Picha: Kikwete amtembelea aliyemwagiwa tindikali

Picha: Kikwete amtembelea aliyemwagiwa tindikali

Status
Not open for further replies.
Hii nchi sasa naona imekuwa kama haina jeshi la polisi, mtu atamwagiwaje tindikali mbele ya kituo kikubwa cha polisi? juzi juzi wezi wamevunja kituo kikubwa cha Polisi Mwanza, hivi mwizi/jambazi anaanzaje kufikiria kuiibia jeshi la polisi? Na tunapenda kufahamu wahusika hapo kituoni bado wanavaa sare za polisi au mmeshawaondoa?

Mr President seriously something is wrong with your Police force naona matukio ya kihalifu yanaongezeka siku hadi siku na sisi wananchi tunakosa imani kabisa sasa na jeshi lako. Tukifika majumbani kwetu usiku magetini tunakaa kwa wasi wasi hadi geti lifunguliwe ndio tunashusha pumzi. Tumeshafika pahala sasa hata ukisimamishwa usiku na polisi hujui kama ni polisi au jambazi.Jeshi liwekeze nguvu kwenye kutafuta source na kama kuna supplier wa hizi kemikali au kuna kikundi ndio kinafanya hizi shughuli kwa malipo plz wapeleke puta hawa ma afande wako warudi kazini watuletee majibu.

Ni aibu sana polisi wanajipanga kando kando ya barabara na bunduki zao wakiona mtu kabeba kochi lake anahama ndio wanasimamisha. No wonder kule Mtwara mmepeleka wanajeshi maana hawa jamaa nguo za khaki wameshindwa kabisa kufanya kazi zao. Tatizo nini vitendea kazi? morale? ujuzi? au yote kwa mpigo? Tulitegemea polisi wawe pro-active wajikite kwenye kutafuta vyanzo ili matukio mengine yazuiwe kabla hayajatokea.

Mr President your police force is a huge dissapointment na kama hauta act sasa utakuwa na trip nyingi za Kutembelea victims wa matukio kama haya !!!
 
Nilichogundua ni Danganyatoto, ngoja nitawajuza kunavigogo wangapi wamesha shuka uko bonde kufatilia ili saga, Mkulu yeye ni kigogo wa 12 ambao mpaka sasa wameshakwenda kutafuta solution ya hii issue.
 
IMG_0684.jpg
 
Haya mashambulizi ya kumwagia watu tindikali yamezidi sasa. Ningependa kuona yanatungiwa sheria kali sana.

Nakubaliana nawe 99% nadhani adhabu iwe kunyongwa hadi kufa. Lakini je uwezekano wa kuwakamata hawa watu upo? Maana pamoja na wingi wa matukio lkn sijawahi kusikia hata mmoja aliyekamatwa
 
Hii nchi sasa naona imekuwa kama haina jeshi la polisi, mtu atamwagiwaje tindikali mbele ya kituo kikubwa cha polisi? juzi juzi wezi wamevunja kituo kikubwa cha Polisi Mwanza, hivi mwizi/jambazi anaanzaje kufikiria kuiibia jeshi la polisi? Na tunapenda kufahamu wahusika hapo kituoni bado wanavaa sare za polisi au mmeshawaondoa?

Mr President seriously something is wrong with your Police force naona matukio ya kihalifu yanaongezeka siku hadi siku na sisi wananchi tunakosa imani kabisa sasa na jeshi lako. Tukifika majumbani kwetu usiku magetini tunakaa kwa wasi wasi hadi geti lifunguliwe ndio tunashusha pumzi. Tumeshafika pahala sasa hata ukisimamishwa usiku na polisi hujui kama ni polisi au jambazi.Jeshi liwekeze nguvu kwenye kutafuta source na kama kuna supplier wa hizi kemikali au kuna kikundi ndio kinafanya hizi shughuli kwa malipo plz wapeleke puta hawa ma afande wako warudi kazini watuletee majibu.

Ni aibu sana polisi wanajipanga kando kando ya barabara na bunduki zao wakiona mtu kabeba kochi lake anahama ndio wanasimamisha. No wonder kule Mtwara mmepeleka wanajeshi maana hawa jamaa nguo za khaki wameshindwa kabisa kufanya kazi zao. Tatizo nini vitendea kazi? morale? ujuzi? au yote kwa mpigo? Tulitegemea polisi wawe pro-active wajikite kwenye kutafuta vyanzo ili matukio mengine yazuiwe kabla hayajatokea.

