Polepole kasema nyuma yake wapo kina Mzee Warioba

Polepole kasema nyuma yake wapo kina Mzee Warioba

Kiti cha urais kinakuwa katika campaign mode baada ya bunge kuvunjwa.
Ni tukio gani linaashiria sasa Rais ambae yuko madarakani yuko kwenye campaign mode. Rais Samia katangaza tangu muda mrefu kuwa atagombea tena, Lissu alitangaza tangu zamani kuwa atagombea tena. Lakini mama anatoa goli la mama na picha yake iko kwenye mabango na t-shirts, pikipiki na baisjeli za SSH zipo tu kwa muda mrefu mitaani, mama anaendelea kuzindua makanisa, migodi, viwanda, reli, bandari, nk kila kona kama Rais. Unaweza kutenganisha vipi kati Samia kama Mwenyekiti wa CCM, Mkuu wa nchi, Rais wa nchi, Amirijeshi mkuu au mgombea urais?. Wakati bodaboda za SSH zikiwa zinaonekana mitaani kwanini wanaopinga hawakupiga kelele? kwanini nao hawakutoa t-shirts za mgombea wao Warioba au Polepole au Gwajima?

Nadhani muende mkasome tena Katiba ili muone kama kuna kifungu kinakataza vyama vya siasa visiwathibitishe wagombea wao wa kiti cha Urais kabla ya bunge kuvunjwa.
 
Nyerere aliiua EAMWS akaunda tiss-kitengo cha bakuwata
Angalia Nyerere alivyomshambulia Ali Hassan Mwinyi akiwa Rais na Nyerere alivyomnyamazia Mkapa alipokuwa anauza makampuni na nyumba za serikali. Alilalamika kidogo sana kwa kusema, unauza hata kiwanda cha bia ambacho wanyaji wapo wengi.
 
Ni tukio gani linaashiria sasa Rais ambae yuko madarakani yuko kwenye campaign mode. Rais Samia katangaza tangu muda mrefu kuwa atagombea tena, Lissu alitangaza tangu zamani kuwa atagombea tena. Lakini mama anatoa goli la mama na picha yake iko kwenye mabango na t-shirts, pikipiki na baisjeli za SSH zipo tu kwa muda mrefu mitaani, mama anaendelea kuzindua makanisa, migodi, viwanda, reli, bandari, nk kila kona kama Rais. Unaweza kutenganisha vipi kati Samia kama Mwenyekiti wa CCM, Mkuu wa nchi, Rais wa nchi, Amirijeshi mkuu au mgombea urais?. Wakati bodaboda za SSH zikiwa zinaonekana mitaani kwanini wanaopinga hawakupiga kelele? kwanini nao hawakutoa t-shirts za mgombea wao Warioba au Polepole au Gwajima?

Nadhani muende mkasome tena Katiba ili muone kama kuna kifungu kinakataza vyama vya siasa visiwathibitishe wagombea wao wa kiti cha Urais kabla ya bunge kuvunjwa.
CCM kumpitisha mgombea ni campaign tayari.

Huwezi kupitishwa kuwa mgombea bila kuomba kupitishwa, na kuomba kupitishwa kuwa mgombea tayari ni campaign.
 
Logical consistency.

Logical consistency haitegemei msemaji wa jambo ni nani.

Kama nyeupe nyeupe tu, kama nyeusi nyeusi tu, bila kutegemea nani anasema.

Sasa kwa nini uangalie nani anasema badala ya kuangalia kama anachosema ni kweli?

Kwani Kiranga akisema hii nyeupe, wakati ni nyeupe kweli, itakuwa nyeusi kwa sababu Kiranga kasema?

Mbona uzunguka sana,
Hoja yako ni nini?
 
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM
Ok kwanini unahoji Polepole kuwa na mtu nyuma ilhali kuna hoja zake alizozitoa.

Kwanini usijibu au kuchambua hoja zake badala yake unaangalia walio nyuma yake?

