Polepole amefanya nimwelewe Magufuli

Polepole amefanya nimwelewe Magufuli

Wakati akiwa hai nilikuwa namuona John Pombe Magufuli pamoja na kutaka aonekane mzalendo, niliona kuwa ni mtu asiye na nia njema Kwa Taifa letu na mtaka sifa.

Lakini baada ya Polepole kuelezea mambo mengi yaliyokuwa yanafanyika nyuma ya pazia, sasa nimeanza kuelewa kuwa Magufuli alikuwa na dhamira njema kwa Tanzania.

Kumbe Magufuli baada ya kugundua fedha zinachotwa serikalini, yeye akaamua kuziwekeza kwenye miradi ili kama ni madeni ni bora watanzania walipe lakini wakiwa wana miundombinu inayowasaidia kuendesha maisha yao.

Zile hotuba zake kama anapambana na mara majeshi au watumishi wa Serikali, Leo zinaleta mantiki zaidi kuliko wakati akizitoa.

Magufuli alikuwa anajua yupo peke yake kwenye harakati za kuijenga Tanzania maana hata watu kama Makonda kumbe nao Wana vimelea vya CCM mtandao.

Ukweli utajulikana siku moja.
Yapo ya msingi sana kama uliyoainisha na kuweka misingi mizuri ya kiutawala!! Ila nilipokuja ingia mashaka ni pale kuongeza kinga kwa viongoz wengine!!!
 
Ukanda siyo kweli.... Hizi ni propaganda tu. Ila la kukataa kukosolewa ndiyo linaloleta ukakasi. Jee ilikuwa ni tabia yake ya asili au ni matokeo ya taarifa alizokuwa anapewa?
Hiyo ilikuwa tabia yake ya asili. Hata alipokuwa waziri tabia hiyo ilikuwa wazi.
 
Lawama kubwa zinaenda Kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama...Wanalinda waovu zaidi ya kulinda watu wema, walio na maamuzi wengi wanakuwa corrupted na wanaobaki wanakuwa hawana namna ya kufanya
Ukiona hivyo ujue hata huko kwenye vyombo waliojaa ni watu waovu ...ndege wafananao huruka pamoja.
 
Kama ni kweli kuna mtu aliondoa uhai wa Magufuli, alitukosea sana. Inaumiza aisee
 
Magufuli alikuwa na mabaya yake pamoja na mazuri yake,lakini ukipima kwenye mizani mazuri aliyoyafanya katik nchi hii ni mengi mno.

Na ninaamini hata mauji mengi yalifanywa na wanamtandao ili kuichafua hadhi yake na urasi wake

Kama yeye tu ndio alikuwa muuaji basi inamaana baada ya kifo chake haya mambo yangekoma,lkn mbona yanaendelea tena kwa kiwango cha juu?

Think big
Wauaji hawa wameiga toka kwake, maana wanaona uovu ni mbinu iliyomsaidia pakubwa.
 
Kwani Kuna upinzani Tanzania? Mbona we mgumu kuelewa? Kwahiyo Kwa akili yako hata Sasa Kuna mtu anayepingwa na yeyote kweli au ni drama tu kuridhisha personal desires?
Magufuli amechangia pakubwa ushenzi huu.
 
nikiwakumbuka keyboard warriors, nyie Netizens wa humu etc
nacheka... u GT wa humu sio wa kila mtu...

Napita kimya hapa kwasababu wengine na mie tusio hata wanachama wa chama chochote...
kama mie sina la kusema siku hizi. Aliyefurahiwa ndio atashine 2025 ni Mwanamke.

Wanawake oyeeeee...
Kazi iendelee....
Duh
 
Magufuli alikuwa na mabaya yake pamoja na mazuri yake,lakini ukipima kwenye mizani mazuri aliyoyafanya katik nchi hii ni mengi mno.

Na ninaamini hata mauji mengi yalifanywa na wanamtandao ili kuichafua hadhi yake na urasi wake

Kama yeye tu ndio alikuwa muuaji basi inamaana baada ya kifo chake haya mambo yangekoma,lkn mbona yanaendelea tena kwa kiwango cha juu?

Think big
Huyu dada gallow bird yeye humwambii kitu kwa samia
 
Polepole has done a noble work of sanitizing a dark legacy of Mzee Magufuli. The diabolical detractors, including Tundu Lissu are now Praising Mzee Magufuli Posthumously.

What a time to be alive. 😆
 
Unaweza kuta mwanamtandao huyo au mnufaika mmoja wapo
Hapana siyo hivyo sababu ni dini

Mimi nilimuuliza kwahiyo wewe ukienda hospital unahudumiwa tofaut na sisi sababu wewe ni mwisilam kama mama Samia?
 
Magufuli ni chanzo cha yote yatokeayo sasa.
Alikua mbinafsi sana na hakuipenda Tanzania
 
Back
Top Bottom