Polepole kasema nyuma yake wapo kina Mzee Warioba

Polepole kasema nyuma yake wapo kina Mzee Warioba

Humphrey PolePole ni kama vile alikuwa akiwahutubia vijana wa bodaboda ambao wengi wao hawakuwepo wakati wa Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete na namna walifanikiwa kuwa Marais wa Tanzania.

Pia alifanikiwa kutuambia kuwa nyuma yake wako pia akina Mzee Warioba na wazee wenzake wa kanda ile.

Na mwisho amefanikiwa kuonyesha kuwa kuna vita ya udini kwenye uongozi; hasa baada ya kuonyesha kuwa Mkapa alipata kura chache alipogombea kwa mara ya kwanza kwa makosa ya matangulizi wake Mzee Mwinyi (mwislam) na Magufuli alipata kura chache alipogombea kwa mara ya kwanza kwa makosa ya Jakaya (mwislamu). Kwenye hili Polepole alisema kuwa unapogombea kwa mara ya kwanza kura utakazopata sio za kwako, bali za Rais aliyekukabidhi kijiti. Hapa natofautiana nae kabisa, kwakuwa kwenye uchaguzi wa 1995 Mkapa alikuwa hajulikani ukilinganisha na mgombea wa upinzani; Lyatonga Mrema. Mwl Nyerere ndiye aliyemsaidia kupiga kampeni vinginevyo angedondoshwa; sio kwasababu ya udhaifu wa uongozi wa Mzee Mwinyi. Mwl Nyerere alidiriki kusema hawezi kulala nyumbani eti kwasababu ya ubaba wa taifa, wakati yuko jukwaani akasema "I can not let my country go to the dogs". Hivyo tatizo ni CCM kumsimamisha mgombea (Mkapa) ambae hajulikani kwa watu.

Magufuli alipata kura chache uchaguzi wa 2015 kwasababu Lowassa alikuwa na nguvu kuliko JPM, sio kwasababu ya uongozi wa JK ulikuwa mbaya. Hapa Humphrey anaongelea udini kwakuwa anafahamu kuwa uchaguzi wa 2020 JPM alishinda kwa kuwaengua wapinzani wote na kuiba kura.

Nijuavyo mimi Humphrey na wenzake wataashindana lakini hawatashinda hii vita ya udini.

Humphrey anawadanganya watoto wachanga kuwa mchakato wa katiba ulivunjika kwasababu ya rasimu ya katiba ilikuwa inawabana viongozi wabadhilifu ndiyo maana JK aliikataa. Huu ni upuuzi sawa na upuuzi mwingine kwakuwa katiba mpya pendekezwa ingeanza kufanyakazi baada ya uongozi wa JK kumalizika na kuondoka madarakani; hivyo, JK hakuwa na sababu ya kuiogopa katiba ambayo ina masharti magumu kwa viongozi. Sababu ya kweli ya kuvunjika uwandishi wa katiba mpya ni Mzee Warioba na Polepole ambao walikuwa wanataka muungano wa serikali 3 badala ya serikali 01 ya sasa; hoja ambayo ilikuwa inahofiwa kuwa itakwenda kuvunja muungano hasa baada ya kuungwa mkono na UKAWA.

The main agenda sasa imefahamika kuwa ni UDINI, UDINI, UDINI kwakuwa kuna watu hawakutaka Samia (mwislamu) kuwa Rais baada ya JPM kufariki. Hii ni ajenda ya kidini kabisa, hakuna lingine hapo. Walimkataa hata kabla ya kujua ataongozaje atakapoapishwa. Sasa tuko tayari watanzania kwa hili.


