Suluhisho la Kudumu la Kero Zote za Muungano, na Dawa ya Kutibu Sumu ya Ubaguzi wa Utanganyika na Uzanzibari ni Kuwa na Serikali Moja ya JMT?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,846
114,397
Wanabodi,
20240526_101928.jpg


Kama kawa, kila nipatapo fursa, ni mwendo wa Kwa Maslahi ya Taifa kwa kwenda mbele, mada ya leo ni mada muendelezo wa wiki iliyopita kuhusu hizi chokochoko zinazoendelea za kuuchokoa huu muungano wetu adimu na adhimu kwa hoja za kibaguzi za Utanganyika na Uzanzibari, ambapo wiki iliyopita nilisema zimesababishwa na ukosefu wa elimu ya uraia kuhusu Muungano wetu Hoja za Utanganyika na Uzanzibari ni Hoja Muflis za Ujinga wa Ukosefu Elimu ya Uraia. Tuwatoe Ujinga Huu Kwa Elimu ya Uraia au Tuwaache na Ujinga Wao?

Kwa wasomaji wapya, wiki iliyopita nilizungumzia kuhusu kauli za kibaguzi za kunyoosheana vidole vya Utanganyika na Uzanzibari, nikazungumzia kuwa zinasababishwa na ukosefu wa elimu ya uraia, na kuaahidi leo nitaumalizia mjadala huu kwa kuangazia chanzo cha ubaguguzi huu na suluhisho la kudumu la kuutibu ugonjwa huu na kuondoa kabisa kwa kumaliza sumu ya ubaguzi wa Utanganyika na Uzanzibari.

Mada ya leo ni historia fupi ya chanzo cha ubaguzi huu wa Utanganyika na Uzanzibari na suluhisho la kudumu la kumaliza kabsa kero zote za Muungano, na suluhisho la kudumu na dawa ya uhakika ya kutibu kabisa hii sumu ya ubaguzi wa Utanganyika na Uzanzibari, ambayo kiukweli kabisa ni kidonge kichungu kumeza kwa wahafdhina, ila kidoge kichungu ndicho kinachotibu maradhi. Swali hapa ni jee dawa ni kuwa na serikali moja ya JMT?.

Baada ya Muungano, kwa miongo kadhaa, tumekuwa na muungano wenye maelewana mazuri licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa kwenye kero za muungano, ila moto wa Utanganyika na Uzanzibari, uliwashwa na kitendo cha Zanzibar kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu, OIC, wakati Tanzania imejinasibu ni nchi isiyo na dini, secular state.

Wabunge 55 wa Bunge la JMT, wakaunda kundi la G-55 na kuidai serikali ya Tanganyika, ili iendelee kuwa haina dini na kuiruhusu serikali ya Zanzibar kuendelea kuwa mwanachama wa OIC.

Bunge lilipitisha Azimio la kuanzisha serikali ya Tanganyika, jambo ambalo lilimuibua Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, kuwakemea wabunge, kwa Bunge kukaa kama kamati ya Chama na kuwaeleza mfumo wa serikali tatu sio sera ya CCM, hivyo hoja hiyo ya kuundwa serikali ya Tanganyika, ikafa kifo cha mende, na kuzikwa jumla.

Zanzibar ikalazimishwa kujitoa OIC, na kuahidiwa, serikali ya JMT itajiunga na OIC, kitu ambacho hakikufanyika mpaka leo. Tuko wakati huo, wahafidhina wa Zanzibar wakawa na dukuduku la chini chini kuwa Zanzibar, haikutendewa haki, hivyo wakaanza vuguvugu za kudai Zanzibar yenye mamlaka zaidi.

Aliyekuwa rais wa Zanzibar, Aboud Jumbe, akapewa ushauri wa kisheria na mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Wolfgang Dourado, wakaandaa hati za kisheria kudai Zanzibar yenye mamlaka kamili, taarifa zikafika kunakohusika, Aboud Jumbe akaitwa Dodoma, akaenda kama rais wa Zanzibar, akarejea kama rais mstaafu na kusindikizwa nyumbani kwake Mji Mwema mpaka Mungu alipomuita, Dourado aliwekwa mahala salama, taarifa iliyotolewa ilisema kumetokea kuchafuka kwa hewa ya kisiasa Zanzibar kulikopelekea Jumbe kujiuzulu urais wa Zanzibar.

Baada ya Rais Nyerere kutoka Bara, alifuatiwa na Rais Mwinyi kutoka Zanzibar, akaja Mkapa kutoka Bara, akitarajiwa anafuatiwa na rais kutoka Zanzibar, hali haikuwa hivyo, akaingia Rais Kikwete, Wazanzibari wakajiona wako marginalized wakakoleza hoja ya Uzanzibari, baada ya Rais Kikwete kufuatiwa na Rais Magufuli kutoka Bara tena, Uzanzibari ukazidi kukolezwa. Akina sisi tuliuliza Je, kunahitajika ‘affirmative action’ ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT?

Mungu akaingilia kati, kukatokea kilichotokea Machi 17, 2021 kwa Rais wa JMT kuwa ni Rais Samia kutoka Zanzibar, hoja za Utanganyika zikaanza kuibuliwa tena na wanasiasa muflis kuanza tena ubaguzi wa kunyoosheana vidole, vya Utanganyika na Uzanzibari.

Kuungana kwa TANU na ASP
Vyama vya TANU na ASP vilipoungana ile 1977, sii wengi humu walikuwa wamezaliwa!, wengi humu wamezaliwa, wameikuta CCM, hawakuikuta TANU na ASP, hivyo hawajui kwanini TANU na ASP viliungana, na viliungana ili iweje?.

Mimi ni mtu wa 60s, hivyo ile 1977, TANU na ASP zilipoungana nilikuwa darasa la tatu, kijijini Itonjanda, nikikaa kwa bibi mzaa Baba, Bibi Wakawombwe, (RIP) baada ya Baba Mzee Mayalla(RIP) kuhusika na yale mambo fulani ya Mwanza ya 1976!.

Sababu ya TANU na ASP kuungana, ni kuelekea kwenye serikali moja!. Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alisema huu muungano wa vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa chama kipya, Chama cha Mapinduzi, CCM, ni mwanzo wa safari ya kuondoka kwenye serikali mbili, kuelekea kwenye serikali moja!. Jee ndoto hii ya Mwalimu Nyerere, kwa Tanzania kuwa nchi moja ya JMT yenye serikali moja na rais mmoja, itakuja kutimia?.

Watanzania wanahitaji sana kuelimishwa kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu, tena ni Rais Samia, ndie kiongozi wa kwanza wa juu aliyetoa ruhusa watu waachwe huru kujadili muungano. Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.

Mkanganyiko wa Katiba.
Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.

Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa.

Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, kimuungano ni mabadiko batili, ila, kwa vile mabadiliko hayo ni kwaajili ya Zanzibar tuu, na hayatambuliwi na katiba ya JMT, serikali ya JMT, imeamua kuyapuuza!, lakini kufuatia hizi kelele, tutapuuza mpaka lini?. Si ni bora twende kwenye serikali moja, haya yote yaishe?.

Hitimisho
Kwa vile Rais Samia, sio tuu anakwenda kutupatia katiba mpya, bali ndiye aliyeruhusu watu waachwe waujadili muungano "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Mimi kwa upande wangu, nashauri hili la mkanganyika wa katiba kati ya katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, pia litarekebishwa, ama kwa katiba ya muungano kulazimishwa kuitambua katiba ya Zanzibar, ama katiba ya Zanzibar kulazimishwa kuuondoa uhaini dhidi ya JMT.

Kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kabisa kero zote za muungano, na huu ubaguzi wa Utanganyika na Uzanzibari, ni kwenda kwenye serikali moja. Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa tumefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye nchi moja, yenye serikali moja na rais mmoja?

Muungano tutaulinda kwa gharama yoyote.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali

Rejea za mwandishi kuhusu serikali moja
 
Wanabodi,
Kama kawa, kila nipatapo fursa, ni mwendo wa Kwa Maslahi ya Taifa kwa kwenda mbele, mada ya leo ni mada muendelezo wa wiki iliyopita kuhusu hizi chokochoko zinazoendelea za kuuchokoa huu muungano wetu adimu na adhimu

Mkanganyiko wa Katiba.
Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.
Serikali moja ya Kidemokrasia inayowajibika kwa Wananchi ndio suluhisho muafaka juu ya kero zote za Muungano nchini Tanzania.
 
Wanabodi,
Kama kawa, kila nipatapo fursa, ni mwendo wa Kwa Maslahi ya Taifa kwa kwenda mbele, mada ya leo ni mada muendelezo wa wiki iliyopita kuhusu hizi chokochoko zinazoendelea za kuuchokoa huu muungano wetu adimu na adhimu kwa hoja za kibaguzi za Utanganyika na Uzanzibari, ambapo wiki iliyopita nilisema zimesababishwa na ukosefu wa elimu ya uraia kuhusu Muungano wetu.

Kwa wasomaji wapya, wiki iliyopita nilizungumzia kuhusu kauli za kibaguzi za kunyoosheana vidole vya Utanganyika na Uzanzibari, nikazungumzia kuwa zinasababishwa na ukosefu wa elimu ya uraia, na kuaahidi leo nitaumalizia mjadala huu
Paskali
Bado hilo linaweza lisiwe suluhisho la kudumu. Kwanini?
Wazanzibar wengi hatuko tayari na mfumo wa serikali moja, kwa kuwa serikali moja itaimeza Zanzibar na visiwa vya Unguja na Pemba vitageuzwa na kuwa wilaya mbili (sio hata mikoa) ndani ya muungano wa Tanzania. Hilo jambo hatulitaki kulisikia kwa kuwa mbali na kuua utambulisho wetu wa kizanzibar, linapingana na katiba ya Zanzibar na mwisho litaididimiza Zanzibar kiuchumi kwa kuwa Zanzibar itakosa upekee wake na kuwa sawa na wilaya za huko Tanganyika mfano wa Namtumbo, Kasulu, Tandahimba nk.

Nadhani suluhisho ni kuwa na serikali tatu (Zanzibar, Tanganyika, Tanzania) kwa sababu ndio muundo unaokubalika na pande zote mbili za muungano huku ukiwa na uwezo wa kuainisha vyema maslahi ya kila upande kwa wazi na usawa.
 
Kwa wazanzibar muungano ni koti tu, na tena unapaswa kuwa koti tu, ukisikia joto unalivua na ukisikia baridi unalivaa. Muungano haupaswi kuwa msingi kamili wa kuanzishwa na kuendesha nchi zetu, ni jambo la ziada baada ya misingi ya nchi zetu kuwa imara.

Tusiwe walevi na watumwa wa muungano.
 
Wanabodi,
Kama kawa, kila nipatapo fursa, ni mwendo wa Kwa Maslahi ya Taifa kwa kwenda mbele, mada ya leo ni mada muendelezo wa wiki iliyopita kuhusu hizi chokochoko zinazoendelea za kuuchokoa huu muungano wetu adimu na adhimu
binafsi sina shaka hata kidogo,
ndoto ya uzalendo ya Baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere ina kwenda kutimia katika ukamilifu wake....

nchi moja, serikali moja na Rais moja ndio suluhu ya kizalendo na ya kudumu, kuhusu Muungano wa waTanzania 🐒
 
Unachokishauri ni kuunda israel na palestina ya Tanzania.

Suluhisho ni Tanganyika ijitafute iko wapi, huu ni muungano wa nchi mbili.

Kama ni serikali moja, basi Tanganyika irudishwe Zanzibar ilikotokea kabla Zanzibar haijagawanywa na wajerumani huko berlin kama keki juu ya meza.
 
Wanabodi,

Kama kawa, kila nipatapo fursa, ni mwendo wa Kwa Maslahi ya Taifa kwa kwenda mbele, mada ya leo ni mada muendelezo wa wiki iliyopita kuhusu hizi chokochoko zinazoendelea za kuuchokoa huu muungano wetu adimu na adhimu kwa hoja za kibaguzi za Utanganyika na Uzanzibari, ambapo wiki iliyopita nilisema zimesababishwa na ukosefu wa elimu yaa!
Pascal Mayalla huu muungano haufai, tuachane nao tu, ni muungano wa kuinufaisha Zanzibar na kuifubaza Tanganyika
 
Wakaombwe itonjanda, kumbe wakaombwe mwenzangu kabisa.
Duh...!, umenikumbusha mbali kwa kunirejesha kwenye roots, ile tarehe 5/2/1977 wakati CCM inazaliwa, nilikuwa darasa la 3, SM ya Itonjanda chini ya Mwalimu Mkuu Paul Kashidye, baba yake Deo, Mati, Faustin . Dada mkuu wa shule alikuwa Kayemba, tulichinja ng'ombe mzima tukala na ugali!.

Ukoo wa Kaombwe au Wakawombwe ndio ukoo wa Bibi mzaa Baba, babu ni Msukuma kutoka Mwanza, akalowea Tabora, akaoa Tabora na kuwa Wasukuma Wanyamwezi.

P
 
dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja.
Mkuu huu ushauri wako una tofauti gani na maoni ya wengi ya kuwa na serikali tatu?
Kumbuka kero za muungano zinatokana na uwepo wa maeneo ambayo sio ya ushirikiano/muungano. Endapo maeneo yote yangekuwa na muungano kusingekuwa na hizi kero kwa sababu hata Zanzibar isingekuwepo (kusingekuwa na serikali ya Zanzibar -SMT). Uwepo wa SMT utatoa uhalali wa uwepo wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika (SJT).
Ndio maana Shekhe Ponda alihoji unaposema unatatua kero za Muungano, hizo kero ni kati ya nani na nani? Nani anamlalamikia nani?
Kwa hivyo sioni hoja mpya kwenye bandiko lako maana yote yameshaelezwa kupitia maoni ya wananchi kwenye katiba ya Warioba kuhusu muundo wa serikali. Je, hoja yako ya kuwa na serikali moja ya JMT unamaanisha mkataba wa muungano ufanyiwe marejeo ili maeneo yote ambayo sio ya muungano yafanywe kuwa ya muungano?
 
Bado hilo linaweza lisiwe suluhisho la kudumu. Kwanini?
Wazanzibar wengi hatuko tayari na mfumo wa serikali moja, kwa kuwa serikali moja itaimeza Zanzibar na visiwa vya Unguja na Pemba vitageuzwa na kuwa wilaya mbili (sio hata mikoa) ndani ya muungano wa Tanzania. Hilo jambo hatulitaki kulisikia kwa kuwa mbali na kuua utambulisho wetu wa kizanzibar, linapingana na katiba ya Zanzibar na mwisho litaididimiza Zanzibar kiuchumi kwa kuwa Zanzibar itakosa upekee wake na kuwa sawa na wilaya za huko Tanganyika mfano wa Namtumbo, Kasulu, Tandahimba nk.

Nadhani suluhisho ni kuwa na serikali tatu (Zanzibar, Tanganyika, Tanzania) kwa sababu ndio muundo unaokubalika na pande zote mbili za muungano huku ukiwa na uwezo wa kuainisha vyema maslahi ya kila upande kwa wazi na usawa.
Visiwa vya Unguja na Pemba vikiwa wilaya we unaathirika kivipi?
 
Wanabodi,

Kama kawa, kila nipatapo fursa, ni mwendo wa Kwa Maslahi ya Taifa kwa kwenda mbele, mada ya leo ni mada muendelezo wa wiki iliyopita kuhusu hizi chokochoko zinazoendelea za kuuchokoa huu muungano wetu adimu na adhimu kNa hili ndo suluhisho pekee la zinazoitwa kero za Muungano.

Wingi wa Serikali ni uroho wa watu kutaka madaraka na vyeo tu. Hauna msingi wowote kwa mwananchi wa kawaida
 
Nyerere na Karume Muungano wao ni wa Serikali 2

Ukitaka 1 au 3 hilo ni jambo jipya Kabisa linalopaswa kuanzia Upya kwa Wananchi wa Tanzania na Wananchi wa Zanzibar
Nyerere kichwani alikuwa amepanga kuwa na serikali moja, Karume kichwani alikuwa anataka tatu, kwa kuwa suala la kuwa na muungano lilikuwa ni shinikizo la lazima kutoka Marekani, basi mpango wa mpito ukawa ni mbili.
 
Nyerere kichwani alikuwa amepanga kuwa na serikali moja, Karume kichwani alikuwa anataka tatu, kwa kuwa suala la kuwa na muungano lilikuwa ni shinikizo la lazima kutoka Marekani, basi mpango wa mpito ukawa ni mbili.
Wakati ule watu wa pande zote mbili hawakuulizwa wanatakaje ,
Sasa ni muhimu watu wa hizo pande mbili wakaulizwa wanataka Muungano wa aina gani 👁😇
 
Back
Top Bottom