Wajumbe hao walio nyuma yako ndio wamechemka kutoa maamuzi na Polepole katoa maelezo yake walichemka wapi wewe badala ujibu unaangalia source ya hoja zimetokea wapi.

Na mimi nikuulize tu swali jepesi pikipiki na baiskeli zenye nembo ya Samia ziligawiwa kwa malengo gani je ni kampeni au msaada?

Toa majibu ya kina kutetea hoja zako.
 
Mbona uzunguka sana,
Hoja yako ni nini?
Hoja yangu ni kukuambia jadili hoja usimjadili mtu.

Wewe umetoka kujadili hoja unanijadili mimi.

Hiyo ni logical fallacy, ad hominem logical fallacy.

Jadili hoja, usimjadili mtu.

Huelewi wapi?
 
CCM kumpitisha mgombea ni campaign tayari.

Huwezi kupitishwa kuwa mgombea bila kuomba kupitishwa, na kuomba kupitishwa kuwa mgombea tayari ni campaign.
Toa ibara ya katiba ya CCM au Katiba ya Jamhuri inayokataza kumpitisha mgombea urais kabla ya bunge kuvunjwa. Tafsiri yangu mimi campaign mode ni pale ambapo bunge limevunjwa na wabunge wako majimboni kuomba upya ridhaa ya kuchaguliwa kuwa wabunge, na mikutano ya hadhara inaitishwa kuwanadi wagombea na kuomba kura.
 
Wait.

Kwa maneno yako hayo.

Kwa hiyo Bunge likivunjwa na wabunge wakaamua kubaki Dodoma hapo inakuwa si campaign mode?

Kinachofanya campaign mode ianze ni ni i? Ni bunge kuvunjwa au ni wabunge kurudi majinboni?
 
Sasa hoja si lazima urudi kwenye msingi wa watu ambao tunawazungumzia?

Unasema wayahudi hawana utaratibu wa kuvua viatu ndio maana nimekuuliza wewe ni myahudi? Jibu ni ndio au hapana then usikilize nataka kusema kitu gani
Hoja ni, je Wayahudi wana utaratibu wa kuvua viatu ama la?

Mimi nasema kuhusu hoja hiyo.

Kwa nini mimi kuwa Myahudi au si Myahudi ni muhimu?

Kama Wayahudi wana utaratibu wa kuvua viatu, mimi nikiwa Myahudi ndiyo kutabadili ukweli huo?

Mimi nikiwa Msukuma si Myahudi kutabadili ukweli huo?
 
Ok kwanini unahoji Polepole kuwa na mtu nyuma ilhali kuna hoja zake alizozitoa.

Kwanini usijibu au kuchambua hoja zake badala yake unaangalia walio nyuma yake?

Wajumbe hao walio nyuma yako ndio wamechemka kutoa maamuzi na Polepole katoa maelezo yake walichemka wapi wewe badala ujibu unaangalia source ya hoja zimetokea wapi.

Na mimi nikuulize tu swali jepesi pikipiki na baiskeli zenye nembo ya Samia ziligawiwa kwa malengo gani je ni kampeni au msaada?

Toa majibu ya kina kutetea hoja zako.
Huwezi kuzipa uzito hoja za Polepole kwakuwa anazitoa akiwa uvunguni mwa kitanda cha mke mdogo, pili Polepole ni mwanachama sawa na mwanachama mwinyine (hana veto), tatu Polepole amebase kwenye mila na desturi na utamaduni wakati anapochafua watu, nne Polepole anafahamu kuwa Mkutano Mkuu wa CCM ndicho chombo cha juu sana cha maamuzi kwenye chama; yaani kwa wakatoliki unaweza kufananisha na Pope of Vatican. Anachokifanya Polepole ni nuisance tu ndani ya chama na mgombea wa CCM. Lakini kwakuwa CCM ndicho chama tawala anahatarisha amani na utulivu wa nchi.

