Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

Kuna tetesi kuwa viongozi waliotoa tamko na wale wanaounga mkono kumfungia babu watapatwa na laana, na km waliwahi kunywa kikombe cha uzima sasa hawataki wengine wanywe basi kuna pigo linafuatia. Kale ka ugonjwa walikokuwa wamepona katawarudia tena na kwa kuwa kikombe cha uzima kina nywewa mara moja sijui watakimbilia wapi.

Hii kuna mdau wa karibu sana na babu kaitoa kwani babu kesha toa tahadhari.
 
Inakadiriwa kwamba hapa nchini karibu robo tatu ya local NGOs na CBOs zinajishughulisha katika kutoa huduma zinazohusiana na hiv. Aidha madawa ya kupunguza makali ya hiv yanachukua sehemu kubwa ya matumizi kwaajili ya manunuzi ya dawa mbali mbali. Kwaajili hiyo, kunasemekana kuna hofu kubwa kwamba ikiwa hiyo tiba anayoitoa huyo Babu wa Loliondo ni kweli inatibu hiv. hii ina maana idadi ya watu wenye ugojwa huo uenda ikashuka ghafla, na kusababisha NGO na makampuni mengi ya madawa kukosa shughuli.


Hivyo kupelekea uchumi kushuka kwa watu kukosa ajira kwenye NGOs. Lakini huoni kama babu kaipunguzia mzigo serkali wa kusupply madawa ya ukimwi bure? pesa hii itumike kujenga hospitali ya kumbu kumbu Loliondo ili kumuenzi Babu.
 
Amesema ni swala la imani, haliwezi kuwekwa kwenye test tube!

Amesema serikali haina mamlaka juu ya mambo ya kiimani. Kwamba hakubaliani na tangazo la serikali ambalo lilitolewa bila kushauriana na kanisa.

Amemtaka Babu aendelee kutoa huduma na kanisa litapeleka miundombinu inayohitajika.

Source: ITV habari usiku
 
Kwa kweli huu ni uhuni. Nimefuatilia habari kupitia Chanel Ten, ITV, na TBC wananchi wanaongea kwa jazba sana na hasira zisizomithilika.

Serikali imemzuia babu baada ya magari yenye DFP,STJ, STK,SM na SU kuwa yameisha Loliondo.

Haiwezekani JK anywe dawa halafu eti walalahoi kukatazwa kwa kisingizio cha kukosekana kwa huduma. Kwani JK alipokwenda hizo huduma zilikuwepo?

Haiwezekani mtu ametoka Mbeya hadi Arusha tena akiwa hoi mahututi, kwa kusindikizwa na ndugu zake tena kwa kulipa gharama kubwa za nauli halafu eti anaambiwa arudi kwao kwa kuwa eti serikali imesitisha huduma.

Huu ni utapiamlo wa fikra. Kivipi serikali wasitishe huduma ambayo hawakuianzisha? Kama wanataka, wakasitishe huduma Muhimbili sio kwa mtumishi wa Mungu mchungaji Ambilikile.

Mwenye uwezo wa kusimamisha huduma ya mchungaji ni Mungu pekee, maana ndiye aliyeianzisha.
 
Askofu Thomas Laizer wa KKKT amesema kuwa ni kinyume cha utaratibu kusitisha huduma ya mchungaji Mwasapile wa huko Loliondo, maana ina element za kiroho, na pia hawajashirikisha wadau katika maamuzi hayo.

Amesema mambo ya Mungu hayawezi kufanyiwa majaribio ya kisayansi, au kupimwa kwenye test-tube, na kuwa maamuzi hayo ni kumkosea Mungu!

Source: ITV newz bulletin saa 2.00 usiku,
 
Wana Jf
Yeyote ambae amekunywa dawa ama jamaa yake amekunywa na akapona nivizuri awe shuhuda wetu humu ndani ,kwani Jk na wenzake wamekunywa lakini wako kimiya hawasemi wamepona ama dawa haiponyeshi
Nawakilisha.
 
Wananchi waliohojiwa nao wamepinga tangazo la serikali kumzuia babu kutoa tiba. Wanadai kama hiyo dawa ingekuwa na madhara watu waliokunywa hiyo dawa wangekuwa wameshadhurika. Kwamba serikali imechelewa kudai inataka kuchunguza kwanza.
 
tena ameongea ukweli kabisa ...hawa serikali wanatka kupima nguvu za mungu sio dawa..mungu anamtumia huyu mzee kama chombo tu ili aweze kuponya.....
 
Imetangazwa kutakuwa na kipindi maalumu cha Babu wa Loliondo leo saa tatu usiku ITV
 
Kwamujibu wa taarifa ya habari ya saa 2 mbunge wa moshi mjini mh. Ndesamburo ameamuakuwasafirisha wagonjwa kwenda kwa babu kupata huduma.
 
wameona magari ya STK, DFP, SM. SU, E1, E 5

HAYAONEKANI hhuko kwa kuwa wamekunywa dawa tayari then wanamzuia babu...wapuuzi wakubwa sana hawa
 
Hivi serikali yetu inashauriwa na nani? kuna dawa za kichina kibao na mbovu, kuna wauza dawa wengi mfano Masai "NAUSA DAWA YA KUONGESA NGUFU" mbona hawa hawakamatwi. Fika kwenye parking ya Mlimani city uone. Leo babu kaja na dawa poa tu eti nongwa wakati vigogo wao walishawahi huko wakanywa na mavx yao.
 
Haya,me nashangaa sana!
Sheh yahaya akiongea mambo yake hata kama ni ya ajabu hakuna wa kumyamazisha!

Huyu mchungaji juzi hapa tu tayari wamesha msimamisha duh,au ndo ........................
 
Wameshindwa kutoa huduma kwenye Hospital zao sasa wanataka walalahoi wahangaike, Eyi nasikia madokta wa hospitali za kifisadi wanalalamika kuwa hawapati pesa za ufisadi ndio Fisadi papa waziri wa Afya akasimamisha ili Mafisadi wadogo wapate mlo
 
Nami nimebaki mdomo wazi,sie maskini tunakabwa na sheria wahali. Ivi serikali inashindwaje kufanya kama kule Congo ambapo serikali ilimpokea mchungaji Kakobe kwa kutumia magari na vyakula vya serikali? Nimependa sana kuona STK 1045 defender kwa kukusanya dawa kwa ajili ya mchungaji. Ila plz waongeze juhudi si kufunga huduma jamani!
 
WAZIRI WA AFYA KUMFUNGIA BABU KUTIBU WALALA HOI
HUU NI UHUNI NA DHULUMA KWA WANYONGE YEYE KAMA ALIKUA NA UBAVO
KWA NINI HASINGEFUNGA KABLA YA VIGOGO KUTIBIWA ILI TUONE KAMA HII JIONI ANGEKUA WAZIRI BADO


HUO NDIO UKWELI KASUBIRI MPAKA FL KAPATA DAWA NDO ANAAMKA KUMFUNGIA!!!:A S 13:
 
Back
Top Bottom