DidYouKnow
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 1,094
- 1,691
Nadhani kuna daktari kama daktari ambaye au ni mbobezi kwenye kitu fulani au generalist, lakini kuna forensic pathologist ambao ni wachache (na labda gynecologists). Hizo issue za swab unaweza ukazisema hapa, kwa sababu umesoma lakini je hawa madaktari wa kawaida wamepata mafunzo kwa ajili ya matukio kama hayo na namna ya kuyawasilisha pale inapobidi au wanaingia kwenye hiyo nafasi kwa kuwa forensic pathologist na au gnecologist hayupo?Daktari alipopelekewa mtoto wa kubakwa, yeye ndiye alitakiwa kufanywa swabs za sehemu za siri za mtoto na kuzihifadhi kama sample ambazo zinaweza kufanyiwa uchunguzi wa DNA. Kumbuka kwamba hata kama mtoto aliogeshwa, ndani ya mwili wake bado angekuwa na vitu kama shahawa za mbakaji. Madaktari wanaelewa utaratibu huu, sasa huyu kwa nini hakufanya?
Ndio maana watu wanafanya kujichukulia sheria mkononi, unaachoamua kumfanya mtuhumiwa mpk shetani lazima akae pembeni ajifunze. Inauma asikuambie mtuHebu fikiria. Mtoto wako wa miaka sita anatoka shule. Akiwa njiani mjinga fulani mwenye akili mbaya kuliko mnyama anamkamata na kumvutia porini, kisha anambaka na kumuumiza sana. Mtoto huyu wa miaka sita analia kwa maumivu, lakini mbakazi anamziba mdomo na kumtishia kumuua ikiwa ataendelea kupiga kelele au kumtaja kwa watu.
Mtoto wako huyu anarudi nyumbani analia na ametapakaa damu kwenye suruali yake. Unamwangalia kwa uchungu na kugundua mtoto wako mdogo kipenzi, miaka sita tu, darasa la kwanza, amebakwa na kuumizwa sana. Unamuuliza nani amefanya hivi anakutajia ni fulani, kwa kuwa anamfahamu aliyembaka.
Unamchukua mtoto na kumpeleka polisi. Polisi wanafungua jarida la kesi, lakini wala hawakuulizi nguo alizobakwa nazo ziko wapi. Mnampeleka mtoto hospitali, daktari anaemtibu wala hafanyi jitihada za kuchukua sampuli ndani ya mtoto na kuzihifadhi ili waje wafanye DNA test.
Kesi inapoenda mahakamani, mbakaji anafungwa kwa ushahidi wa kutambuliwa na mtoto. Lakini baadaye, jaji mtukuka wa mahakama ya rufaa anasema mbakaji aachiliwe huru kwa kuwa wakati wa kesi ile suruali yenye damu aliyokuwa amevaa mtoto haikuletwa mahakamani kama ushahidi. Mbakaji yuko huru.
Fikiria kama huyo mtoto wa miaka sita ni wa kwako, waangalie watoto wako, au watoto wa ndugu yako wa karibu, halafu piga picha wao ndio wamefanyiwa hivyo. Unajisikiaje?
Hii sio hadithi, ni tukio la kweli. Hawa ndio polisi wetu. Hawa ndio madaktari wetu. Hawa ndio majaji wetu. Hodari na makini sana katika kufuatilia kesi za siasa na kufunga watu kwa kesi za kubambikiwa, lakini sio kesi za watoto wa miaka sita kubakwa na kuumizwa.
Sasa niambie kama nikisema nchi yetu Tanzania ni banana republic, una sababu gani za kunibishia?
Reference: Suruali yenye damu ilivyotengua hukumu
Kama daktari umepewa case ya kutibu mtoto aliyebakwa, na unajua huna uwezo wa kufanya forensic pathology, kwa nini usiwasiliane na uongozi wako kuwaeleza hilo?Nadhani kuna daktari kama daktari, lakini kuna forensic pathologist ambao ni wachache. Hizo issue za swab unaweza ukazisema hapa, kwa sababu umesoma lakini je hawa madaktari wamepata mafunzo kwa ajili ya matukio kama hayo au wanaingia kwenye hiyo nafasi kwa forensic pathologist hayupo?
