Picha ya Kimkakati: Rais Samia na Watoto wa Kitanzania nchini Namibia

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alirejea nchini jana kutoka nchini Namibia.
Akiwa nchini humo baada ya kuhitimisha Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Troika Jijini Windhoek nchini Namibia, alipata wasaa wa kuzungumza na sehemu ya Watanzania waishio nchini humo, baadhi wakiwa na familia zao tarehe 08 Mei, 2023.


Katika baadhi ya picha zilizotolewa na kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Rais Samia alionekana akiwa mwenye furaha na watato wa Watanzania wananoishi nchini humo huku nyingine akionekana anapiga nao "soga" kidogo baada ya kuzungumza na Watanzania (Diaspora) katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek

Katika picha nyingi ambazo wapiga picha wa Rais huwa wanapiga sehemu kubwa huwa "hazizungumzi" na zikiwa zinakosa "context" lakini kwa picha hizi za watoto nchini Namibia pengine sasa wameanza kugundua kuwa kumpiga picha Rais sio tu kubonyeza Camera na kutoa picha.

Kila picha ya Kiongozi wa nchi inapaswa kuzungumza, inapaswa kubeba ujumbe unaojitosheleza bila hata kuandikiwa maelezo "caption",. Vitengo hivyo kwa nchi za wenzetu hapa jirani tu kama Rwanda wameliweza sana hilo kwa picha wanazozitoa za Rais PK. (Angalizo neno picha wanazozitoa halijatumia bahati mbaya hapa"

Siku za karibuni tumekuwa na picha zenye mwelekeo wa matakwa niliyoyataja hapo juu lakini binafsi niwapongeze kwa picha za Rais Samia akiwa na watoto nchini Namibia, waendelee kushikilia hapohapo.

Vipi kwako mdau, ipi ni picha bora ya Rais Samia tangu aingie Ikulu.

FvsTQDLaQAET6Ez.jpeg
Fvs4LwDWcAAnC2I.jpeg
 
Sawa Sawa
Mama Anaupiga Mwingi Sana Na Wajukuu Huko Namibia 🇳🇦
Neema Nyingi, Huku Bwawa La Mwalimu Nyerere Limejaa Maji
Kule Rasimu Ya Katiba Mpya, Mchele Tunakula Taratibu
Tanzania 🇹🇿 Imetulia Imekuwa Ya Asali Na Maziwa

Ikulu Imekamilika Inangoja Kufunguliwa, Dodoma Sasa Ya Kijani
Maji Yanamwagika Jiji Lote Tena Baridii
Aweso Anaongeza Maji Toka Bwawa La Mtera Hapo Dodoma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom