Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

hayo ni mambo yake binafsi, bora tu awe mzima na aachie madaraka salama.. Watu wachukue nchi (chadema) ...
 
Habari zimeenea kuwa rais Jakaya Kikwete alikunywa dawa ya mchungaji Ambillikile Mwasapile alipokuwa ziarani mkoani Manyara.

Wale ndugu zetu (wavivu wa kufikiri) ambao wengi wao wanatoka kile chama cha zamani (CCM), bila kufanya utafiti wowote wakaanza kueleza eti habari hizo ni UVumi na majungu ya kutaka kumchafua rais Kikwete.

Watu hao ambao bila kushirikisha ubongo wamekuwa wakipinga kila madai yanayotolewa kwa Chama na Serikali yao napenda kuwaeleza yafuatayo.

Ni kweli kuwa Rais Kikwete alikunywa dawa hiyo alipokuwa ziarani mkoani Manyara kuzindua shughuli za ufukuaji wa nyayo za binadamu wa kale, zilizogunduliwa na Archiologist Mary Leakdy mke wa Dr.Leakey.

Kulingana na taarifa kutoka kwa kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, msafara wa rais Kikwete wakati wa kurudi kutoka Ngorongoro ulipaswa kupita kata ya Samunge na baadae mji mdogo wa Mto wa Mbu.

Kata hiyo ya Samunge ndipo alipo Mchungaji Ambilikile, na wakati msafara wa rais Kikwete unapita hapakuwa na msongamano kama ilivyo sasa.

Kwa hiyo nawashauri wote wanaobisha kabla ya kubisha wafanye utafiti na ikiwezekana wamuulize Mchungaji Ambilikile mwenyewe, kuliko kubisha kishabiki.

Pia wafute mawazo mgando kuwa wanaotoa taarifa za Rais Kikwete kutumia dawa hiyo eti wanamchafua. Badala yake waamini kuwa taarifa hizo ZINAMSAFISHA MNO rais Kikwete kwani sasa atakuwa ametakasika kutokana na maradhi SUGU na ya MUDA MREFU yaliyokuwa yakimsumbua na kumfanya aanguke jukwaani mara kwa mara.

MUNGU IBARIKI AFRIKA,
Mungu mbariki mchungaji Ambilikile,
Mungu mbariki rais wetu Kikwete, ili dawa aliyopewa ifanye kazi.
 
Na aache kuchanganya na mambo ya kichawi ama sivyo dawa haitafanya kazi.
 
Mbona Sheikh Yahya na wengineo wamefanya uponyaji kwa muda mrefu na kwa watu wengi tu lakini serikali haikuwahi kutilia shaka au kusimamisha huduma zake. Au ndio kusema imethibisha huduma za Yahya? Jamani, masuala ya imani tuwaachie wenye imani zao tena ukizingatia serikali haina dini wala haifungamani na imani yoyote.
 
Habari zimeenea kuwa rais Jakaya Kikwete alikunywa dawa ya mchungaji Ambillikile Mwasapile alipokuwa ziarani mkoani Manyara.

Wale ndugu zetu (wavivu wa kufikiri) ambao wengi wao wanatoka kile chama cha zamani (CCM), bila kufanya utafiti wowote wakaanza kueleza eti habari hizo ni UVumi na majungu ya kutaka kumchafua rais Kikwete.

Watu hao ambao bila kushirikisha ubongo wamekuwa wakipinga kila madai yanayotolewa kwa Chama na Serikali yao napenda kuwaeleza yafuatayo.

Ni kweli kuwa Rais Kikwete alikunywa dawa hiyo alipokuwa ziarani mkoani Manyara kuzindua shughuli za ufukuaji wa nyayo za binadamu wa kale, zilizogunduliwa na Archiologist Mary Leakdy mke wa Dr.Leakey.

Kulingana na taarifa kutoka kwa kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, msafara wa rais Kikwete wakati wa kurudi kutoka Ngorongoro ulipaswa kupita kata ya Samunge na baadae mji mdogo wa Mto wa Mbu.

Kata hiyo ya Samunge ndipo alipo Mchungaji Ambilikile, na wakati msafara wa rais Kikwete unapita hapakuwa na msongamano kama ilivyo sasa.

Kwa hiyo nawashauri wote wanaobisha kabla ya kubisha wafanye utafiti na ikiwezekana wamuulize Mchungaji Ambilikile mwenyewe, kuliko kubisha kishabiki.

