Connection hii ya Nyoka, Hawa, Kaini.. Je ndio ufunuo ulioleta kizazi cha nyoka?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,914
Kwa nini Mungu aliruhusu Abel auliwe na ndugu yake Kaini wakati kimsingi Kaini ndiye ambaye sadaka yake haikumfurahisha Mungu? Kuna ujumbe mzito sana hapa!
Connection ya maisha yaliyofuata baada ya pale Eden yanatupa majibu kwenye hii dunia tuliyo nayo leo, dunia yenye watu wabaya, wabinafsi, wachoyo, waroho, wasotosheka, wauaji nk

Nyoka baada ya kumlaghai na kumshawishi Hawa ale tunda la mti wa kati la UJUZI wa MEMA na MABAYA (chukulia hayo matendo mawili yakatengeneza roho mbili za wema na ubaya (Kaini akiwakilisha ubaya na nduguye Abeli akiwakilisha wema) na ujuzi ukiwa kwenye kila tendo!

Hawa akaliona tunda/matunda AKALA na kumpa mumewe Adam naye akala....
Yakatokea mengi hapo katikati mpaka wote watatu kufukuzwa toka Eden na kila mmoja wao akipewa,adhabu yake kulingana na kosa lake
Nyoka atembelee tumbo... Ina maana alikuwa na miguu mwanzoni
Hawa azae kwa uchungu.. Kama si kula lile tunda la mti wa kati asingezaa kwa uchungu( hapa tunapata ufunuo mwingine kwamba kumbe Mungu alishamchagua Hawa awe ndio kibebeo cha uzazi ama la hiyo plan ilikuja baada ya 'kula tunda'
Adam yeye akaambiwa atakula kwa jambo.. Kabla ya hapo ndani ya Eden ilikuwa bata full time..

Baada ya kutoka Eden nyoka akashika njia yake na Adam na Hawa wakashika njia yao.. Kwa kile kibali cha Mungu Adam akamjua mkewe! Zingatia hapo.. Yaani ndio kwa mara ya kwanza Adam akamuingilia mkewe kimwili..! Naye akapata mimba... Ufunuo uliopo hapa ni kwamba Hawa hakuwa kigoli kwa maana ya bikira! Je ni nani alimbikiri Hawa?

Hiyo ni tofauti kabisa na habari za bikira Maria mama wa Yesu ambaye anatajwa kwamba hakuwahi kumjua mwanaume na hata mimba yake ilikuwa kwa uwezo wa roho mtakatifu.. Kwahiyo kuna kitu kiliwahi kumtokea Hawa kilichosababisha kupoteza usichana wake!

Tufupishe kwa mengi yaliyotokea.. Baada ya Adam kumjua mkewe akapata ujauzito uliopelekea kupatikana Kaini.. Hapa ikisemwa kaini akiwa na vinasaba vya nyoka na ile laana ya kwanza ya kula tunda la mti wa kati.. Kizazi cha nyoka.. Hapa kwenye yale matendo mawili ya mema na mabaya! Matendo mabaya kupitia Kaini yakapata mwakilishi wake
Baada ya hapo Adam akamjua tena mkewe na kupata mimba iliyozaa mtoto wa pili Abeli.. Huyu akiwa ni kiwakilishi cha uumbaji na yale matendo mema...huyu hakuwa na vinasaba na nyoka.. Akawa mjuzi wa ufugaji na kaka yake akawa mkulima..
Matendo mabaya kupitia Kaini, yakayashinda matendo mema. Kaini akainua upanga wake na kumuua ndugu yake wa damu! Kuuliwa kwa Abeli kuliwakilisha kuondoshwa kwa matendo mema duniani.. Dhuluma ikawa mshindi dhidi ya haki!

Ufunuo wa kutatanisha.. Kaini mchoyo, mbinafsi, muuaji akaenda nchi ya mbali huko akaoa na kuendeleza ukoo.. Yaani kile kinasaba cha nyoka tangu pale Eden kikapata mwendelezo..
Imagine kama Kaini ndio angekufa na Abeli kuishi mambo yangekuwa tofauti kabisa na vile yalivyo leo hii. Dunia isingekuwa hii. Abel asingewaacha wazazi wake na kwenda nchi ya mbali..

Ukoo alioenda kukutana nao Kaini hautokani na Eden, je ulitokana na ninini? Je alifika huko kwa msaada wa baba wa vinasaba Nyoka? Je ndio asili ya kizazi kilichofuatwa kuitwa kizazi cha nyoka?
Tuendeleee kujifunza

CC: mjingamimi
 
Back
Top Bottom