Nina mtoto mdogo wa karibu umri huo Mkuu.Aisee mleta mada umeandika kwa uchungu sana. Nikajiuliza swali je iwapo huyo mtoto aliyefanyiwa unyama huo angekuwa mtoto au mjukuu wa huyo jaji je angemfunga huyo mbakaji au angemwachia huru kwanza mpaka suruali iletwe mahakamani?
Tupo pamoja,yaani kabinti kangu katendwe hivyo,namteka mbakaji,namtatua Malinda,nikishindwa haki ya nani nitakodi gari nimgonge,navunja miguu,napasua kichwa,NAMI nalala mbele,hatuwezi kuishi wote hapa dunianiMimi sidhani kama tutapelekana polisi, shingo ya mbakaji itakuwa halali bora nifungwe kwa mauaji.
Inaumiza sana.
Ikiwa tutakutana, niko tayari kumwambia huyu jaji mbele za watu kwamba hajui sheria na hana sifa zinazomfanya astahili kuwa jaji, na kwamba ujaji wake ulipaswa kukoma siku Magufuli alipokufaHata ingeletwa angeipima hiyo damu kwa kipimo gani kuthibitisha anayoyataka.
Ndiyo hao Msukuma aswatolea mfano kwamba Mwendazake aliwasaidia kwa kuwapa nafasi za uongoziIkiwa tutakutana, niko tayari kumwambia huyu jaji mbele za watu kwamba hajui sheria na hana sifa zinazomfanya astahili kuwa jaji, na kwamba ujaji wake ulipaswa kukoma siku Magufuli alipokufa
Tena ni mwanamke!!!!!!Nina wasiwasi sana na huyu jaji
Haaa🙄Sasa polisi ukafanye nini wakati we ndo mzazi???😎
Ndiyoo! Sitaki kusema mengi nisije nikatukana wanawake, maana kuna wakunga humu JF!Tena ni mwanamke!!!!!!
Una maanisha alisingiziwa Mkuu. Ndio maana nikasema, hapa kulikuwa na ushahidi wa mtoto. Hivi kweli kwa unavyoona, nikitaka kukubambikia kesi, nitatumia mtoto wa miaka sita kama shahidi wangu mkuu?Ila waza pia kama huyo anayeitwa mbakaji akawa si mbakaji alisia itakuwaje?
Ni kweli ni mambo yanayoumiza sana, lakini kesi ina jengwa toka polisi, ushahidi ukishaharibiwa tu, basi na mala nyingi mahakama za chini hata huwa sielewi maamuzi mengine huwa wanayafikia vipi, na yakifika kwa majaji, mengi huwa yanatupiliwa mbali!!sasa kweli ushahidi wa suruali nao ulikuwa mgumu kuwa nao?mambo ya sheria ndugu ni magumu usichukulie tu kwa kuwa ni mtoto kasema basi ni ushahidi tosha!kuna kesi ngapi ambazo watu wamewatumia watoto kuwabambikizia kesi maadui zao, na baada ya muda watoto hao walipokuja kuwa wakubwa wakakiri kuwa haikuwa kweli?!!wakati mtu ameshachezea miaka kibao tu jela?Nadhani ushahidi wa kesi nyingi za ubakaji /ulawiti zinaharibiwa toka mwanzo kabisa, ngazi ya familia, hospitalini na polisi.Hebu fikiria. Mtoto wako wa miaka sita anatoka shule. Akiwa njiani mjinga fulani mwenye akili mbaya kuliko mnyama anamkamata na kumvutia porini, kisha anambaka na kumuumiza sana. Mtoto huyu wa miaka sita analia kwa maumivu, lakini mbakazi anamziba mdomo na kumtishia kumuua ikiwa ataendelea kupiga kelele au kumtaja kwa watu.