Mr President your police force is a huge dissapointment na kama hauta act sasa utakuwa na trip nyingi za Kutembelea victims wa matukio kama haya !!!

Huyo unayemlalamikia ndie ''a huge dissapointment''.
 
Ukisoma michango mingi ya wadau wa uzi utajua kuna mengi kati ya mwathirika na jk au jk na serikalu yake. Wekeni wazi ni nini kilichonyuma ya pazia?

Kinacho kuwa nyuma ya pazia si ni DIRISHA au MLANGO, eti?
 
Jamani muwe mnakamikisha habari, wapi South Afrika kwa mmiliki wa Home Shopping Centre au Arusha kwa sheikh aliyemwagiwa tindikali??

quote_icon.png
By Ushindi2015
Bila shaka kila mtanzania analamikia wimbi la sasa la madawa ya kulevya. Karibia kila kiongozi mkuu kama Rais, viongozi wadini mbali mbali, wakuu wa vyombo vya usalama wamezungumzia madawa ya kulevya. Wakiyalaani. Rais alidiriki kusema kwamba anawafahamu wauza madawa ya kulevya huku akisema maaskofu wanahusika lakini hakuwataja. Mchezo huu unaendelea kila kikicha kiasi cha kuweka taifa katika hali mbaya.

Mnamo mwezi wa Aprili, msanii Ngewa alifariki Afrika kusini. Ndugu yetu Kinje Ngombale Mwiru akawa mtu wa kwanza kujitolea kuratibu shuguli za kumrejesha nyumbani Tanzania. Tunamshukuru kwa hilo. Ila pia Ndugu Kinje pia atuelezee kinaga ubaga na kile kilichotokea na ripoti ya madaktari kuhusiana na kifo cha huyo msanii. Ripoti wa wanasaji wetu ilibahini kwamba bwana Kinje ana mtandao mkubwa wa wasafirishaji wa hiyo bidhaa kwenda Afrika kusini.

Mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, mabinti wawili wa Kitanzania walikamatwa na shehena kubwa ya madawa ya kulevya Johanesburg Afrika Kusini wakitokea Tanzania. Katika mazungumzo na mmoja wa wanafamilia zao, mmoja ya hao mabinti alisema waziwazi kwamba wasingeweza kupita airport ya Dar kama siyo mtoto wa Rais na mkubwa serikalini. Huyu mtoto wa rais ni nani? Na huyu mkubwa ni nani.

Sakata la mtoto wa Rais pia lilitokea nchini China, na mwisho wake ni mtihani ambao wengi wanashindwa kuelewa

Hii weekend iliyopita mkuu wetu wa nchi alikuwa nchini Afrika kusini kwenye ziara ambayo haikutangazwa kwenye vyombo vya habari. Kulikoni hii ziara ilikuwa ya nini kwa sababu Rais alikutana na viongozi wa maswala ya usalama wa Afrika kusini? Tunaomba umma wa kitanzania usiyumbishwi hadi kieleweke. Hawa mabinti wawili wasitoweke, kwani kuwepo kwao kutawaumbua wakubwa walionyuma yao............

Umma tunaomba mtuvumilie. Hawa viongozi wasipotoa majibu ya uhakika, tutawaanika. Wengi wao ni viongozi waandamizi ndani ya chama tawala
 
Huyu jk anadhalilisha kiti cha Rais, na heshima ya Taifa kwa ujumla. Mkuu wa nchi hapaswi 'kuwatembelea' wagonjwa... Hasa kwenye maswala 'controversial' yanayohitaji uchunguzi wa kipolisi. Dunia nzima haikubaliki, kuna nini kinachoendelea hapa?

kaka, uchugnuzi wa zilke kilo 150, ukifanyika unamungukia mtoto wa mkulu, sasa unategemea nini?
 
kwa hili kwa nini watu wasijilinde?
Alaf safari hii ya jk haikutangazwa kabisa......... Kuna kitu hapa
bila shaka kuna watu wataachiwa huru na kufutiwa mashitaka.

thubutu!!!!!! Sio kwa zuma. Kwani kuna dongote bwagamoyo?
 
Hii nchi sasa naona imekuwa kama haina jeshi la polisi, mtu atamwagiwaje tindikali mbele ya kituo kikubwa cha polisi? juzi juzi wezi wamevunja kituo kikubwa cha Polisi Mwanza, hivi mwizi/jambazi anaanzaje kufikiria kuiibia jeshi la polisi? Na tunapenda kufahamu wahusika hapo kituoni bado wanavaa sare za polisi au mmeshawaondoa?

