Pombe ni Ndugu wa madeni

Saad30

JF-Expert Member
May 26, 2020
2,696
5,364
Salamu wakuu.

Kwanza namshukuru Mungu mmoja kwa imani yangu kunijalia afya na pia kunifanya niwe mbali na pombe yaani kunywa pombe.

Kimaisha nashukuru hapa nilipofika lakini bado safari ni ndefu japo kuwa umri wangu bado kijana sana.

Mimi nilikuwa mnywaji wa pombe mzuri sana nilianza na kunywa beer kadhaa enzi hizo kipato ni kidogo kipindi nipo nyumbani Bongo.

Sasa naishi huku South Africa 🇿🇦 mambo yanaenda kipato kimeongezeka nashukuru lakini sasa nikisema niende nikanywe Beer basi nitakunywa mbili ila baada ya hapo ni Hennessy tu kwenda mbele....Nilikwa nanunua Hennessy moja mimi nikiwa na washkaji zangu afu mimi ndio mtoaji pesa bei zinajulikana kwa ambao wanaishi hapa South Africa 🇿🇦 ukienda club ni R1300 kwa Hennessy ya kawaida ila VSOP ni R2100 ila bei zinakuwa tofauti kwenye club nyingine.

Sasa ilifika kipindi nikawa nanunua hadi chupa tatu za Hennessy daah nachukuwa hadi hela za biashara yaani hii tunaita (KUJIKOPESHA).

Balaa linakuja nikiamka asubuhi nawaza ile hela niliotumia jana na kuanza kusema mimi siendi tena club lakini daah skufichi bana ukiwa na washkaji wanywa pombe ni balaa yani weekend ikifika tu utaskia simu oya twenzetu tukajipongeze.

Wakati mwingine huwa nawaektiaga tu daah wanangu leo sina maisha sipo fresh kabisa basi utaskia wee njoo tu tunywe beer na siunajua bana ukiitwa club lazima utabeba pesa kidogo kwahiyo natoka na R1000 hivi asee nikifika nakuta totoz kali nasi pale Sasa akili ya KUJIKOPESHA inaanza kuja taratibu nampigia kijana wangu asee njoo na R3000 hapa fasta, dogo anakuja asee.

Pombe ni nyoko unakuta hela haitoshi mademu wanataka mitungi tu...unafurahi lakini akili ya kweli ni maumivu tu.

Pombe imenifanya hadi sijamaliza kumjengea mama yangu mzazi 😢😢 nyumba imeishia katikati asee mama akinipigia simu mwanangu mbona mimi nitalipa kodi hadi lini daah namwambia mama tutaweka sawa mwezi wa saba...mwezi ndio huo unajakata.

Naamini kwasasa naenda maliza nyumba ya mama na ataamia kwakwe huu mwaka haushi Inshaallah....Nitaleta mlejesho kwenye jukwaa la Ujenzi na makazi nikimaliza vyumba ya mama.

Sasa bana stori zimefika hadi kwa wazazi daah imenikata sana wazazi kutoa machozi yao juu yangu mimi kwajili ya pombe imenikata sana na nimeumia.

Rasmi mimi sinywi pombe tena na washkaji zangu watanichukia kwa hilo maana wamemkosa mcheza muhimu sana...

NAAMINI MUNGU MMOJA YUPO NA MIMI.

Nashauri vijana wenzangu pombe sio nzuri pombe ni hasara tu unafanya kazi kwabidii alafu pesa unaipeleka bar.
 
Salamu wakuu.

Kwanza namshukuru Mungu mmoja kwa imani yangu kunijalia afya na pia kunifanya niwe mbali na pombe yaani kunywa pombe.

Kimaisha nashukuru hapa nilipofika lakini bado safari ni ndefu japo kuwa umri wangu bado kijana sana.

Mimi nilikuwa mnywaji wa pombe mzuri sana nilianza na kunywa beer kadhaa enzi hizo kipato ni kidogo kipindi nipo nyumbani Bongo.

