Pombe ni Ndugu wa madeni

Hivi nyie mnakunywa pombe gani hizo zinafikia hadi ku control maisha yenu na maamuzi yenu. Inafikia hatua hadi inakuletea financial insecurity.

Nafikiri ni ulimbukeni na kutojitambua. Mkuu Jifunze kusema HAPANA
Kuiga mambo kuna waponza.Akiniona nawanunulia bia na yeye anataka afanye hivyohivyo.Nakunywa kila slku na yeye anatamani iwe kwake.Ujinga.Anajua mimi natoa hela wapi?Nenda kula bia kwa akili mingi.Halafu kwenye bia kuna stori za uongouongo asizifuatilie atafilisika tu.😂😂😂😂
 
Hivi nyie mnakunywa pombe gani hizo zinafikia hadi ku control maisha yenu na maamuzi yenu. Inafikia hatua hadi inakuletea financial insecurity.

Nafikiri ni ulimbukeni na kutojitambua. Mkuu Jifunze kusema HAPANA
Vijana hawana akili ananunua Hennessy huku kashikilia macho matatu hata geto Hana na Wana viburi hao
 
Hivi nyie mnakunywa pombe gani hizo zinafikia hadi ku control maisha yenu na maamuzi yenu. Inafikia hatua hadi inakuletea financial insecurity.

Nafikiri ni ulimbukeni na kutojitambua. Mkuu Jifunze kusema HAPANA
HAPANA
 
Acha kusingizia pombe.
Nakunywa pombe kila siku ila sharti Ni moja nakunywaga mwenyewe tu marafiki Zangu wananijua hamna Cha kupitisha round huo Ni ujinga kila mtu ale hela yake .
Nalewa nakua na chamoyo wangu ananilinda yeye anakunywa Maji sometimes Malta nikilewa ndo ananiendesha mpka maskani maisha burudani.
Una hela ya kuunga unakunywa Hennessy? Huna hela unamiliki sim ya miliooo vijana wa ovyo .
Wewe umeshatoboa mkuu ila kazana umakize ile nyumba yako ya tatu
 
Salamu wakuu.

Kwanza namshukuru Mungu mmoja kwa imani yangu kunijalia afya na pia kunifanya niwe mbali na pombe yaani kunywa pombe.

Kimaisha nashukuru hapa nilipofika lakini bado safari ni ndefu japo kuwa umri wangu bado kijana sana.

Mimi nilikuwa mnywaji wa pombe mzuri sana nilianza na kunywa beer kadhaa enzi hizo kipato ni kidogo kipindi nipo nyumbani Bongo.

Sasa naishi huku South Africa mambo yanaenda kipato kimeongezeka nashukuru lakini sasa nikisema niende nikanywe Beer basi nitakunywa mbili ila baada ya hapo ni Hennessy tu kwenda mbele....Nilikwa nanunua Hennessy moja mimi nikiwa na washkaji zangu afu mimi ndio mtoaji pesa bei zinajulikana kwa ambao wanaishi hapa South Africa ukienda club ni R1300 kwa Hennessy ya kawaida ila VSOP ni R2100 ila bei zinakuwa tofauti kwenye club nyingine.

Sasa ilifika kipindi nikawa nanunua hadi chupa tatu za Hennessy daah nachukuwa hadi hela za biashara yaani hii tunaita (KUJIKOPESHA).

Balaa linakuja nikiamka asubuhi nawaza ile hela niliotumia jana na kuanza kusema mimi siendi tena club lakini daah skufichi bana ukiwa na washkaji wanywa pombe ni balaa yani weekend ikifika tu utaskia simu oya twenzetu tukajipongeze.

Wakati mwingine huwa nawaektiaga tu daah wanangu leo sina maisha sipo fresh kabisa basi utaskia wee njoo tu tunywe beer na siunajua bana ukiitwa club lazima utabeba pesa kidogo kwahiyo natoka na R1000 hivi asee nikifika nakuta totoz kali nasi pale Sasa akili ya KUJIKOPESHA inaanza kuja taratibu nampigia kijana wangu asee njoo na R3000 hapa fasta, dogo anakuja asee.

Pombe ni nyoko unakuta hela haitoshi mademu wanataka mitungi tu...unafurahi lakini akili ya kweli ni maumivu tu.

Pombe imenifanya hadi sijamaliza kumjengea mama yangu mzazi nyumba imeishia katikati asee mama akinipigia simu mwanangu mbona mimi nitalipa kodi hadi lini daah namwambia mama tutaweka sawa mwezi wa saba...mwezi ndio huo unajakata.

Naamini kwasasa naenda maliza nyumba ya mama na ataamia kwakwe huu mwaka haushi Inshaallah....Nitaleta mlejesho kwenye jukwaa la Ujenzi na makazi nikimaliza vyumba ya mama.

Sasa bana stori zimefika hadi kwa wazazi daah imenikata sana wazazi kutoa machozi yao juu yangu mimi kwajili ya pombe imenikata sana na nimeumia.

Rasmi mimi sinywi pombe tena na washkaji zangu watanichukia kwa hilo maana wamemkosa mcheza muhimu sana...

NAAMINI MUNGU MMOJA YUPO NA MIMI.

Nashauri vijana wenzangu pombe sio nzuri pombe ni hasara tu unafanya kazi kwabidii alafu pesa unaipeleka bar.
Mnakunywaga pombe gani hizo?!!

Principal ya kwanza, usinywe pombe ya mtu ili nawe usim-mnyweshe mtu ..yaan pombe za kampani marufuku.

Principal ya pili, nenda bar na fixed budget ..na usiwe na card ya bank, tigo pesa wala namba ya mtu anayeweza kukutumia hela either yako au mkopo.

Ukifata hizo principals utaenda bar hadi uzeeni na hutakaa uyumbe wala kujilaumu, ukiskia story za hivi..unasema hiiiiii (in jiwe voice).
 
Ujinga wapombe ni pale bar unapokunywa. Usiku kunywa bia hata za m5 kisha nenda asubuh kawaombe supu wanayouza wakupe bure hata ya elf 3 tu hawakupi. Hapo ndio utaelewa kwao wewe ni mjinga flani anaekuja kuwapa hela za bure,bora ukalishe masikini kuna siku watakusaidia ila sio wenye Bar au wahudumu
 
Mnakunywaga pombe gani hizo?!!

Principal ya kwanza, usinywe pombe ya mtu ili nawe usim-mnyweshe mtu ..yaan pombe za kampani marufuku.

Principal ya pili, nenda bar na fixed budget ..na usiwe na card ya bank, tigo pesa wala namba ya mtu anayeweza kukutumia hela either yako au mkopo.

Ukifata hizo principals utaenda bar hadi uzeeni na hutakaa uyumbe wala kujilaumu, ukiskia story za hivi..unasema hiiiiii (in jiwe voice).
Mkuu umeshafika miaka 50 au bado?
 
Afadhali nyinyi aisee mimi nikinywa pombe nakuwa na sifa za kijinga kabisa lazima niache keep change na keep change si chini ya laki 1.
Asubuhi naaza kujuta kabisa shenzi zangu.
Barmaid wakiona gari yangu tu wanaanza kuikimbilia kama kumbikumbi wanaacha kuhudumia wateja wengine wanakuja kwangu basi bichwa linavimba kwa sifa.
Band za wacongo wakija kutumbuiza lazima waniite jina langu Kama wanavyoitwa papaa msofe au ndama mtoto wa ng'ombe naenda kuwatupia laki mbili .
Nikiamka asubuhi najuta mno ,Zitakuja kunifirisi kimasihara
Hawa mabamedi wanaangalia mfuko tu asee ukikata basi wanaanza kukuonea huruma na kukuona mjinga.
 
Tatizo ni washkaji na si pombe
Mkuu pombe ndio huleta hao watu wewe kuna kwenda bar na club hivi ni vitu viwili tofauti

Bar unaenda kutumia Sh 15000 na club unaenda kutumia sio chini ya Sh laki 500000
 
Mkuu pombe ndio huleta hao watu wewe kuna kwenda bar na club hivi ni vitu viwili tofauti

Bar unaenda kutumia Sh 15000 na club unaenda kutumia sio chini ya Sh laki 500000
Mimi nakunywa kila siku kakini siendi kunywa bar, badili lifestyle ili utumie pesa kidogo kwenye kunywa kuliko kumaliza pesa kwa marafiki.
 
Mimi nakunywa kila siku kakini siendi kunywa bar, badili lifestyle ili utumie pesa kidogo kwenye kunywa kuliko kumaliza pesa kwa marafiki.
Kama umefika umri wa miaka 50 basi siwezi shangaa maneno yako ila kama una umri kuanzia 30+ basi nitakuwa nimeeleweka
 
Back
Top Bottom