Mr President seriously something is wrong with your Police force naona matukio ya kihalifu yanaongezeka siku hadi siku na sisi wananchi tunakosa imani kabisa sasa na jeshi lako. Tukifika majumbani kwetu usiku magetini tunakaa kwa wasi wasi hadi geti lifunguliwe ndio tunashusha pumzi. Tumeshafika pahala sasa hata ukisimamishwa usiku na polisi hujui kama ni polisi au jambazi.Jeshi liwekeze nguvu kwenye kutafuta source na kama kuna supplier wa hizi kemikali au kuna kikundi ndio kinafanya hizi shughuli kwa malipo plz wapeleke puta hawa ma afande wako warudi kazini watuletee majibu.

Ni aibu sana polisi wanajipanga kando kando ya barabara na bunduki zao wakiona mtu kabeba kochi lake anahama ndio wanasimamisha. No wonder kule Mtwara mmepeleka wanajeshi maana hawa jamaa nguo za khaki wameshindwa kabisa kufanya kazi zao. Tatizo nini vitendea kazi? morale? ujuzi? au yote kwa mpigo? Tulitegemea polisi wawe pro-active wajikite kwenye kutafuta vyanzo ili matukio mengine yazuiwe kabla hayajatokea.

Mr President your police force is a huge dissapointment na kama hauta act sasa utakuwa na trip nyingi za Kutembelea victims wa matukio kama haya !!!
Sijaamimi kama aliyetoa hii coment ni Maundumula, ni muda mrefu humu Jukwaani watu wengi wameonyesha wasiwasi wao juu ya Jeshi la Polisi, lakini wenzetu nyie mmekuwa wepesi wa kuweka siasa na kupotosha ukweli wa malalamiko.

Hata hivyo, watu wa pwani husema kilichomkuta kibeku, ungo ujiandae. Ni kweli kabisa, unapatwa na matumaini baada ya kufunguliwa geti hata hivyo, hauna amani kwani huenda unajua kesho hakutakucha salama kabla ya kuvamiwa na kuvunjiwa. Sasa kama kituo kimevamia, iweje kijumba chako ambacho silaha kubwa ni kisu cha kachumbari?

Hili suala la usalama limekuwa likiniudhi kuliko umaskini wetu. Ni kutokana na mashaka hayo ndio sababu kubwa iliyonifanya nitafute maisha kwingineko duniani. Ukiwa masikini dhiki ukiwa na ahueni mashaka. So what, Tukafungua vitabu vya hekma, tukakutana na maneno yasemayo ni ruksa kuhama mji/nchi kwa ajili ya kutafuta usalama na maisha yanayojali haki za binaadamu na kumuabudu muumba. Si haba, Lakini serious, serikali isifanye mchezo hata kidogo katika hili kwa sababu hata Congo DR mambo yalianza kama hivi hatimaye watu wakaweza kuanzisha vikundi vya kibabe na leo hii nchi haina raha tena.

Hongera kama nawe umeliona hili naamini utawaambia pro-wenzako walau wawe wanachangia kwa kutanguliza ubinadamu kama hivi.
 
Sasa naanza kuunganisha mistari......... maafisa wa polisi kwenda south........... mambo yakaenda ndivyo sivyo...... mkuu akaona aende mwenyewe............... siku si nyingi............ wasichana watarudishwa nchini na kupewa dhamana na case kusahaulika mazima.
....endelea kuunganisha dot, dili za madawa huwa hazijulikani mpaka mmoja miongoni mwao achome utambi. Na hilo likitokea huwa "revancha" haikosekani. Na revenge zake huwa zinakuwa na mshtuko mkubwa na kwa watu wakubwa. Endelea kuunganisha mistari vipi mtu mwenye fedha zake kumwagiwa hii kitu karibu na kituo cha usalama wa raia! Kwa hiyo endelea kuunganisha dot unaweza kupata mengi yahusuyo (tindikali na Nyongo= chumvi na...?)
 
Jk alikua Afrika kusini kuokoa jahazi la msanii wa filamu nchini Agness Masogange baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya!.

Kama ni kweli, basi vita dhidi ya wanaojihusisha na madawa ya kuelvya imeshindikana!
 
Hadi leo watu makini na watuatiliaji au wadadisi wa mambo wamekuwa wakiuliza, Rais wetu alivyo mtu wa kutoa pole na kushiriki misiba, ilikuwaje hadi leo, yeye na serikali yake, wakashindwa hata kutoa salaam za pole kwa msiba wa Ally Singano Zona, aliyeuwawa pale Morogoro kwenye shughuli za kisiasa.

