IGP hili la kifo Bariadi wahusika wawajibike, tukatae vifo vya kufia polisi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,153
Kufuatia kifo cha Limbu Kazilo (41), Mkazi wa Mtaa wa Kilulu, Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, familia yake imegoma kuuzika mwili wa ndugu yao huyo wakidai kuna mazingira ya utata kwenye kifo chake na hivyo wanataka kujua chanzo.

Mama mzazi wa marehemu, Nyahoga Nandi amesema mwanaye alikamatwa na Polisi akiwa nyumbani kwake Desemba 31, 2023, Saa 7 Usiku kwa tuhuma za mgogoro wa shamba wa muda mrefu, akashambuliwa kwa kupigwa na Askari hao hadharani, akapelekwa Kituo cha Polisi Bariadi, alipozidiwa akapelekwa Hospitali ya Bariadi na akafariki Januari 2, 2024.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Maulidi Shaban amezungumza na JamiiForums na kusema “Marehemu na mwenzake mmoja walikamatwa kwa tuhuma za mauaji, alipofikishwa kituoni akapata Homa, akapelekwa hospitali huko ndipo akafariki Dunia. Ndugu wamekataa majibu ya uchunguzi wa hapa wanataka uchunguzi wa Bugando, pia si kweli kuwa alipigwa, hayo ni maneno tu.”
 
Kufuatia kifo cha Limbu Kazilo (41), Mkazi wa Mtaa wa Kilulu, Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, familia yake imegoma kuuzika mwili wa ndugu yao huyo wakidai kuna mazingira ya utata kwenye kifo chake na hivyo wanataka kujua chanzo

Mama mzazi wa marehemu, Nyahoga Nandi amesema mwanaye alikamatwa na Polisi akiwa nyumbani kwake Desemba 31, 2023, Saa 7 Usiku kwa tuhuma za mgogoro wa shamba wa muda mrefu, akashambuliwa kwa kupigwa na Askari hao hadharani, akapelekwa Kituo cha Polisi Bariadi, alipozidiwa akapelekwa Hospitali ya Bariadi na akafariki Januari 2, 2024

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Maulidi Shaban amezungumza na JamiiForums na kusema “Marehemu na mwenzake mmoja walikamatwa kwa tuhuma za mauaji, alipofikishwa kituoni akapata Homa, akapelekwa hospitali huko ndipo akafariki Dunia. Ndugu wamekataa majibu ya uchunguzi wa hapa wanataka uchunguzi wa Bugando, pia si kweli kuwa alipigwa, hayo ni maneno tu.”
Ukifanya uchunguzi wa kina ulio huru kabisa, utagundua kwamba Jeshi la Polisi Tz limepoteza uhalali wote wa kuwa Jeshi ktk nchi hii ya Tz.
 
Back
Top Bottom