Yeyote aliyemsifia kikwete analazimika kujibu swali lifuatalo; UKIMKUTA SHETANI KANISANI UTASHANGILIA NA KUSHUHUDIA YA KUWA SHETANI AMEOKOKA, MAJARIBU KWISHNEHI??!!!!!!!!!!! R.I.P REGIA
Jogi Mwanadamu akimkosea Mungu ageuki shetani hapa duniani,kwa kuwa Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake hivyo, kama Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake basi kimpatacho mwanadamu baada ya kukiuka maagizo ya Mungu wake ni kugeuka kuwa mfuasi wa shetani na si Shetani,kwa kuwa unapokuwa mfuasi wa kitu unakuwa na hiari yako binafsi uache au ufuate ndio maana wanadamu tofauti na wanyama tunakitu kikubwa Mungu katupatia nacho ni utashi.
Na kikubwa Mungu hakuja duniani kwa wema pekee bali alikuja kwa wakosefu,kwa kuwa ukombozi umewekwa kwa ajili ya wakosefu,ambao ni mimi,wewe na mwingineyo yoyote hapa duniani na kipimo cha ubaya ni wema.
Kilichofanya na Mheshimiwa Rais ni chema hata kama kuna yale ambayo sisi tunaona anamakosa nayo lakini tuna nafasi pia ya sisi kupima uzuri na hatujui nafsi yake yeye kwa msiba huo anajisikia kuwajibika kwa lipi kimatendo ila jukumu ni lake yeye na mola wake nasi wengine kama binadamu wenzie tutampima kibinadamu kwa matendo yake ikiwemo hili la kuhudhulia kwenye msiba wa Binti wa Nchi ambae yeye ni Rais wake.
Siri ya Mungu juu ya kwanini haya yatokee na kwanini Jakaya audhulie msibani anayo Muumba na kwa kila mmoja wetu mioyoni mwake kama Wanadamu tulio umbwa na Mungu.Ndio maana mambo uwa hayatokei hivi hivi yanatokea kwa sababu Mungu anasababu zake.
Ndio maana mimi kuna thread niliandika humu ndani kuwa msiba wa Regia, Mungu anasababu na Watanzania [
BOFYA HAYA HAPA].
Alichofanya Rais Jakaya Kikwete ndicho Mungu alichopanga, na ndio maana humu ndani kuna watu wameanza kuhoji na walitamani kuona picha ya Dk Jakaya na Dk Slaa,zikipamba kulasa za magazeti ya Watanzania,hakika hata mimi ninatamani,lakini Mungu ndie anaeujua atawakutanisha wapi na kwa sababu gani.Amepanga tumemuona Jakaya kwenye msiba,ambao wewe unaona ni shetani kaingia kanisani.
Ushauri wangu kwako uko katika picha hii ni nani hasa Shetani? Kati yako wewe ulie hoji udhulio la Rais Jakaya Kikwete ambae tunamtizama kuhudhulia kwenye msiba wa mpendwa wetu Regia Mtema akiwa kama Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Chama cha CCM ambacho ni chama shindani cha Chadema,na kama Mtanzania wa kawaida na wewe uliyetoa kauri ya kishetani.
Kwa kuwa kialisia mtu ambae ana akili timamu na si za kiwendawazimu yani akili za kishetani, msiba uwa hauna ndugu tunajua dhahiri hilo licha ya kuupokea kwa tafsiri ya ushiriki wetu hapa duniani na mahusiano yetu na Mungu, pia tunaupokee kwa tafsiri ya tendo la kibinadamu na hasa kiafrika tunapofiwa na wenzi wetu kisha ndugu, jamaa na marafiki wakafika kuja kushiriki nasi kwenye maombolezo, jamii nzima ujisikia auheni kuwa Mungu ametwaa mwenzi wao lakini Mungu huyo huyo ametuma waja wake kuja kuwapa wafiwa matumaini mapya kwenye tukio ilo la kuondokewa na mpendwa.
Hivyo kuhudhuria kwake na wengineo wote waliodhuria na watakao hudhuria mpaka dakika ya mwisho kumfikisha mpendwa wetu Regia kwenye makazi yake ya milele.
Basi kama shetani atakuwa na sura ya ubinadamu atafanana na ni yule aliyehoji watu wote wa Mungu ambao, Mungu aliwaumba kwa mfano wake,kisha kwa mfano wake huo leo kawapa dhamila ya kuwatuma waudhurie msiba wa Regia kuwafariji wafiwa mpaka kwenye kumsitili mpendwa wao huyo.
Pole sana Jogi,Mungu bado anakupenda anakupa nafasi kwa kuwa usijione umesimama, Mungu hakuja kwa wema kwa kuwa wema tayari ni wake,bali alikuja kwa wakosefu.
Ndio maana aliye mwema wake Regia Mtema kesha mchukua.
RIP Regia.