Polepole kasema nyuma yake wapo kina Mzee Warioba

Polepole kasema nyuma yake wapo kina Mzee Warioba

Actually Warioba alishajiuzulu u Waziri Mkuu uongozi wa Mwinyi. Ndiyo Malecwla akachaguliwa kuwa Waziri Mkuu. Kwa hiyo hoja ya Warioba hajajiuzulu si kweli. Labda mliambiwa tu Rais kabadili baraza la mawaziri kwa kumlindia heshima rais tu.

Na kuhusu katiba, hii katiba ingekuwa mbaya zaidi kama si juhudi za kina Warioba.

Huwezi kutegemea Warioba wa 1977 mpaka 1984 adai katiba ya 2025 mwaka 1977.

Kina Warioba ndio waliodai Bill of Rights mpaka Nyerere akaleta Bill of Rights Tanzania.

Unajua Bill of Rights ni nini? Unajua ilikuja mwaka gani Tanzania? Inajua Nyerwre alikataa kuiweka kwa miaka mingapi?

Uongozi ni kupokezana. Kwa nini unampa Warioba mzigo wa kumaliza matatizo yote ya Tanzania ya miaka ya uongozi wake na miaka yote iliyofuata?
Wacha urongo aisei, Katiba hii ilikuwa hivihivi wakati wa kuchagua NDIYO au HAPANA na Warioba akiwepo, alikuwepo wakati vyama vingi vinakuwa incorporated kwenye Katiba miaka ya 1990s, alikuwepo wakati wa G55 ya akina Nyelu Kasaka, hupo hata sasa wakati anaibuka na Katiba ya serikali tatu baada ya kuona Nyerere kafa; coward. Warioba yupo alikuwepo wakati mwanawe anapewa ubunge na Magufuli, eti sasa anawaona wenzake wanaowapa watoto wao ubunge wanakosea lakini akina Pipi, John Mongela, Vita Kawawa, nk ilikuwa sawa.
 
Mambo magumu yanajibiwa Kwa lugha nyepesi

Mtu ambae amewahi kula kiapo Kwa Marais 3 anajibiwa na mtu ambae ajawahi hata kula kiapo cha kumpa mtu dhamana mahaka ya mwanzo
😂😂😂
 
Harakati za siasa
Haya ndiyo yanayompaisha Samia kimataifa. Ni Rais mwanamke lakini anaezimudu changamoto za kisiasa bila kuyumba. Wanaume na suluali zao wananguruma wakiwa mafichoni wakti Samia akiwa bize na kufungua miradi ya kimataifa inayoinufaisha nchi. Wanaume waoga wanaomuogopa mwanamke mwanagenzi kisiasa. Nadhani demokrasia itamkumbuka Samia kama shujaa wa Tanzania.

Mpaka sasa Samia hajavunja sheria yoyote wala Katiba. Wanaolalamika wanalia kuvunjwa kwa desturi na mila eti za regime change; huo msamiati sijawahi kusikia ukitamkwa na Baba wa Taifa hata siku moja. Mila za desturi ndizo zilizotufikisha hapa kimaendeleo.

Tuache chuki za kidini, andaeni wagombea wenu kwa 2030. Samia ameahidi kuwaletea katiba matata sana kabla ya 2030.
 
Genge la wahalifu
Yanatafunana kwa kutumia mila na desturi. Ukianzisha mila kuwadhulu wengine, wenzako watatumia mila hiyohiyo kukutafuna pia; presidency. CCM walipoamua kumfanya Rais kuwa mwenyekiti wao wa CCM pia walidhani wanawakomoa wapinzani, sasa inawala hata wao wenyewe ndani kwa ndani. Polepole sasa hivi anaongelea uvunguni mwa kitanda chake anaogopa kila mtu hadi kivuli chake mwenyewe kwakuwa mwenyetiki wake wa chama ndiye Mkuu wa nchi na Amirijeshi Mkuu wa majeshi yote ya Tanzania anaeteua Majaji, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi, wakuu wooooote unaowajua wewe. Inawatafuna wao wenyewe.
 
Shule ya uongozi walimpia vita sana nakuambia akae kwa taharuki sasa alishakua na uthubutu na ndiyo maana akatupiwa cuba
Angekuwa na uthubutu angemsema Magufuli alivyovunja katiba.

