Pingu ya Muro

Pingu ya Muro

Sasa kama polisi ndio wanamnail mtu namna hiyo basi tuna kazi ya kupambana na mafisadi kwa kweli. Muro kuna vitu kachemsha na yeye; ni nani aliyempigia simu kumuambia juu ya mkutano wa waandishi wa habari. Hamtaji.

hii habar tangu itoke imekuwa ya kuunga unga sana kwa kweli....biafsi jana nilishindwa kupata picha naona bado kuna mambo hayapo wazi kabisa!!!!!!
 
Katika mambo ya kujadili kama taifa tunapoteza muda mrefu kabisa kuzungumzia non-issues! Polisi na Jerry wote wamechemsha! Kwa hiyo watacancel each other.. ila atakayeibuka winner hapa (though bruised) ni Jerry hasa kama Polisi watashindwa kuleta mashtaka yoyote dhidi yake..
 
Individual Vs The System .............and the winner is.....................
 
ahlan wa sahlani
mzee wa bush salaam
leo kweli tafrani
pingu kitu ya hanjam
usanii wa jeshi letu, polisi kweli aibu

nimesoma tenzi zako
nikapata kesi yako
pingu na chikichiki
hakika hii habari
usanii wa jeshi letu, polisi kweli aibu

hii ni rap katuni
eti kwanza rushwa
kisha ni utishaji
sasa na pingu ndani
usanii wa jeshi letu, polisi kweli aibu
 
@Mwanakijiji u cracked me up!! Actually nilipofungua hili jukwaa nikawaza imekuwaje hii iko kwenye jukwaa la mapenzi na mahusiano! U creative lol..na naona tuna watunzi wengi humu!! Mtakuwa wachombezaji wzr kwa wake zenu!

Rejea issue ya Muro jamani kweli hii Tz ina mambo aah!...sasa Kova anaongea kwa uhakika kama alienda?? Yaleyale ya kombe
Kwa kweli!! Mara ooh hamna mtu alijua kuwa ni Muro ndo mtuhumiwa wakati Muro anasema uyo mtu aliitwa amtambue akasema huyuhuyu ndio Jerry Muro yani hii kesi haiitaji expert kuifanyia upelelezi!! Ukisikilza watu wanne tu waliohusika kwenye tukio zima utaona kuna jambo!!?
 
cha msingi muro aseme kama anahitaji wanasheria ili kuweza kumsaidia kwani kwa kesi kama yake jamii isipoangalia itakuwa ndio mwanzo wa mwisho wa harakati za muro, cha msingi ni jinsi polisi walivyompeleka kwa upole ninavyowajua wangeweza kumsingizia mwizi na kumshuti kwani wako wapi akina zombe walioua mtu bila kutiwa hatiani, yuko wapi kombe waliyemsingizia mwizi wa gari na kumshuti


muro kama utapenda upatiwe wanasheria tutakupa bure
 
Nilikuwa sifahamu matumizi yake mengine nami niko mbioni kununua
..Usiniambie pingu ina matumizi mengine mwana...mi nilidhani nikufungia yale mahalifu tu...hebu tujuzane basi wajameni...
 
Sasa kama polisi ndio wanamnail mtu namna hiyo basi tuna kazi ya kupambana na mafisadi kwa kweli. Muro kuna vitu kachemsha na yeye; ni nani aliyempigia simu kumuambia juu ya mkutano wa waandishi wa habari. Hamtaji.
Hapa napo nimejiuliza baada ya kumsikliza Jerry jana nimeconclude kuwa, bado mazingira yanaonyesha police kuna kitu wamefanya, ila!! Nimejiuliza level ya shule ya Jerry!! Hizi kazi ni kama wamezivamia bila kujua tactcs zake!!
Maana kwa kazi anayofanya ni kama ushushushu, sasa how comes unaitwa mahali unaenda tu bila kudoubt kitu na mtu humjui!! Na je ndo style zinatumikaga kuitana kwenye vikao vyao!!? Annonymous callin na una obey tu??? Alafu mara 'hata ningejua kuna police nisingeenda'!! Wtf??? Yani wanajamvi mnisaidie level ya Elimu ya Jerry kuna maneno anaongea mpaka unajiuliza!! But still nasimamia Jerry sizan kama ana hatia ila hajui kujieleza au amepanick!!... Watanzania tuko upande wake atusaidie kutupa maelezo mazuri!..
 
..Usiniambie pingu ina matumizi mengine mwana...mi nilidhani nikufungia yale mahalifu tu...hebu tujuzane basi wajameni...

Laligeni karibu!!!!!!!!!! hahaaaaaaaaaaaa
 
hii habari ina maswali mengi, kwanza ukisikiliza maelezo ya kamanda, anasema vijana wake waliamua kumkamata baada ya kuona hataki kuingia ndani ya hoteli, kama kulikuwa na askari 6 wenye silaha na defender, kwanini wasingemruhusu mshtaki wao afanye vile jeri alivyotaka, kwanini wasingesubiri ili jamaa amkabidhi fungu lake ndio wamkamte?
 
Eti pingu ya mapenzi, watembea nayo garini
Huu kama si ushenzi,basi tuuite nini?
Tummulike kurunzi,huyu Jerry kwa undani
Kama pingu ya mapenzi na ingeachwa nyumbani.

Eti pingu ya mwandani, ya kutumia chumbani
Halafu iko garini, kwa pembeni ya miwani
Ya Wage hiyo miwani,kaisahau jamani
Kama pingu ya mapenzi na ingeachwa nyumbani.

Kama ni penzi la pingu, basitola ni ya nini?
Mapenzi yenye kiwingu, ya kumtisha mwandani !
Akijificha kwa uvungu, hivi talaumu nani ?
Kama pingu ya mapenzi na ingeachwa nyumbani.
 
Jamani mwenye taarifaa zaidi atufahamishe kesi ya Jerry itakuaje according to the reliable sources? Tufahamisheni sie tulio mbali na bongo.
 
alirashidou
user_online.gif

alirashidou has no status.
Junior Member
red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png
green.png
green_right.png

Join Date: Wed Mar 2008
Posts: 5
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 0
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif



dah!wazee mambo mengine ni kama hayawezekani hivi
 
alirashidou
user_online.gif

alirashidou has no status.
Junior Member
red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png
green.png
green_right.png

Join Date: Wed Mar 2008
Posts: 5
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 0
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif



dah!wazee mambo mengine ni kama hayawezekani hivi

goeff goeff hakuna lisilowezekana chini ya jua why are pretending that u hv 4goten this!!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom