Kama Mungu alimuumba Adam na Hawa katika asili ya muafrika, hawa wazungu, wachina, wahindi watakuwa wametoka wapi?

crankshaft

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,410
3,376
Kwa mujibu wa special creation theory ni kwamba wanadamu Waliumbwa na Mungu katika namna ambayo wapo Leo. Baada ya uumbaji waliambiwa wakazae ambapo walitumia njia ya sexual reproduction.

Ukuaji wa sayansi katika biology specifically katika genetics umeonesha kwamba wazazi Wana influence katika namna mtoto wao anaweza kuwa kupitia vinasaba vyao.

Kwa mfano katika races,kama wazazi wako ni waafrika (weusi) tunategemea hata mtoto atakuwa mweusi.

Na hizo Tabia haziwezi kuathirika iwapo kutakuwa na mabadiliko Kwa wazazi kutokana na mazingira. Mfano kama mama kabadilika rangi ya ngozi Kwa matumizi ya mafuta ya ngozi,basi haiwezi kumfanya mtoto wake naye awe mweupe.

Now we go,
Kama mungu alimuumba Adam na hawa katika race ya muafrika, je hawa wazungu, wachina, wahindi,n.k watakuwa wametoka wapi? Kwa sababu Kwa mujibu wa genetics, haiwezekani wazungu kuzaa waafrika.

Sasa kama ni hivi, je hii inaweza kuhalalisha kuwa hadithi za biblia ni za uwongo Kwa sababu mzizi wake una walakini?

Na kama basi mungu aliwaumba hawa watu wa race nyingine, kwa nini nao wanakula Kwa jasho wakati hawakuhusika kula tunda?

Karibuni wadau.
 
MUNGU alimwumba Adamu akiwa na vinasaba vya rangi zote unavyoona kwa wanadamu.hakuna sehemu kwnye biblia inayosema adamu alikuwa rang fulani bali inasema esau alikuwa mwekundu.fikiri toka adamu hadi ibrahimu ni zaidi ya miaka 2000.
 
MUNGU alimwumba Adamu akiwa na vinasaba vya rangi zote unavyoona kwa wanadamu.hakuna sehemu kwnye biblia inayosema adamu alikuwa rang fulani bali inasema esau alikuwa mwekundu.fikiri toka adamu hadi ibrahimu ni zaidi ya miaka 2000.
 
Back
Top Bottom