Picha: Rais Samia atumia sayansi kuzuia mikutano ya wapinzani

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Wakati Rais wa awamu ya tano mheshimiwa John P. Magufuli anaingia madarakani, miongoni mwa vitu vya kwanza kabisa alivyovifanya katika uongozi wake ni kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa akiamini kwamba mikutano hiyo ilichangia uzorotaji wa kuleta maendeleo katika nchi yetu. Kwani ilifika kipindi watu walishindwa au kukataa kwenda kufanya kazi na badala yake kwenda kushinda mikutanoni.

Hali hii iliwaumiza sana wapinzani, kwani hawakuwa na pa kusemea, wengi waliamini kwamba nguvu ya upinzani hupatikana kupitia mikutano mbali mbali ya hadhara, hivyo kukataa mikutano ni kuuwa nguvu za wapinzani indirect. Hivyo walipaza sauti na kulalamika kwa kila hali ili mikutano hiyo ifunguliwe bila mafanikio.

Alipofariki Magufuli, na kuingia raisi Samia madarakani, yeye alikubali kufanya mabadiliko kwa baadhi ya mambo ili aweze kwenda sawa na wapinzani wake.

Moja kati ya mambo aliyokubaliana na wapinzani wake ni kuruhusu mikutano ya vyama, kwa masharti ya kufanya mikutano hiyo kwa njia ya amani, bila matusi wala fujo.

Marufuku ikatolewa wapinzani haswa Chadema wakaanza kazi kwa kuandaa mikutano, na operation mbali mbali za kuzunguka nchi. Baada ya muda hali ikabadilika, alieruhusu mikutano ifanyike ambae ndio mkuu wa nchi akaanza kuambiwa ana akili za ma..to..pe na makamu mwenyekiti wa chama fulani cha upinzani, eti kisa ni mkataba wa bandari.

Hali ikawa mbaya matusi yakatamalaki, hadi vyombo vya usalama vikaingilia kati ili kuzuia zile siasa za majitaka za 2010 hadi 2015 zisijirudie tena.

Baada ya vyombo vya usalama kuingilia kati, makamu akatimkia Ulaya kuangalia familia yake na kupeleka hela za ada za watoto wanaosoma kule baada ya kuzipata hela hizo kupitia michango ya wanachama wao masikini na wanyonge mbali mbali.

Wakati makamu akiwa Ulaya, mwenyekiti nae hakutaka kuonekana kuwa yeye anategemea nguvu ya soda kutoka kwa makamu, mwenyekiti nae akaanza kuzunguka na chopa huku akisema aliyoyasema.

Alieruhusu mikutano akaangalia aina ya siasa wanayofanya wapinzani wake, akaona dawa ya hao wapinzani ni kuwaletea kijana atakaewapeleka mchaka mchaka hadi wale wasiosema waseme.

Sasa kijana yuko kazini, wapinzani waliokuwa wanalalamika kuhusu mikutano, leo hii kwa hiari yao wenyewe wameacha kuendelea na mikutano, na hakuna njia tena ya kumlaumu raisi kuwa anakataza mikutano na wakati ni wenyewe ndo wamekataa kuendelea na mikutano kutokana na kukosa ushawishi kama wa kijana wa raisi.

Kwa sasa hasikiki, wala kuonekana Zito, Lisu, Mbowe, Mbatia, Lipumba wala mzee wangu wa ubwabwa mh Hashim Rungwe.
 
Attachments

  • IMG-20230520-WA0008.jpg
    IMG-20230520-WA0008.jpg
    109.8 KB · Views: 8
  • images (7).jpeg
    images (7).jpeg
    96.1 KB · Views: 7
  • images (4).jpeg
    images (4).jpeg
    53.4 KB · Views: 8
  • images (9).jpeg
    images (9).jpeg
    88.6 KB · Views: 7
  • 1699857405632.jpg
    1699857405632.jpg
    104.2 KB · Views: 4
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Wakati Rais wa awamu ya tano mheshimiwa John P. Magufuli anaingia madarakani, miongoni mwa vitu vya kwanza kabisa alivyovifanya katika uongozi wake ni kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa akiamini kwamba mikutano hiyo ilichangia uzorotaji wa kuleta maendeleo katika nchi yetu. Kwani ilifika kipindi watu walishindwa au kukataa kwenda kufanya kazi na badala yake kwenda kushinda mikutanoni.

Hali hii iliwaumiza sana wapinzani, kwani hawakuwa na pa kusemea, wengi waliamini kwamba nguvu ya upinzani hupatikana kupitia mikutano mbali mbali ya hadhara, hivyo kukataa mikutano ni kuuwa nguvu za wapinzani indirect. Hivyo walipaza sauti na kulalamika kwa kila hali ili mikutano hiyo ifunguliwe bila mafanikio.

Alipofariki Magufuli, na kuingia raisi Samia madarakani, yeye alikubali kufanya mabadiliko kwa baadhi ya mambo ili aweze kwenda sawa na wapinzani wake.

Moja kati ya mambo aliyokubaliana na wapinzani wake ni kuruhusu mikutano ya vyama, kwa masharti ya kufanya mikutano hiyo kwa njia ya amani, bila matusi wala fujo.

Marufuku ikatolewa wapinzani haswa Chadema wakaanza kazi kwa kuandaa mikutano, na operation mbali mbali za kuzunguka nchi. Baada ya muda hali ikabadilika, alieruhusu mikutano ifanyike ambae ndio mkuu wa nchi akaanza kuambiwa ana akili za ma..to..pe na makamu mwenyekiti wa chama fulani cha upinzani, eti kisa ni mkataba wa bandari.

Hali ikawa mbaya matusi yakatamalaki, hadi vyombo vya usalama vikaingilia kati ili kuzuia zile siasa za majitaka za 2010 hadi 2015 zisijirudie tena.

Baada ya vyombo vya usalama kuingilia kati, makamu akatimkia Ulaya kuangalia familia yake na kupeleka hela za ada za watoto wanaosoma kule baada ya kuzipata hela hizo kupitia michango ya wanachama wao masikini na wanyonge mbali mbali.

Wakati makamu akiwa Ulaya, mwenyekiti nae hakutaka kuonekana kuwa yeye anategemea nguvu ya soda kutoka kwa makamu, mwenyekiti nae akaanza kuzunguka na chopa huku akisema aliyoyasema.

Alieruhusu mikutano akaangalia aina ya siasa wanayofanya wapinzani wake, akaona dawa ya hao wapinzani ni kuwaletea kijana atakaewapeleka mchaka mchaka hadi wale wasiosema waseme.

Sasa kijana yuko kazini, wapinzani waliokuwa wanalalamika kuhusu mikutano, leo hii kwa hiari yao wenyewe wameacha kuendelea na mikutano, na hakuna njia tena ya kumlaumu raisi kuwa anakataza mikutano na wakati ni wenyewe ndo wamekataa kuendelea na mikutano kutokana na kukosa ushawishi kama wa kijana wa raisi.

Kwa sasa hasikiki, wala kuonekana Zito, Lisu, Mbowe, Mbatia, Lipumba wala mzee wangu wa ubwabwa mh Hashim Rungwe.
Aliyeelewa huu uharo anisaidie.
 
Back
Top Bottom