Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

Tena huo mti anaoutumia Babu unafahamika maana uko nje hapo na wenyeji wanautumia kama dawa kwa miaka yote. Pia matunda yake wenyeji huyala kwa miaka yote. Ila la zaidi Babu dawa anatengenezea nje mbele ya watu wote ameongea Mkuu wa wilaya alipo Babu kupitia Wapo Redio leo saa moja jioni kwa njia ya simu!
 
Kila kitu kizunguzungu, utasikia sasa hivi watasema Laiza anataka kuifanya nchi isitawalike!
 
Swala la imani, haliwezi kuwekwa kwenye test tube!

Serikali haina mamlaka juu ya mambo ya kiimani.

Viongozi wapuuzi hufanya maamuzi ya kipuuzi siku zote!! Ukimuangalia waziri mwenyewe utajua kuna something with him:A S 13:!!
 
Itv kuonyesha kipindi maalumu cha babu huko lolionda saa baada ya taarifa ya habari ya saa 2 usiku tufuatilie tujue yanayojiri huko.
 
Ni kweli kabisa dawa ya babu imetawaliwa na tendo la kiimani hivyo serikali haina mamlaka juu ya imani. Na kama serikali hii ya Jk inatafuta hasira za wananchi itazipata. Vigezo vya kumzuia babu wizara walivyovitoa havina mantiki. Mfano kama dawa inaweza ponya gonjwa sugu waliloshindwa wanasayansi iweje hiyo imani ya kuponya ishindwe kuzuia ugonjwa mwingine wenye tiba kisayansi utakaosababishwa na watu kushiriki kikombe kimoja. Kanisa pelekeni miundo mbinu ili muwe msaada kwa wenye shida kwani huo ndio msingi mkuu wa uinjilisti. Serikali inaonekana inachokwepa hapa ni gharama ya kutengeneza miundo mbinu.
.
 
Viongozi wapuuzi hufanya maamuzi ya kipuuzi siku zote!! Ukimuangalia waziri mwenyewe utajua kuna something with him:A S 13:!!

huyo waziri wa afya Anatakiwa akapate dawa kwa babu apate akili ili asifanye tena maamuzi ya hovyo hovyo
 
Hii ndo bongo sasa, serikali ya JK, inataka kushindana na MUNGU, MAKAMBA wew vipi, na wewe toa kauli yako , si mmezoea CCM, kuongea ovyoovyo tu.
 
Sure imetANGAZWA...Stay tuned out there...hasa wale wasioamini!
 
Kutokana na ubovu wa barabara ya kuelekea loriondo kwa babu, mbunge wa moshi mjini ndesamburo ametoa helcopta yake kupeleka wagonjwa mahututi kupata tiba kwa babu. Source: tbc-habari.
 
Hii nchi kwa kuunda tume inaongoza!! Halaf tume zenyewe majibu hazitoi, ile tume iliyoundwa ni janja ya nyani kule wizarani wamekaa wameona njia nzuri ya wao kwenda kupata kikombe kwa babu ni kujifanya wanaenda kuchunguza...wameona waziri wa afya amekunywa wanataka kukataza! Sisi wananchi hatukubali hata kidogo....
 
Huyu Waziri lazima afe asipoangalia asicheze na Mungu. Hizo dawa na mahirizi wanayopata Bagamoyo kwa sangoma wao huwa yamesajiliwa wizara gani mpaka wamtake Babu akasajili dawa. Hapa akikosea tu akienda kusajili majibu ya usajili au kibali atapata baada ya miaka mitatu au wamsubiri hadi akishaitwa na Mungu.

Huyu waziri sijui ametoa wapi pumzi na ujasiri wa kuongea upuunzi na pumba kiasi hicho. Huyu mzee wa watu anatoa dawa bure sasa wao wanazuia inawahusu nini?. MWELEZENI KAMA ANATAKA AJE LOLIONDO KUZUIA AONE CHA MTEMA KUNI , BORA ABAKIE KUONGELEA HUKOHUKO DAR. Akikosea akija watu watamshukia kama mwizi kwani hiyo dawa si yao wala hawajampa Babu na pale ni nyumbani kwa Babu kwake . Ubabaishaji wao waupeleke huko mwananyamala na siyo kwa babu kwani hana uhusiaono wowote na wizara ya afya
 
Hivi vigogo waliotumia magari ya serikali kwenda kwa babu hawajakiuka uwajibikaji?
 