Mtoto wako huyu anarudi nyumbani analia na ametapakaa damu kwenye suruali yake. Unamwangalia kwa uchungu na kugundua mtoto wako mdogo kipenzi, miaka sita tu, darasa la kwanza, amebakwa na kuumizwa sana. Unamuuliza nani amefanya hivi anakutajia ni fulani, kwa kuwa anamfahamu aliyembaka.
Unamchukua mtoto na kumpeleka polisi. Polisi wanafungua jarida la kesi, lakini wala hawakuulizi nguo alizobakwa nazo ziko wapi. Mnampeleka mtoto hospitali, daktari anaemtibu wala hafanyi jitihada za kuchukua sampuli ndani ya mtoto na kuzihifadhi ili waje wafanye DNA test.
Kesi inapoenda mahakamani, mbakaji anafungwa kwa ushahidi wa kutambuliwa na mtoto. Lakini baadaye, jaji mtukuka wa mahakama ya rufaa anasema mbakaji aachiliwe huru kwa kuwa wakati wa kesi ile suruali yenye damu aliyokuwa amevaa mtoto haikuletwa mahakamani kama ushahidi. Mbakaji yuko huru.
Fikiria kama huyo mtoto wa miaka sita ni wa kwako, waangalie watoto wako, au watoto wa ndugu yako wa karibu, halafu piga picha wao ndio wamefanyiwa hivyo. Unajisikiaje?
Hii sio hadithi, ni tukio la kweli. Hawa ndio polisi wetu. Hawa ndio madaktari wetu. Hawa ndio majaji wetu. Hodari na makini sana katika kufuatilia kesi za siasa na kufunga watu kwa kesi za kubambikiwa, lakini sio kesi za watoto wa miaka sita kubakwa na kuumizwa.
Sasa niambie kama nikisema nchi yetu Tanzania ni banana republic, una sababu gani za kunibishia?
Reference: Suruali yenye damu ilivyotengua hukumu
Una point nzuri sana. Ila sisi kutoa judgement kwa kusoma tu kilichoandikwa kwenye gazeti nadhani tunaweza tusitende haki kwa jaji aliyesikiliza. Bila kusoma hukumu yote na jinsi cross examination ilivyokwenda tunaweza tusijue kama mtoto alionekana kusema ukweli au uongo. Lawama nyingi ziwaendee polisi walioshughulikia hii case. Hata kama huna vifaa vya utambuzi kwa wakati ule lakini kitu kama hiyo suruali na mabaki ya manii kama yalikuwepo ilikuwa ni muhimu kabisa kabisa vichukuliwe na kuhifadhiwa. Ulaya sasa hivi kuna cases za miaka ya nyuma kabisa wakatika DNA haijagundulika zinateguliwa kwa sababu waliweka exbit za matukio. Polisi waliohusika wote inabidi waondolewe kazini kwa uzembe.Mkuu, unajua uzito wa ushahidi wa mtoto katika kesi? Katika kesi hii inawezekana kusiwe na collaborating evidence, lakini haiondoi uzito wa ushahidi wa mtoto. Hivyo jaji alitakiwa aangalie sana upande huu.
Mtoto wa miaka sita ukimwambia akadanganye ni fulani kambaka, ukimfanyia cross examination ya juu kutumia mtaalamu wa saikolojia, ataishia kusema baba alisema nimtaje fulani. Jaji anajua kabisa kwamba kama mtoto alisema ni fulani kanibaka uwezekano wa kuwa si kweli ni o.o1%, kwa hiyo hakupaswa kusimamia rufaa kwenye suruali, bali alipaswa kusimamia kwenye ukweli wa aliyosema mtoto.
Kama rufaa ingejenga shaka juu ya ushahidi wa mtoto hapo ningekubaliana na jaji. La sivyo huyu lazima ni jaji kihiyo tu, wale majaji wa Magufuli labda.
Jamhuri inatakiwa kukata rufaa ili hukumu ya huyu jaji mpuuzi itupiliwe mbali.