Angekuwa na uthubutu angesema mchakato wa kupata mgombea wa CCM urudiwe, angesema anataka kushindana na Samia tuone nani atateuliwa. Au angempigia kampeni mgombea wake.

Hapo ndipo angeweza kusema ana uthubutu.

Unasema ana uthibutu wakati anamkataa Samia hata hatuambii anataka nani awe rais?

Sasa mtu mwenye uthubutu anaenda kujificha nyuma ya desturi na tamaduni katika nchi na chama ambamo kuna katiba na sheria? Anataka kupewa ushindi wa mwzani Samia asiruhusiwe kugombea urais, kumvunjia Samia haki yake ya kikatiba (mind you simtetei Samia, natetea katiba) bila ya yeye kupambana na Smaia?

Huo ni uthubutu au u Makaveli?
 
Wacha urongo aisei, Katiba hii ilikuwa hivihivi wakati wa kuchagua NDIYO au HAPANA na Warioba akiwepo, alikuwepo wakati vyama vingi vinakuwa incorporated kwenye Katiba miaka ya 1990s, alikuwepo wakati wa G55 ya akina Nyelu Kasaka, hupo hata sasa wakati anaibuka na Katiba ya serikali tatu baada ya kuona Nyerere kafa; coward. Warioba yupo alikuwepo wakati mwanawe anapewa ubunge na Magufuli, eti sasa anawaona wenzake wanaowapa watoto wao ubunge wanakosea lakini akina Pipi, John Mongela, Vita Kawawa, nk ilikuwa sawa.
Mwanawe kapewa ubunge na Magufuli?

Mwanawe gani? Mtaje jina. Kapewa ubunge na Magufuli lini?
 
Actually Warioba alishajiuzulu u Waziri Mkuu uongozi wa Mwinyi. Ndiyo Malecwla akachaguliwa kuwa Waziri Mkuu. Kwa hiyo hoja ya Warioba hajajiuzulu si kweli. Labda mliambiwa tu Rais kabadili baraza la mawaziri kwa kumlindia heshima rais tu.

Na kuhusu katiba, hii katiba ingekuwa mbaya zaidi kama si juhudi za kina Warioba.

Huwezi kutegemea Warioba wa 1977 mpaka 1984 adai katiba ya 2025 mwaka 1977.

Kina Warioba ndio waliodai Bill of Rights mpaka Nyerere akaleta Bill of Rights Tanzania.

Unajua Bill of Rights ni nini? Unajua ilikuja mwaka gani Tanzania? Inajua Nyerwre alikataa kuiweka kwa miaka mingapi?

Uongozi ni kupokezana. Kwa nini unampa Warioba mzigo wa kumaliza matatizo yote ya Tanzania ya miaka ya uongozi wake na miaka yote iliyofuata?
Mwamba unajua mambo mengi sana wewe bwana Kiranga
 
Bahati nzuri 2015 nilikuwa mkubwa tu,kwahyo acha kubwabwaja

Hakuna kipindi ambacho watz waliichoka ccm kama kipindi hicho,unajua kwanini?

Kwasababu watanganyika walikuwa wameshasikia habari nyingi za uongozi wa kikwete kutoka kwa wapinzani
 
Mwamba unajua mambo mengi sana wewe bwana Kiranga
Mkuu,

Sasa hawa watu wengine wanawasikia na kuwasoma tu wakati mimi ni watu wangu, family friends, personal friends, relatives.

Mtu atamzungumzia Warioba hapa wakati hata hajamuona wakati mimi nilikuwa naenda kulala kwa Warioba Haile Selassie kwa rafiki zangu.

Mtu atamzungumzia Mkapa hata hajamuona wakati mimi nilikuwa nakwenda kwa Mkapa Sea View kabla hata hajawa rais.

Siku moja rafiki yangu kaniagiza nimpelekee mzigo fulani kwao kwa Mkapa pale Sea View, basi na mimi nikawa nimetingwa na kazi, nikaunganisha safari za kazi na wenzangu wa kazini. Nikasema naomba mnipitishe Sea View hapo kuna mzigo namuachia mtu.

Wale jamaa kuja kustuka, naenda kuacha mzigo kwa Mkapa. Walishangaa sana. Toka siku hiyo wakawa wananiangalia kama si mtu wa kawaida. Wananiambia yani wewe unajuana na familia ya rais? Nikasema sasa hawa mbona tunajuana zamani tu tangu parties za utotoni kabla hata ya urais?