Mimi binasfi namuona Polepole kama kielelezo cha kukua kwa demokrasia nchini kuhusu uhuru wa kusema tulionao katika awamu hii ya sita. Kama angetokea mtu kama Polepole kwenye awamu ya tano ya JPM huenda angeshaikimbia nchi. Mama Samia ni bingwa wa demokrasia ndiyo maana akina Polepole unawasikia sauti zao.
 
Humphrey PolePole ni kama vile alikuwa akiwahutubia vijana wa bodaboda ambao wengi wao hawakuwepo wakati wa Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete na namna walifanikiwa kuwa Marais wa Tanzania.

Pia alifanikiwa kutuambia kuwa nyuma yake wako pia akina Mzee Warioba na wazee wenzake wa kanda ile.

Na mwisho amefanikiwa kuonyesha kuwa kuna vita ya udini kwenye uongozi; hasa baada ya kuonyesha kuwa Mkapa alipata kura chache alipogombea kwa mara ya kwanza kwa makosa ya matangulizi wake Mzee Mwinyi (mwislam) na Magufuli alipata kura chache alipogombea kwa mara ya kwanza kwa makosa ya Jakaya (mwislamu). Kwenye hili Polepole alisema kuwa unapogombea kwa mara ya kwanza kura utakazopata sio za kwako, bali za Rais aliyekukabidhi kijiti. Hapa natofautiana nae kabisa, kwakuwa kwenye uchaguzi wa 1995 Mkapa alikuwa hajulikani ukilinganisha na mgombea wa upinzani; Lyatonga Mrema. Mwl Nyerere ndiye aliyemsaidia kupiga kampeni vinginevyo angedondoshwa; sio kwasababu ya udhaifu wa uongozi wa Mzee Mwinyi. Mwl Nyerere alidiriki kusema hawezi kulala nyumbani eti kwasababu ya ubaba wa taifa, wakati yuko jukwaani akasema "I can not let my country go to the dogs". Hivyo tatizo ni CCM kumsimamisha mgombea (Mkapa) ambae hajulikani kwa watu.

Magufuli alipata kura chache uchaguzi wa 2015 kwasababu Lowassa alikuwa na nguvu kuliko JPM, sio kwasababu ya uongozi wa JK ulikuwa mbaya. Hapa Humphrey anaongelea udini kwakuwa anafahamu kuwa uchaguzi wa 2020 JPM alishinda kwa kuwaengua wapinzani wote na kuiba kura.

Nijuavyo mimi Humphrey na wenzake wataashindana lakini hawatashinda hii vita ya udini.

Humphrey anawadanganya watoto wachanga kuwa mchakato wa katiba ulivunjika kwasababu ya rasimu ya katiba ilikuwa inawabana viongozi wabadhilifu ndiyo maana JK aliikataa. Huu ni upuuzi sawa na upuuzi mwingine kwakuwa katiba mpya pendekezwa ingeanza kufanyakazi baada ya uongozi wa JK kumalizika na kuondoka madarakani; hivyo, JK hakuwa na sababu ya kuiogopa katiba ambayo ina masharti magumu kwa viongozi. Sababu ya kweli ya kuvunjika uwandishi wa katiba mpya ni Mzee Warioba na Polepole ambao walikuwa wanataka muungano wa serikali 3 badala ya serikali 01 ya sasa; hoja ambayo ilikuwa inahofiwa kuwa itakwenda kuvunja muungano hasa baada ya kuungwa mkono na UKAWA.

The main agenda sasa imefahamika kuwa ni UDINI, UDINI, UDINI kwakuwa kuna watu hawakutaka Samia (mwislamu) kuwa Rais baada ya JPM kufariki. Hii ni ajenda ya kidini kabisa, hakuna lingine hapo. Walimkataa hata kabla ya kujua ataongozaje atakapoapishwa. Sasa tuko tayari watanzania kwa hili.

