Polisi: Kagera yaongoza kwa mauaji na kujinyonga, Mwaka 2022 kulikuwa na matukio 190

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Kagera Maketi Msangi amesema mkoa huo unaendelea kuongoza kwa matukio ya mauaji, kujinyonga na kujeruhi, ambapo kwa kipindi cha mwaka jana kulikuwa na matukio yasiyopungua 190.

Akizungumza katika kikao cha kujadili namna gani ya kukabiliana na vitendo vya mauaji, kilichoitishwa na Kamishna wa polisi jamii Tanzania na kuwashirikisha viongozi wa dini, kimila, wazee maarufu askari na watendaji wa kata kamanda Msangi amesema Mkoa unaongoza katika matukio makubwa ambayo yanavuta hisia za wananchi na wakati mwingine kupunguza hamasa kwao, ya kwenda kujitafutia riziki.

"Lakini kuna Wilaya ambazo zinaongoza kwa mfano Wilaya ya Muleba kwa mwaka jana pekee kulikuwa na matukio 40, ikifuatiwa na Ngara matukio 36 na ya tatu ni Bukoba matukio 30" amesema Msangi

"Kumejitokeza matukio hivi karibuni ya mauaji, ambayo mengi ukiangalia yamekuwa yakisababishwa na migogoro ya ardhi, wivu wa mapenzi na ushirikina, tumekuja hapa kukutana na viongozi mbalimbali, lengo ni kukumbushana tunafanya nini kutokomeza matukio ya aina hii yasitokee, tumetoka na jambo la msingi kwamba turudi katika maeneo yetu, tuhakikishe yanakuwa salama kwa kutoa elimu na kuwafuatilia watu wote wanaojihusisha na mauaji" amesema kamishna wa polisi jamii Tanzania, Faustine Shilogile.

Kwa upande wake mratibu wa kitengo cha kusuruhisha migogoro na kutetea haki za binadamu kutoka Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi (DKMG) Naomi Kanyonyi amesema kuwa jamii, wazee wa kimila na taasisi za kidini wamewaacha vijana waingine kwenye ndoa bila elimu yoyote ya uvumilivu, na matokeo yake wanapoingia kwenye ndoa wanafikiri wakitumia ukatili kumaliza ukatili watafaulu, kumbe wanaongeza matukio.

"Katika Wilaya sita tunazofanya nazo kazi, tumepokea migogoro 771, mingi inahusu ndoa changa za umri wa kuanzia miaka 0 hadi 5 na wanaoongoza kuleta migogoro ni wanawake ambayo ni 507, migogoro 264 imeletwa na wanaume lakini wanaume wengi wanaripoti kunyimwa unyumba, ina maana wao hawapigwi, maana kwa miaka 12 niliyofanya kazi hii ni mwanaume mmoja aliripoti kupigwa katika ndoa" amesema Kanyonyi.

Chanzo: EATV
 
Hicho ni kikao cha mkoa, sidhani kama wana data za mikoa yote kujua nani anaongoza na nani anafuatia. Ingekuwa ni taarifa ya kitaifa sitarajii kukosa Shinyanga, Geita na Njombe kwenye top 5. Tafuta nyuzi za mauaji humu zimejaa mikoa hiyo
 
Hujaelewa hata wew uliopost...yaani mauaji 190 tu iongoze mauaji Tz?

Kwenye hiyo taarifa hajatoa data za mikoa mingine ni kagera tu
 
Hujaelewa hata wew uliopost...yaani mauaji 190 tu iongoze mauaji Tz?

Kwenye hiyo taarifa hajatoa data za mikoa mingine ni kagera tu
Ripoti current tena imetoka Bado Kagera inaongoza kwa mauaji
1683189733200.jpg
 
Back
Top Bottom