In fact wakati Mkapa anakwenda kusoma Columbia University Uncle wangu ndiye aliyemsindikiza uwanja wa ndege na uncle wangu alipewa jukumu la kuhakikisha huyu kijana mdogo Mkapa anayeonesha matumaini makubwa kuwa msomi mzuri atafanikiwa huko Columbia University, New York City.

Mtu ataongelea habari za Usalama Tanzania, wakati mimi nilikuwa napiga stories na Mkurugenzi Mkuu wa TISS, uncle wangu mwingine.

Mtu atasema habari za Ikulu, wakati mimi nimeanza kutembea corridors za Ikulu tangu nipo tumboni mwa mama yangu. By the time Mwinyi rais mtoto wake nilikuwa nampiga vibao tu na hanifanyi kitu alikuwa ananijua, yeye mtoto wa rais, mimi mtemi wake.

Wengine hatusomi kwenye magazeti tu hizi habari.
 
Wacha urongo aisei, Katiba hii ilikuwa hivihivi wakati wa kuchagua NDIYO au HAPANA na Warioba akiwepo, alikuwepo wakati vyama vingi vinakuwa incorporated kwenye Katiba miaka ya 1990s, alikuwepo wakati wa G55 ya akina Nyelu Kasaka, hupo hata sasa wakati anaibuka na Katiba ya serikali tatu baada ya kuona Nyerere kafa; coward. Warioba yupo alikuwepo wakati mwanawe anapewa ubunge na Magufuli, eti sasa anawaona wenzake wanaowapa watoto wao ubunge wanakosea lakini akina Pipi, John Mongela, Vita Kawawa, nk ilikuwa sawa.
Thread zako nyingi zimejaa uongo. Mtoto gani wa warioba alipewa ubunge na magufuli?
Hakuna mtoto wa warioba aliyeteuliwa kuwa mbunge
 
Angekuwa na uthubutu angemsema Magufuli alivyovunja katiba.

Angekuwa na uthubutu angesema mchakato wa kupata mgombea wa CCM urudiwe, angesema anataka kushindana na Samia tuone nani atateuliwa. Au angempigia kampeni mgombea wake.

Hapo ndipo angeweza kusema ana uthubutu.

Unasema ana uthibutu wakati anamkataa Samia hata hatuambii anataka nani awe rais?

Sasa mtu mwenye uthubutu anaenda kujificha nyuma ya desturi na tamaduni katika nchi na chama ambamo kuna katiba na sheria? Anataka kupewa ushindi wa mwzani Samia asiruhusiwe kugombea urais, kumvunjia Samia haki yake ya kikatiba (mind you simtetei Samia, natetea katiba) bila ya yeye kupambana na Smaia?

Huo ni uthubutu au u Makaveli?
Eti mgombea wao wa 2015 alikuwa Mzee Warioba; wako serious hawa?

Samia kama alijitangaza mwenyewe kuwa atagombea 2025 na wao wangejitangaza kumtangaza atagombea wao 2025 kisha fataki zingegongana angani, lakini woga unawatafuna, It is too late to change maamuzi ya Mkutano Mkuu yaliyompitisha Samia. Locuta causa finita; "Rome has spoken, the case is closed"
 
Humphrey PolePole ni kama vile alikuwa akiwahutubia vijana wa bodaboda ambao wengi wao hawakuwepo wakati wa Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete na namna walifanikiwa kuwa Marais wa Tanzania.

Pia alifanikiwa kutuambia kuwa nyuma yake wako pia akina Mzee Warioba na wazee wenzake wa kanda ile.

Na mwisho amefanikiwa kuonyesha kuwa kuna vita ya udini kwenye uongozi; hasa baada ya kuonyesha kuwa Mkapa alipata kura chache alipogombea kwa mara ya kwanza kwa makosa ya matangulizi wake Mzee Mwinyi (mwislam) na Magufuli alipata kura chache alipogombea kwa mara ya kwanza kwa makosa ya Jakaya (mwislamu). Kwenye hili Polepole alisema kuwa unapogombea kwa mara ya kwanza kura utakazopata sio za kwako, bali za Rais aliyekukabidhi kijiti. Hapa natofautiana nae kabisa, kwakuwa kwenye uchaguzi wa 1995 Mkapa alikuwa hajulikani ukilinganisha na mgombea wa upinzani; Lyatonga Mrema. Mwl Nyerere ndiye aliyemsaidia kupiga kampeni vinginevyo angedondoshwa; sio kwasababu ya udhaifu wa uongozi wa Mzee Mwinyi. Mwl Nyerere alidiriki kusema hawezi kulala nyumbani eti kwasababu ya ubaba wa taifa, wakati yuko jukwaani akasema "I can not let my country go to the dogs". Hivyo tatizo ni CCM kumsimamisha mgombea (Mkapa) ambae hajulikani kwa watu.