Pia wafute mawazo mgando kuwa wanaotoa taarifa za Rais Kikwete kutumia dawa hiyo eti wanamchafua. Badala yake waamini kuwa taarifa hizo ZINAMSAFISHA MNO rais Kikwete kwani sasa atakuwa ametakasika kutokana na maradhi SUGU na ya MUDA MREFU yaliyokuwa yakimsumbua na kumfanya aanguke jukwaani mara kwa mara.

MUNGU IBARIKI AFRIKA,
Mungu mbariki mchungaji Ambilikile,
Mungu mbariki rais wetu Kikwete, ili dawa aliyopewa ifanye kazi.

Kaka unasema kweli,na kama ni kweli mhe.jk atangazie umma umuhimu wa dawa hiyo maana yeye aliitumia na anajua fika rais wetu jinsi inavyomsadia.
 
WanaJF tuache siasa kwenye jambo hili.Tuache wataalam wafanye kazi.Tunajua serikali yetu haina dini,haifungamani na imani za kidini na ni wajibu wake kulinda uhai wa watu wake.Serikali needs to take babu seriously kwasababu magonjwa ambayo babu anasema anayatibu ni magonjwa sugu,yana mateso sana,na hayatibiki mpaka sasa pamoja na maendeleo makubwa ya sayansi ya tiba duniani na yanaua sana duniani kote.Wengine yameshatupotezea ndugu zetu wengi wa karibu na kweli tunatamani sana,siku moja dawa ya kuyaponya ipatikane.Lakini hii dawa isiwe ya kubahatisha na labda kumuongezea matatizo zaidi au hata kumuua mgonjwa in a long run.Hivyo huyu Babu anaposema anatibu lazima tujue kwanza active ingredient(s) ya/za hiyo dawa yake ni nini?Lazima pia tujue targets za dawa mwilini na mechanism of action ya hiyo dawa na side effects zake.Kuna aina nyingi za kansa na huwa zinakuwa katika grades na stages tofauti at diagnosis hivyo kufanya na matibabu kuwa tofauti pia.Hawezi kuchemsha maji na majani fulani halafu akasema anatibu kansa,eti kaoteshwa na Mungu.Hata Kisukari nacho kipo tofauti na matibabu yake pia ni tofauti.HIV/AIDS ndiyo kabisaa
Askofu Laizer kwa maoni yangu anakosea anapopinga tiba ya babu kupelekwa maabara kwanza.Huyu babu hatibu kwa imani bali kwa miti shamba.Kutibu kwa imani ni kwa kuamuru/maombezi/kusali kama walivyofanya manabii wa kale kina Elisha,Elijah na hata Yesu mwenyewe na wanafunzi wake.Hawa walikuwa 'wanaongea' tu na wagonjwa wanapona.Hawakuwa wanachemsha maji na mizizi/majani kama babu wa loliondo.Angekuwa anatibu kwa imani,serikali isingetaka kufanya utafiti,kwavile hata hizo samples/specimens za kuchukua kwa ajili ya utafiti zisingekuwepo!
my 2 cents wakuu!
 
'Babu wa Loliondo' acharuka
Imeandikwa na Marc Nkwame, Arusha; Tarehe: 10th March 2011 @ 07:31

BAADA ya kutumia musuli wa fedha na kuweza kuonana na Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila wilayani Loliondo mkoani Arusha, na kuwaacha wanyonge wakisota, sasa vigogo hao huenda mambo yakawatumbukia nyongo.

Mchungaji Masapila ameapa kuwa vigogo waliofanya hivyo kwa kutumia njia za mkato na kufanikiwa kumwona na kunywa dawa, hawatapona magonjwa sugu yanayowakabili.

Mchungaji huyo mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) amesema hali hiyo imesababishwa na kitendo chao cha kukiuka baadhi ya masharti ya tiba yake ambayo inakataza kufanyiwa biashara na wala kupewa upendeleo.

Hivi karibuni, baadhi ya maofisa wenye vyeo katika sekta mbalimbali nchini, walidaiwa kutumia nafasi zao kushawishi askari wanaolinda usalama katika makazi ya Mchungaji Masapila, ili kuwavusha foleni na kupata tiba haraka. (lazima wachakachuwe!)

Polisi walio eneo hilo kijijini Samunge, tarafa Sale, pia wamedaiwa kutumia nafasi zao kupitisha ndugu, jamaa na marafiki zao, jambo ambalo Mchungaji Masapila alionya kuwa halitawasaidia kwani dawa hiyo haifanyi kazi katika mazingira hayo.