Sasa naishi huku South Africa mambo yanaenda kipato kimeongezeka nashukuru lakini sasa nikisema niende nikanywe Beer basi nitakunywa mbili ila baada ya hapo ni Hennessy tu kwenda mbele....Nilikwa nanunua Hennessy moja mimi nikiwa na washkaji zangu afu mimi ndio mtoaji pesa bei zinajulikana kwa ambao wanaishi hapa South Africa ukienda club ni R1300 kwa Hennessy ya kawaida ila VSOP ni R2100 ila bei zinakuwa tofauti kwenye club nyingine.

Sasa ilifika kipindi nikawa nanunua hadi chupa tatu za Hennessy daah nachukuwa hadi hela za biashara yaani hii tunaita (KUJIKOPESHA).

Balaa linakuja nikiamka asubuhi nawaza ile hela niliotumia jana na kuanza kusema mimi siendi tena club lakini daah skufichi bana ukiwa na washkaji wanywa pombe ni balaa yani weekend ikifika tu utaskia simu oya twenzetu tukajipongeze.

Wakati mwingine huwa nawaektiaga tu daah wanangu leo sina maisha sipo fresh kabisa basi utaskia wee njoo tu tunywe beer na siunajua bana ukiitwa club lazima utabeba pesa kidogo kwahiyo natoka na R1000 hivi asee nikifika nakuta totoz kali nasi pale Sasa akili ya KUJIKOPESHA inaanza kuja taratibu nampigia kijana wangu asee njoo na R3000 hapa fasta, dogo anakuja asee.

Pombe ni nyoko unakuta hela haitoshi mademu wanataka mitungi tu...unafurahi lakini akili ya kweli ni maumivu tu.

Pombe imenifanya hadi sijamaliza kumjengea mama yangu mzazi nyumba imeishia katikati asee mama akinipigia simu mwanangu mbona mimi nitalipa kodi hadi lini daah namwambia mama tutaweka sawa mwezi wa saba...mwezi ndio huo unajakata.

Naamini kwasasa naenda maliza nyumba ya mama na ataamia kwakwe huu mwaka haushi Inshaallah....Nitaleta mlejesho kwenye jukwaa la Ujenzi na makazi nikimaliza vyumba ya mama.

Sasa bana stori zimefika hadi kwa wazazi daah imenikata sana wazazi kutoa machozi yao juu yangu mimi kwajili ya pombe imenikata sana na nimeumia.

Rasmi mimi sinywi pombe tena na washkaji zangu watanichukia kwa hilo maana wamemkosa mcheza muhimu sana...

NAAMINI MUNGU MMOJA YUPO NA MIMI.

Nashauri vijana wenzangu pombe sio nzuri pombe ni hasara tu unafanya kazi kwabidii alafu pesa unaipeleka bar.
Mkuu ni kwamba unapanga kuacha au ushaacha?

Utatumia/umetumia njia gani kuacha?
 
Mkuu kama umeacha 🍻 katoe ushuhuda kwenye nyumba ya ibada sisi bado tupo bar ila sema mi zikikolea zina shuka huku chini ndio hasara inaanziaga hapo, leo mkuu yeyoye aliyopo Dodoma tuonane Waswanu sina usafiri kwaio stoki nje ya maeneo haya, tugonge bia kadhaa
 
Acha kusingizia pombe.
Nakunywa pombe kila siku ila sharti Ni moja nakunywaga mwenyewe tu marafiki Zangu wananijua hamna Cha kupitisha round huo Ni ujinga kila mtu ale hela yake .
Nalewa nakua na chamoyo wangu ananilinda yeye anakunywa Maji sometimes Malta nikilewa ndo ananiendesha mpka maskani maisha burudani.
Una hela ya kuunga unakunywa Hennessy? Huna hela unamiliki sim ya miliooo vijana wa ovyo .
 
Back
Top Bottom