View: https://youtu.be/0j3WOvqNL_A?si=LrrfTy6_Ek55Bzso

View: https://www.facebook.com/reel/1785835091953566
 
Mzee Warioba na Butiku wanataka kujipa nguvu za Nyerere ambazo hawana. Hata Nyerere mwenyewe alishazipotezaga nguvu hizo kabla hajafa. Akiwa hai Mzee Mwinyi aliua Azimio la Arusha na kuleta Azimio la Zanzibar na Mkapa aliyapiga mnada mashirika ya umma yeye akiwepo. Mzee warioba na butiku wanadhani Tanzania ni ya Nyerere, hivyo ni ya Butiyama.

Mkutano mkuu ndiye Pope kwenye hili, ukishapitisha hamna wa kujadili tena labda uende mahakamani kama unayo hoja other than desturi na utamaduni.
Uko sahihi hawa wazee vikongwe Warioba na Butiku bado wanaota Nyerere

Hizi zama sio za Nyerere

Kila zama na kitabu chake Raisi Mzee Mwinyi alisema

Wao wanadhani na huyo kizee Polepole wanadhani kitabu cha enzi za Nyerere ni cha enzi zote Sio kweli Hata vitabu vyao sio vya enzi zote

Kila enzi na zama zina vitabu vyao

Watulie kimya walee wajukuu na vitukuu
Waache wenye zama zao za sasa waandike vitabu vyao

Porojo zao za kellele za oooh wakati wa Nyerere ilikuwa hivi zimepitwa na wakati
 
Humphrey PolePole ni kama vile alikuwa akiwahutubia vijana wa bodaboda ambao wengi wao hawakuwepo wakati wa Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete na namna walifanikiwa kuwa Marais wa Tanzania.

Pia alifanikiwa kutuambia kuwa nyuma yake wako pia akina Mzee Warioba na wazee wenzake wa kanda ile.

Na mwisho amefanikiwa kuonyesha kuwa kuna vita ya udini kwenye uongozi; hasa baada ya kuonyesha kuwa Mkapa alipata kura chache alipogombea kwa mara ya kwanza kwa makosa ya matangulizi wake Mzee Mwinyi (mwislam) na Magufuli alipata kura chache alipogombea kwa mara ya kwanza kwa makosa ya Jakaya (mwislamu). Kwenye hili Polepole alisema kuwa unapogombea kwa mara ya kwanza kura utakazopata sio za kwako, bali za Rais aliyekukabidhi kijiti. Hapa natofautiana nae kabisa, kwakuwa kwenye uchaguzi wa 1995 Mkapa alikuwa hajulikani ukilinganisha na mgombea wa upinzani; Lyatonga Mrema. Mwl Nyerere ndiye aliyemsaidia kupiga kampeni vinginevyo angedondoshwa; sio kwasababu ya udhaifu wa uongozi wa Mzee Mwinyi. Mwl Nyerere alidiriki kusema hawezi kulala nyumbani eti kwasababu ya ubaba wa taifa, wakati yuko jukwaani akasema "I can not let my country go to the dogs". Hivyo tatizo ni CCM kumsimamisha mgombea (Mkapa) ambae hajulikani kwa watu.

Magufuli alipata kura chache uchaguzi wa 2015 kwasababu Lowassa alikuwa na nguvu kuliko JPM, sio kwasababu ya uongozi wa JK ulikuwa mbaya. Hapa Humphrey anaongelea udini kwakuwa anafahamu kuwa uchaguzi wa 2020 JPM alishinda kwa kuwaengua wapinzani wote na kuiba kura.

Nijuavyo mimi Humphrey na wenzake wataashindana lakini hawatashinda hii vita ya udini.