Imetakiwa ufanyike uchunguzi huru wa Tume ya Kimahakama/ Kijaji, ili ukweli wa kifo hicho chenye utata, ujulikane. Hadi leo tuhuma zimelielemea Jeshi la Polis kuhusika na tukio hilo. Maana bomu na risasi ni moja ya vitu vizito na wamiliki na watumiaji wakubwa wa hivyo vitu vizito ni askari polisi.

Hadi leo, Rais Kikwete, mtu wa misiba, ameshindwa kutoa salaam za pole kwa kifo cha Mwanahabari Daudi Mwangosi...pamoja na kuuwawa kikatili namna ile...tuhuma zikilielemea Jeshi la Polisi, lakini kibaya kabisa amempandisha cheo, Michael Kamuhanda ambaye alipaswa kuwa ameshawajibishwa kwa yeye kujiuzulu au kufukuzwa kazi na kufikishwa mbele ya mikono ya sheria, haki itendeke!

Matukio ni mengi ya namna hii...watu wanajiuliza kulikoni?!

Tukio la bomu kutupwa na kulipuka kwenye mkutano wa hadhara wa CHADEMA, viwanja vya AICC, Soweto, mjini Arusha limeongeza maswali zaidi, Rais Kikwete ni mtu wa misiba, ilikuwaje yeye na serikali yake waka-treat kwa namna hiyo? Kama CHADEMA walivyosema. Tunawanukuu hapa;
" Kamati Kuu imefadhaishwa na kauli ya Serikali bungeni iliyolenga kulikosha Jeshi la Polisi kwa kuhusika kwake na shambulio hilo dhidi ya CHADEMA na wananchi wa Jiji la Arusha na kuilaumu CHADEMA wakati CHADEMA ndio mhanga wa shambulio hilo;

 Kamati Kuu imeshangazwa na kitendo cha Serikali kupuuza maafa yaliyowafika wananchi wa Arusha kwa kushindwa kushiriki katika mazishi ya wahanga wa mauaji ya Soweto na kuwashambulia kwa mabomu ya machozi, vipigo na maji ya sumu waombolezaji waliokusanyika kuwaaga marehemu waliouawa kwenye shambulio;

 Kamati Kuu imesikitishwa na Rais Kikwete kuendelea kukaa kimya juu ya shambulio la Arusha na kushindwa kwake kuunda Tume huru ya Kimahakama kuchunguza kwa uwazi shambulio hilo. Aidha, Kamati Kuu inaamini kwamba ukimya huu wa Rais Kikwete na kushindwa kwake hata kuwatembelea wafiwa na wahanga wengine wa shambulio hilo ni ushahidi mwingine wa kuhusika kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya Serikali katika kupanga na kutekeleza shambulio la Arusha;

 Kamati Kuu imefadhaishwa na kitendo cha Bunge la Jamhuri ya Muungano kuendelea na vikao vya Bunge kama kawaida; kukataa kutoa mchango wowote kwa wahanga na kushindwa kupeleka ujumbe wa Bunge kuwatembelea na kuwafariji wahanga na waathirika wa shambulio kinyume na utaratibu uliozoeleka wa Bunge kutambua na kushiriki katika majanga na misiba ya aina hii.

Kamati Kuu inautaka uongozi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano uwaeleze Watanzania kama maafa ya shambulio la Arusha yalikuwa na tofauti yoyote na maafa ya shambulio la bomu la Olasiti, au na maafa ya mabomu ya Gongo la Mboto, ajali ya MV Skargit au maafa mengine yaliyosababisha Bunge la Jamhuri kuahirisha shughuli zake, kutoa michango kwa waathirika pamoja na kupeleka ujumbe wa Bunge kuwafariji wafiwa na wahanga wa matukio hayo;" mwisho wa kunukuu.
 
Huyu jk anadhalilisha kiti cha Rais, na heshima ya Taifa kwa ujumla. Mkuu wa nchi hapaswi 'kuwatembelea' wagonjwa... Hasa kwenye maswala 'controversial' yanayohitaji uchunguzi wa kipolisi. Dunia nzima haikubaliki, kuna nini kinachoendelea hapa?

Kweli kabisa mkuu.

Na tangu aanze kutembelea waliokumbwa na mikasa mbali mbali ni hatua gani serikali yake imechukua kuhakikisha hayatokei tena?!

Huu ni usanii tu kuonyesha yuko karibu na watu lakini hakuna lo lote.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom