Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 6,954
- 12,409
Habari zenu wana JF na wazalendo wenzangu wote mliopo humu kwa ujumla,
Ndugu zangu wana JF, hapa nchini au duniani tunapozungumzia Mkoa wa Dar es Salaam basi ni ukweli ulio wazi kwamba ni kama vile tunakuwa tumeizungumzia Tanzania nzima. Nasema hivi kwa sababu kuu mbili.
1. Dar es Salaam ndio iliyobeba taaswira halisi ya nchi, ndio maana mkoa huu uliongoza mapambano yote ya kudai uhuru, na mambo mengine mengi ya kiserikali na kijamii yalifanyikia Dar es Salaam, kabla na baada ya uhuru.
2. Dar es Salaam ndio Mkoa uliokusanya makabila yote kutoka mikoa na maeneo mbali mbali ya nchi (kabila langu likiwa moja wapo wa wahamiaji wa Mkoa huu). Hivyo kila linalofanyika mkoa huu linakuwa limegusa kwa kiwango kikubwa mikoa mingine na watu wake kwa ujumla.
Sasa ukiona kiongozi au mtu maarufu anakataliwa katika mkoa wa Dar es Salaam, basi anatakiwa ajitafakari vizuri, kuliko kukimbilia kuwapa vijana vijihela na data za kuja mitandaoni kumsafisha na kutunga propaganda mbalimbali, sababu kuna uwezekano mkubwa wa kukataliwa nchi nzima.
Mwaka 2020 katika kampeni za uchaguzi mkuu, kuna chama kilimsimamisha mgombea kutoka ulaya, kwa kufikiri labda wana Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla watadanganyika, watetemeke na kumpa kura mgombea huyo. Lakini kumbe hali ikawa tofauti kwa kuanza kupuuzwa na wana Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla, hivyo kupelekea mgombea huyo kutoka ulaya kuangukia pua katika uchaguzi ule.
Na yeye kwa aibu siku mbili tatu baada ya uchaguzi akakimbilia ulaya kwa kudanganya umma kuwa anasakwa na serikali ili iwe rahisi yeye kupewa hifadhi ya ukimbizi na pia kujitoa katika kashfa ya aibu ya kushindwa uchaguzi.
Watu wenye akili tulijiuliza, kama kweli alitakiwa kuuwawa, kwanini asingeliuwawa wakati wa kampeni, badala yake aje auwawe baada ya uchaguzi, tena uchaguzi ambao yeye ndo ameshindwa!
Hilo likapita, sasa likaja hili la bandari chama hicho kilichoangukia pua Dar katika uchaguzi mkuu, kikalivalia njuga na swala hili wakiamini kuwa lingewabeba katika mkoa huo wenye mamilioni ya watu.
Cha kushangaza, pamoja na kualika viongozi njaa wa dini, wanasheria uchwara na wanasiasa wachumia tumbo kutoka maeneo mbali mbali ya nchi lakini bado wana Dar es Salaam wakaendelea kukiadhibu chama hicho na genge lake bila huruma.
Ndio maana nashauri viongozi wa chama hicho wajitafakari upya kuhusu kuelekeo wao. Kuruhusu wapitisha madawa ya kulevya, wezi, wakwepa kodi na ushuru wa bandari wawatumie katika ajenda zao kwa sababu ya malipo madogo tu yanayoliwa na viongozi wachache wa chama lilikuwa ni kosa la kiufundi.
Pia hii style ya kusambaza vijana wenye ID kumi kumi mitandaoni, kwani katika mkutano huonekana watu na sio wingi wa ID zao. Mfano humu tulitangaziwa mkutano wa bandari pale temeke, masham masham mitandaoni yakawa mengi, lakini siku ilipofika watu hawakujitokeza kama ilivyodhaniwa.
Hii ni dalili kuwa hii pinga pinga ya bandari ni ya mitandaoni tu lakini mitaani na nchini hakuna anaepinga.