"Huu ni uponyaji wa Mungu na Mungu huwa hatambui cheo au nafasi ya mtu, ukikosea utaratibu dawa inabaki kuwa maji ya kawaida," alifafanua Masapila.

Maelfu ya watu kutoka pande zote za nchi na nchi jirani wako katika kijiji hicho kwenye mbuga ya Sonjo, kata ya Digo-digo, Ngorongoro wakitumaini kupata tiba hiyo ya ajabu.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, alisema jana kuwa ofisi yake inafikiria kutenga siku maalumu na hasa Jumamosi, kwa watumishi wa umma na Serikali kwenda kupata tiba hiyo ili kupunguza msongamano na kuwawezesha kurudi mapema kwenye kazi zao za utumishi kwa Taifa.

Hata hivyo, haijulikani kama Mchungaji Masapila atakubaliana na wazo hilo, kwa maana alisisitiza kuwa mtoaji huyo wa dawa anazingatia kutokuwapo kwa upendeleo katika utoaji tiba hiyo.

Katikati ya wiki hii, vurugu zilidaiwa kuzuka karibu na eneo la tiba, baada ya watu wanaodhaniwa kuwa vigogo kulazimisha kuwapita wananchi wengine waliopanga foleni kwa ajili ya kupata tiba.

Hivi sasa watu wanalazimika kukesha kwa siku nne wakisubiri zamu ya kupewa dawa na Mchungaji Masapila ambaye sasa amepata usaidizi wa wachungaji wengine watatu wanaomsaidia kuchota dawa.

Hata hivyo, Masapila analazimika kugawa dawa hiyo kwa mkono wake mwenyewe, maana bila hivyo, tiba hiyo inayotokana na mizizi iliyochemshwa na maji, haitafanya kazi.

Mkazi wa Sonjo aliyevamia moja ya masufuria na kujichotea dawa na kuinywa Jumatatu alipata msukosuko mkubwa kwani tumbo lilipata maumivu makali na kulazimisha ‘Babu’ Masapila kuingilia kati kumsaidia.

Wakati hayo yakiendelea, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Akili Mpwapwa, alisema Jeshi bado halijapokea taarifa rasmi za vifo vinavyodaiwa kutokea katika mbuga ya Sonjo ambako maelfu wamepiga kambi wakisubiri tiba.

Hata hivyo Lali juzi alithibitisha vifo sita kati ya 14 vinavyodaiwa kutokea katika eneo la Samunge.

Lali alipozungumza jana na gazeti hili, alisema misururu ya watu wanaofuata matibabu imepungua na kubaki umbali wa kilometa 15 huku magari yakibaki kati ya 1,000 na 1,500 kutoka ya awali 3,000.

Alisema katika magari hayo yakiwamo malori na mabasi na magari madogo kila gari lina watu wasiopungua watano.

Kwa mujibu wa Lali, mtu mmoja alifariki dunia wakati akisubiri matibabu na alikutwa jana walipotembelea eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya alisema watu wamekuwa wabishi kwa kutoa wagonjwa hospitalini wakiwa mahututi na kuwaweka mistarini kwa ajili ya kupata dawa na hivyo kuzidiwa na kufariki dunia.

Mchungaji Masapila hutoa dawa hizo anazodai kuoteshwa na Mungu kwa Sh. 500 huku akidai kutibu magonjwa sugu yakiwamo ya Ukimwi, pumu, kisukari na mengineyo huku dozi yake ikiwa kikombe kimoja tu cha dawa hiyo.

Inadaiwa kuwa kutokana na misururu hiyo, gharama za magari zimeendelea kupanda kwani sasa wanaokwenda kwa magari ya kitalii wanalazimika kulipa kati ya Sh. 120,000 na Sh 150,000 na mabasi ni kati ya Sh 30,000 na Sh 50,000.

Wana JF saizi kuna coverage ya kilichokuwa kinafanyika kwa mchungaji loliondo have a look on ITV.
 
hayo ni mambo yake binafsi, bora tu awe mzima na aachie madaraka salama.. Watu wachukue nchi (chadema) ...

Ni kweli kaka Ivuga. Bora apate walau nguvu ya kukimbilia uhamishoni Saudi Arabia (maana ndiko kijiwe cha viongozi mabazazi walioshindwa).

Akaungane na mafedhuli wenzake kina Mubarak na Ben Ali.
 