Atakuwa ameshauriwa kufanya hivyo,inawezekana kabisa sio uamuzi wake
nilishawahi kumsikiliza live baada ya kuteuliwa tu kushika wizara,sina imani naye
nadhani ni kati ya walioingia hapo kibahati
 
maslahi yao yataisha na ngos yao. But hawataweza kushindana na nguvu ya imani. Babu ni mtu ambaye kasoma na sio mbumbumbu.
 
Habari zimeenea kuwa rais Jakaya Kikwete alikunywa dawa ya mchungaji Ambillikile Mwasapile alipokuwa ziarani mkoani Manyara.

Wale ndugu zetu (wavivu wa kufikiri) ambao wengi wao wanatoka kile chama cha zamani (CCM), bila kufanya utafiti wowote wakaanza kueleza eti habari hizo ni UVumi na majungu ya kutaka kumchafua rais Kikwete.

Watu hao ambao bila kushirikisha ubongo wamekuwa wakipinga kila madai yanayotolewa kwa Chama na Serikali yao napenda kuwaeleza yafuatayo.

Ni kweli kuwa Rais Kikwete alikunywa dawa hiyo alipokuwa ziarani mkoani Manyara kuzindua shughuli za ufukuaji wa nyayo za binadamu wa kale, zilizogunduliwa na Archiologist Mary Leakdy mke wa Dr.Leakey.

Kulingana na taarifa kutoka kwa kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, msafara wa rais Kikwete wakati wa kurudi kutoka Ngorongoro ulipaswa kupita kata ya Samunge na baadae mji mdogo wa Mto wa Mbu.

Kata hiyo ya Samunge ndipo alipo Mchungaji Ambilikile, na wakati msafara wa rais Kikwete unapita hapakuwa na msongamano kama ilivyo sasa.

Kwa hiyo nawashauri wote wanaobisha kabla ya kubisha wafanye utafiti na ikiwezekana wamuulize Mchungaji Ambilikile mwenyewe, kuliko kubisha kishabiki.

Pia wafute mawazo mgando kuwa wanaotoa taarifa za Rais Kikwete kutumia dawa hiyo eti wanamchafua. Badala yake waamini kuwa taarifa hizo ZINAMSAFISHA MNO rais Kikwete kwani sasa atakuwa ametakasika kutokana na maradhi SUGU na ya MUDA MREFU yaliyokuwa yakimsumbua na kumfanya aanguke jukwaani mara kwa mara.

MUNGU IBARIKI AFRIKA,
Mungu mbariki mchungaji Ambilikile,
Mungu mbariki rais wetu Kikwete, ili dawa aliyopewa ifanye kazi.
 
maslahi yao yataisha na ngos yao. But hawataweza kushindana na nguvu ya imani. Babu ni mtu ambaye kasoma na sio mbumbumbu.

Hivi shehe yahya amesoma hadi kiwango gani?
 
Hapa sasa kuna contradiction wakuu. Tiba inahusiana na imani au ndio mnatafuta lawama? Hivi zile dawa za kichocho, malaria na kifafa ni imani au scientific research? Sasa huyo babu wa loliondo si kama sheikh yahaya tu anaenda kutibu wagonjwa wake wa nguvu za giza!!!! Mweh ndugu zanguni nyie mna matatizo hamnaga msimamo akisema sheikh yahaya amepata dawa mtasema nguvu za giza ila dawa ya huyu isiyo na kichwa wala miguu ni imani!!! Sawa sawa serikali kuzuia this auspicious practices of witchcraft.
 
please, tusimulieni wale ambao jamaa zenu au ndugu wamesaidiwa, kupona, au kupunguza maumivu na kikombe cha dawa ya babu.
 
Back
Top Bottom