Polepole amefanya nimwelewe Magufuli

Polepole amefanya nimwelewe Magufuli

Wakati akiwa hai nilikuwa namuona John Pombe Magufuli pamoja na kutaka aonekane mzalendo, niliona kuwa ni mtu asiye na nia njema Kwa Taifa letu na mtaka sifa.

Lakini baada ya Polepole kuelezea mambo mengi yaliyokuwa yanafanyika nyuma ya pazia, sasa nimeanza kuelewa kuwa Magufuli alikuwa na dhamira njema kwa Tanzania.

Kumbe Magufuli baada ya kugundua fedha zinachotwa serikalini, yeye akaamua kuziwekeza kwenye miradi ili kama ni madeni ni bora watanzania walipe lakini wakiwa wana miundombinu inayowasaidia kuendesha maisha yao.

Zile hotuba zake kama anapambana na mara majeshi au watumishi wa Serikali, Leo zinaleta mantiki zaidi kuliko wakati akizitoa.

Magufuli alikuwa anajua yupo peke yake kwenye harakati za kuijenga Tanzania maana hata watu kama Makonda kumbe nao Wana vimelea vya CCM mtandao.

Ukweli utajulikana siku moja.
Ukweli gani? Sasa mbona hakuna miundombinu aliyokamilisha badala yake waliokamilisha kwamkukopa wanasutwa?
 
Sawa,vipi hoja zake nazo tuzipuuze?
Hoja zipi?. Mbona haongelei kupigwa risasi Lissu pale Dodoma?.

Unyama wote umefanyika awamu ya tano Polepole akiwa mwenezi wa CCM akiwa mtu wa karibu na hayati.

Leo anataka kuuvuta umma upande wake kwa kuzinyooshea vidole dhambi za SSH, za kwake nani azinyooshe vidole?.
 
Back
Top Bottom