View: https://youtu.be/0j3WOvqNL_A?si=LrrfTy6_Ek55Bzso

Warioba ndio nani kwa siasa za sasa? Kazeeka aende kulea vitukuu huko

Vijana wengi ambao ndio population kubwa kwa sasa hawamjui huyo kizee kikongwe warioba ni nani na kwenye historia wala hawajamsoma au hata kwenye somo la uraia au civics yeye na Butiku.na huyo Polepole

Wanajitutumua kwenye generation isiyowajua

Nyerere wanamjua kwenye somo la uraia lakini Warioba au Butiku au Polepole hawawajui

Wanapoteza muda tu hii sio generation yao hawamjui Farao Warioba au Butiku au Polepole
 
Watu hawanashida na Mama polepole nae kalisema ila wanasema wale watu ambao wako nyuma yake ndo tatizo la wanachama wazalendo koko wa CCM but hii nchi ina matapeli wengi na wengine hawajapewa Power tu polepole ni mzuri wa kujenga hoja sema hoja zake zinakosa nguvu sana Japokua zina nguvu ila Past ya polepole ina muhukumu. Kama z
Lissu kushindwa kutoka kumkataa Lowassa kipindi amekuja Chadema Japokua pia Lowasa hakua mchafu hivo ziadi ya Propaganda za watu walele wale kumchafua mzee Muacheni mama ale Maisha ila Maombi yangu Mama muachie Lissu JK kua karibu na Samia kama Mkapa alivyokua karibu na Magu japo JK kazidi
 
Actually Warioba alishajiuzulu u Waziri Mkuu uongozi wa Mwinyi. Ndiyo Malecwla akachaguliwa kuwa Waziri Mkuu. Kwa hiyo hoja ya Warioba hajajiuzulu si kweli. Labda mliambiwa tu Rais kabadili baraza la mawaziri kwa kumlindia heshima rais tu.
Siyo kweli. Warioba aliangishwa ubunge na Wasira akiwa mgombea Jimbo la Warioba kupitia nccr .
 
Mambo magumu yanajibiwa Kwa lugha nyepesi

Mtu ambae amewahi kula kiapo Kwa Marais 3 anajibiwa na mtu ambae ajawahi hata kula kiapo cha kumpa mtu dhamana mahaka ya mwanzo
Sio tu mahakamani yaan hajawai hata kumdhanini mtu kituo Cha polisi
 
Bahati nzuri 2015 nilikuwa mkubwa tu,kwahyo acha kubwabwaja

Hakuna kipindi ambacho watz waliichoka ccm kama kipindi hicho,unajua kwanini?

Kwasababu watanganyika walikuwa wameshasikia habari nyingi za uongozi wa kikwete kutoka kwa wapinzani
Acha uongo, habari mbaya za kuuza mashirika ya umma, nyumba za serikali na mauaji ya watu zanzibar alikuwa nazo mkapa. Wananchi walikuwa wamekasirika sana akina Daniel Yona, Basil mramba, Ana mkapa walivyokuwa mafisadi hadi Nyerere akakasirika sana. Nadhani ugonjwa wake ulianzia hapo hata kufa.
 
Sikubaliani nawe kuwa Rome has spoken. Kuna malalamiko mengi sana.

Pia, hata kama Rome has spoken, what is Rome?

That logical fallacy is an argument from authority fallacy.

Ila inaonekana kuna woga huo unaousema.

La sivyi, angwjitangaza mtu anayetaka kugombea urais kwa tiketi ya CCM akisema yeye kavunjiwa haki yake na anataka mchakato urudiwe.

Hizi habari za kusema kwa desturi na utamadu i Samia hafai ni woga tu. Ni jitihada za kumuondoa Samia kinyume na katiba. Na mimi nasema jivyo si kama mtetezi wa Samia, SMia namuona kapwaya, mimi nasema hivyo kama mtetezi wa ukatiba.

