Pingu ya Muro

Kawaida Polisi wakikukamata na kosa hili na kuikuta kosa lingine basi ujue utawajibika kwa yote.mbona mtu akipekuliwa mfano labda nyumbani kwake wakiisi kitu wakikuta bangi na wakikuta Gongo pia wakikuta Bastola hayo yote ni makosa tofauti walikuja kusaka bangi wakakuta na makosa mengine yoote unashtakiwa nayo. hiyo ndio Sheria ya Nchi ilivyokaa nyie si mnapiga kura tuu sheria hamuijui sasa ndo hiyo na yeye kosa lililompeleka ni Rushwa na amekutwa na kosa la kukutwa na pingu sasa yote atapelekwa mahakamani. kwani si sheria kuwa na pingu bila kibali. Nawashauri msinunue pingu bila kuwa na kibali. mimi nimetoka keko kulivyoo du usiombe upelekwe asante.
 
lipo jambo litabainika kitambo kifupi tu, umwamba wa kutuonyesha bastola na pingu kama kielelezo ni kiini macho, nakumbuka wakati zombe akituaminisha kina Chigumbi ni majambazi , alicheza mchezo huu ambao Kova anajitahidi kuucheza.
Tangu lini upelelezi wa polisi hufanywa mbele ya vyombo vya habari ? rejea pale walipokua wakipekua gari la Muro, inaonesha walikua na hakika kuwa kuna kitu watakipata humo, maana kwanini uite waandishi wa habari .

__________________
 
Jamani wewe mwanakijiji ..naomba nitungi shairi spesho kwa mwandani wangu ..

unaweza kunambia zile Pingu zilikuwa zinatafuta nini kwenye gari ya Kijana wetu Jery ,,iweje ziwepo pale kwani yeye police
Nakosa imani na vyombo vyetu vya ulinzi
 
You peole Mwanakijiji, Mundu etc...
Mmeifanya niianze siku yangu vizuri.
I wish mngekuwa na TV show fulani...
You are so great!
 
Kakutwa mtu na pingu
Sasa yazua majungu
Imeleta kiwingu
Polisi waja na rungu
Kumbe pingu ya mapenzi!!-Polisi wamechemsha!

Akisharudi nyumbani
Muro na wake mwandani
Wakijifunga chumbani
Uwanja wa kitandani
Kumbe pingu ya mapenzi! - Polisi wamechemsha!

Afungwa mtu mkononi
Upande mwingine kichagani
Sisemi chafuata nini
Ni mambo ya mtimani
Kumbe pingu ya mapenzi- Polisi Wamechemsha

Swali: Ni kosa kukutwa na pingu ya mapenzi kwenye gari?

Hujatulia mwanakijiji lol!
 
Duh Pingu za mapenzi hiyo hatari anayefungwa nani sasa kidume au kijike?
 
Kakutwa mtu na pingu
Sasa yazua majungu
Imeleta kiwingu
Polisi waja na rungu
Kumbe pingu ya mapenzi!!-Polisi wamechemsha!

Akisharudi nyumbani
Muro na wake mwandani
Wakijifunga chumbani
Uwanja wa kitandani
Kumbe pingu ya mapenzi! - Polisi wamechemsha!

Afungwa mtu mkononi
Upande mwingine kichagani
Sisemi chafuata nini
Ni mambo ya mtimani
Kumbe pingu ya mapenzi- Polisi Wamechemsha

Swali: Ni kosa kukutwa na pingu ya mapenzi kwenye gari?

mkubwa kweli huu mwezi mzuri!!!!!! tenzi zinashika!!!!!
 
wana JF hasa mnanishangaza! .....mbona watu huwa wanawafung sana wandani wao ...sikuwaikijiskia wanataka kumfaidi bila ya kuwa interrupted?

sidhani kaa za muro ni za kimahaba ......lakini zikiwa JEE KOVA anaweza kuzitofautisha? hahahhaha .............

nafikiri waliowahi kuwa na wapenzi wa kiamerika watakuwa lazima mshakubwa na RPG!
 
Pingu ile ya mapenzi
wala si ya ujambazi
polisi Muro hamumwezi
yupo juu kama mkwezi

Polisi lazima mtaumbuka
kwa kushindwa mashtaka
miguu juu mtaanguka
kama mende anavyokauka

Jerry wewe ni shupavu
na wala si mpumbavu
Polisi hawana ubavu
watakuzidishia mashavu

Na wakimaliza kesi yao
Kawafungulie na wao
Uwadai mamilioni yao
Na kudhalilisha jeshi lao

Kamanda punguza sifa
kwa kushabikia yasiyofaa
utakuja kuumbuka
Siku Muro atakapotoka

Pingu ile ya mapenzi
Mwanakijiji ayaenzi
polisi fanya chunguzi
utakuja kumaizi

To be continued....
 
