Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,755
Tumeshuhudia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akivalia njuga wanawake wanaojiuza almaarufu makahaba. Zoezi lilianzia kwenye kuvamia na kuvunja vibanda maarufu vijjlikanavyo kama Vibanda vya Wahaya na kuwatia mbaroni baadhi yao.
RC Chalamila anayesifika kwa tabia za ufyatu ambapo aliwahi kusikika akisema kuwa akimkuta kibaka nyumbani kwake anamuua na hata aliwahi kusema hivi karibuni kuwa akiliamsha dude hakuna wa kumfanya lolote (hata sheria), amenadi kuwa ataendelea kuwasaka wanaojiuza miili yao kila kona ya mkoa wa Dar.
Juzi tu kumetokea mauaji mjini Dar es salaam kwenye Bar moja iliyopo Sinza iitwayo Boardroom (mlinzi wa bar hiyo aliuawa kwa risasi kutoka bunduki ya askari wetu), chanzo cha mauaji hayo yaliyofanywa na Askari Mbumbumbu ni kwenda kuwasaka makahaba hapo Bar!
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa chini ya mwenyekiti wake wanawajibika na tukio hili la kinyama. Serikali inaendaje kuwasaka wanawake wanaojiuza kwa kutumia mtutu?
Chalamila ni mteule wa Rais, na kama inavyozoeleka mama huwalinda wale anaowapenda. Tunaamini kuwa Chalamila akiendelea kuwepo ofisini inapelekea jamii kuamini kuwa mteuzi anaridhika na mwenendo na maadili ya RC Chalamila.
Tunataka uwajibikaji na sheria ichukue mkondo wake kwa sababu maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa yamepelekea mauaji ambayo yangeweza kuepukika endapo busara zingetumika. Kuanzia muuaji na wote wanaohusika na sakata hili wanapaswa kufikishwa mbele ya sheria ili haki ipatikanike.
Maadili ya viongozi wengi wa CCM imepelekea chama hiko kuwa kichaka cha wahalifu
Pia Soma Boniface Jacob: Polisi walioua Mlinzi wa Bar ya Boardroom Sinza wadaiwa kutumwa na RC Chalamila kukamata Wanaojiuza