Polepole amefanya nimwelewe Magufuli

Polepole amefanya nimwelewe Magufuli

Aliminya kwakua alijua hao pia wanatumiwa na siyo demokrasia kama inavyodaiwa...Mbona mnaelezwa hizo proxies zilizoundwa Kwa sababu maalumu? Au hata kumwelewa Slow slow bado?

Wewe unajua unacheza na midoli ambayo inakupiga makwenzi hatari utaendelea kuwapa good time tu Ili wakukwamishe?

Magufuli aliukataa mfumo mzima wa upinzani wakati alipaswa apambane na hao "wasaliti" na sio kutaka kufuta kabisa mfumo wa vyama mbadala...

Tazama sasa madhara ya alichokifanya sasa, hakuna mbadala na wenye CCM 'wamemuondoa' na wala hakuna wanaoweza pambana na jinamizi CCM...
 
Ukanda siyo kweli.... Hizi ni propaganda tu. Ila la kukataa kukosolewa ndiyo linaloleta ukakasi. Jee ilikuwa ni tabia yake ya asili au ni matokeo ya taarifa alizokuwa anapewa?
Mkuu, heshima sana. Uko sahihi. Kwangu mimi nasema Magufuli alikuwa anajua chanzo cha matatizo yetu, lakini hakuwa na uelewa wa namna ya kuyaondoa. Alikuwa anatumia nguvu kuliko akili. Na pia alikuwa anapenda kuabudiwa na mtu ukimsifia kidogo tu japo kwa unafiki, anakuamini na kukusogeza karibu. Na tatizo lake kubwa ni kudhani CCM ikibaki peke yake basi ataweza kui-control Tanzania kwa urahisi. Kwa kifupi hakuwa anataka challenge ya aina yoyote. Huwezi kuwa rais mwenye maono halafu ukalazimisha watu kama kina Kibajaji ndiyo wawe wabunge. Hata kumwacha Samia awe makamu kwenye uchaguzi wa 2020 lilikuwa ni kosa kubwa.
 
Magufuli aliukataa mfumo mzima wa upinzani wakati alipaswa apambane na hao "wasaliti" na sio kutaka kufuta kabisa mfumo wa vyama mbadala...

Tazama sasa madhara ya alichokifanya sasa, hakuna mbadala na wenye CCM 'wamemuondoa' na wala hakuna wanaoweza pambana na jinamizi CCM...
Kwani Kuna upinzani Tanzania? Mbona we mgumu kuelewa? Kwahiyo Kwa akili yako hata Sasa Kuna mtu anayepingwa na yeyote kweli au ni drama tu kuridhisha personal desires?
 
Nilichojifunza watu hawawi wema kwa kuwa aliyeko madarakani ni mwema, bali ni kutokana na mfumo unaowalazimisha wawe wema.

Makonda alifikishwa kwenye Tume ya maadili ya umma, nini kilitokea... Sabaya alifikishwa mahakamani, mahakama iliamua nini?
Ulichoandika hata chizi atakucheka, hizo tume na mahakama zimeundwq au zinasimamiwa na nani?. Magufuli hakuwq na wema wowote wala hakuna mwanaccm atakuwa mwema kwa Taifa!. Wote wanapambania maisha yao... Huyu polepole angekuwa ndani ya mfumo angeyasema haya?.
 
Magufuli aliukataa mfumo mzima wa upinzani wakati alipaswa apambane na hao "wasaliti" na sio kutaka kufuta kabisa mfumo wa vyama mbadala...

Tazama sasa madhara ya alichokifanya sasa, hakuna mbadala na wenye CCM 'wamemuondoa' na wala hakuna wanaoweza pambana na jinamizi CCM...
Sema tena na tena. Alikuwa anatumia approach ya ajabu kabisa kwenye kuongoza. Nikupe mfano mwingine: Polepole anasema yule mbunge mjinga aliyependekeza eti Magufuli aongozewe muda wa urais, alitumwa na wana mtandao ili kumfanya Magufuli aonekane kuwa ni mroho wa madaraka. Well, inaweza kuwa ni kweli. Lakini hatua alizochokuwa ku deal na huyo mbunge zilikuwaje? Alimwita Polepole na kumlalamikia kuwa anahujumiwa na mtangulizi wake na kumwambia aseme kuwa Magufuli hataki kuongezewa muda. Je, alifanya nini kwa huyo mbunge mjinga ambaye alikuwa anamhujumu? Mbona hatukusikia anapewa onyo au adhabu nyingine yoyote?
 
Kwani Kuna upinzani Tanzania? Mbona we mgumu kuelewa? Kwahiyo Kwa akili yako hata Sasa Kuna mtu anayepingwa na yeyote kweli au ni drama tu kuridhisha personal desires?