Kama Samia hafai kweli, waombe mchakato wa kumpata mgombea wa CCM urudiwe halafu wajumbe wamteue upya mgombea wa CCM, Samia aruhusiwe kuweka jina lake tena pamoja na wengine, tuone wajumbe wataamua vipi.
Rome kwenye hili ni wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM. Fanya ufanyavyo hawa ndiyo wenye chama, they have spoken (ratified)
 
Warioba ndio nani kwa siasa za sasa? Kazeeka aende kulea vitukuu huko

Vijana wengi ambao ndio population kubwa kwa sasa hawamjui huyo kizee kikongwe warioba ni nani na kwenye historia wala hawajamsoma au hata kwenye somo la uraia au civics yeye na Butiku.na huyo Polepole

Wanajitutumua kwenye generation isiyowajua

Nyerere wanamjua kwenye somo la uraia lakini Warioba au Butiku au Polepole hawawajui

Wanapoteza muda tu hii sio generation yao hawamjui Farao Warioba au Butiku au Polepole
Mzee Warioba na Butiku wanataka kujipa nguvu za Nyerere ambazo hawana. Hata Nyerere mwenyewe alishazipotezaga nguvu hizo kabla hajafa. Akiwa hai Mzee Mwinyi aliua Azimio la Arusha na kuleta Azimio la Zanzibar na Mkapa aliyapiga mnada mashirika ya umma yeye akiwepo. Mzee warioba na butiku wanadhani Tanzania ni ya Nyerere, hivyo ni ya Butiyama.

Mkutano mkuu ndiye Pope kwenye hili, ukishapitisha hamna wa kujadili tena labda uende mahakamani kama unayo hoja other than desturi na utamaduni.
 
kavulata said:
Mzee Warioba na Butiku wanataka kujipa nguvu za Nyerere ambazo hawana. Hata Nyerere mwenyewe alishazipotezaga nguvu hizo kabla hajafa.
Duh, wengine tulikuwepo na bado tupo. kavulata masikini, ukipata nafasi ya kula kivulini bila kuhangaika juani, usije ukachezea shilingi karibu na tundu la choo...huo ni ushauri tu!
 
Duh, wengine tulikuwepo na bado tupo. kavulata masikini, ukipata nafasi ya kula kivulini bila kuhangaika juani, usije ukachezea shilingi karibu na tundu la choo...huo ni ushauri tu!
Dawa pekee ya kuwaadhibu wajumbe wa Mkutano Mkuu ni Polepole na kundi lao la akina Warioba, Butiku, Gwajima, Kitima, nk (Wakristu) watoke CCM/TANU/TAA wakaunde chama chao kipya halafu Warioba anakuwa mgombea, au wagombee kupitia chama cha siasa kidogo cha upinzani na mgombea wao agombee kupitia chama hicho ili wakishinde CCM na Samia wao. Vinginevyo, CCM hakuna mtu mmoja au kikundi ambacho kina kura ya veto kama vile Polepole na wenzake wanavyotaka wafahamike. Polepole ni mwanachama sawa na mwanachama mwingine ndani ya CCM. Hiyo desturi ya regime change kila miaka 10 imeandikwa na kusimuliwa wapi wapi ili wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wakaisome au wakaisikilize?.

Sasa ndiyo tunajua watu waliompotosha Mh. Ndugai wakati wa kutafuta mtu wa kubeba mikoba ya JPM baada ya mwenyeziMungu kumuondoa duniani.

CCM hakikuwa chama cha Nyerere; hata yeye alisemaga CCM sio baba wala mama yake, angeweza kukihama. Ukitaka ukweli wa MwenyeziMungu wamiliki wa CCM halisi ni watu wa pwani, ndio waanzilishi wa TAA iliyounda TANU na ASP na baadae ikatokea CCM. Tuko macho na wahuniwahuni ambao wanataka kuiteka CCM na kuiweka mabegani mwao na kuitoa kwa wadhamini na Mkutano Mkuu wa chama.
 
Rome kwenye hili ni wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM. Fanya ufanyavyo hawa ndiyo wenye chama, they have spoken (ratified)
Wajumbe wamesema kwa kufanyiwa ambush.

Wajumbe wamesema Kabla bunge halijavunjwa?

Wajumbe wamesema kwenye kikao chenye ajenda tofauti?

Waliotaka kushindana na Samia wamepewa nafasi wapi kishindana naye?