WanaJF tuache siasa kwenye jambo hili.Tuache wataalam wafanye kazi.Tunajua serikali yetu haina dini,haifungamani na imani za kidini na ni wajibu wake kulinda uhai wa watu wake.Serikali needs to take babu seriously kwasababu magonjwa ambayo babu anasema anayatibu ni magonjwa sugu,yana mateso sana,na hayatibiki mpaka sasa pamoja na maendeleo makubwa ya sayansi ya tiba duniani na yanaua sana duniani kote.Wengine yameshatupotezea ndugu zetu wengi wa karibu na kweli tunatamani sana,siku moja dawa ya kuyaponya ipatikane.Lakini hii dawa isiwe ya kubahatisha na labda kumuongezea matatizo zaidi au hata kumuua mgonjwa in a long run.Hivyo huyu Babu anaposema anatibu lazima tujue kwanza active ingredient(s) ya/za hiyo dawa yake ni nini?Lazima pia tujue targets za dawa mwilini na mechanism of action ya hiyo dawa na side effects zake.Kuna aina nyingi za kansa na huwa zinakuwa katika grades na stages tofauti at diagnosis hivyo kufanya na matibabu kuwa tofauti pia.Hawezi kuchemsha maji na majani fulani halafu akasema anatibu kansa,eti kaoteshwa na Mungu.Hata Kisukari nacho kipo tofauti na matibabu yake pia ni tofauti.HIV/AIDS ndiyo kabisaa
Askofu Laizer kwa maoni yangu anakosea anapopinga tiba ya babu kupelekwa maabara kwanza.Huyu babu hatibu kwa imani bali kwa miti shamba.Kutibu kwa imani ni kwa kuamuru/maombezi/kusali kama walivyofanya manabii wa kale kina Elisha,Elijah na hata Yesu mwenyewe na wanafunzi wake.Hawa walikuwa 'wanaongea' tu na wagonjwa wanapona.Hawakuwa wanachemsha maji na mizizi/majani kama babu wa loliondo.Angekuwa anatibu kwa imani,serikali isingetaka kufanya utafiti,kwavile hata hizo samples/specimens za kuchukua kwa ajili ya utafiti zisingekuwepo!
my 2 cents wakuu!

Umeongea point mkuu kila kitu udini humu JF na huyu Askofu Laizer inaelekea ni mdini anataka kuleta uchochezi tu na kauli zake zisizokuwa na mantiki ya kujenga umoja na mshikamano katika jamii.
 
tena ameongea ukweli kabisa ...hawa serikali wanatka kupima nguvu za mungu sio dawa..mungu anamtumia huyu mzee kama chombo tu ili aweze kuponya.....

Kama ni uponyaji kutoka kwa Mungu mimi sina hakika; na kama sivyo sijui. Ila nilijualo ni kuwa muda ndio utaamua (Mdo 5:34-39).

Acts 5:34-39
34 But a Pharisee named Gamaliel, a teacher of the law, who was honored by all the people, stood up in the Sanhedrin and ordered that the men be put outside for a little while. 35 Then he addressed them: "Men of Israel, consider carefully what you intend to do to these men. 36 Some time ago Theudas appeared, claiming to be somebody, and about four hundred men rallied to him. He was killed, all his followers were dispersed, and it all came to nothing. 37 After him, Judas the Galilean appeared in the days of the census and led a band of people in revolt. He too was killed, and all his followers were scattered. 38 Therefore, in the present case I advise you: Leave these men alone! Let them go! For if their purpose or activity is of human origin, it will fail. 39 But if it is from God, you will not be able to stop these men; you will only find yourselves fighting against God." NIV

Licha ya serikali kutangaza kusimamisha, babu yeye anaendele kupika tu dawa yake kama alivyo agizwa na mwenyezi Mungu. Sasa yule anayepingana na imani yake akaimwage aone. Ukombozi wa afya kwanza....
 
kwani akiinywa cha ajabu nini. Na je unadhani hicho ulichotype ndio ushahidi wa yeye kunywa? JK ni mwanadamu kama wanadamu wengine, au wewe unamchukulia ni mungu wako kiasi kwamba yeye asiugue? kama anamaradhi ya siri ni yake yeye.

Vipi Slaa hajanywa? maana uzee unamzingira sasa sijui ana isue gani. msitue akanywe fasta maana ccm wakigundua hajanywa itakula kwake
 
Kila kitu kizunguzungu, utasikia sasa hivi watasema Laiza anataka kuifanya nchi isitawalike!