Humphrey anawadanganya watoto wachanga kuwa mchakato wa katiba ulivunjika kwasababu ya rasimu ya katiba ilikuwa inawabana viongozi wabadhilifu ndiyo maana JK aliikataa. Huu ni upuuzi sawa na upuuzi mwingine kwakuwa katiba mpya pendekezwa ingeanza kufanyakazi baada ya uongozi wa JK kumalizika na kuondoka madarakani; hivyo, JK hakuwa na sababu ya kuiogopa katiba ambayo ina masharti magumu kwa viongozi. Sababu ya kweli ya kuvunjika uwandishi wa katiba mpya ni Mzee Warioba na Polepole ambao walikuwa wanataka muungano wa serikali 3 badala ya serikali 01 ya sasa; hoja ambayo ilikuwa inahofiwa kuwa itakwenda kuvunja muungano hasa baada ya kuungwa mkono na UKAWA.

The main agenda sasa imefahamika kuwa ni UDINI, UDINI, UDINI kwakuwa kuna watu hawakutaka Samia (mwislamu) kuwa Rais baada ya JPM kufariki. Hii ni ajenda ya kidini kabisa, hakuna lingine hapo. Walimkataa hata kabla ya kujua ataongozaje atakapoapishwa. Sasa tuko tayari watanzania kwa hili.

View: https://youtu.be/0j3WOvqNL_A?si=LrrfTy6_Ek55Bzso

Huyo Polepole anapoteza muda wake. Watanzania wanakusikiliza ukiwa unabebwa na umaarufu wa wakati fulani ukishaondoka huo wakati unabakia kuwachosha masikioni mwao.

Ni umaarufu wa muda ambao huenda ukipotea baada ya watu kutaka kusikia hoja mpya zenye kuwasisimua kwa aina tofauti na ule msisimko walioupata kutoka kwako.

Udini haumsumbui Polepole peke yake, na wote walio nyuma yake wanaopita njia zile zile za hoja anazoziweka hadharani.

JPM aliwapa ulinzi wa kisaikolojia watu wote waliokuwa karibu na awamu yake. Alipokufa kundi lake halikuwa limejiandaa na kipindi kile cha majonzi waliumiza vichwa kwa haraka kutaka 'kumuondoa' Samia juu ya uso wa dunia lakini Malaika Mabeyo akajitokeza na kutumia nguvu ya jeshi katika kumkingia kifua Samia aliyetaka kunyanyaswa na kudhulumiwa na wasaidizi wa hayati.

Huyo atapita tu sawa na yule bondia maarufu mwenye kelele nyingi alipokuja kila mtu alimuimba lakini hivi sasa watu wameshamchoka hakuna anayelikumbuka jina lake.
 
Wacha urongo aisei, Katiba hii ilikuwa hivihivi wakati wa kuchagua NDIYO au HAPANA na Warioba akiwepo, alikuwepo wakati vyama vingi vinakuwa incorporated kwenye Katiba miaka ya 1990s, alikuwepo wakati wa G55 ya akina Nyelu Kasaka, hupo hata sasa wakati anaibuka na Katiba ya serikali tatu baada ya kuona Nyerere kafa; coward. Warioba yupo alikuwepo wakati mwanawe anapewa ubunge na Magufuli, eti sasa anawaona wenzake wanaowapa watoto wao ubunge wanakosea lakini akina Pipi, John Mongela, Vita Kawawa, nk ilikuwa sawa.
Jesca Magufuli kapewa uongozi na Samia. Rais muislam kampa ubunge mtoto wa rais wa zamani ambaye ni mkristo!.

Samia hana roho mbaya na huo upendeleo umegusa kwa watu wa dini zote.
 
Wait.

Kwa maneno yako hayo.

Kwa hiyo Bunge likivunjwa na wabunge wakaamua kubaki Dodoma hapo inakuwa si campaign mode?

Kinachofanya campaign mode ianze ni ni i? Ni bunge kuvunjwa au ni wabunge kurudi majinboni?
Kama ukitumia akili kubwa kuangalia kwa makini kilichokuwa kwenye akili ya walioandika kipengele hiki cha "baada ya bungwe kuvunjwa" kwenye Katiba, utagundua kuwa walikuwa wakiwalenga wabunge tu. Lengo lao huenda walikuwa wanataka kuzuia kuvuruga shughuli za bunge la Katiba kwa wabunge kwenda majimboni kuweka mambo sawa ya kuteuliwa kuwa wagombea. Vinginevyo ziko shughuli nyingi za uchaguzi kama vile kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura, kuchapisha makaratasi ya uchaguzi, kusaini maadili na kanuni za uchaguzi, kutoa elimu ya uchaguzi yanafanyika kabla ya bunge kuvunjwa.
 
Huwezi kuzipa uzito hoja za Polepole kwakuwa anazitoa akiwa uvunguni mwa kitanda cha mke mdogo,
Hii inahusianaje na swali kwahiyo siku hizi kutoa hoja inakuhitaji kuwepo mahali fulani ?

Wewe umejuaje kazitoa kwa "mke mdogo" au wewe ndio mke mkubwa?

Kama hazina uzito kwanini walivamia kwa dada yake na mama yake , kumtafuta walikua wanazuia kitu gani?

Kwanini akiwa anaongea traffic katika mitandao ya YouTube na Facebook inapunguzwa hadi watu wawashe VPN?

pili Polepole ni mwanachama sawa na mwanachama mwinyine (hana veto), tatu Polepole amebase kwenye mila na desturi na utamaduni wakati anapochafua watu
Hivyo ukiwa mwanachama sawa na wengine uko "barred" kutoa mawazo tofauti/kinzani na wanachama wengine?
, nne Polepole anafahamu kuwa Mkutano Mkuu wa CCM ndicho chombo cha juu sana cha maamuzi kwenye chama; yaani kwa wakatoliki unaweza kufananisha na Pope of Vatican.
Kwahiyo mkutano mkuu ukikosea hakuna namna wanaweza kureverse maamuzi?

Hivyo basi wewe na chama chako ni wazi ni waumini wa hii katiba ambayo inazuia rais kushtakiwa awapo madarakani au atokapo hata kama alifanya makosa na rais huyo huyo ndio mwenyekiti wa mkutano mkuu.
Anachokifanya Polepole ni nuisance tu ndani ya chama na mgombea wa CCM. Lakini kwakuwa CCM ndicho chama tawala anahatarisha amani na utulivu wa nchi.
Nipe matishio matano[5] ya kiusalama ambayo unadhani yatatokea /yametokea tangu Polepole ameanza kuongea au akiendelea kuongea katika press zake.
Mimi binasfi namuona Polepole kama kielelezo cha kukua kwa demokrasia nchini kuhusu uhuru wa kusema tulionao katika awamu hii ya sita
Kama wewe binafsi unaamini hivyo kwanini hukubali Polepole anachoamini na kina mzee Warioba?

Awamu ya 6 imekuzaje demokrasia [taja sababu 5] .

Na kama awamu ya 6 imekuza demokrasia ni awamu gani iliua demokrasia?

Je awamu ya 6 iliyokuza demokrasia ilitoka sayari ya Zuhura au ni muendelezo wa awamu ile iliyoua demokrasia?
. Kama angetokea mtu kama Polepole kwenye awamu ya tano ya JPM huenda angeshaikimbia nchi.
Wewe unajuaje Polepole hajakimbia nchi?

Na unafikiri kwanini imekuwa ni utamaduni wa watu kukimbia nchi kama kuna demokrasia?
Mama Samia ni bingwa wa demokrasia ndiyo maana akina Polepole unawasikia sauti zao.
Elezea "ubingwa" wa mama Samia katika demokrasia ila usiweke habari ya kuruhusu mikutano ya kisiasa January 2022[hii ni haki kikatiba]

Je ameonyeshaje ubingwa katika demokrasaia nakupa premises za kujadili.

Wakosoaji kutoketwa je wameachwa kutekwa?

Wakosoaji kutofunguliwa kesi batili je hatendi hivyo?

Magazeti na vyombo vya habari vimeacha kufungiwa?

Je kuna uchaguzi wowote uliofanyika chini yake ukawa "huru na wa haki"?
 
Back
Top Bottom