HIvi kweli unadhani polisi wakinidaka mimi na kukuta pingu ndani ya gari langu watauliza ninaitumiaje? shoot!

Jerry anaweza kukopa hii atumie kama defence!!!! ajisemeee alikuwa na kidate na baada ya hapo walikuwa waendezao nyumba ya wageni!!! so he carried the needful!!!
 
Jamani wewe mwanakijiji ..naomba nitungi shairi spesho kwa mwandani wangu ..

unaweza kunambia zile Pingu zilikuwa zinatafuta nini kwenye gari ya Kijana wetu Jery ,,iweje ziwepo pale kwani yeye police
Nakosa imani na vyombo vyetu vya ulinzi

siyo kosa kukutwa na pingu jamani; hivi ndugu zangu mkisikia "polisi wamesema" au "serikali imesema" ndiyo inakuwa kama mmelambishwa limbwata?
 
tatizo hii defense ikiwekwa hadharani na wa waswahili wakajua mambo ya pingu (wale ambao walikuwa hawajui) tutajikuta tunapata murder case hivi hivi; mara mtu kapigwa picha na katoto kashule kakatia pingu kwenye mlingoti! Au mbabu mmoja mtakuta ananing'inia kitandani!!
 
HIvi kweli unadhani polisi wakinidaka mimi na kukuta pingu ndani ya gari langu watauliza ninaitumiaje? shoot!

Kuna tofauti gani kati ya kamba na pingu? Unaweza kumfunga mtu pingu au ukatumia kamba; sasa mapolisi basi wawakamate wale wote wanaokutwa na kamba kwenye magari yao!! Wanajanvi nisaidieni, kuna sheria gani inayomkataza mtu kuwa na kamba au pingu? Raia ukimkamata mwizi na ukamfunga kamba au pingu ni kosa? Je pingu mtu hawezi kuzinunua popote duniani bila kuwa na kibali tofauti na silaha?
 
siyo kosa kukutwa na pingu jamani; hivi ndugu zangu mkisikia "polisi wamesema" au "serikali imesema" ndiyo inakuwa kama mmelambishwa limbwata?

yaa mie sina uhakika na hili kama ilikuwa ya mahaba ,malavidav iz ok najua hawa police kuna jambo wamefanya ndio maana nimeishiwa na imani nao
 
yaa mie sina uhakika na hili kama ilikuwa ya mahaba ,malavidav iz ok najua hawa police kuna jambo wamefanya ndio maana nimeishiwa na imani nao

jerry aliwachokoza 'kuwaanika' wakipokea rushwa......sasa wanam-nail!!!!!! (kisasi)
 
tatizo hii defense ikiwekwa hadharani na wa waswahili wakajua mambo ya pingu (wale ambao walikuwa hawajui) tutajikuta tunapata murder case hivi hivi; mara mtu kapigwa picha na katoto kashule kakatia pingu kwenye mlingoti! Au mbabu mmoja mtakuta ananing'inia kitandani!!

hakika baadhi ya watu watai-misuse hiyo defence!!!!! ukipata loopholes kwenye sheria lazima uitumie ipasavyo lol!!!
 
Sasa kama polisi ndio wanamnail mtu namna hiyo basi tuna kazi ya kupambana na mafisadi kwa kweli. Muro kuna vitu kachemsha na yeye; ni nani aliyempigia simu kumuambia juu ya mkutano wa waandishi wa habari. Hamtaji.
 
yaa mie sina uhakika na hili kama ilikuwa ya mahaba ,malavidav iz ok najua hawa police kuna jambo wamefanya ndio maana nimeishiwa na imani nao

well.. wacha nikutungie la kwako kwa mwandani wako.. tuachane na kina Kova!
 
siyo kosa kukutwa na pingu jamani; hivi ndugu zangu mkisikia "polisi wamesema" au "serikali imesema" ndiyo inakuwa kama mmelambishwa limbwata?

weeeeeeeee MM hizo ni dola wenzio tunaogopa misystem hiyo haishindwagi!!!!! si unaona kamanda mwenyewe kasema ni wao tu ndo pilato kawapa ruhusa kuzimiliki!!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom