Dennis Robert Shughuru
JF-Expert Member
- May 30, 2024
- 4,626
- 7,073
MPAKA SAHIVI NAAMINI HARAKATI ZA POLEPOLE NI ZA KIMASLAI ZAIDI NA SIO KWAMBA ANA-UCHUNGU NA NCHI HAPANA KWANINI ZIANZE TU BAADA YA SPONSOR (MAGUFULI) WAKE KUFARIKI
Moja ya mambo ambayo kutoka kwa polepole binafsi siyapendi ni kujaribu kuonyesha hali wakati wa Magufuli ilikuwa ni nzuri sana ilihali sio sahii hata kidogo ni uongo, na mabaya yote wakalaumiwa ni watu wa mtandao sio sahii
Yako mazuri magufuli alifanya na anahitaji pongezi mfano
Kabla ya mwaka 2019 uchaguzi ulikuwa na marue rue ila angalau sauti za wananchi kwa mbali zilikuwa zinasikilizwa mpinzani alikuwa anaweza Tangazwa ila magufuli aliaminisha kwa vitendo unaweza iba uchaguzi kwa asilimia mia moja bila hata ya tone la aibu na alianza mwaka 2019, na akaja 2020 hapo huwezi walaumu mtandao
Mfano:-Baadae kuna watu wako kwenye system ya samia watabadilisha gia na kuanza kuuponda utawala wa samia na watu wataanza kuwashangilia na kuwasifia wana akili sana hii ndo Tanzania
KUTAWALA HII NCHI NI RAHISI SANA SABABU WATU NIWASAHAULIFU KUPITA MAELEZO
"No matter where you go
Remember the road that will lead you"

- kuhamishia serikali Dodoma,
- kuwa na uwajibikaji kwenye ofisi za serikali
- Kufikisha huduma muhimu kama za maji kwa wananchi wakazi wa dsm watanielewa kwa hili magufuli anahitaji pongezi kubwa sana
- Magufuli alitamka waziwazi Mkurugenzi nakulipa mshahara na umtangaze mpinzani mshindi ntakushangaa sana, baada ya hii kauli demokraia ýetu iliabakwa waziwazi kwa hili huwezi walaumu wanamtandao
- Magufuli aliwaambia watu wa majimbo ya upinzani hatawapelekea maendeleo kwa sababu hawakuichagua ccm serious alijimilikisha nchi kama yake na hapa huwezi walaumu mtandao, mfano alikuwa na ziara lindi akasimama ili aongee na wananchi mtu mmoja akapewa kipaza sauti kwanza magufuli alimuuliza mbunge wako ni nani akasema ni bwege alimshambulia vibaya mno mwananchi akataka kuondoka akasema arudishwe akaendelea kumchamba lilikuwa jambo la ajabu sana mbele ya kamera na la hovyo kwa mtu kama Rais na pale huwezi walaumu wanamtandao
- Mtandao wa Internet unazimwa karibu na uchaguzi mkuu hakuna aliyetegema ingetokea ila ilitokea na hapa huwezi walaumu-wanamtandao
- Mwaka 2019 uchaguzi uliharibiwa maksudi kwa baraka zake, mwaka 2020 uchaguzi uliharibiwa maksudi sasa hapa unalaumuje wanamtandao
- Wakati ndugai anasema hajui Tundu lisu alipo magufuli alikuwepo kwanini hakuingilia na kuzui anakuaje mwema na hapa tena unawalaumuje wanamtandao
- Baada ya Assad kusema Trillion 1.5 hazina maelezo tuliona alivyopata harassment kuanzia kwa spika ndugai kwa kumtaka aende kwenye kamati ya bunge ikiwezekana kwa pingu, baadae tena magufuli akamtoa kinyume na katiba ya nchi sasà hapo huwezi laumu watu wa mtandao
- Wakati wa magufuli kuna wabunge wa upinzani walikuwa wanaunga juhudi wanahamia upande wa pili uchaguzi unarudiwa fedha za wananchi zinachezewa mfano mbunge wa kinondoni wakati wa CUF alikua anaitwa mtulila alihamia ccm akachaguliwa tena na budget ya ule uchaguzi ulikuwa ni billion na ushee watu walilaani sana na hapa huwezi walaumu mtandao
- Wakati wa utawala wa kikwete na mapungufu mengi ila vyama vya siasa vilikuwa vinafanya mikutano, kulikuwa na midahalo vyuoni, kwenye radio na tv kulikuwa na kipindi cha kipima joto nilikuwa sikosi wakina lisu, renatus mkinga, sengodo mvungi kwa uchache walikuwa wanaongea bila uoga alivyoingia magufuli yote hayo yakafa sasa hapo utalaumu mtandao si upunguani
- Magufuli kwa kinywa chake alisema hakuahidi katiba mpya baada ya watu kupiga kelele leo polepole anatuambia habari nyingine eti alisubiria mwaka 2024 ndo mchakato uanze simakosa yale yale anarudia ya kikwete sasa kama sio uongo ni nini alafu unakuja kuwalaumu mtandao
- Kuna wakati magufuli alitamka waziwazi watu wenye kesi za uhujumu uchumi wanaweza lipa chochote kitu serious nchi yenye mahakama Rais anasema watuhumumiwa flani wanaweza lipa fedha ambayo haijalikani inaenda serikalini au mifukoni mwa watu ni kama nchi ilikuwa inaelekea kwenye kuwa kama cartel sasa hii blunder huwezi tupia lawama wanamtandao