Mwali
JF-Expert Member
- Nov 9, 2011
- 7,014
- 5,610
- Thread starter
- #21
Hapa napenda tusahihishe kweli kadhaa kuhusu tunda linalodaiwa ni tendo la ndoa. Mungu tayari alishamuumba Adamu na Hawa na akamleta Hawa kwa Adamu akampa agizo "Zaeni mkaongezeke". Kabla ya hapo ni budi ujue jinsi Mungu alivyomleta Hawa duniani na kwa Adamu; soma Mwanzo 2:21 kuendelea
"Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
25 Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya."
Kama Adamu ameshaletwe mwanamke na kupewa maagizo ya kuzaa, itakuwaje kweli tutafsiri kuwa tunda walilokula Adamu na Hawa ni tendo la ndoa ambalo tayari walikuwa wamehalalishiwa? Nadhani kuna tatizo kwenye uelewa wetu wa mambo na tafsiri zake. Jamani tunda hilo ni literal tunda, na wala si tendo la ndoa kama ambavyo nimesikia wengi wakitafsiri
Ndio, hata mimi sijui kwanini wanadhani ni tendo la ndoa.
Na ndio maana nimesema huenda litakua ni tunda hili
This is a literal tunda na linaliwa (pun intended) Pastequizzi