Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 17,571
- 27,647
Siyo kuminya Siasa mbadala tu, Ongeza na hizi:-Wabongo wengi ni kama walianza kumjua Magu akiwa Rais...
Lakini ka utakuwa ulimfuatilia tangu akiwa waziri, jamaa alikuwa mwamba sana...
Kuminya siasa mbadala na CCM hii ndio kasoro pekee katika uongozi wake iliyoweka doa jeusi...
1. Kuitisha Mahakama na kuifanya kibaraka wa Mhimili wa Serikali. Mahakama imebakia kupokea maelekezo ya Serikali, hii kitu inasumbua sana haki za watu. Angalia hata kesi ya TAL inavyopigwa danadana
2. Kuminya uhuru wa maoni na vyombo vya habari
3. Kuliendesha bunge kwa remote control. Kumbuka maelezo aliyokuwa anampa Ndugai, anamuambia awabane wabunge ndani ya bunge na yeye atawabana nje
4. Kuiba uchaguzi wote wa 2019 na wa 2020. Michezo ya kuharibu uchaguzi kwa kuwa disqualify wagombea wa upinzani ilianzishwa na Magufuli
5. Kuanzisha kikundi cha utekaji na mauaji (rogue unit within the security system) maarufu kama wasiojulikana chini ya Daudi Bashite
Hitimisho:-
Yaani kama mtu ameharibu hiyo misingi 5 hapo juu sielewi mnaomtetea mnatumia mantiki gani. Maana haya machafu ya Samia kipindi hiki cha 2021-25 ni muendelezo wa uchafu wa Magufuli ambao zamani haukuwapo. Hata hivyo Samia amejitahidi kwa kiasi kikubwa kupunguza uchafu huo japo hajamaliza.
Watanzania too wepesi wa kusahau. Hebu kumbukeni historia ya nchi yetu hadi November 2015, haikuwa na haya mambo tunalalamika. Ni Magufuli ndiyo katufikisha hapa