aliyetoa ruhusa watu waachwe huru kujadili muungano. Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.

Elimu ya Uraia Kuhusu Muungano wetu adimu na adhimu!.
Duniani kuna miungano ya aina mbili Kuu,

1. Miungano ya union, nchi mbili au zaidi zinaungana kuunda nchi moja. Zile nchi zote zinakufa na inazaliwa nchi moja mpya.

2. Miungano ya federation, ni nchi mbili au zaidi zinaungana na kuunda nchi moja, ila zile nchi zote zinakuwa na serikali ya muungano, Federal Government na State Government, kila nchi ina utawala wake wa ndani.

Muungano wetu ni very unique, ndio maana unaitwa muungano adimu na adhimu, kwasababu ni muungano pekee duniani ambao upande mmoja ni muungano wa union kwa nchi mbili kuungana kuunda nchi moja ya JMT, na upande wa pili ni muungano wa federation wenye serikali mbili, marais wawili, mabunge mawili na mahakama mbili.

Muungano wetu kimataifa ni muungano wa union, Tanzania kimataifa ni nchi moja ya JMT, yenye serikali moja ya JMT, chini ya rais mmoja wa JMT, ambaye ni mkuu wan chi, mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu.

Lakini Kitaifa, nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, yenye katiba mbili, katiba ya JMT, na katiba ya Zanzibar, yenye serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya Zanzibar, SMZ, yenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa Zanzibar

Mkanganyiko wa Katiba.

Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.

Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa.

Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, kimuungano ni mabadiko batili, ila, kwa vile mabadiliko hayo ni kwaajili ya Zanzibar tuu, na hayatambuliwi na katiba ya JMT, serikali ya JMT, imeamua kuyapuuza!, lakini kufuatia hizi kelele, tutapuuza mpaka lini?. Si ni bora twende kwenye serikali moja, haya yote yaishe?.

Hitimisho
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, nashauri hili la mkanganyika wa katiba kati ya katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja. Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa tumefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye nchi moja, yenye serikali moja na rais mmoja?

Hongera kwa miaka 60 ya Muungano wetu adimu na adhimu,
Sasa twende kwenye nchi moja, serikali moja na rais mmoja!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea za mwandishi kuhusu muungano na serikali moja.
 
ndio tunataka muondoke ili mkaishi peke yenu huko zanji. muondoke kigamboni na DSM na mikoani, mrudi tu kwenu, manake hakuna usawa. kwanza iweje kamkoa kenye watu 2m kajifanye kako sawa na nchi yenye watu 58m. haiji akilini. mmelishwa kila kitu lakini hamridhiki, ajira, ardhi everything hadi ulinzi ila hamridhiki.

View attachment 2978448

Sasa jibu swali
kupata hayo ndiyo mje kuwauwa ndugu na wazee wetu kila ufikapo uchaguzi na kuwaweka vibaraka wenu ??
 
Sasa jibu swali
kupata hayo ndiyo mje kuwauwa ndugu nz wazee wetu kila ufikapo uchaguzi na kuwaweka vibaraka wenu ??
nani ameuwa ndugu zako aisee mbona unaongea makorombwezo? haueleweki. tukisema muondoke unarukia kuwa tunauwa ndugu zako, wepi? na ninyi mbona mnatubagua tukija huko na mnaturushia mabom ya petroli?
 
Unajifanya kama huelewi namna jeshi linavyomwagwa wakati wa uchaguzi pamoja na Polisi na Usalama wa taifa wenu

Yule Mkuu wenu wa usalama Diwani alipiga kambi pale Government press .

nakuonyesha namna tunavyoteswa kila uchaguzi na vyombo vyenu vya ulinzi ili kuwaweka madarakani vibaraka wenu

View: https://www.youtube.com/watch?v=gmxrblkDnbc&t=19s
 
Back
Top Bottom