Mkuu, kama judgement ya rufaa ingetokana na ushahidi wa mtoto, kwa nini gazeti liandike imetokana na suruali? Hapo unalaumu tunatoa judgement, lakini wewe ndio unatoa judgement kwa kitu ambacho hakipo kwenye taarifa ya gazeti.Una point nzuri sana. Ila sisi kutoa judgement kwa kusoma tu kilichoandikwa kwenye gazeti nadhani tunaweza tusitende haki kwa jaji aliyesikiliza. Bila kusoma hukumu yote na jinsi cross examination ilivyokwenda tunaweza tusijue kama mtoto alionekana kusema ukweli au uongo. Lawama nyingi ziwaendee polisi walioshughulikia hii case. Hata kama huna vifaa vya utambuzi kwa wakati ule lakini kitu kama hiyo suruali na mabaki ya manii kama yalikuwepo ilikuwa ni muhimu kabisa kabisa vichukuliwe na kuhifadhiwa. Ulaya sasa hivi kuna cases za miaka ya nyuma kabisa wakatika DNA haijagundulika zinateguliwa kwa sababu waliweka exbit za matukio. Polisi waliohusika wote inabidi waondolewe kazini kwa uzembe.
Hoja yangu ni kuwa ili uweze kujua kama jaji alipotoka, ni lazima upitie kesi nzima. Usome mashahidi wote walivyowasilisha ushahidi wao, walivykuwa cross examined nk. Uandishi wa Tanzania mimi najua, na pengine hata wewe unaujua. Hapa inawezekana jaji alitilia maanani vipengele vingine pamoja na cha hiyo suruali. Mimi skutoa judgement yoyote ila nimetoa tahadhari kuwa inatakiwa tujue mwendendo mzima wa kesi. Kitu ambacho mimi naona kipo wazi hapa ni uzembe wa polisi katika kuchukua vielelezo. Au pengine inaweza isiwe ni uzembe bali ni makusudi baada ya mshukiwa kuwashikisha kitu kidogo. Otherwise inauma sana sana kwa kitendo alichofanyiwa huyo mtoto na zinatakiwa hatua zaidi zichukuliwe ili kama yeye ndiye mhusika basi apate haki yake.Mkuu, kama judgement ya rufaa ingetokana na ushahidi wa mtoto, kwa nini gazeti liandike imetokana na suruali? Hapo unalaumu tunatoa judgement, lakini wewe ndio unatoa judgement kwa kitu ambacho hakipo kwenye taarifa ya gazeti.
View attachment 1855026
Mkuu yote yanawezekana na ndio maana Mahakama haina desturi ya kutumia hisia kutia hukumu na wengi wanaotumia hisia huwa wanafeli.Una maanisha alisingiziwa Mkuu. Ndio maana nikasema, hapa kulikuwa na ushahidi wa mtoto. Hivi kweli kwa unavyoona, nikitaka kukubambikia kesi, nitatumia mtoto wa miaka sita kama shahidi wangu mkuu?
Huhitaji kuwa na PhD ya saikolojia au hata ya kubangua korosho kama ya Magufuli kujua kwamba huyu mtoto wa miaka sita anadanganya kaambiwa cha kusema
Point unazotoa huna tofauti na huyu jaji. Mie ninasema, kesi hiiinapaswa kusimamia kwenye ushahidi wa mtoto, wewe unachomaanisha i kuwa mtoto anaweza kudanganya. Ngoja mwanao wa miaka sita siku aje anavuja damu na kukuambia amebakwa na jirani ndio umtilie shaka kuwa anadanganyaMkuu yote yanawezekana na ndio maana Mahakama haina desturi ya kutumia hisia kutia hukumu na wengi wanaotumia hisia huwa wanafeli.
Kuna msemo Mahakamani, "Ni bora kumuachia mkosaji huru kuliko kumfunga asiye na hatia" huu unajibu kila jambo hapo juu Mkuu.