Ruvuma: Watu 40 washikiliwa na Jeshi la Polisi katika msako wa Mauaji ya Askari wa kampuni ya ulinzi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linawajulisha wananchi kuhusiana na tukio Moja la mauaji lililotokea Novemba 2023 kama ifuatavyo:

Tukio lilitokea Novemba 19, 2023 majira ya saa saa mbili asubuhi katika Kijiji cha Mkali kilichopo Wilaya ya Nyasa Mkoa Ruvuma ambapo mwanaume aliyefahafika kwa jina la Boliva Betram Mapunda, (26), askari wa kampuni ya ulinzi ya Suma Guard, Mkazi wa Kijiji cha Mateka Songea akiwa kambini kwenye lindo la hifadhi ya misitu ya safu za Milima ya Livingstone iliyoko mpakani mwa Wilaya ya Nyasa na Mbinga inayomilikiwa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS).

16bd6a06-7d3f-4229-aec0-8b851e7b0736.jpeg

8ca94746-af3e-4be9-a8c6-6109fbe5de76.jpeg

Akiwa na askari wenzake ambao ni Yohana Angelus Komba, Kelvin Godfrey Mtitu na Daudi Kambanga Kufabasi walivamiwa na kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi kutoka vijiji vya Namkuka na Mkuwani, Kitongoji cha Mairo na Wilaya ya Mbinga kwa Silaha za jadi ambazo ni Mapanga, Mishale na Nyengo kitendo kilichomsababishia majeraha kwa askari Boliva Betram sehemu mbalimbali za mwili wake na kupelekea kuvuja damu nyingi na kusababisha kifo chake wakati akipatiwa matibabu katika kituo cha afya mbambabay.

Chanzo tukio hilo ni kwamba wananchi wa kijiji hicho kudai kuwa maeneo hayo ya hifadhi yanayomilikiwa na wakala wa misitu (TFS) ni maeneo yao ambayo yalichukuliwa na serikali bila wao kulipwa fidia.
9fb7e8f2-d04a-4ba5-b7b0-fda157c1af81.jpeg

Baada ya tukio hilo, Tarehe 20.11.2023 Jeshi la Polisi liliendesha Operesheni kali kuwasaka wale wote waliohusika na kitendo hicho cha mauaji ambapo liilifanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 40 wakiwa wamejificha katika Mapango ya Safu za milima ya Livingstone jirani na Kijijini cha Mkalia na Mkuwa wakiwa na Mapanga, Nyengo, na Silaha moja aina ya Gobole.

Watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya Upelelezi kukamilika kwa hatua za kisheria.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma bado linaendelea na Operesheni hiyo kuwabaini na kuwakama wale wote waliohusika kwenye mauaji ya mlinzi huyo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa pamoja na mkuwafikisha mahakamani.

Natoa rai kwa wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma kuacha mara moja vitendo vya kujichukulia sheria mkononi badala yake niwatake kufuate taratibu kwa kufikisha taarifa za shida zao katika mamlaka husika ili kuweza kupata suluhu ya kwa njia ya amani.

Aidha, niwatake wale wote walioshiriki kwa njia nyoyote kusababisha mauaji na askari huyo wajisalimishe wenyewe haraka kwani Jeshi la Polisi tutahakikisha tunawasaka popote pale walipo, kuwakamata na kuwafikisha mahakamini kwa hataua zaidi.

Pamoja na hilo nawaagiza Wamiliki wa Makampuni yote ya ulinzi Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha kuwa bunduki zao zinakuwa na Risasi. Jeshi la Polisi litafanya ukaguzi kwenye malindo yao na ikigundulika bunduki haina risasi tutachukua hatua kali kwa wamiliki wa kampuzi ya ulinzi husika.

Imetolewa na:
Marco G. Chilya- ACP
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Ruvuma.
 
Back
Top Bottom