Polisi: Mmiliki wa shule ZamZam amefariki kwa matatizo ya moyo, hakuna viashiria vya mauaji. Familia yatofautiana na Polisi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema kuwa kufeli kwa moyo na kukosa msaada wa haraka wa matibabu, ndiyo chanzo cha kifo cha Sheikh Rashid Bura, ambaye ni mmiliki wa shule za Zamzam mkoani humo.

Kamanda Muroto amebainisha hayo leo Disemba 27, 2019, na kusema kuwa mara baada ya kupata taarifa hiyo, Polisi walifika eneo la tukio na kwamba hawakukuta viashiria vyovyote vya mauaji, badala yake uchunguzi umebainika kuwa alifariki baada ya kukosa msaada kwa kuwa hali hiyo ilimkuta ofisini akiwa peke yake.

"Taarifa za kiuchunguzi za awali zinaonesha kifo chake kimetokana na kufeli kwa moyo na kwakuwa alikuwa ofisini kwake hakupata msaada na simu yake ilikuwa imezima ndugu zake walishindwa kumpata na ofisini tulikuta kupo salama na hakukuwa na wizi wowote uliofanyika" amesema Kamanda Muroto.

Kwa mujibu wa Kamanda Muroto, mwili wa Bura uligundulika siku ya Disemba 25, 2019, na kuwataka waandishi wa habari, kuacha kusambaza taarifa ambazo wanakuwa hawajazithibitisha kutoka kwenye vyanzo halisi likiwemo Jeshi la Polisi ama kwa Daktari

FAMILIA YATOFAUTIANA NA POLISI

Ali Rashid Bura (26), mtoto wa marehemu na msemaji wa familia ya marehemu, Abdillah Mboryo wamesema mwili wa marehemu ulikutwa ofisini kwake bila nguo huku ukiwa na makovu matatu mkono wa kushoto, kwenye paja na mgongoni.

Mtoto wa marehemu amesema baada ya kumtafuta baba yake maeneo mengine bila mafanikio, alikwenda ofisini kwake na kukuta mlango ukiwa umefungwa na alipoufungua kwa kuupiga teke ulifunguka.

“Ndipo nikauona mwili wa baba ukiwa umeharibika sana huku akiwa amekaa chini na nguo zote zikiwa pembeni,” anasema kijana huyo.

Naye Mboryo alisema: “Mwili wa marehemu ulikuwa na majeraha matatu; mkono wa kushoto, kwenye paja na mgongoni ambayo siwezi kuyazungumzia kwa sababu mimi si polisi lakini niliyaona.”

Habari zaidi, soma



 
Kweli sasa lazima tuyale tu matango mwitu na kuyaita tikiti maji. Waliotuambia kuwa alikutwa kanzu pembeni na kuwa, "Mashine yake " ilikuwa imekatwa huyo kamanda kaa mwenye mbwembwe nyingi leo ndio anatuambia kuwa ati alikufa kimya kimya tu kwa gonjwa la moyo??
Hatuna shida yeyote, kitu bora Sheikh kafia ofisini kwa gonjwa la moyo. Ila endapo atachunguza zaidi na kuona kisu pembeni ya kamba basi atuambie tufanye zile duwaa zetu zile tuweke ubani kabla ya 40 yake.
Alotenda hayoo atajulikana tu
 
Hee! Sasa na kule kukatwa dyudyu ilikuwaje..? Au taarifa tuliyoletewa ilikuwa ni saiba kraimu!!
Mnaosema huyo muroto anaongopa inamaana kaiongopea hadi familia ya marehemu..? Hawaukagui mwili..?
Familia ya marehemu kama tunayoambiwa hapa ni uongo na wakanushe! Na hata hivyo sioni sababu ya huyo kamanda kuongopa ila walakini unakuja sehemu moja tu ni hizo siku tano!!!
 
Hee! Sasa na kule kukatwa dyudyu ilikuwaje..? Au taarifa tuliyoletewa ilikuwa ni saiba kraimu!!
Mnaosema huyo muroto anaongopa inamaana kaiongopea hadi familia ya marehemu..? Hawaukagui mwili..?
Familia ya marehemu kama tunayoambiwa hapa ni uongo na wakanushe! Na hata hivyo sioni sababu ya huyo kamanda kuongopa ila walakini unakuja sehemu moja tu ni hizo siku tano!!!
Hivi weye wamjua tunayesema kafa alikuwa "Sheikh"? Tangu lini mwili wa muislam ukakaguliwa?? Hata huyo anayemuweka pema peponi hufunikwa gubi gubi huko huko kaburini sasa nnani alienda chunguza ka kakatwa?? Kanzu ilikuwa "Haina" doa la damu wala mkunjo wa vurumai. Nadhani tukubaliane na kamanda wetu. Wa kwenda keshaenda kama vipi tufukize ubani
 
Back
Top Bottom