Hapo umenena. Wasira hachelewi kusema dini inaingilia siasa. Mara utasikia baraza la Ulamaa na Mashiek nao watatoa tamko lao pale Anatoglo la kumpinga Askofu Laizer
 
tehe tehe teheeeee! waliochagua wabunge kwa kuangalia rangi walie tu!
 
Waziri wa afya mbovu may rot in hell!!! Hatuwezi kukubali ujinga huo!! Wakati wao wanaendakunywa dawa TFDA hakuwepo????
 
Hivi serikali yetu inashauriwa na nani? kuna dawa za kichina kibao na mbovu, kuna wauza dawa wengi mfano Masai "NAUSA DAWA YA KUONGESA NGUFU" mbona hawa hawakamatwi. Fika kwenye parking ya Mlimani city uone. Leo babu kaja na dawa poa tu eti nongwa wakati vigogo wao walishawahi huko wakanywa na mavx yao.
Teh teh teh!
 
Umeongea point mkuu kila kitu udini humu JF na huyu Askofu Laizer inaelekea ni mdini anataka kuleta uchochezi tu na kauli zake zisizokuwa na mantiki ya kujenga umoja na mshikamano katika jamii.

Mkuu navyoiona hiyo post ya annamaria haikosowi udini bali anatofautisha sayansi na dini. Sasa wewe unamchomeka askofu Laiza humo kwamba ni mdini nadhani unapotosha haja ya annamaria
 
WanaJF tuache siasa kwenye jambo hili.Tuache wataalam wafanye kazi.Tunajua serikali yetu haina dini,haifungamani na imani za kidini na ni wajibu wake kulinda uhai wa watu wake.Serikali needs to take babu seriously kwasababu magonjwa ambayo babu anasema anayatibu ni magonjwa sugu,yana mateso sana,na hayatibiki mpaka sasa pamoja na maendeleo makubwa ya sayansi ya tiba duniani na yanaua sana duniani kote.Wengine yameshatupotezea ndugu zetu wengi wa karibu na kweli tunatamani sana,siku moja dawa ya kuyaponya ipatikane.Lakini hii dawa isiwe ya kubahatisha na labda kumuongezea matatizo zaidi au hata kumuua mgonjwa in a long run.Hivyo huyu Babu anaposema anatibu lazima tujue kwanza active ingredient(s) ya/za hiyo dawa yake ni nini?Lazima pia tujue targets za dawa mwilini na mechanism of action ya hiyo dawa na side effects zake.Kuna aina nyingi za kansa na huwa zinakuwa katika grades na stages tofauti at diagnosis hivyo kufanya na matibabu kuwa tofauti pia.Hawezi kuchemsha maji na majani fulani halafu akasema anatibu kansa,eti kaoteshwa na Mungu.Hata Kisukari nacho kipo tofauti na matibabu yake pia ni tofauti.HIV/AIDS ndiyo kabisaa
Askofu Laizer kwa maoni yangu anakosea anapopinga tiba ya babu kupelekwa maabara kwanza.Huyu babu hatibu kwa imani bali kwa miti shamba.Kutibu kwa imani ni kwa kuamuru/maombezi/kusali kama walivyofanya manabii wa kale kina Elisha,Elijah na hata Yesu mwenyewe na wanafunzi wake.Hawa walikuwa 'wanaongea' tu na wagonjwa wanapona.Hawakuwa wanachemsha maji na mizizi/majani kama babu wa loliondo.Angekuwa anatibu kwa imani,serikali isingetaka kufanya utafiti,kwavile hata hizo samples/specimens za kuchukua kwa ajili ya utafiti zisingekuwepo!
my 2 cents wakuu!

Siyo mara zote Yesu wala manabii waliponya kwa kusema tu neno kwa mfano Yesu aliwahi mponya mtu kipofu kwa kumpaka tope machoni na kumwambia akanawe then akapona. Pia Nabii Eliya aliwahi mponya mtu anaitwa Naamani kwa kumwambia atumbukie mto yordani mara saba. Je angekuwepo Eliya leo wizara ya afya ingemwambia aache mpaka wakapime active ingredient iliyoko kwenye maji ya mto yordani? au wangemwambia Yesu aache wakapime tope kwanza?.

Dada tofautisha Imani na sayansi na kwa taarifa maabara hawataona hiyo active ingredients unazotaka kuchunguza ili mtengeneze dawa inayofanania muuze kwa bei ya kifisadi.

We subiri ikapimwe wakati watu wameshapona.
 
Back
Top Bottom