bht
JF-Expert Member
- May 14, 2009
- 10,336
- 1,860
Hiyo pingu ya mapenzi,
Walahi yanishangaza,
Wake anaye muenzi,
amfunge kwa kukaza?
Kioja pingu ya penzi.
Mwanakijiji nijuze,
Mila hii ni ya wapi?
Kwa pingu mwili ukaze,
utazihitaji ngapi?
Kioja pingu ya penzi.
Uanze kufunga miguu,
Kisha wende mikononi?
Halafu domo la juu,
hayo yote kulikoni?
Kioja pingu ya penzi.
mkubwa hii ni pande yako nyingine eeeeh!!!!!!!!!!! safi sana!!!! Mungu kweli ametupa talanta!!!