Magufuli alipata kura chache uchaguzi wa 2015 kwasababu Lowassa alikuwa na nguvu kuliko JPM, sio kwasababu ya uongozi wa JK ulikuwa mbaya. Hapa Humphrey anaongelea udini kwakuwa anafahamu kuwa uchaguzi wa 2020 JPM alishinda kwa kuwaengua wapinzani wote na kuiba kura.

Nijuavyo mimi Humphrey na wenzake wataashindana lakini hawatashinda hii vita ya udini.

Humphrey anawadanganya watoto wachanga kuwa mchakato wa katiba ulivunjika kwasababu ya rasimu ya katiba ilikuwa inawabana viongozi wabadhilifu ndiyo maana JK aliikataa. Huu ni upuuzi sawa na upuuzi mwingine kwakuwa katiba mpya pendekezwa ingeanza kufanyakazi baada ya uongozi wa JK kumalizika na kuondoka madarakani; hivyo, JK hakuwa na sababu ya kuiogopa katiba ambayo ina masharti magumu kwa viongozi. Sababu ya kweli ya kuvunjika uwandishi wa katiba mpya ni Mzee Warioba na Polepole ambao walikuwa wanataka muungano wa serikali 3 badala ya serikali 01 ya sasa; hoja ambayo ilikuwa inahofiwa kuwa itakwenda kuvunja muungano hasa baada ya kuungwa mkono na UKAWA.

The main agenda sasa imefahamika kuwa ni UDINI, UDINI, UDINI kwakuwa kuna watu hawakutaka Samia (mwislamu) kuwa Rais baada ya JPM kufariki. Hii ni ajenda ya kidini kabisa, hakuna lingine hapo. Walimkataa hata kabla ya kujua ataongozaje atakapoapishwa. Sasa tuko tayari watanzania kwa hili.

View: https://youtu.be/0j3WOvqNL_A?si=LrrfTy6_Ek55Bzso

Wewe ni mjinga ? Polepole ametamka wapi neno linalohusiana n dini ya mtu?
Ujaribu kuelewa na kujibu hoja kama zilivyowasilishwa siyo kubinua makarios na kusingizia watu. Udini kwenye hoja ya polepole uko wapi?
Kwa hiyo Muislam kukosolewa na mkrisyo kwako wewe huo ni udin??
Huu ndio ujinga sasa
 
Eti mgombea wao wa 2015 alikuwa Mzee Warioba; wako serious hawa?

Samia kama alijitangaza mwenyewe kuwa atagombea 2025 na wao wangejitangaza kumtangaza atagombea wao 2025 kisha fataki zingegongana angani, lakini woga unawatafuna, It is too late to change maamuzi ya Mkutano Mkuu yaliyompitisha Samia. Locuta causa finita; "Rome has spoken, the case is closed"
Sikubaliani nawe kuwa Rome has spoken. Kuna malalamiko mengi sana.

Pia, hata kama Rome has spoken, what is Rome?

That logical fallacy is an argument from authority fallacy.

Ila inaonekana kuna woga huo unaousema.

La sivyi, angwjitangaza mtu anayetaka kugombea urais kwa tiketi ya CCM akisema yeye kavunjiwa haki yake na anataka mchakato urudiwe.

Hizi habari za kusema kwa desturi na utamadu i Samia hafai ni woga tu. Ni jitihada za kumuondoa Samia kinyume na katiba. Na mimi nasema jivyo si kama mtetezi wa Samia, SMia namuona kapwaya, mimi nasema hivyo kama mtetezi wa ukatiba.

Kama Samia hafai kweli, waombe mchakato wa kumpata mgombea wa CCM urudiwe halafu wajumbe wamteue upya mgombea wa CCM, Samia aruhusiwe kuweka jina lake tena pamoja na wengine, tuone wajumbe wataamua vipi.
 
Back
Top Bottom