Dr. Malisa kafungua kesi kuweka rekodi mtamdhibiti kwa hukumu ya amri kutoka juu lakini tunajua mmezoea magoli ya mkono.
 
What if me ni myahudi na unapinga tamaduni zetu? That's why nataka nikujue Kwanza ili usije na reference za kusoma vitabu
Ukweli utabaki ukweli bila kujali nani kausema.

Ukweli haubadiliki kuwa uongo kwa sababu umesemwa na Kiranga.
 
Wajumbe wamesema kwa kufanyiwa ambush.

Wajumbe wamesema Kabla bunge halijavunjwa?

Wajumbe wamesema kwenye kikao chenye ajenda tofauti?

Waliotaka kushindana na Samia wamepewa nafasi wapi kishindana naye?

Dr. Malisa kafungua kesi kuweka rekodi mtamdhibiti kwa hukumu ya amri kutoka juu lakini tunajua mmezoea magoli ya mkono.
Katiba ya Jamhuri haipangii vyama vya siasa namna ya kuwapata wagombea wake. Hata zoezi la kuandikisha wapiga kura ni sehemu ya uchaguzi, lakini linafanyika kabla ya bunge kuvunjwa. Hakuna kifungu kwenye Katiba ya jamhuri imetaja specifically kwamba vyama vya siasa visiwatambue wagombea wao wa urais kabla ya bunge kuvunjwa. Katiba haikusema ni kitu gani na gani na gani hakiruhusiwi kufanyika kabla ya bunge kuvunjwa. Je, kuandikisha wapiga kura kwenye daftari la wapigakura, vyama vya siasa kusaini maadili ya uchaguzi sio mchakato wa uchaguzi?
 
Katiba ya Jamhuri haipangii vyama vya siasa namna ya kuwapata wagombea wake. Hata zoezi la kuandikisha wapiga kura ni sehemu ya uchaguzi, lakini linafanyika kabla ya bunge kuvunjwa. Hakuna kifungu kwenye Katiba ya jamhuri imetaja specifically kwamba vyama vya siasa visiwatambue wagombea wao wa urais kabla ya bunge kuvunjwa. Katiba haikusema ni kitu gani na gani na gani hakiruhusiwi kufanyika kabla ya bunge kuvunjwa. Je, kuandikisha wapiga kura kwenye daftari la wapigakura, vyama vya siasa kusaini maadili ya uchaguzi sio mchakato wa uchaguzi?
Kiti cha urais kinakuwa katika campaign mode baada ya bunge kuvunjwa.

Kabla ya hapo akiingia kwenye campaign inakuwa kaanza campaign kabla ya muda.

Hata Usain Bolt, mwanariadha mahiri kabisa, alivyoanza kukimbia kabla ya bastola ya kuruhusu kukimbia haijapigwa alirudishwa kuanza mbio upya.

Wajumbe mmewaburuza hata Kikwete mwenyewe mleta hoja kajua kasema tusiharibu sana mambo, ina maana alijua anaharibu ila hakutaka kuharibu sana.

Watu wengine wa CCM waliotaka kushindana na Samia walipewa nafasi lini kushindana naye?
 
Mtu aliyeelimika hata kwa level ya baby class hawezi kuandika a logical fallacy kama hii. Ni wewe tu kwa uwazi huu umethibitishia dunia ijayokusoma hapa bado uko na ignorance ya asilimia 99. 9! Maana hauko scientific
Sorry!
Huna akili, kwa hiki kingereza chako cha unga unga mwana ndiyo unajiona umeelimika?
 
Reference yako ya ukweli ni ipi?
Logical consistency.

Logical consistency haitegemei msemaji wa jambo ni nani.

Kama nyeupe nyeupe tu, kama nyeusi nyeusi tu, bila kutegemea nani anasema.

Sasa kwa nini uangalie nani anasema badala ya kuangalia kama anachosema ni kweli?

Kwani Kiranga akisema hii nyeupe, wakati ni nyeupe kweli, itakuwa nyeusi kwa sababu Kiranga kasema?
 
Back
Top Bottom