Polisi Tanzania kuanza msako wa kuwakamata wanaotaka kujinyonga, ole wako ukionekana kama mtu uliyezongwa na maisha

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,760
48,408
Wenzetu mnashauriwa mtembee vifua mbele huku mkikenua meno na kuonyesha furaha, usionyeshe dalili zozote za kutaka kujiua kisa ugumu wa maisha hayo mara mgao wa umeme, maji, jua kali n.k.
===

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Barnabas Mwakalukwa amesema Jeshi la Polisi mkoani humo litaanza msako wa kuwabaini watu wanaotaka kujinyonga kufuatia kupokea taarifa ya watu kujinyonga.

Kamanda Mwakalukwa amesema kufuatia kupokea taarifa ya watu wawili kujinyonga, mwaka huu wataanza msako kuwabaini wanaotaka kujinyonga.

Hata hivyo amewakanya watu wanaotegemea kujinyonga kuwa tabia hizo zikome kwani wao wataanza kufanya doria na kuwakamata kabla hawajajinyonga na kisha kuwapeleka Mahakamani.

“Tunaomba viongozi wa Taasisi za Kiroho wafanye doria za Kiroho za kuzima matukio ya namna hiyo kwa kutoa nasaha, elimu na Wataalamu wa Afya waende kwa wagonjwa wenye matatizo ya akili ili wawape faraja kuwa bado wana nafasi ya kuwa na maisha bora.” amesema kamanda Mwakalukwa.

Ameongeza kuwa wakati mwingine tunapoteza Wataalamu ambao wangesaidia nchi yetu “Tumepoteza Mwalimu, Mjasiriamali labda hawa baada ya miaka miwili wangekuwa Maprofesa au matajiri wa Afrika.”

Chanzo; Dar24.com
 
Back
Top Bottom