Naona tuna mitazamo na uelewa tofauti wa siasa za Tanzania zilivyo na zinavyopaswa kuwa, hatuwezi fika muafaka...

Naona bado umekazana kutazama "ilivyo" na sio "inavyopaswa kuwa"...

Na kwa mtazamo wako huo maana yake hata hakuna haja ya kuwa na vyama including CCM kwa sababu watu wote kwenye siasa ni corrupt...
 
Haukuelewa hata hili? JPM hakuwa msukuma na maadui wangetumia hiyo kumdhoofisha ikabidi aji align na hao wa Kanda ya huko Ili angalau awe na uhakika na support Yao na hapo alifanikiwa. Ili watu waku support si lazima kuonyesha kuwa upande wao?

Shida ya watu wetu wengi hata waliosoma hawajafundishwa critical thinking...Wanachukua vitu at face value na lip service. They cannot discern intents. Na waovu wanajua hilo
Uhakika, watu wetu hawawezi ku reason
 
Wakati akiwa hai nilikuwa namuona John Pombe Magufuli pamoja na kutaka aonekane mzalendo, niliona kuwa ni mtu asiye na nia njema Kwa Taifa letu na mtaka sifa.

Lakini baada ya Polepole kuelezea mambo mengi yaliyokuwa yanafanyika nyuma ya pazia, sasa nimeanza kuelewa kuwa Magufuli alikuwa na dhamira njema kwa Tanzania.

Kumbe Magufuli baada ya kugundua fedha zinachotwa serikalini, yeye akaamua kuziwekeza kwenye miradi ili kama ni madeni ni bora watanzania walipe lakini wakiwa wana miundombinu inayowasaidia kuendesha maisha yao.

Zile hotuba zake kama anapambana na mara majeshi au watumishi wa Serikali, Leo zinaleta mantiki zaidi kuliko wakati akizitoa.

Magufuli alikuwa anajua yupo peke yake kwenye harakati za kuijenga Tanzania maana hata watu kama Makonda kumbe nao Wana vimelea vya CCM mtandao.

Ukweli utajulikana siku moja.
Pamoja na hayo mazuri, mabaya yalikuwepo pia.
 
Kwani Kuna upinzani Tanzania? Mbona we mgumu kuelewa? Kwahiyo Kwa akili yako hata Sasa Kuna mtu anayepingwa na yeyote kweli au ni drama tu kuridhisha personal desires?
Mawazo ya kijinga kama haya ndiyo yalimwangusha Magufuli na yakatufikisha hapa. Haya nikubaliane na huu ujinga kuwa hakuna upinzani wa kweli... kwa nini wasiweke mazingira mazuri kwa upinzani kuwepo kwa sababu ni jambo muhimu sana kwa nchi?
 
Wakati akiwa hai nilikuwa namuona John Pombe Magufuli pamoja na kutaka aonekane mzalendo, niliona kuwa ni mtu asiye na nia njema Kwa Taifa letu na mtaka sifa.

Lakini baada ya Polepole kuelezea mambo mengi yaliyokuwa yanafanyika nyuma ya pazia, sasa nimeanza kuelewa kuwa Magufuli alikuwa na dhamira njema kwa Tanzania.

Kumbe Magufuli baada ya kugundua fedha zinachotwa serikalini, yeye akaamua kuziwekeza kwenye miradi ili kama ni madeni ni bora watanzania walipe lakini wakiwa wana miundombinu inayowasaidia kuendesha maisha yao.

Zile hotuba zake kama anapambana na mara majeshi au watumishi wa Serikali, Leo zinaleta mantiki zaidi kuliko wakati akizitoa.

Magufuli alikuwa anajua yupo peke yake kwenye harakati za kuijenga Tanzania maana hata watu kama Makonda kumbe nao Wana vimelea vya CCM mtandao.

Ukweli utajulikana siku moja.
Magufuli alisema mtamkumbuka kwa mazuri yake.
 
Vipi kuhusu;-
1. Tsh 1.5 Trillion zilizoibuliwa na CAG 2016/17 na kisha kumfukuza CAG kazi

2. Fedha za Plea bargain feki alizokuwa anakusanya na DPP Biswalo Mganga na kuzificha China

3. Ununuzi wa ndege kupitia Boeing bila kufuata sheria ya manunuzi ya umma??

4. Mikataba ya akina Mayanga construction kujenga Chato International Airport

Nimesema machche lakini nataka nikuhakiishie hata Magufuli hakuwa na uchungu na mali za umma, bali alikuwa ni fisadi sawa na mafisadi wengine wa CCM.

Sina huruma naye kwa kuwa hata yeye Magufuli alikuwa anapanga kuwauwa wenzie, ni kwamba tu walimtaimu akaondoka yeye.

Polepole hana jipya
 
Back
Top Bottom